Wednesday, June 24, 2015

Kundi la Sauti Sol kutoka Kenya ambalo linaiwakilisha Afrika Mashariki kwenye BET Awards 2015 zinazotarajiwa kutolewa Jumapili hii June 28 nchini Marekani, wameonesha mfano unaopaswa kuigwa na wasanii pamoja na mashabiki wa muziki wa Tanzania kuwaunga mkono wasanii wetu wanaowania tuzo za kimataifa.

Kupitia akaunti yao ya Instagram Sauti Sol wameutambua uwakilishi wa Diamond katika tuzo za BET za mwaka jana, na kumpigia kampeni ya kupigiwa kura kwenye tuzo za MTV MAMA 2015 ambapo anawania tuzo tatu.

“Mwaka jana ni @diamondplatnumz ndiye aliyetuwakilisha nchini Marekani kwenye #BETAwards2014 This year we’re so humbled to be the ones representing African music at @bet_intl @bet_africa #Betawards2015 on 28th June at the Nokia Theatre, LA. Shukran sana kwa sapoti aliyetuonyesha. Je, wamkubali? Haiya basi, check link kwenye bio ya @wcb_wasafi kisha umpigie kura #BestMale As many times as you possibly can, ni wakati wa Afrika mashariki”

Endelea kuwapigia kura Diamond na Vanessa wanaoiwakilisha Tanzania kwenye tuzo za MTV MAMA mwaka huu. Diamond anashindania vipengele vitatu, Best Male, Best Collaboration na Best Live. Vee Money anawania kipengele kimoja cha Best Female.

Ingia hapa uweze kuwapigia kura mara nyingi uwezevyo.

Watanzania tuungane kuwapigia kura wasanii wote wanaotajwa kuwania tuzo za kimataifa ili kusaidia kuukuza muziki wa nyumbani.

Kampuni ya usimamazi wa muziki inayofanya kazi na Alikiba, Rockstar4000 imeomba ipewe muda ili kuzungumzia tuhuma dhidi yake zilizotolewa na uongozi wa Diamond Platnumz kuwa inauza nyimbo zake na za wasanii wengine mtandaoni bila ridhaa yake.

Malalamiko hayo yalitolewa na meneja wa Diamond, Salam kupitia mtandao wa Instagram:

“iTunes the company below as #Rockstar4000 who act as they have license to sell the songs of my artist @diamondplatnumz on @iTunes they are THIEVES. They don’t have any contract or any relationship with us this is Unacceptable to let companies sell contents of the Artists without any agreement both sides,” aliandika.

“Wizi kwa Wasanii wetu HAUKUBALIKI. Naomba hii Kampuni ya Rockstar4000 iachane na Wizi wake wa kuuza kazi za @diamondplatnumz hatuna makubaliano yoyote na kampuni yako kuuza Nyimbo za @diamondplatnumz Tutakutana Mahakamani. Uvumilivu umetushinda.”

Bongo5 ilimtafuta mkurugenzi wa vipaji na muziki wa Rockstar 4000, Seven Mosha ili kujibu malalamiko ambaye hata hivyo alisema hawezi kulizungumzia hilo na kututaka tumtafute afisa uhusiano wa kampuni hiyo, Lucy Ngongoteke.

Muimbaji mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja maarufu kama Banza Stone, ameibuka na kuufuta uzushi unaoenea kuwa amefariki dunia.

BANZA STONE YUKO HOI, HAZUNGUMZI, AMEGOMA KULA CHAKULA NA KUNYWA DAWA, WASANII WENGI WAMEMTENGA – MAMA MZAZI

Banza Stone ameongea na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Jumatano hii.


  • “Ndio naumwa kichwa kina nisumbua sana lakini sasa hivi naendelea vizuri yaani hizo habari za kuzushiwa kifo naona sasa hivi kwangu sijui hata itakuwa mara ya ngapi, maana nimeshazushiwa sana. Mimi mzima na huyo anayeeneza azunguke na mikoa mingine aeneze vizuri,” alisema Banza.



  • “Lakini mimi nipo nyumbani hapa Sinza kwa Mama yangu sasa hivi hapa napata juice yaani marehumu anaongea,” aliongeza Banza kwa kicheko.


