MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaonya Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu
Lipumba na wenzake kwa kuchelewa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa
kutohudhuria mahakamani.
Washtakiwa hao walionywa kwa nyakati tofauti jana wakati kesi zao zilipokwama kuendelea kusikilizwa kwa sababu yao.
Kesi inayomkabili Profesa Lipumba na
wenzake 31 ilitakiwa kuendelea kusikilizwa, lakini iliahirishwa kwa
sababu hakimu anayeisikiliza, Cyprian Mkeha hakuwapo na washtakiwa
walichelewa kufika mahakamani.
“Mahakama inatoa onyo kwa Profesa
Lipumba na wenzako 31 kwa kuchelewa kufika mahakamani, utaratibu wa
mahakama kesi zinaanza saa tatu kamili asubuhi, mnatakiwa kuheshimu muda
sababu kila mtu anaishi mbali.
“Nimewapa onyo, kesi itaendelea Julai
10 mwaka huu washtakiwa wote mnatakiwa kuwahi,” alisema Hakimu Huruma
Shahidi aliyeahirisha kesi hiyo.
Profesa Lipumba na wenzake
wanakabiliwa na mashtaka ya kufanya maandamano bila kibali na kukaidi
amri halali ya polisi iliyowataka kutawanyika Januari 27, mwaka huu.
Wakati huo huo, mahakama hiyo mbele ya
Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda imemuonya Mdee kwa kutohudhuria
mahakamani na kwamba iwapo hatafika Julai 6, mwaka huu itatoa hati ya
kumkamata.
“Kinachoendelea ni maneno yasiyo na
ushahidi, mshtakiwa hayupo na wadhamini hawapo, tutenganishe siasa na
mahakama, ifike wakati tuheshimu mahakamani, hakuna sababu ya kuendelea
na kesi kama mshtakiwa hayupo.
“Tarehe ijayo Julai 6 awepo mahakamani
ili kesi iendelee kusikilizwa, iwapo hatafika sitajali mbunge wala
katibu kata, nitatoa hati ya kumkamata,” alisema Kaluyenda.
Awali Wakili wa Serikali Mkuu, Benard
Kongola akisaidiana na Joseph Maugo, waliomba mahakama itoe hati ya
kumkamata mshtakiwa kwani sababu za kutofika mahakamani hazina msingi.
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala
akisaidiana na John Mallya walidai Mdee anahitaji ruhusa ya Spika wa
Bunge ndiyo atoke bungeni.
Mbali na Mdee, washtakiwa wengine ni Renina Leafyagila na Sophia Fanuel.
Washtakiwa wengine, Rose Moshi, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Edward Julius, Martha Mtiko na Beatus Mmari waliachiwa huru.
Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa
Oktoba 4, mwaka huu, katika Mtaa wa Ufipa, uliopo Kinondoni, jijini Dar
es Salaam, isivyo halali, washtakiwa walikiuka amri halali ya Mrakibu wa
Polisi (SP), Emmanuel Tillf iliyowataka kutawanyika.
Ilidaiwa kuwa siku na mahali
lilipotokea tukio la kwanza, washtakiwa walifanya mkusanyiko isivyo
halali kwa lengo la kuandamana kwenda Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
- See more at:
http://mtanzaniaforums.com/index.php/siasa/item/575-mahakama-yawaonya-prof-lipumba-na-halima-mdee#sthash.afeV8VuZ.dpuf

Na Hamida Hassan
Kuanzia Jumamosi iliyopita, viongozi mbalimbali wamekuwa wakijitokeza
na kutangaza nia ya kugombea nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM).Hakika idadi ni kubwa lakini mwisho wa siku lazima apatikane
mmoja ambaye atachuana na mgombea kutoka Ukawa.
Rose Ndauka.
Kutokana na hilo, mastaa wa hapa Bongo
nao wamekuwa sehemu ya kutangaza nia kwa waheshimwa hao kwani wapo
walioonesha wazi kuwa wanamuunga mkono nani huku wengine wakibaki na
siri moyoni.Mwandishi wa makala haya amejaribu kuzungumza na baadhi ya
mastaa hao kujua wako upande gani na wanazungumziaje upepo wa kisiasa
kwa sasa.
Wastara Juma
Kiukweli sipendi sana mambo ya siasa lakini linapokuja hili la watangaza
nia ya kugombea urais, naomba niseme tu kwamba nataka kuongozwa na mtu
ambaye hatakuwa na tamaa ya kujinufaisha yeye.
Awe ni kiongozi
asiyekuwa na njaa ambaye akiingia ikulu hataangalia tumbo lake na watu
wake wa karibu bali kushughulikia matatizo ya wananchi.
Rose Ndauka
Ninaye
ambaye ningependa awe rais wa nchi hii lakini kwa sasa siwezi kumuweka
wazi. Hata hivyo, natamani apatikane mtu mwenye nia ya dhati ya
kuiongoza nchi hii kwa haki.
Maimartha Jesse.
Maimartha Jesse
Mimi bwana ni Team Lowassa! Sababu ya kumuunga mkono kiongozi huyu ni
kwamba, anajitambua na ni mtu anayeweza kuchukua maamuzi magumu.Mimi
nina imani naye na naamini akipewa nafasi ya kuingia ikulu, mambo mengi
yatakuwa sawa likiwemo hili la elimu ambalo limekuwa ni kipaumbele
chake.
Miriam Jolwa - Kabula
Kwenye hili la urais nawaunga mkono watu wawili, kati yao akipita mmoja
itakuwa poa tu. Kwanza ni Makongoro Nyerere ambaye ni mtu wa nyumbani
lakini pia Lowassa ambaye licha ya mimi kumkubali pia anaonekana
kukubalika kwa wananchi.
Ester Kiama.
Ester Kiama
Mchuano kwa sasa uko kwa Membe na Lowassa. Wote ni viongozi wenye sifa ya kuliongoza taifa hili vizuri tu.
Lakini sasa ukiniambia nichague mmoja nitasema Lowassa. Unajua kwa
nini? Ni mtu ambaye amejitosheleza, hana shida kiasi kwamba hata
akiingia pale ikulu hataanza kwanza kujikusanyia mali na fedha.
Kulwa Kikumba ‘Dude’
Mimi huniambii kitu kwa Lowassa. Ni mtu makini, ana nia thabiti ya kuliongoza taifa hili lenye matatizo kibao.
Halima Yahya ‘Davina’
Mimi siyo mshabiki wa mambo ya siasa na ndiyo maana hata upepo
unavyokwenda mimi naona sawa tu. Ila kwa uzalendo lazima nitapiga kura
na kiongozi atakayepitishwa na Chama Cha Mapinduzi basi nitampigia kura.
Mbali na mastaa hao waliojaribu kuweka
wazi hisia zao, wengine walionekana kuchenga na kutotaka kusema wapo
upande gani. Mastaa hao ni pamoja na Elizabeth Michael ‘Lulu’, Blandina
Chagula ‘Johari’ Jacqueline Wolper, Jokate Mwegelo na Mahsein Awadh ‘Dk.
Chen’.
- See more at: http://mtanzaniaforums.com/index.php/gossip/item/574-mastaa-na-upepo-wa-kisiasa-bongo#sthash.j2eYnyGE.dpuf