Thursday, June 25, 2015

KINANA AFANYA AMSHA AMSHA KUBWA KATIKA JIMBO LA KWIMBA LEO, AKAGUA MIRADI, MWENYEKITI WA CHADEMA AHAMIA CCM, MKUTANO NGUDU MJINI WAFURIKA WANANCHI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara aliofanya leo katika Uwanja wa CCM, katika mji mdogo wa  Ngudu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uahi wa Chama katika wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo alipohutubia mkutano wa hadhara aliofanya kwenye viwanja vya CCM kwenye mji mdogo wa Ngudu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza leo
 Wananchi waliofurika katikaUwanja wa CCM katika mji mdogo wa Ngudu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, abdulrahman Kinana alipowahutubia katika mkutano wake wahadhara uliofanyika kwenye viwanja hivyo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama wilayani Kwimba mkoani Mwanza leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wananchi katika mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, uliofanyika leo kwenye viwanja vya CCM kwenye mji mdogo wa Ngudu wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
 Mbunge wa Kwimba, Shanif Mansoor akihutubia mkutano wa katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo, kwenye Viwanja vya CCM, kwenye mji mdogo wa Ngudu, wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, magesa Mlongo, alipowasili kwenye Viwanja vya CCM, kwenye mji mdogo wa Ndugu, kuhutubia mkutano wa hadhara, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na uhai wa Chama wilayani Kwimba mkoani humo,leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasili katika Viwanja vya CCM, kwenye mji mdogo wa Ngudu, kuhutubiamkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza leo. Wapili kushoto ni Mbung wa Kwimba, Shanif Mansoor
 Kinamama wakiwa na vyerehani ambavyo walikabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu aliufanya leo katika viwanja vya CCM katika mji mdogo wa Ngudu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama, katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza leo. vyerehani hivyo vimetolewa na mbunge wa Kwimba, jimbo la Shanif Mansoor

ALIPOWASILI KUANZA ZIARA KATIKA JIMBO LA KWIMBA
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia baadhi ya viongozi wa CCM, wakati wa mapokezi yaliyofanyika eneo la Njiapanda ya Mwamashimba, wakati akitokea jimbo la Misungwi, kuingia katika jimbo la Kwimba, kuendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Mwanza leo. Kushoto ni Katibu wa  CCM wilaya ya Kwimba, Tabu Ngesi.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akilakiwa kwa ngoma ya Sungusungu, wakati wa mapokezi yaliyofanyika katika eneo la Njiapanda ya Mwamashimba, wakati akitokea jimbo la Misungwi, kuingia katika jimbo la Kwimba, kuendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Mwanza leo. Kushoto ni Katibu wa  CCM wilaya ya Kwimba, Tabu Ngesi.
Katibu Mkuu wa CCM akivalishwa mavazi ya kiongozi wa Sungusungu, wakati wa mapokezi ya kuingia jimbo la Kwimba, yaliyofanyika  eneo la Njiapanda ya Mwamashimba, wakati akitokea jimbo la Misungwi, kuingia katika jimbo hilo, kuendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Mwanza leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiongoza msafara wa Sungusungu, wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika eneo la Njiapanda ya Mwamashimba, wakati akitokea jimbo la Misungwi, kuingia katika jimbo la Kwimba, kuendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Mwanza leo. Kushoto ni Katibu wa  CCM wilaya ya Kwimba, Tabu Ngesi.
 Komredi Kinana akiwa rasmi Ki-Sungusungu
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mlongo akiwasalimia wananchi wakati Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipowahutubia wananchi baada ya kupokewa katika eneo la Njiapanda ya Mwamashimba, na kufika Kijiji cha Hungumalwa, wakati akitokea jimbo la Misungwi, kuingia katika jimbo la Kwimba, kuendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Mwanza leo.Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Mbunge wa jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor, akiwahutubia wananchi katika Kijiji cha Hungumalwa, mwanzoni mwa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika jimbo la Kwimba, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Mwanza leo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana  akiwahutubia wananchi katika Kijiji cha Hungumalwa, mwanzoni mwa ziara yake katika jimbo la Kwimba, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Mwanza leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasha taa kuzindua mradi wa umeme  katika kijiji cha Hungumalwa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Cham katika jimbo la Kwimba, mkoani Mwanza leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokewa kwa ngoma, alipowasili katika kijiji cha Hungumalwa,kushiriki ujenzi waZahanati katika kijiji hicho leo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa chama, katika jimbo la Kwimba mkoani Mwanza.
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema katika kijiji cha Ilula, Amara Malelelemki, akitangaza kuhamia CCM, wakati Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipozungumza na wananchi baada ya kuzindua ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Hungumalwa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika jimbo laKwimba mkoani Mwanza leo.
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mlongo akishiriki ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Hungumalwa, wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto), alipozindua ujenzi wa Zahanati hiyo, leo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika jimbo la Kwimba mkoani Mwanza. Wapilikshoto ni Mbunge wa jimbo hilo, Shanif Mansoor

