Thursday, May 7, 2015

Latest News
Loading...

Info Post
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa ratiba kwa wanachama wake wanaotaka kugombea udiwani, ubunge na urais kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2015 kujitokeza kuchukua fomu.

Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alitangaza ratiba hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam kuhusiana na maazimio yaliyofikiwa na Kamati Kuu ya chama hicho katika mkutano wake wa siku mbili.

Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Jumapili hadi juzi.

UDIWANI
Alisema uchukuaji na urejeshaji wa fomu za udiwani katika kata ambazo CHADEMA hakina madiwani utaanza Mei 18 hadi Juni 25, mwaka huu wakati kwa kata ambazo chama hicho kina madiwani utaanza Julai Mosi hadi Julai 20 mwaka huu.

Mbowe alisema uteuzi wa mwisho wa wagombea udiwani wa kata pamoja na viti maalum ambao utafanywa na Kamati Tendaji za Majimbo, utafanyika Julai 15 hadi 20 mwaka huu.

UBUNGE

Mbowe alisema kuchukua na kurejesha fomu za ubunge wa majimbo na ubunge wa viti maalum katika majimbo ambayo CHADEMA hawana wabunge uchukuaji fomu na urejeshaji fomu utaanza Mei 18, hadi Juni 25, mwaka huu.

Kwa upande wa majimbo ambayo CHADEMA ina wabunge kwa sasa utafanyika Julai 6 hadi 10, mwaka huu na uteuzi wa awali wa wagombea ubunge utafanyika kati ya Julai 20 na 25, mwaka huu.

Mwenyekiti huyo alisema uteuzi wa mwisho utakuwa kati ya Agosti 1 na 2, mwaka huu.

URAIS

Kuhusu urais, Mbowe alisema kuchukua na kurejesha fomu kutafanyika kati ya Julai 20 na 25, mwaka huu na Agosti 3 na 4, mwaka huu vikao vya Baraza Kuu la Taifa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CHADEMA vitakutana.

Alisema wanachama watakaochukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania urais mwaka huu, watapelekwa kwenye mchujo wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kupatikana mgombea mmoja atakayesimama kwa niaba ya vyama vinavyounda Ukawa.

Vyama vinavyounda UKAWA ni CHADEMA, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na National League for Democracy (NLD).

Yanga VS Azam.. Matokeo haya yameisogeza Azam hatua moja mbele michuano ya Kimataifa !!

AzamFC3-660x280
Kwa mara nyingine Kikosi cha timu ya Simba wanakosa kushiriki wa michuano ya kimataifa kwa msimu wa pili mfululizo baada ya Azam kufanikiwa kushinda dhidi ya mabingwa wa ligi kuu Yanga kwenye uwanja wa Taifa.
Azam wamejihakikishia nafasi hiyo ya kimataifa baada ya ushindi wa mabao 2-1 walioupata Azam dhidi ya mabingwa wapya wa ligi kuu msimu huu Yanga.
Kwa ushindi wa Azam ambao walikuwa wakichuana na Simba kusaka nafasi ya pili, sasa imefikisha pointi 48 ambazo haziwezi kufikiwa na Simba wenye pointi 44 ambao wamebakiza mchezo mmoja na hata wakishinda watakuwa wamefikisha pointi 47.
DSC_1346
Kingine kilichoweka headlines ni hii ya wachezaji wa Azam kujipanga na kuwapigia makofi Yanga wakati wanaingia Uwanjani.
Chanzo cha habari: salehjembe.blogspot.com
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye TwitterFacebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Makonda Atangaza Kamati Kusaidia Madereva.


Serikali imetimiza masharti ya madereva kwa kuunda kamati ya kushughulikia kero na matatizo ya madereva ambayo inatarajia kuanza kazi yake Ijumaa.

Akizungumza Dar es Salaam jana,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisema kamati hiyo itakuwa ya kudumu ambayo itakuwa ikishughulikia kero na matatizo ya barabarani nchini.

