Wednesday, March 30, 2016

WADAU WA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA WAKUTANA KUJADILI MPANGO KAMAMBE WA USAFIRI WA ANGA ( CIVIL AVITIATION MASTER PLAN) JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho(katikati) Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari(Kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mhandisi George Sambali (kushoto) wakiwa kwenye warsha ya kujadili rasimu ya Mpango Kamambe Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) warsha hiyo ilifanyika katika ofisi za Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) ), Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho akifungua warsha ya kujadili rasimu ya Mpango Kamambe wa Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) iliyofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA). Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wadau mbali mbali wa sekta ya usafiri wa anga wakishiriki warsha ya kujadili rasimu ya Mpango wa Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
 
Wadau wa sekta ya Usafiri wa anga nchini ,wamekutana katika warsha ya siku moja kujadili rasimu ya mpango kamambe wa usafiri wa anga  yaani ( the Civil Aviation Master Plan) makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini(TCAA), Banana-Ukonga. 
Warsha  hiyo iliyowakutanisha wadau kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi  na Mawasiliano, mashirika yanayotoa huduma za usafiri wa anga  nchini , Mamlaka ya Viwaja vya Ndege na mwenyeji Mamlaka ya Usafiri wa Anga  imefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho.
Lengo la warsha hiyo ni kupata maoni ya wadau kuhusu rasimu hiyo ya mpango kamambe wa sekta ya usafiri wa anga nchini  ambayo imetayarishwa na kampuni ya LEAPP ya Australia chini ya udhamini wa Benki ya Dunia. Kampuni hiyo ilianza kuanda rasimu hiyo mwaka 2015 kazi ambayo imefanyika kwa miezi 12. 
Akizungumza  wakati wa ufunguzi huo , katibu Mkuu wa wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema lengo la serikali ni kuwezesha  Tanzania kutoa huduma za usafiri wa anga  kwa mujibu wa viwango na taratibu zinazokubaliwa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) pamoja na kuweka mazingira mazuri yatakayoruhusu  ushindani wa kibiashara katika sekta hii.  
Ameongeza kuwa sekta ya usafiri wa anga imekuwa ikikua , mathalani  takwimu zinaonyesha safari za ndege zimeongezeka kwa asilimia 8  katika mwaka 2015 ikilinganishwa na zile zilizofanyika mwaka 2014. Kadhalika idadi ya abiria imekuwa ikikua kwa kiwago cha asilimia 1.5- 2 kwa mwaka.  
Lengo la warsha hiyo ni kupata maoni ya wadau kuhusu rasimu hiyo ya mpango kamambe wa sekta ya usafiri wa anga nchini  ambayo imetayarishwa na kampuni ya LEAPP ya Australia chini ya udhamini wa Benki ya Dunia.
BENKI YA KILIMO YAJIDHATITI KUSAIDIA UPATIKANAJI WA MASOKO NCHINI‏ Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) akiwa naMkurugenzi wa Biashara na Mikopo Bw. Robert Pascal wakifuatilia mada wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Robert Pascal (Kulia) akiwasilisha Mada kuhusu Wajibu wa TADB katika kuendeleza kilimo nchini wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo, na Uvuvi, Mhe. William Ole Nasha (Kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Wapili kulia) wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania, Bibi Janet Bitegeko ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo, na Uvuvi, Mhe. William Ole Nasha (Kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania, Dkt. Sinare Yusuf Sinare (Kushoto) na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Wapili Kushoto) wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania, Dkt. Sinare Yusuf Sinare (Wapili