Sunday, June 28, 2015

Mafuriko Ya Lowassa Yatua Jijini Dar......Kingunge Amwaga Wino Hadharani Kumdhamini, WanaCCM 212,150 Wajitokeza Kumdhamini


WAZIRI  Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa amepata udhamini wa kishindo katika mkutano uliofanyika jana  katika ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni.
 
Lowassa alipata udhamini huo baada ya wanachama kujitokeza katika ofisi za Makao Makuu ya CCM ya Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni, Dar, ambapo alipata zaidi ya wadhamini  212,150 huku akisema Dar  imevunja  rekodi  ya mikoa yote ya Tanzania.
 
Akizungumza na maelfu ya wananchi waliofika katika mkutano huo Lowassa alisema kuwa amefurahishwa na watu waliojitokeza kumdhamini kwa kishindo kikubwa na hivyo hatavunjwa moyo  na maneno ya watu yanayovumishwa  kuwa anawapatia fedha ili wafike kwenye mkutano wake .
 
Lowassa aliongeza kuwa anawaomba Watanzania wampe ridhaa ya kuwa rais wao kwani atahakikisha mianya yote ya rushwa na utendaji mbovu  wa kusuasua anausimamia kwa haki na weredi na ndani ya miezi sita tayari matokeo yatakuwa yameonekana.
 
“Nawaombeni wananchi mnipeni ridhaa ya kuingia ikulu yaani nitahakikisha mianya yote ya rushwa na ufisadi nautokomeza, muyapuuze maneno na minong’ono ya watu kutaka kunichafua,” alisema.
Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akisani fomu ya udhamini mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono mgombea huyo. 

Zoezi hili lilifanyika jana jioni ya Juni 27, 2015 kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni Jijini Dar ambapo Lowassa  alipata  jumla  ya  Wadhamni 212, 150 na kuifanya Dar es salaam kuwa Mkoa wa kwanza kuwa na idadi kubwa ya WanaCCM waliomdhamini .

Wema Sepetu Amtaja Mtu Anayemzuia Kupata Mimba


Ishu ya  Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutopata ujauzito imeshazungumzwa mara kadhaa na hata yeye mwenyewe alishawahi kujitokeza na kuizungumzia lakini safari hii amelizungumzia kwa njia tofauti. 
 
Wema ambaye pia ni muigizaji wa filamu, awali alisema sababu kubwa ya kutopata ujauzito ni masuala ya kiafya lakini safari hii ametoa kauli tata ambayo inahusiana na imani za nguvu za giza.
 
Wema ambaye alifunguka hayo hivi karibuni, anadai kuwa yawezekana marehemu Steven Kanumba anahusika kwenye suala hilo.
 
Mizimu ya Kanumba
“Unajua hili suala la mtoto linanisumbua sana yaani na linaniuma kwa sababu napenda watoto sana na pia napenda kuitwa mama, nimehangaika sana katika kuhakikisha nafanikiwa katika hili lakini ndiyo hivyo imeshindikana.
 
“Serious! Ilifika kipindi yaani nilikuwa nachukia nilipokuwa nikiziona siku zangu, nilikuwa sipendi kukutana na hiyo hali kwa sababu naumia sana lakini ndiyo hivyo baada ya kuhangaika sana inabidi nimwachie Mungu tu. Nahisi kukata tamaa lakini bado sijakata tamaa.
 
“Watu wananiambia mimi bado mdogo kwa hiyo sitakiwi kuwa na wasiwasi sana ila muda unakwenda, sasa nina miaka 27. Niliwahi kupata mimba mwaka 2008, aliyenipa alikuwa marehemu Kanumba, lakini baadaye ilitoka na aliposikia hivyo (Kanumba) alikasirika kwa kweli.
 
“Lakini baadaye ikawa kawaida, hata nilipokuja kuachana naye, bado alikuwa rafiki yangu na tulikuwa tunaongea vizuri na kupigiana simu kama kawaida ila alikuwa ananiambia ‘unajua una deni, nakudai watoto wangu na nitafanya juu chini ili unilipe’.
 
“Basi ikawa kawaida yake kuniambia hivyo, wiki chache kabla ya kufariki aliniomba tuonane lakini haikuwezekana kutokana na ratiba zetu kutofautiana.
 
“Kuna muda huwa nafikiri au mizimu yake inahusika katika hii ishu! (anacheka sana).
 
“Unajua ile mimba ya Kanumba hata mimi sikuwa tayari kupata mtoto wakati ule, niliona ndiyo kwanza naingia kwenye mapenzi halafu ndiyo nimetoka kuwa miss tu, sasa itakuwaje, lakini huwezi jua labda pengine kwenye ‘abortion’ walivuruga baadhi ya vitu ndiyo maana mpaka leo imekuwa hivi.”
 
Ujauzito wa Zari
Wema ambaye pia aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa ‘on-off’ na msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, anafunguka juu ya ujauzito wa mpenzi wa sasa wa Diamond, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
 
“Unajua hiyo mimi hainisumbui, sababu nilishakubali kwamba sasa nimeachana na Nasibu kwa hiyo ishu nyingine zote ziko poa. Najua jinsi gani alivyokuwa anatafuta mtoto, namtakia kila la kheri.”
 
Gari alilopewa na Diamond
“Ile Murano niliiuza kwa kuwa ilikuwa mbovu na sikuwa naipenda kwa sababu ilikuwa inanisumbua, niliamua hivyo kwa kuwa lilikuwa langu