KUMBUKUMBU MUHIMU YA MWALIMU NYERERE KATIKA WILAYA YA KWIMBA

 Jengo la Ofisi ya CCM wilya ya Kwimba mkoani Mwanza ambalo lilizinduliwa ujenzi wake na Baba wa Taifa hayati Mwalimu Nyerere, tarehe 15/ 2/ 1975
 Wajumbe wakiwa kwneye Kikao cha Jimbo la Kwimba, ambacho Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alikiongoza leo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na Uhai wa Chama katika jimbo hilo mkoani Mwanza
 Katibu wa CCM wilaya ya Kwimba, Tabu Ngwesa akitoa maelezo ya uhai wa Chama wakati wa kikao hicho cha jimbo kilichoongozwa na Kinana leo
 Mkuu wa wilaya ya Kwimba, Pili Moshi, akitoamaelezo ya Utekelezaji wa ilani ya CCM katika wilaya hiyo, wakati wa kikao cha jimbo la Kwimba, wakati wa kikao cha jimbo kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (watatu kulia), kilichofanyika ofisi ya CCM wilaya hiyo leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua mradi wa maji wa Ngudu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na uhai wa Chama katika jimbo la Kwimba mkoani Mwanza leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Mwanahamisi Pascal, baada ya kuzindua mradi wa maji wa Ngudu akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na uhai wa Chama katika jimbo la Kwimba mkoani Mwanza leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda mbegu katika  kwenye vitalu ya uoteshaji miche ya miti, alipotembelea mradi wa Vijana wa Ngudu wa kutunza mazingira, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika jimbo la Kwimba mkoani Mwanza leo
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akishiriki kupanda mbegu kwenye vitalu hivyo

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wauguzi na madaktari alipotembelea wodi mpya ya wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya mji mdogo wa Ngudu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama wilayani Kwimba mkoani Mwanza leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Adulrahman Kinana akikagua chumba cha agonjwa mahututi alipotembelea wodi hiyo mpya katika hospitali ya mji mdogo wa ngudu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Kushoto ni Mbunge wa Kwimba Shanif Mansoor
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye wakitoka kukagua wodi hiyo


NYUMBANI KWA BALOZI WA NYUMBA KUMI
 Mjumbe wa Shina namba 12, Spezioza Balele akifungua kikao cha Shina hilo, ambacho kilihudhiriwa na katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati), katika Mtaa wa Ngumo kwenye mji mdogo wa Ngudu, akiwa katika  ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza leo
Mjumbe huyo akimkaribisha Kinana baada ya kufungua kikao
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa kikao cha shina namba 12, kilichofanyika nyumbani kwa Balozi wa shina hilo, Spesioza Balele, mtaa wa Ngumo, katika mji mdogo wa Ngudu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na uhaiwa chama katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO NA ADAM MZEE

By Zitto,
Juzi nilipokuwa jijini Mbeya niliulizwa na wananchi iwapo nami nitachukua kiinua mgongo cha tshs 238 milioni kitakacholipwa kwa wabunge. Nimewajibu kuwa msimamo wangu upo wazi kwenye masuala haya.

Chochote ambacho sio haki yangu sitachukua. Fedha yote ya ziada ya kile ninachostahili kwa mujibu wa sheria nitapeleka kusaidia ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi Shule ya Buhangija na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road. Buhangija nilitembelea mwezi Aprili na kukuta watoto wanalala kwa shida sana.

Niliamua kusaidia juhudi zinazofanywa na Miss. Tanzania Briggite Alfred ambaye anajenga Bweni pale. Ocean Road ni mchango wangu katika kusaidia wagonjwa wa saratani, ugonjwa uliomchukua mama yangu Hajjat Shida Salum.

Source: His facebook page.

Huyu Zitto kweli ni akili kubwa. Muda si mrefu wanafiki na wapenda sifa nao wataanza kumuiga, japo moyoni hawapendi kuachia hiyo mihela.

Mtangazaji mwenye sauti nzito Bongo kupitia Clouds FM, Millard Ayo, Jumatatu iliyopita alibanwa azungumzie uhusiano wake na warembo wenye majina makubwa nchini, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’,  Jacqueline Wolper na Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambapo alimfungukia mmojammoja.