Kamati hiyo itaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Uchukuzi, Shabaan Mwinjaka na wajumbe wake ni Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wawakilishi watatu kutoka Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) na Kakoa.

Wengine ni  Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na washiriki watano kutoka kwa chama cha madereva nchini.

Wema Sepetu, Aunt Ezekiel Watibuana Kisa Zari wa Diamond


Gazeti la Risasi la leo limeripoti kuwa Mataa wa bongo movies ambao ni  mashosti wa kufa na kuzikana, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson wanadaiwa kugombana baada ya Aunt ‘kuposti’ kwenye ukurasa wake wa Instagram tangazo lililohusiana na pati ya mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ iliyofanyika Mlimani City jijini Dar wikiendi iliyopita.
 
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao wa sinema za Kibongo, baada ya Aunt kuposti tangazo hilo akiwalaumu watu wa mtandao wa huduma za simu waliomtumia ndipo Wema akaona na kuja juu.
 
Ilielezwa kwamba baada ya Aunt kutupia picha ya tangazo hilo, Wema alichukizwa na kitendo hicho huku akimuona Aunt kuwa amemsaliti.
 
Ilisemekana kwamba katika utetezi wake, Aunt hakupendezwa na tangazo hilo alilotumiwa na mtandao huo wa simu.
 
“Wema alivyoona alichukia na kusema Aunt alikuwa akimsaliti na alitumia tangazo lile kijanja kwa ajili ya kuwatangazia watu kuhusu pati ya Zari wakati anajua kabisa kuwa Wema hazipandi na Zari kwa sababu anatoka na aliyekuwa mchumba’ke (Diamond),” kilisema chanzo hicho.
 
Katika sakata hilo, kuna watu ambao waliona Aunt hakuwa na kosa lakini wapo walioona hakuwa sahihi, jambo ambalo lilichochea ugomvi wao huku wakidaiwa kukesha wakitukanana.
 
Gazeti hilo lilipozungumza na Aunt kuhusiana na sakata hilo, alikiri kutokea akisema kuwa hakuwa na maana mbaya kuposti tangazo hilo lakini kila mtu ana mtazamo wake.
 
“Mimi sikumaanisha chochote kibaya kuhusu hilo tangazo na wala sikujua kama kuna mtu anaweza akalichukulia tofauti kabisa na hapo na mimi ndiyo nashindwa cha kuzungumza,” alisema Aunt.
 
Alipopigiwa Wema simu yake iliita bila kupokelewa.

Ray na Davina Nusura Wazichape Ukumbuni......Chanzo cha Varangati Hilo ni Ray Kushika Makalio ya Davina


Mastaa wa Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Halima Yahaya ‘Davina’ nusura wazichape kavukavu katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar baada ya Ray kudaiwa kumshika mwenzake huyo sehemu nyeti.
 
Kwa mujibu wa chanzo ambacho kilikuwa shuhuda wa tukio hilo, Davina alikuwa amekaa na wasanii wengine pamoja na Mlezi wa Bongo Movies, mama Loraa wakipata vinywaji ndipo Ray alipofika na kuharibu shughuli.

“Wakati Davina anaendelea kupata kinywaji na mama Loraa, alitokea Ray akiwa tayari ‘ameshakula vyombo’ na kumshika Davina kalio kitendo kilishomkasirisha sana msanii huyo na kuanza kumcharukia Ray,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
 
“Davina alinyanyua glasi ya kinywaji chake, akammwagia Ray huku akimuuliza kwa nini alimshika makalio ndipo Ray naye alipopandisha hadi wakataka kukunjana.”
 
Baada ya vurugu hizo kuanza kushika kasi, alitokea mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na wenzake ambao waliwasihi wawili hao waachane na mambo hayo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Nchini, Johnson Minja Kufikishwa Mahakamani LEO

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja mwenye shati la Drafti akiongoza na baadhi ya wanachama wa jumuia hiyo.

Mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya ya Dodoma leo inatarajia kuanza kusikilizwa kwa maelezo ya awali ya kesi ya uchochezi inayomkabili mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara nchini, Johnson Minja.

