Imelda Mtema
Baada ya kula viapo vya kutozikana, wasanii wawili wa filamu Bongo, Wema
Isaac Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel Grayson wamejikuta wakiangua vilio
wakati wakipatanishwa na rafiki yao mkubwa ambaye ni pedeshee
anayejulikana kwa jina la Daudi Mambya.
Habari kutoka kwa shuhuda wetu zilieleza kwamba, tukio hilo lilijiri
wikiendi iliyopita kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar ambapo Daudi
aliwaita kwa mwaliko wa mishikaki bila wenyewe kujua kinachoendelea.
Habari zilieleza kuwa, Daudi ambaye kwake huwa hawafurukuti, amekuwa
akiumizwa mno na tofauti ya wasanii hao kwa sababu ni watu walikuwa
wakipendana hivyo kugombana kwao kulikuwa kunaleta shida kwa marafiki
zao wengine.
Imefahamika kwamba, Daudi alitumia ujanja wa kuzungumza na kila mmoja
kwa wakati wake ambapo alibaini kuwa hakuna aliyekuwa tayari kupatana na
mwenzake.
Ilisemekana kuwa, Daudi alitumia ujanja wa kitaalamu ili kila mmoja kumuweka sawa bila kujijua.
“
Unajua Daudi ni rafiki yao sana, sasa hakuwa anapendezwa na tatizo
ambalo limejitokeza hivyo alitumia njia tofauti ili kuweza kuwakutanisha
pamoja tena waweze kupatana,” alieleza mtoa habari huyo.
Ilielezwa kwamba Daudi alianza kwa kumtafuta Wema na kumpeleka Coco
Beach akimuambia kuwa anataka akamnunulie mishikaki huku wakati huohuo
akimwambia Aunt naye wakutane ufukweni hapo.Shushushu wetu alizidi
kufunguka kuwa Daudi alitangulia Coco na Wema, huku akifanya mawasiliano
na Aunt na baada ya muda, Aunt naye aliwasili huku kila mmoja akibaki
katika mshangao usioelezeka baada ya kukutana uso kwa uso.
Sosi huyo alisema kuwa Wema na Aunt walipoonana kila mmoja alikuwa kimya
lakini Daudi aliamua kuwasomea risala ndefu iliyomwingia kila
mmoja.Mambo yakipokaa vizuri, wawili hao walishuhudiwa wakiwa
wamekumbatiana huku kila mmoja akiangua kilio kilichochukua takribani
nusu saa hivyo kufanya eneo hilo kuwa kama kuna msiba.
“Yaani mpaka Daudi mwenyewe alidondosha machozi baada ya Wema na Aunt kukumbatiana na kuanza kulia.
“
Yaani ilikuwa simanzi kubwa sana,” alimalizia shuhuda
huyo.Akizungumza na gazeti hili, Daudi alisema kuwa aliamua
kuwapatanisha wawili hao kwa kuwa alikuwa hapendezwi na tatizo hilo na
kwamba wote ni rafiki zake.
Kwa upande wake, Aunt alifunguka ya moyoni:
“
Tulipokutana kila mtu alijua tatizo lake na tukaona ni mambo ya kijinga, ikabidi tuweke tofauti pembeni maisha yaendelee.”
Wema alisema: “
Mambo ya kugombanagombana hayana msingi na kwa vile ni
mtu mzima (Daudi) aliwakutanisha, nikaona yaishe.”Wema na Aunt ambao
walikuwa marafiki wakubwa waliingia kwenye mgogoro hivi karibuni baada
ya Wema kumtuhumu Aunt kuunga mkono shoo ya Zari All White Party ya
mwanadada Zari Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mpenzi wa aliyekuwa
mpenzi wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.