Katika mahojiano maalum na Kipindi cha Sporah Show, mtangazaji alimbana Millard akimtaka aseme ukweli kuhusu warembo hao ambapo  alianza kwa kumzungumzia Lulu kuwa hajawahi kuwa mpenzi wake zaidi ya kumfahamu katika sanaa.

“Kuhusu Lulu! Hapana sijawahi kabisa kuwa na uhusiano naye. Yaani hata kuwaza sijawahi. Namfahamu kuwa ni mwigizaji na ni mtu ambaye nimekuwa nikimfuatilia kupitia kazi zangu za utangazaji,” alisema mtangazaji huyo staa.

Millard aliendelea kupangua, ikafika zamu ya Wolper. Alikana vikali kuwa naye hata kujuana kwao si kwa ukaribu. Alisema:


“Haa! Wolper ndiyo kabisa, nimekuwa nikimuona na kumsikia tu, wala sikuwahi kumuwazia kwa lolote lile isipokuwa ninamjua kama msanii wa Bongo Muvi na huwa nakutana naye kama ninavyoweza kukutana na mtu mwingine yeyote ambaye hatujuani.”

Kwa upande wa Jokate, hapo alipiga kituo kidogo na kuanza kumzungumzia kwamba, amemfahamu miaka mingi na alikuwa akimpenda kama ‘girl friend’ wake kwani wakati anasoma alishawahi kupanda naye daladala na wakapiga stori.

“Nampenda Jokate kwa sababu mpole, anatoka katika familia ya wachakarikaji, hivyo nimekuwa nikimshirikisha katika mambo yangu. Nampenda kwa sababu hiyo ila huwezi kuamini, nilipotezana naye na baadaye tumekuja kukutana tayari yeye ni maarufu na sikuwahi kumwambia chochote juu ya kumpenda kwangu kwa kuwa tayari ana ‘boy friend’ wake.

“Jokate naye anamjua mchumba wangu ingawa hajawahi kumuona. Kwa sasa namchukulia kama dada yangu tu kwa kuwa hakuna popote ambapo nimewahi kutoka naye kimapenzi hata kwa dakika moja zaidi ya kuwasiliana naye kikazi. Mara kadhaa nimekuwa nikimtafuta hata kama ni usiku wa manane nikiwa na jambo na huwa sisiti kumshirikisha,” alisema Millard.

Kwa upande wa Jokate baada ya kufikishiwa taarifa ya maneno ya Millard alishangaa, akasema yeye hajui chochote. Kwanza aliwekewa mtego kama angeuingia kwa kuambiwa Millard amemtaja yeye kuwa ni mchumba wake, akashtuka na kusema:

“Huh! Kasema hivyo lini? Maana mimi sijasikia lolote na siyo kweli kama ni mpenzi wangu na sijui kwa nini kaongea hivyo. Kwa kweli sijasikia wala kuongea naye.”

Wolper yeye alipoulizwa juu ya maneno ya Millard kwamba hawajahi kuwa karibu kwa jambo lolote zaidi ya kuonana barabarani alishtuka:

“He! Ni kweli lakini. Hata mimi namwonaga tu. Hivi yupo kwani hapa Bongo? Sina koneksheni ya kitu chochote na yeye.”

Lulu alipotafutwa juzi, simu yake iliita kwa muda mrefu lakini hakupokea.

Kuhusu Millard na Jokate, baadhi ya vyombo vya habari vimewahi kuripoti kuwa wako karibu kiasi kwamba, maswali ni mengi kuliko majibu.

Kwenye ‘bethidei’ ya Millard iliyofanyika Januari 26, mwaka huu nyumbani kwake, Ubungo Msewe jijini Dar, Jokate alishiriki kwa kumpelekea keki ya ‘kumuwishi’ ambayo ilizua utata.

Wolper: Mimi ni Freemason Kitambo tu


Mtoto mzuri katika tasnia ya uigizaji Bongo, Jacqueline Wolper Massawe ‘Twiga wa Jangwani’ amesema haoni sababu ya kuukana uanachama wa taasisi ya Wajenzi Huru (Freemason) kwani ni dini kama zilivyo zingine na kama katiba inavyoelekeza, kila mtu anayo haki ya kujiunga na dini au taasisi yoyote ya kuabudu kulingana na matakwa ya imani yake.

Akiongea na mwandishi wetu, Wolper alisema ni kweli yuko katika kundi hilo huku akishangaa watu kustaajabu kuona mtu yuko Freemason wakati walioanzisha dini hiyo ni binadamu kama wengine.
 
“Freemason si ni taasisi au dini kama zingine? Kuna ajabu gani mimi kuwa mwanachama? Tena nataka nikuhahakikishie kuwa, nimekuwa muumini halisi wa Freemason kwa muda mrefu sasa,” alisema Wolper.