kushoto) akizungumza na Balozi wa Norway nchini, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad (Kushoto) wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo, na Uvuvi, Mhe. William Ole Nasha (Kulia), Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Wapili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu-SAGCOT, Bw. Geoffrey Kireng Mbunge wa Babati Vijijini, Mhe. Jitu Soni (Kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Robert Pascal (Katikati) wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mmoja wa wadau waliohudhuria warsha hiyo. Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo, na Uvuvi, Mhe. William Ole Nasha (Kulia) akiagana na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Katikati) na Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania, Dkt. Sinare Yusuf Sinare (Kushoto) mara baada ya kufungua Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Wapili Kushoto) akizungumza na Mbunge wa Babati Vijijini, Mhe. Jitu Soni (Kulia) wakati alipotembelea Meza ya TADB wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania, Dkt. Sinare Yusuf Sinare (Wapili kulia) na Afisa Maendeleo ya Biashara Mwandamizi wa TADB, Bw. George Nyamrunda. Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Saidi Mkabakuli akitoa maelezo ya kuhusu TADB kwa mmoja wa wadau waliotembela Meza ya TADB wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Mbunge wa Babati Vijijini, Mhe. Jitu Soni (Kulia) akioneshwa moja ya bidhaa zilizokuwa zikioneshwa katika Meza ya TADBwakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Anayemuonyesha ni Afisa Maendeleo ya Biashara Mwandamizi wa TADB, Bw. George Nyamrunda. Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria kusaidia upatikanaji wa Masoko ili kuongeza Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini ili kuchagiza na kusaidia kuwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini. Akizungumzia katika Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam, yenye Mada Kuu ya Warsha hiyo, “Wazalishaji Tuanze na Soko, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi amesema kuwa ukosefu wa masoko ya mazao unaowakabili wakulima umekuwa ni moja ya changamoto kuu zinazorudisha nyuma maendeleo ya sekta ya kilimo nchini. Bw. Samkyi amesema kuwa ili kusaidia kutokomeza changamoto hiyo na nyinginezo Serikali iliamua kuanzisha TADB ili kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa mikopo na masoko katika sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika kilimo nchini. “Katika kutekeleza majukumu yetu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imeanza huduma zake kwa kulenga minyororo michache ya ongezeko la thamani katika kilimo ambapo mikopo ya aina mbalimbali hutolewa kuwezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini Tanzania,” alisema Bw. Samkyi. Kwa mujibu wa Bw. Samkyi, Benki inatoa mikopo kwa ajili ya uwekezaji kwenye ujenzi viwanda vya kusindika mazao, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya usindikaji wa mahindi na kuongeza thamani, ununuzi wa vifaa vya uvunaji wa kisasa wa mahindi, vifungashio vya kisasa vya kuhifadhia mahindi na teknolojia ya uhifadhi wa mahindi kupunguza upotevu wa mazao. “Kwa sasa tumejikita katika mnyororo mzima wa uongezaji wa thamani kuanzia uandaaji wa shamban hadi kwa upatikanaji wa masoko, ikiwemo mahitaji ya uzalishaji wenye tija kwenye sekta nzima ya kilimo kuanzia hatua za awali za utayarishaji wa mashamba, kupima ubora wa udongo na virutubisho vinavyohitajika kwenye uzalishaji wa mahindi, upatikanaji wa pembejeo za kilimo zikiwemo mbegu bora, mbolea, madawa na vifaa na teknolojia mbali mbali za umwagiliaji na fedha kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali za uzalishaji wa mahindi,” aliongeza. Mkurugenzi Samkyi, ameongeza kuwa Benki imejipanga kutoa mikopo ya ununuzo wa mitambo na mashine za ukaushaji, usafishaji na uchambuzi wa madaraja ya mahindi pamoja na mitambo ya usindikaji na usagaji wa nafaka na ujenzi wa viwanda vya kusindikia mazao ikiwamo fedha kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali za uendeshaji katika kuongeza thamani ya mazao Pia, Benki inatoa mikopo kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya kilimo katika kuimarisha minyororo ya thamani katika kilimo ambapo inajumuisha ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na mitambo ya umwagiliaji, uchimbaji wa visima vya maji ya umwagiliaji, ujenzi wa mabawa ya uvunaji maji ya mvua, ujenzi wa maghala bora ya kuhifadhia mahindi na ujenzi wa miundombinu ya masoko. Akizungumzia aina ya mikopo itolewayo na benki hiyo, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo Bw. Robert Pascal amesema kuwa Benki inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya muda mfupi (Short term loans), mikopo hii ni ya muda mfupi usiozidi miaka miwili (au miezi 24), Mikopo ya muda wa kati (Medium term loan), mikopo ya muda wa kati hutolewa kwa kipindi cha miaka 2 hadi 5 (yaani kati ya miezi 24 na 60) na Mikopo ya muda mrefu, mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kugharamia shughuli za uwekezaji mkubwa kwenye kilimo na ambazo marejesho yake yatafanyika katika kipindi cha miezi 60 hadi 180 (yaani kati ya miaka 5 hadi 15). Bw. Pascal ameongeza kuwa riba itozwayo kwa upande wa Mikopo ya muda mfupi (Short term loans) ni riba ya asilimia saba (7%) mpaka (8%) kwa mwaka. Ambapo mikopo hii Hutolewa kwa ajili ya kufanikisha shughuli za kilimo kwenye mnyororo wa thamani. Kwa mfano, kugharamia shughuli za kilimo zinazofanywa kabla ya mazao kuvunwa, na mara baada ya kuvunwa, ununuzi wa mazao, ununuzi wa zana na mashine za kilimo na mahitaji mengine ya kifedha katika mnyororo wa thamani. Ameongeza kuwa mikopo ya muda wa kati hutolewa kwa kipindi cha miaka 2 hadi 5 (yaani kati ya miezi 24 na 60) na hutozwa riba ya asilimia tisa (9%) mpaka (10%) kwa mwaka. Na mikopo hii hutolewa ili kufanikisha mahitaji maalumu, mathalani: kupanua mashamba, kuzalisha aina mpya za mbegu, mifugo, na samaki na kuongeza kiwango cha rasilimali au uwekezaji, kuboresha miundombinu, pamoja na kuziba pengo la mahitaji mengine ya muda wa kati kwenye mnyororo wa thamani. Na kwa upande wa Mikopo ya muda mrefu hutozwa riba ya asilimia kumi na moja (11%) mpaka (12%). Mikopo hii hutolewa kugharamia mahitaji ya muda mrefu, mathalani: gharama za kupata rasilimali, kujenga miundombinu mikubwa ya kilimo, kupanua mashamba makubwa na ya kati, pamoja na shughuli nyingine za kilimo zinazohitaji mikopo ya muda mrefu. Mikopo ya muda mrefu inalenga kufanikisha uwekezaji kwenye miradi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na mahitaji mengine ya muda mrefu. “Mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kujenga/kukarabati miundombinu katika sekta ya kilimo kwenye mnyororo wa thamani, kwa mfano: skimu/mifumo ya umwagiliaji, maghala ya kisasa ya kuhifadhia mazao, pamoja na mahitaji mengine ya miundombinu ya kilimo,” aliongeza Bw. Pascal. TADB ilianzishwa kwa Sheria Namba 5 ya mwaka 2006 inayosimamia Benki na Taasisi za Fedha, pamoja na Kanuni za Uanzishaji wa Benki na Taasisi za Fedha (Development Finance) za mwaka 2012. Lengo la msingi la kuanzishwa kwa TADB ni kutoa mikopo ya muda mfupi, kati na muda mrefu kwa sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi ya kilimo nchini. Habari na picha na: Bw. Saidi Mkabakuli Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)

