Thursday, July 23, 2015


.
.
Good morning mtu wangu..
Kutoka Dar es Salaam Tanzania leo Alhamisi July 24 2015 tayari nimeyakusanya Magazeti yote na stori zake kubwakubwa kukusogezea hapa, headlines baada ya headlines kwenye Magazeti ya Udaku, Michezo na Hardnews, zote ziko hapa.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

BAADA mikasa na vituko kibao vya kidume kuchezea kichapo na kuvumilia kitambo huku thamani ya uume ikidhalilishwa front, kijana Nuhu Mziwanda kabwaga mazima, ni Couple iliyounganishwa na yeye na mwanadada mwenye kesi kwa Pilato Basata kwa kumwaga radhi Ughaibu Shilole.

FC baada ya kupata mtonyo iliwaibukia artist hao wenye uwezo wa kuact kila kunapokucha katika kupata data kama ni sinema na wanaendelea na Movie yao mpya ya maisha kama walivyozoeleka? Lakini hii ni real mtu kambwaga mtu naye kaipokea safi.

“Mwanaume umjali mpenzi wake na kumfanyia kile atakacho, lakini si kwa huyu ni mwanamke asiyejua kupendwa na chochote nilichofanya ilikuwa kwa ajili ya upendo tu, nimemwacha na aje mwanaume mwingine naye ajaribu,”Mziwanda

Pia msanii huyo wa muziki amekanusha kuwa kuwepo kwake na mwenye jina la Zuwena Mohamed jina linalofunikwa na hili la ugali la Shilole kuwa hakuwa anamtegemea sana kama ni kwenda Uropa ilikuwa ni mialiko ya kila mmoja kwa dili lake.

FC ilimtafuta mdada makeke awapo kwa stage hadi kusaula viwalo na kuingia matatizoni na wenye mamlaka ya sanaa simu zake zote zilikuwa hazina majibu once mambo yanaendelea, FC imebaini kuwa hakuna watu kubwagana wala nini bali ni mchongo wa machizi hao kutafuta kiki wamepata.

Ilikuwa ngumu kwa wanaomjua Mziwanda eti akijitoe kirahisi hivyo kwa Shilole? Bali wamejipa majina yao ambayo Shilole anaitwa Asha ngedere na Mziwanda jina la Ganda la Ndizi utelezi mwanzo mwisho afanye nini kijana wa watu, maisha ndio yalivyo.

Kumbe walikuwa wanataka Kiki tu, kama Ulaya au wapi hiyo hizi Kiki bhana kuna siku mtu anamua hata Mshua ili mambo yaende. Danganya toto hiyo imebainika baada ya wimbo wao walioshirikiana wasanii hao kuachiwa katika moja ya Redio hivyo hiyo ni movie tu.

Kambi ya Halima Mdee Yafurugika 


KAMBI ya aliyekuwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), imeanza kusambaratika baada ya wafuasi wake kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo.
 
Wafuasi wake hao wakiongozwa na diwani aliyemaliza muda wake katika Kata ya Kunduchi, Janeth Rithe, wamejiunga jana ACT-Wazalendo na kukabidhiwa kadi na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Msafiri Mtemelwa.
 
Wengine waliopewa kadi za ACT ni Mary Mongi aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Bawacha, Jimbo la Kawe, James Wambura (Katibu wa mbunge Kawe) na Manase Busa aliyefanikisha kwa kiasi kikubwa kuhakikisha Mdee anaingia bungeni katika uchaguzi wa 2010.
 
Wamo pia Katibu Bawacha Tawi la Wazo, Modesta Kalukula na Sizya Issa, Yamoyo Salehe, Sheilah Khamis, Tabia Mohamed, Ashura Salehe, Sophia Makoba na Fatuma Mikidadi.
 
Mbali na hao, chama hicho pia kimepokea wanachama wengine 198 kutoka CCM, Chadema na NCCR-Mageuzi waliojiunga kutoka jimbo hilo.
 
Akizungumza baada ya kuwapokea, Msafiri alisema wanachama hao wameungana ili kuendeleza uzalendo kwa Taifa, hivyo chama hicho kinawakaribisha na wengine.

Jana ilikuwa siku ya kwanza kati ya siku kumi za kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa Biometric Voters Registry (BVR) katika jiji la Dar es Salaam.