Mahakama ilishindwa kusikiliza maelezo hayo ambayo yalikuwa yatolewe April 9 mwaka huu baada ya upande wa mashtaka kuiambia mahakama kuwa ilikuwa bado haijakamilisha kuandika wa maelezo hayo.
 
Akitoa maelezo yake mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Dodoma, Rhoda Ngimilanga, wakili mwandamizi wa serikali, Rose Shio aliiomba mahakama kuiahirisha kesi hiyo kwani upande wa mashtaka ulikuwa bado haujaandika maelezo ya awali kwa ajili ya kesi hiyo.
 
Kauli hiyo iliungwa mkono na wakili wa Mshtakiwa, Godfrey Wasonga ambaye alimwomba hakimu kutoa muda wa mwezi mmoja ili upande wa mashtaka uweze kukamilisha kazi ya uandikaji wa maelezo hayo ya awali ya kesi hiyo.
 
Mwenyekiti huyo alifikishwa mahakamni hapo kwa mara ya kwanza Januari 28 mwaka huu akikabiliwa na mashtaka mawili ya uchochezi wa kuwashawishi wafanyabiashara kugomea kutumia mashine za kukusanya kodi za EFDs pamoja na kuwachochea wafanyabiashara mjini Dodoma kufanya kosa.
 
Minja yupo nje kwa dhamana.

Godbless Lema Atamba Kushinda tena Ubunge bila Kampeni.


Mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema amesema kuwa atashinda tena ubunge kwa tiketi ya chama hicho, hata asipopiga kampeni.
 
Aidha amesema ni vyema wananchi wa Jiji la Arusha na maeneo mbalimbali nchini wakajitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura, ili waweze kupiga kura na kuchagua wagombea wanaotaka kuongoza.
 
Lema amesema hata asipopiga kampeni za kutetea kiti hicho yeye bado ni mbunge na uchaguzi huu ataendelea kushinda kwani wagombea wanaopitapita kutangaza nia na baadhi yao kugawa unga, bila mboga anawafananisha na bendera zinazoendelea kupepea bila kuwa na mafanikio yoyote.
 
Amesema ni vyema wananchi wanajitokeza kwa wingi kujiadikisha ili waweze kutumia haki yao siku ya uchaguzi na kuongeza idadi ya wabunge na madiwani wengi kupitia Chadema.
 
Lema amesema kwa jinsi anavyoona hadi sasa maandalizi ya uchaguzi mkuu yanasuasua, hivyo yawezekana daftari hilo likitangazwa kuhamia mkoani Arusha siku zinaweza kuwa chache hivyo ni vyema wananchi wakawa makini, wakisikia daftari linapita mkoa fulani wajitokeze kwa wingi kujiandikisha, ili waweze kuchagua wabunge wengi kutoka Ukawa.
 
Amesema anatarajia kufanya mkutano Ijumaa ya wiki hii, ataongelea mambo mbalimbali ikiwemo suala la uandikishwaji wa daftari la kupiga kura, sambamba na kujadili jinsi fedha ya Tanzania thamani yake inavyozidi kushuka.

Profesa Lipumba Aieleza Mahakama ya Kisutu kuwa Polisi WALIMPIGA, Akana Kufanya Maandamano


MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa, hawakufanya maandamano wala kupata barua ya zuio badala yake alipigwa na polisi.

Prof. Lipumba aliyasema hayo mahakamani hapo jana wakati yeye na washtakiwa wengine waliposomewa maelezo ya awali, mbele ya Hakimu Mkazi, Cyprian Mkeha.

Mawakili wa Serikali, Tumaini Kweka, Joseph Maugo na Mohamed Salum, walidai kesi hiyo imekuja mahakamani hapo kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Akisoma maelezo hayo, Salum alidai CUF waliandika barua Januari 22, mwaka huu, kwenda kwa Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kutoa taarifa ya kufanya maandamano kuanzia Ofisi za CUF Wilaya ya Temeke kwenda Mbagala Zakhiem.