Copy the BEST Traders and Make Money : http://ow.ly/KNICZ

Wizara ya afya yalifanyia ukarabati tanuri la kuchomea takataka za Hospitali Chakechake

WIZARA ya Afya Pemba, imeanza kazi ya ukarabati wa Tanuri maalumu la kuchomea takataka zinazotoka katika Hospitali ya Chake Chake, kilio ambacho Makamo wa Pili wa Rais Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, kilimsikitisha sana kutokuwepo kwa tanuri hilo wakati alipotembelea kisiwani Pemba Mwanzoni mwa mwezi huu.

(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

Muonekano wa Jengo la Mahkama Kuu Pemba

JENGO la Mahkama kuu ya Pemba, likiwa katika monekano mpya baada ya kumaliza kufanyiwa ukarabati wa hali ya juu, jengo hilo linasubiri fanicha mpya, ili liweze kuhamiwa na kurudi kufanya kazi zake za kama zamani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

Jobs & Employment Opportunities in Serengeti Breweries Limited

by Kazi Bongo  |  at  4:51:00 AM
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); Serengeti Breweries Limited (SBL) is a fully integrated beverage business in Diageo Africa (supply and demand for beer and spirits) It is a subsidiary of East Africa Breweries Limited (EABL), the largest business unit in Diageo Africa and the largest listed Company on the NSE in Kenya. SBL operates exclusively in Tanzania and is the second largest beer... Read More »

Employment Opportunities at Tanzania Health Promotion Support (THPS)

by Kazi Bongo  |  at  4:48:00 AM
Tanzania Health Promotion Support (THPS) As CDC prime awardee; THPS is currently seeking committed and motivated Tanzanians to fill in the following positions: 1.0 Procurement and Logistics Manager 2.0 Internal Compliance Manager 3.0 Sub Grants Officer How to apply: Interested applicants should apply through THPS website (www.thps.or.tz) using vacancy link located under career opportunities, attaching their application cover letter one page maximum and... Read More »

NAFASI ZA KAZI CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA - College Of Business Education JOBS

by Kazi Bongo  |  at  4:47:00 AM
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); Applications are invited from suitable qualified and experienced Tanzanians to fill the following vacant positions, at the College of Business Education (CBE). College of Business Education was established by Act of Parliament, Act No. 31 of 1965. College of Business Education is a Public Training Institution which provides, Training, Research and Consultancy Services in the fields of Accountancy,... Read More »

EMPLOYMENT OPPORTUNITIES IN MBEYA

by Kazi Bongo  |  at  4:41:00 AM
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); ... Read More »

JOBS IN MOROGORO

by Kazi Bongo  |  at  4:41:00 AM
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); NATURAL WOODLAND AND CONSERVATION MANAGERKVTC is the largest grower of teak in Africa and has established plantations in Tanzania since 1992. The Company manages teak plantations and natural woodlands as well as a timber processing plant located in the Ulanga District. The Company is the largest exporter of timber products from Tanzania and employs around 300 people. For... Read More »

140616Messi-jpg
Kwenye mchezo wa soka kwa sasa kuna vita kubwa kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Vita hiyo imepelekea mpaka baadhi ya mashabiki kupoteza uhai.Messi amefanikiwa kuitumikia timu ya taifa ya Argentina kwa kucheza mechi 107 mpaka sasa na amefanikiwa kufunga magoli 50, akiwa nyuma ya mchezaji wa zamani wa timu hiyo Gabriel Batistuta ambaye alicheza mechi 78 na kufunga magoli 56.

Miaka kadhaa iliyopita kabla ya kupewa kitambaa cha unahodha, Messi alionekana hafanyi vizuri kwenye timu ya taifa wakati kwenye timu yake ya Barcelona alikuwa anaonekana kuwa mwiba mkali na kuchukua tuzo kadhaa za mchezaji bora.
‘Hakuna marefu yasiyo na ncha’, kilikuwa ni kipindi cha mpito kwa Messi, baada ya kitambaa cha unahodha kupita kwa Javier Mascherano na Carlos Tevez hatimaye kikamuangukia Messi.

Hakuna anayependa kufungwa kwenye mchezo wa soka, baada ya muda lawama zote za kufanya vibaya kwa Messi zimefutika na mashabiki wengine wameenda mbali zaidi kwa kumfananisha na Maradona aliyeichezea timu hiyo ya taifa kwa miaka 17, akicheza mechi 91 na kufunga magoli 34.

Maajabu ya Messi yalionekana kuwakuna mashabiki wengi kwenye fainali za kombe la dunia 2014 zilizofanyika nchini Brazil, timu ya Argentina ilipambana na New Zealand kwenye hatua ya robo fainali. Hakika Messi alionyesha ubora wake wa kustahili kuvaa kitambaa cha unahodha.