“Inshallah nikiwa vizuri mashabiki wangu wataniona tu lakini nipo mzima.”

Msanii maarufu wa nyimbo za injili Rose Mhando ametuhumiwa kutapeli zaidi ya shilingi milioni 3 pesa alizoziomba kwa ajili ya tamasha la burudani ya injili kwa wakazi wa mkoa wa Njombe lilikokuwa lifanyike Jumapili iliyopita na kufunguliwa kesi.

Akizunguimza na waandishi wa habari baada ya msanii huyo kutoonekana katika tamasha la injili alilotakiwa kutumbwiza, Mkurugenzi wa The Comfort Gospel Promotion na mratibu wa tamasha hilo, Gerald Sedekia amesema kuwa Mhando alitakiwa kutumbwiza katika tamasha ambaloliliandaliwa kwa ajili ya kuchangisha pesa kwa ajili ya mfuko wa kuchangia watoto yatima.
Gerald amesema kuwa walipo kutana mjiji Dodoma na kujaza mkataba alihitaji kupewa pesa zote ili wasiwe wanadaiana ana walimlipa pesa zote za tamasha ambazo ni shilingi milioni tatu.
Gerald ameongeza kuwa katika mkataba wao ulikuwa unasema kuwa asipofika katika tamasha atatakiwa kuirudisha pesa za gharama na asilimia 10.
Jitihada za kumsaka Rose Mhando ili kusikia naye kwa upande wake anazungumza nini juu ya tukio hili bado zinaendelea.

Ilianza kama ishu ya kawaida hivi lakini muda ulivyozidi kwenda ikazidi kuchukua headlines kwenye mitandao ya kijamii kwamba eti kuna watu wananunua sarafu za shilingi mia tano za Tanzania alafu wanatumia madini ya sarafu hiyo kutengeneza vito kama mikufu hivi !

Nimepitia kwenye channel ya Youtube ya blogger mkubwa Tanzania, Issa Michuzi >>>Michuzi TV na nimekutana na hii stori nikaona niisogeze hapa kushare na wewe pia.

Anayehojiwa ni Abdul M. Dollah ambaye ni Meneja Msaidizi wa Huduma za Kibenki Benki Kuu TZ… Majibu yake ni haya kuhusu hiyo ishu; “Huu uvumi tumeusikia wananchi wengi wanakuja na kuulizia habari hiyo, huo ni uvumi tu na sio kweli kwamba kuna madini yoyote katika hii sarafu ya mia tano ambayo yanaweza kutengeneza vito vya thamani” >>> Abdul M. Dollah

“Wakati tunaizindua hii sarafu mwaka jana tuliwaambia kwamba humu ndani kuna madini ya chuma kwa asilimia 94 na madini ya Nikel asilimia sita tu… Benki Kuu inaamini kwamba Wananchi wanadanganywa” >>> Abdul M. Dollah

WemasMiss Tanzania 2006 na Staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu akipokea maelekezo kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Ikungi, Bw. Alluu Ismaili Segamba kwenye Mkutano uliofanyika Mkoani Singida wiki iliyopita.
Gladness Mallya
BARAKA! Siku chache baada ya mwanadada anayefanya vizuri kwenye filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kutangaza nia ya kugombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), chama hicho kimempa baraka mrembo huyo kwa uamuzi wake huo.
wemass…Wema akipokelewa na Makada wa Chama cha Mapinduzi, CCM mkoani  Singida.
Akistorisha na gazeti hili, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi wowote ule ilimradi awe mwanachama hai, hivyo kwa Wema kugombea ubunge wa viti maalum ni haki yake na amefanya uamuzi sahihi.
“Kugombea uongozi ni haki ya kila mwanachama, Wema ana haki, kwanza ni mwanachama hai na baba yake alikuwa mwanachama mzuri sana wa CCM mpaka anafariki dunia, hivyo chama chetu huwa hakikutani na watu barabarani tu, bali wanakuwa ni halali kabisa mpaka wanatangaza kugombea,” alisema Nape.
Hata hivyo, alisema wasanii wote waliotangaza kugombea kupitia chama hicho hawajakurupuka bali ni wanachama hai na wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali za kichama, tangu kwenye kampeni za mwaka 2010.
Wasanii wengine waliotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM licha ya Wema ni Ndumbagwe Misayo ëTheaí (Viti Maalum, Kinondoni) na Wastara Juma (Viti Maalum Morogoro Vijijini).