Alidai mshtakiwa wa kwanza, Prof. Lipumba ndiye aliyepanga kuongoza maandamano na baadaye kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa ufanyike Viwanja vya Zakhiem.

Aliongeza kuwa, Januari 26, mwaka huu, Jeshi la Polisi lilijibu barua hiyo na kuwataka wasitishe maandamano kutokana na sababu mbalimbali zilizoelezwa ndani ya barua hiyo.

Baada ya maelezo hayo, Prof. Lipumba alisema barua hiyo ilifika saa 12:30 jioni hivyo hakupata ujumbe wowote kama wamezuiwa kufanya maandamano hayo.

Alisema Januari 27, alifika katika Ofisi ndogo za CUF zilizopo Temeke kuzungumza na maofisa wa chama hicho na baadaye walianza maandamano kuelekea Zakhiem.

Hata hivyo, upande wa Jamhuri ulidai kabla ya maandamano hayo hayajaanza, polisi walitoa onyo la kuwataka wasitishe maandamano na kutawanyika kwani wanachokifanya ni kinyume cha sheria.

Licha ya kutolewa kwa onyo hilo, washtakiwa walikaidi amri hiyo,kuendelea na maandamano na walipofika eneo la Mtoni Mtongani, walikutana na polisi ambao walitoa ilani ya  kusitishwa kwa maandamano hayo lakini waliendelea kukaidi.

Baada ya washtakiwa kukaidi amri ya polisi, waliwakamata, kuwapandisha kwenye gari na kupelekwa Kituo cha Polisi Kati ili kutoa maelezo.

Hata hivyo, baada ya kusomewa maelezo na upande wa Jamhuri, mshtakiwa wa kwanza hadi 29, walikana na kudai hawakukaidi amri hiyo wala kufanya maandamano.

"Hatukufanya maandamano, huo ni uongo mtupu kwanza sikupata hiyo barua, isipokuwa polisi waliamua kutukamata na kutupiga tu," alidai Prof. Lipumba.

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa, mshtakiwa wa 30 na 31 walikamatwa katika Viwanja vya Zakhiem wakiwa wamekusanya watu kwa ajili ya kufanya mkutano shtaka ambalo walilikana.

Kweka aliieleza mahakama kuwa, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, hivyo aliomba ipangwe tarehe ya kusikilizwa.

Baada ya kueleza hayo, upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Twaha Taslima aliomba apatiwe maelezo ya mlalamikaji.

Hakimu Mkeha aliahirisha shauri hilo hadi Juni 4, mwaka huu kwa ajili ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa na kuutaka upande wa Jamhuri kuja na mashahidi wawili.

Hivi karibuni, viongozi wa CUF na wafuasi wao walifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashtaka matatu ikidaiwa kosa la kwanza walilitenda Januari 27, mwaka huu, eneo la Temeke ambapo wote kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha taratibu.

Katika shtaka la pili, inadaiwa siku hiyo ya tukio, washtakiwa, wakiwa katika Ofisi ya CUF karibu na Hospitali ya Wilaya ya Temeke bila ya kuwa na uhalali, walifanya mkusanyiko kwa nia ya kufanya maandamano kwenda Mbagala Zakhiem.

Shtaka la tatu, ilidaiwa siku hiyo ya tukio katika eneo la Mtoni Mtongani, waligoma na kutojali tangazo halali lililotolewa na polisi likiwataka wasiandamane na kutofanya mkusanyiko usio halali.

Washtakiwa hao ni Shabani Tano (29), Shabani  Abdallah (40), Juma (54), Athuman Ngumwai (40), Shaweji Mohamed, Hassan Said (37), Mohamed Ibrahim (31), Allan Ally (53) na Abdina Abdina (47).

Wengine ni Allawi Msenga (47), Abdi Hatibu (34), Abdallah Ally (32), Said Mohamed (40), Salim Mwafisi, Salehe Rashid (25), Rehema Kawambwa (47), Salma  Ndewa (42), Athuman Said (39), Dickson Leasson (37) na Nurdin Msati (37).