Namshukuru Mungu tayari nina kadi yangu kwa ajili ya kuwapata viongozi wangu bora hapo 25 Oktoba mwaka huu.

Sikufaidi tu kupata hiyo hati, la hasha! Katika kubadilishana mawazo na wajiandikishaji wenzangu, nikabahatika kuongea na kiongozi wa chama cha Wananchi CUF ngazi ya kijiji.

Pamoja na mambo mengine nilivuna kutoka kwake msimamo wa CUF kwenye UKAWA,nani mgombea urais kupitia UKAWA na nani hakubaliki na kwanini.

Ambalo lilinivutia sana ni msimamo wa ACT kuhusu mgombea wa UKAWA atakayeteuliwa.

Kimsingi kiongozi huyo alinihakikishia kuwa CUF bado hawajajitoa kwenye UKAWA. Kuhusu mgombea ambaye viongozi wengi kutoka vyama vinavyounda UKAWA wanaona anafaa kupeperusha bendera ya UKAWA ni Prof. IBRAHIM HAROUNA LIPUMBA.

Lipumba anaungwa mkono na FREEMAN MBOWE na HALIMA MDEE kwa vigezo kuwa ana busara, ni mtu mwenye subira na staha na asiyekurupuka kufanya maamuzi.

Slaa anaelezwa kuwa mwenye jazba na visasi jambo ambalo kwenye kuunda serikali linaweza kuwagharimu.

Nilitaka kujua sababu za Mbowe kutomkubali Katibu wake Mkuu, Wilbroad Slaa kupeperusha bendera ya UKAWA.

Inasemekana kuna maandamano waliandaa yeye MBOWE na SLAA lakini mambo yalipoharibika, Slaa akamruka na akashtakiwa yeye jambo ambalo Mbowe aliona ni usaliti na anachokifanya sasa ni kulipiza kisasi. Kitendo cha Lowassa kutakiwa na Mbowe ndani ya CHADEMA huku SLAA hamtaki nayo ni sababu nyingine.

Chama cha Alliance for Change & Transparency ( ACT) kama chama cha Upinzani na ambacho bado ni kichanga kabisa kwa mujibu wa kiongozi huyo wa CUF kinasema endapo UKAWA watamsimamisha LIPUMBA kama mgombea urais wao ACT hawatamsimamisha mgombea na badala yake watamuunga mkono Lipumba vinginevyo watamsimamisha mgombea wao.

kwa mujibu wa kiongozi huyo, kuna uwezekano mkubwa wa CUF kujitoa UKAWA na kutengeneza muungano na ACT na kumuweka mgombea urais atakayepeperusha bendera ya vyana hivyo viwili.

Tusubiri tuone namna itakavyokuwa.

Aliyekuwa Mbunge wa Muleba Kusini, Prof Anna Tibaijuka anayewania jimbo hilo kwa mara ya pili, jana alishushwa jukwaani kwa kuzomewa na wananchi wake katika kata ya Nshamba wilayani Muleba. Prof Tibaijuka alishushwa jana wakati wa kampeni za kura za maoni kupitia CCM. Hali ya kuzomewa ilidumu kwa dakika kadhaa jambo lililofanya Wagombea hao kulazimika kuondoka. Kwa mara ya kwanza alizomewa juni 8, wakati wa ziara ya katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika kata hiyo hiyo. Akiwa na Kinana wananchi walimtuhumu ufisadi wa fedha za Escrow na kushindwa kutekeleza ahadi ya kuwajengea barabara ya lami.
Source: Mwananchi
Nini maoni yako kuhusu hilo?


Mbunge wa Mbeya Mjini na msanii wa muziki Joseph Mbilinyi, maarufu kama Mr. Sugu ameelezea kujivunia kipindi chake cha miaka 5 bungeni.

Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi aka Sugu
Hii imekuja baada ya lawama na fikra za wengine kuwa amekuwa na mchango mdogo tu katika kuipigania sanaa kwa nafasi aliyopata.
Mr. Sugu ameeleza hayo na kusisitiza kuwa, hakuwa mbunge wa wasanii bali mbunge wa Mbeya, akieleza kuwa, kama msanii hakuwa anajituma na kazi yake, ni lazima abakie kuwa mtu wa lawama mara zote.