Dkt. Nchimbi Atangaza Rasmi Kutogombea Ubunge Songea


Katika hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya wananchi wakiwemo wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma, wamejikuta katika hali ya sintofahamu huku wengine wakimwaga machozi baada ya mbunge wa jimbo hilo, mh. Dkt. Emmanuel Nchimbi kutangaza rasmi kutogombea tena ubunge katika jimbo hilo.

Nchimbi aliyelitumikia jimbo hilo kwa miaka 10 alikutana na wanachama wa chama cha mapinduzi Katika uwanja  wa majimaji mjini Songea pamoja na kuelezea mafanikio mbalimbali ya maendeleo aliyoyafanya katika jimbo hilo ikiwemo ujenzi wa barabara, zahanati na shule za sekondari lakini pia akatumia nafasi hiyo kutangaza rasmi kutogombea tena ubunge katika jimbo la songea mjini.

Tamko hilo la dkt. Nchimbi lilizua simanzi kwa baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM  Songea huku wengine wakishindwa kujizuia na kujikuta wakimwaga machozi.

Katika maelezo yao wanachama hawa walisema kuachia ngazi kwa Dkt, Nchimbi kutogombea katika jimbo hilo kunatoa fursa kubwa kwa vyama vya upinzani kuchukua jimbo hilo hali ambayo hawakubaliani nayo.

Hata hivyo wanachama hao walimuomba mbunge huyo kutengua msimamo wake na kumtaka arejee tena kugombea jimbo la Songea mjini, jibu la dkt. Nchimbi likawa anaenda kufikiria.

MTOTO WA KIGOMA MH; RAIS MTARAJIWA ATUWA MIKOAI

Mkulima Msaka urais Atua Morogoro Kusaka Wadhamin


MKULIMA wa Kigoma anayewania kupitishwa na CCM agombee urais kwa chama hicho, Idelphonce Bilole, ametua mkoani Morogoro akiendelea kutafuta wadhamini katika mikoa 15 nchini, huku akisisitiza elimu si kigezo cha yeye kushindwa kuwania nafasi hiyo ya juu.
 
Bilole aliyasema hayo jana katika ofisi ya CCM Wilaya ya Morogoro ambapo alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kiongozi ni lazima ajue kusoma na kuandika na kwamba CCM ni chama pekee ambacho hakina ubaguzi.
 
Aidha, alisema mwaka 2003 alifuatwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho wakimtaka ajiandae ili aweze kuwania nafasi hiyo kwa mwaka 2005 ambapo alisema alikubali na aliandika barua ya kuomba kuteuliwa, lakini kutokana na sababu ambazo yeye hakuzifahamu barua ile ilichelewa na hivyo kuamua kuvuta subira.
 
Hata hivyo alisema kuwa mwaka huu ameona ni muda muafaka wa yeye kuwania nafasi hiyo ambayo wanachama wenzake wamekuwa wakimuomba kugombea ambapo alisema kuwa ameshafika katika mikoa kadhaa ikiwemo Dodoma, Kigoma, Mwanza, Simiyu, Singida, Shinyanga, Geita na sasa Morogoro kwa ajili ya kutafuta wadhamini.

TANZIA: Mbunge wa Geita, Donald Max afariki Dunia.


Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Geita (CCM) Mheshimiwa Donald Kevin Max (58)(picha) amefariki dunia.

Kufuatia taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda (Mb) kwa Waheshimiwa Wabunge wote pamoja na umma kwa ujumla, Mhe. Max amefariki dunia tarehe 23 Juni, 2015 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa hii, taarifa zaidi juu ya msiba huu zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia kadri zitakavyopatikana ikiwa ni pamoja na ratiba ya Mazishi.

“BWANA ametoa, BWANA ametwaa,
Jina la BWANA lihimidiwe.” Amina.

Imetolewa na:
Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,

DODOMA

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Tarehe 24 Juni 2015