Zitto Kabwe Afunguka Kuwa Alipofukuzwa CHADEMA Alitamani Kujiunga NCCR-Mageuzi......Kazungumzia Pia Anakotoa Pesa za Kufanya Mikutano


Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa alipofukuzwa Uanachama katika chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alitamani kujiunga na Chama Cha NCCR-Mageuzi kwani ndicho chama ambacho kilikuwa  kinaendana na itikadi yake anayoifuata na kuiamini ambayo ni itikadi ya Ujamaa.
 
Zitto Kabwe alifunguka haya jana alipokuwa akichat Live kupitia ukurasa wa facebook wa EATV katika kipengele cha KIKAANGONI .

Zitto Kabwe alisema kuwa alishindwa kujiunga na Chama hicho cha NCCR-Mageuzi kutokana na kuwepo kwa matatizo hivyo aliona siyo vyema kujiunga nacho, ndiyo maana alifikiri kuwa na chama cha siasa ambacho kitakuwa na misingi na itikadi ambayo yeye anaiamini na kuisimamia. 
 
Katika hili moja ya shabiki alitaka kujua kwanini aliamua kujiunga na ACT Wazalendo na kuacha kujiunga na chama kilichokomaa kisiasa kama TLP,NCCR-Mageuzi,CUF, au CCM na majibu ya Zitto yalikuwa kama hivi.
 
"Nilifikiria hivyo pia lakini nikaona kuwa ni vema sasa kuwa na chama cha siasa ambacho kina itikadi ninayoifuata na kuiamini nayo ni itikadi ya Ujamaa.
 
"Chama cha NCCR-M mageuzi pekee ndio kinakaribia kuwa na itikadi hiyo lakini napo kulikuwa na matatizo ambayo kujiunga kwangu nao ingekuwa sio vema. Pili mimi ni mpiganaji. 
 
Wengine wananiita jeshi la mtu mmoja! Sio kweli lakini. Hivyo kwenda chama kichanga ni ujasiri wa hali ya juu. Mungu atasaidia hakitakuwa chama kichanga baada ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2015".
 
"Mimi sio mwanzilishi wa ACT Wazalendo isipokuwa waanzilishi walikuwa watu ninaoshabihiana nao kwenye itikadi kama Prof. Kitila Mkumbo na Ndugu Mwigamba" Aliongeza Zitto Kabwe.
 
Kiongozi huyo wa ACT Wazalendo ambaye kwa sasa amekuwa akiitwa majina mengi ya ajabu ajabu kama msaliti,Yuda, kibaraka wa CCM na mengine mengi alisema kuwa hilo ni suala la kawaida katika siasa maaana hayo ni maneno tu ambayo hata baadhi ya viongozi wakubwa katika vyama vya siasa walishaitwa majina hayo ila anasisitiza jambo kubwa na la muhimu ni kumpima kwa kazi zake ambazo amezifanya bungeni katika kipindi chote alipokuwa mbunge na jinsi alivyoweza kujenga uwajibikaji kwa baadhi ya viongozi.
 
"Hayo ni maneno ya kisiasa tu. Hata Marando aliwahi kuitwa Msaliti. CUF waliwahi kuitwa mashoga. NCCR na Mbatia waliwahi kuitwa pandikizi. 
 
"Ni maneno ya kisiasa tu ambayo hayaongezi ugali kwenye sinia. Muhimu ni kuni judge kwa kazi ambazo nimefanya Bungeni katika kipindi changu. Kazi ya kujenga uwajibikaji." 
 
Lakini mbali na kuonyesha kuwa kumekuwa na changamoto katika siasa za Tanzania hususani ndani ya vyama vya siasa Zitto Kabwe alizidi kusisitiza kuwa chama cha siasa ni itikadi hata hivyo umoja wa vyama vya siasa ni muhimu sana katika kujenga Demokrasia imara.
 