Afande Sele amchana Sugu, adai hajafanya lolote bungeni kutetea muziki, Sugu ajibu


Rapper Afande Sele amesema wasanii hawajanufaika na ubunge wa Joseph Mbilinyi aka Sugu licha ya kumsaidia kumpigia kampeni katika uchaguzi uliopita.

Akizungumza na Planet Bongo ya East Afrika Radio, Afande alisema Sugu ameshindwa kuwatumikia wasanii na kujinufaisha yeye mwenyewe.
 
“Sisi tuliamini akienda kule ndio mdomo wetu, kasahau kabisa wasanii wenzake,” alisema.
 
“Kipindi ambacho wasanii wa antivirus wanalalamika kwamba kawatosa porini, akasema yeye sio mbunge wa wasanii ni mbunge wa Mbeya. Huyu ni msaliti kwa wenzake, sasa mtu msaliti namna hii jinsi kumuondoa ni sisi kuamua kuingia bungeni wenyewe kupigania maslahi yetu,” aliongeza.
 
Baada ya kauli hiyo, Sugu amemjibu kwa kusema kuwa yeye hakuwa mbunge wa wasanii bali alikuwa mbunge kwaajili ya watu wake wa Mbeya mjini.
 
“Nafikiri hafuatilii bunge, unajua uzuri wa vitu vya bunge vinaenda kwa rekodi, labda atakuwa hafuatili bunge. Lakini kwa wanaofuatilia bunge wanajua. Mimi sio mbunge wa wasanii, mimi ni mbunge wa Mbeya mjini,” alisema Sugu.
 
“Kwahiyo chochote ninachokifanya bungeni ninakifanya kwa mapenzi yangu na pia kama waziri kivuli. Kwa msanii anayefanya kazi sawa ila kwa mtu anayelala lala kama yeye lazima atakufa njaa. Lazima utakufa njaa lakini kwa msanii kama Professor Jay, msanii kama Shetta wana- appreciate kazi ambayo tunaifanya bungeni kwa kauli zao.”
Mpekuzi blog

Wakati Joto la Mbio la Urais Tanzania Linaendelea , Wakuu wa Vyama vya Upinzani Wanao unda kundi la Ukawa Wamemwambia Lowassa Huko alipo sasa inatosha amedhihakiwa vya kutosha na Kwamba wanamkaribisha Ukawa kwa mikono miwili kama walivyofanya wengine wakiwemo Mh Limbeli na Mh Ester Bulaya pamoja na Wale Madiwani wa Monduli....

Tetesi zinasema kuwa Muda wowote Lowassa anaweza Tangaza uamuzi wake wa Kujiunga na Upinzani ili apate nafasi ya kuwania Urais 2015.....

DU! Kazi kwelikweli! Habari ya mjini kwa sasa ni mtoto mzuri Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwania Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini nyuma yake kuna habari zinazodai kuwa mrembo huyo ameingiwa na hofu ya kukatwa jina kama ilivyotokea kwa Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliyekuwa mmoja wa watia nia ya kugombea urais, Amani lina mkanda kamili.


ALIVYOENGULIWA LOWASSA

Lowassa alikuwa miongoni mwa makada 33 kati ya 38 walioenguliwa na Kamati ya Maadili ambayo ilipitisha majina matano pekee katika kikao cha Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na baadaye Mkutano Mkuu kupitisha Mbunge wa Chato, Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kwa Tiketi ya CCM.

TUJIUNGE NA CHANZO

Chanzo kilicho karibu na staa huyo kimepenyeza ‘ubuyu’ kuwa, Wema ambaye anashikilia Taji la Miss Tanzania 2006/07, ameingiwa na hofu hiyo baada ya kuona Lowassa ambaye ana sifa ya kukubalika kama alivyo yeye ameenguliwa na kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM.

“Bibie (Wema) anajiamini, anakubalika kweli lakini kitendo cha Lowassa ambaye alikuwa anaonekana kukubalika kimemtia hofu na kuona kumbe kukubalika pekee si silaha ya ‘kuwini’ kupitishwa na chama,” kilisema chanzo hicho.

