BIKIRA WA KISUKUMA Ampigia Magoti JOKATE na Kumuomba Msamaha Baada ya Video Aliyomrekodi Akicheza Wimbo wa Diamond Kuzua Utata leo...
Hata siku Haijaisha toka Diamond Platnumz Apate Tuzo ya MTV Mama, Mchana wa leo Ametibua Mashabiki wake Baada ya Kupost Video ya Mpenzi wake wa Zamani Joketi Akicheza Moja ya Nyimbo zake huku akiandika caption ya Maneno haya 'Mbona Bado, Mtanyooka tu"Video Hiyo inasemekana ilirekodiwa na Bikira wa Kisukuma Aka Seth miezi sita iliyopita na leo Diamond kaipost kama Dongo kwa Jokate ambae siku za karibuni ameonyesha Kumsupport Ali Kiba...
Seth Ameingia Mtandaoni na Kuandika Haya:
Bikira_wa_kisukuma - IAM DEEPLY SORRY!Kama rafiki yako,sikujua yatakuja kuwa hivi...Tulirekodi Video hii tukiwa tunaenjoy NEWS CAFE zaidi ya MIEZI 6 iliyopita na haikuwa na madhara na nilipenda ulipopigwa wimbo huu na wewe ukaanza kuucheza and I liked it kwamba u still support ur Ex Music na sio maadui..A good thing!
Leo imeleta matatizo na kukusababishia maumivu ya moyo...Haikuwa dhamira yangu na Unajua na hata tulipoongea tulicheka na kufurahi na tulitaniana kuhusu Video ile.. I hope Diamond hakuwa na nia mbaya kiivyo kuiweka kwa sababu inaonyesha ulikuwa unacheza wimbo wake which means u love his music na unamsapoti...Pengine Diamond alipaswa kutumia maneno mazuri zaidi kuhusu Video ile instead of what he wrote kwa sababu imeonekana kama ni uchonganishi wakati bottom line haiko hivyo... Again JOKATE mpenzi,Iam sorry!
USHAURI WANGU KWA DIAMOND:
Jaribu kuepuka Misunderstanding zisizo za lazima,haikuwa na sababu kulikoroga kiasi hiki especially kwa muda huu ambao tulipaswa kama Watanzania kushangilia Ushindi wako..This was very Unnecessary especially kwa muda huu ambao Mashabiki waliokuwa wamegawanyika wameanza kurudi pamoja kama WATANZANIA...Ulipaswa kutumia moment hii kama GUNDI...From my heart IAM DEEPLY SORRY!