"Chama cha siasa ni itikadi. Hata hivyo umoja wa vyama ni muhimu sana katika kujenga demokrasia imara"
 
Uchaguzi Mkuu 2015
Kiongozi huyo wa ACT Wazalendo ameonyesha kuwa huenda kwa mwaka huu katika uchaguzi mkuu Tanzania ikaandika historia nyingine kwa Rais wa chama kimoja kukabidhi nchi kwa Rais wa chama kingine, hii inamaana kuwa huenda Rais Jakaya Kikwete akakabidhi nchi kwa Rais kutoka chama cha upinzani.
 
"Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu Rais wa chama kimoja anaweza kukabidhi nchi kwa Rais kutoka chama kingine." 
 
Lakini hapo hapo kiongozi huyo ndipo alipoonyesha wazi kuwa kwa upande wake yeye atagombea nafasi ya ubunge kupitia chama chake cha ACT Wazalendo na kusema kuwa mpaka sasa hajajua ni jimbo gani anakwenda kugombea nafasi hiyo ya ubunge. 
 
"Nitagombea Ubunge mungu akipenda. Jimbo gani bado sijaamua" 
 
Kutokana na hili mashabiki walihitaji kujua siku akiweza kufanikiwa kushika nafasi ya Rais wa nchi hii ni jambo gani la kwanza kuanza kufanya .
 
"Ikitokea nimekuwa Rais wa Tanzania Kila Waziri ataandika kabisa barua ya kujiuzulu na inabakia kuweka tarehe tu ili akiboronga anawajibika bila hiyana. Uwajibikaji ni nguzo muhimu sana katika kuleta maendeleo nchini."
 
Lakini Zitto Kabwe aliweka sawa kuwa katika kipindi cha sasa ikitokea uchaguzi wa Oktoba hautofanyika au mwaka huu usipofanyika uchaguzi anaamini nchini itaingia katika machafuko. 
 
ACT Inatoa  Wapi Pesa za Ziara
Moja wa shabiki wa ukura wa facebook alihoji kuwa pesa zinazosaidia cha cha ACT Wazalendo kuweza kufanya ziara zake mikoani tena kwa speed kubwa na ni chama kichanga hizo pesa wanatoa wapi ukizingatia kuna vyama vya siasa vipo miaka mingi sana lakini havijaweza kufanya hata ziara ndani ya mji wa Dar es Salaam sababu vinakosa pesa za kufanya hivyo, kiongozi huyo wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe alisema kuwa ni dhamira tu na yeye pesa za kufanya hivyo anachangiwa na wananchi wanaopenda harakati zake.
 
"Ni dhamira tu. Wapo watanziania wengi sana wanaoamini katika kazi za Zitto Kabwe hawawezi kukubali nishindwe kufanya siasa sababu ya fedha. Ninachangiwa hata na mama lishe."
 

Natamani  Kujiunga UKAWA
Katika hatua nyingine Zitto Kabwe ameweka wazi kuwa katika moja ya mipango yao ilikuwa ni kuunganisha nguvu kama ambavyo awali ametuleza kuwa ili kujenga demokrasia imara ni lazima vyama vya siasa viweze kuunganisha nguvu zao hivyo anadai alitamani waweze kuungana na UKAWA katika kuona ni jinsi gani wanaweza kufumua mfumo wa uongozi ulipo sasa wa chama tawala ila akadai kuwa UKAWA walikataa.
 
Kiongozi huyo wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe alimaliza kwa kuwaambia mashabiki kuwa kuna matapeli wanatumia jina lake na kujifanya wanatoa mikopo hivyo yeye hausiki nao na wananchi wanapaswa kutambua hao watu ni matapeli na amesema mara nyingi huwa anatoa taarifa sehemu husika juu ya watu wao.
 
"Hao ni matapeli. Akaunti yangu ni hii na Zitto Z Kabwe pekee. Nyingine ni watu tu wanatengeneza na huwa tunazitolea taarifa."-Zitto  Kabwe