CHANZO CHAZIDI KUTIRIRIKA

Chanzo hicho kilizidi kwenda mbali zaidi kwa kudai hofu hiyo iliongezeka kwa Madam hususan baada ya kusambaa kwa kuwepo kwa watu wasiompenda kupandikiza chuki kwamba baadhi ya skendo zilizomgusa zinaweza kumpotezea sifa ya jina lake kupitishwa na Halmashauri Kuu ya chama chake.

“Si unajua tena Madam kwenye maisha yake ya sanaa amepitia skendo za hapa na pale, hiyo inaweza kuchangia kumtia hofu maana wabaya wake wanaweza kuitumia kama silaha hivyo amekuwa akitoa chozi na kumuomba Mungu amfanikishe,” kilisema chanzo hicho.

SKENDO INACHANGIA KUMPOTEZEA SIFA?

Duru mbalimbali za habari zinaonesha kwamba kitu kikubwa kinachoangaliwa kwa kiongozi ni suala la uwajibikiaji na si tabia binafsi au skendo.

Wapo viongozi ambao walikuwa na skendo lakini wameweza kupitishwa na wananchi wao na kuwatumikia vizuri kuliko hata wale walionekana wasafi.

“Si kweli kwamba skendo ndiyo kigezo kikuu cha kumpitisha mgombea, mbona watu kama akina Mike Sonko (alikuwa Mbunge wa Kenya), marehemu Amina Chifupa (alikuwa Mbunge Viti Maalum, Vladimir Vladimirovic Putin (rais wa urusi) na wengine wengi, walikuwa au walipata skendo lakini walifanya vizuri katika uongozi wao,” alisema mwanaharakati mkubwa wa siasa nchini aliyeomba hifadhi ya jina.

NAPE ANENA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa kama kuna uwezekano wa kumuengua mgombea yeyote kutokana na skendo au chuki zinazoezwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho, alisema si kweli bali wao wanafUata taratibu na kanuni walizojiwekea na si vinginevyo.

“Sisi tuna kanuni na taratibu za chama, hiyo ndiyo misingi yetu. Hatumuengui mtu kwa chuki binafsi wala kitu kingine chochote zaidi ya kufuata kanuni zetu,” alisema Nape.

WEMA ANASEMAJE?

Akizungumza na mwanahabari wetu hivi karibuni, Wema alikiri kupata hofu hiyo kwa muda lakini ameshajiamini kutokana na kumuomba Mungu ambaye amekuwa akimtanguliza katika kila jambo analolifanya.

“Kusema kweli mtu unapotaka kufanya jambo unapaswa kujiamini, hata mimi mwanzo nilikuwa nimejipa matumaini ya hali ya juu kwamba Lowassa atapita, lakini bahati mbaya akakatwa, naamini Mungu yupo, mimi naswali usiku na mchana, Mungu atanisimamia katika hili,” alisema Wema.

Mbowe Asema UKAWA Wana Mgombea Makini.......Asema Atajulikana hivi punde

Mpekuzi blog

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe amesema pamoja na changamoto wanazokumbana nazo katika Ukawa, lakini wanajitahidi kumpata mgombea mmoja.
 
Mbowe alisema hayo jana katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika jijini Mwanza, ambapo pia aliwatambulisha wabunge waliohamia Chadema kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbunge wa Kahama, James Lembeli na mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Mara, Ester Bulaya.
 
Mbowe alisema viongozi wanaounda Ukawa, wanaendelea kushirikiana ingawa kuna changamoto kadhaa. Lakini, watatumia kila mbinu kuhakikisha anapatikana mgombea mmoja kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Ukawa katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
 
“Tunaendelea kushirikiana lakini kuna changamoto, kama viongozi tutatumia kila mbinu tuwe na mgombea mmoja wa Ukawa na mazungumzo yoyote yanahitaji uvumilivu, kuheshimiana na kushirikiana,” alisema Mbowe ambaye ni mbunge wa Hai.
 
Hata hivyo, Mbowe alisema umoja huo hautatangaza mgombea wao kwa haraka, kama ambavyo wananchi wanatarajia, kwa sababu tu CCM wamekwisha kumtangaza wao, ambaye ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli.
 
“Tutamtangaza mgombea wetu kwa muda muafaka na watanzania wote watafurahi…hatuwezi kutangaza kwa sababu tu CCM wametangaza mgombea wao,” alisema Mbowe.