Gabriel Batistuta anaongoza kuwa mfungaji wa muda wote kwenye timu ya taifa ya Argentina, amefanikiwa kufunga magoli 56, Messi 50, Hernan Crespo 35, Diego Maradona 34 na Sergio Aguero 32.
Messi ni mchezaji aliyeweka rekodi ya dunia kwa kuchukua tuzo ya mchezaji bora kwa mara tano huku mpinzani wake Ronaldo akifanikiwa kuchukua mara tatu.

KASI YA UONGOZI WA RAIS MAGUFULI NI WA 4G, AFYEKA MISHAHARA MIKUBWA YA VIGOGO KATIKA SERIKALI YAKE.

Chato. Rais John Magufuli ametangaza kiama cha watendaji wakuu wa mashirika na taasisi za umma waliojipangia mishahara minono kufikia Sh40 milioni akiahidi kuifyeka hadi kiwango kisichozidi Sh15 milioni kuanzia bajeti ijayo ya fedha ikiwa ni punguzo la asilimia 63.

“Atakayeona kiwango hicho ni kidogo namshauri aanze kutafuta kazi sehemu nyingine kwa sababu hatuwezi kuendelea kulipana mishahara minono kiasi hicho katikati ya wananchi wanaoishi katika lindi la umaskini,” alisema Rais Magufuli na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mazaina mjini Chato jana katika siku yake ya kwanza nyumbani kwake tangu achaguliwe kushika wadhifa huo, Rais Magufuli aliahidi kupandisha mishahara ya watumishi wa chini ili kupunguza tofauti ya kipato kati yao na wale wa juu. 

“Katika Serikali ninayoongoza, sitegemei kumlipa mtumishi zaidi ya Sh15 milioni; tayari nimeunda tume kushughulikia suala hilo,” alisema na kuongeza: “Kiwango tunachopunguza kutoka kwenye mishahara minono ya wakubwa tutawaongezea watumishi wa chini ambao baadhi wanalipwa mishahara midogo inayoanzia Sh300, 000.”

Kodi ya mishahara
Akizungumzia malalamiko ya muda mrefu ya wafanyakazi kuhusu kodi kwenye mishahara, Rais alisema Serikali inakusudia kupunguza kiwango hicho hadi kufikia tarakimu moja, akibainisha kuwa haitazidi asilimia tisa kuanzia bajeti ijayo ya Serikali.

Ushuru wa mazao

Rais pia aligusia suala la kodi nyingi kwenye mazao aliyosema ni mzigo kwa wakulima na kuahidi kuzipunguza ili pamoja na kuwapa nafuu wakulima ambao ndiyo hubeba mzigo wa kodi hizo, pia kuleta tija kwenye sekta ya kilimo kinachoajiri zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania. 

“Tunalenga kuhakikisha kodi na ushuru kwenye mazao yetu hayazidi tatu au mbili; hii itawawezesha wakulima siyo tu kunufaika na kilimo, bali pia kumudu ushindani wa soko la mazao ndani na nje ya nchi,” alisema.

Shule zenye matokeo mabaya

Rais alisema hatakuwa tayari kutumia mabilioni ya fedha za umma kutekeleza sera ya elimu bure ya msingi halafu wanafunzi wafeli darasa la saba au kupata alama sifuri katika mitihani ya kidato cha nne. 

“Maofisa elimu, walimu wakuu, wakuu wa shule, wajumbe kamati na bodi za shule zilizofanya vibaya katika matokeo yaliyopita wajitathmini na kutafakari kama wanastahili kuendelea kushika nafasi zao,” alisema.

Aliwaomba Watanzania kila mmoja kwa nafasi na uwezo wake, kujitokeza kuchangia maendeleo ya elimu, hasa changamoto ya madawati na vyumba vya madarasa iliyotokana na sera ya elimu bure ya msingi.