Saturday, June 6, 2015

Nay wa Mitego bado ana hamu ya kuiongeza zaidi familia yake.

Rapper huyo mwenye watoto watatu amesema ana hamu ya kupata mtoto wa nne.


  • “Suala la uzazi wa mpango nalizingatia sana. Sasa hivi nina watoto watatu bado mmoja tu. Unajua hutakiwi uzae watoto wengi halafu waje kushangaa tu bila msaada,” amesema Nay.



  • “Mimi hawa wa nne watasoma vizuri kwa sababu tayari toka naanza maisha nilipanga kuja kuwa na watoto wanne.”


Wimbo Mpya wa Diamond Platnumz Wavuja Mitandaoni Kabla Hajautoa Rasmi..Usikilize Hapa Chini Nimekuwekea

Brighton masalu
VUNJA ukimya! Baada ya kuhusishwa kwa muda mrefu na fununu za kutembea na wanaume kadhaa tangu kufariki kwa aliyekuwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’, msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma hatimaye amefunguka na kujiapiza kwa kulamba kidole, kuchovya mchanga na kukipitisha shingoni akidai tangu kuondoka kwa Sajuki hajawahi ‘kuchangia shuka’ na mwanaume yeyote na kama yupo, ajitokeze hadharani!

‘Akibadilishana sentensi’ na ‘kiruka’ njia wetu kwa njia ya simu hivi karibuni, Wastara ambaye bado anafanya vyema kwenye sanaa, alishutumu na kuonekana kuchukizwa vikali na tetesi juu yake akihusishwa na wanaume kadhaa akiwemo msanii mwenzake, Bond Bin  Suleiman.


  • “Nashangazwa sana na wanaoeneza uvumi wa mimi kutembea na wanaume wengi baada ya kifo cha mume wangu, kwani mimi sina haki kama mwanamke jamani? Kama kuna mwanaume mwenye uthibitisho wa kutembea na mimi si ajitokeze!” alisema Wastara huku akiashiria jazba.

Wakati watu kama Sitta wakikodi magari maalum kwa ajili ya zoezi la utafutaji wadhamini na watu kama Makongoro wakijikongoja na magari ya marafiki zao; hali imekuwa tofauti kabisa kwa Lowassa kwani yeye amepatiwa ndege maalum kwa ajili ya shughuli hiyo ya kutafuta wadhamini!

Ndege hiyo 'private jet' ambayo Lowassa amepatiwa na wafadhili wake katika safari yake hii ya matumaini imetolewa mahususi kwa ajili ya kuhakikisha Lowassa anazunguka mikoa yote nchini bara na visiwani kabla ya julai 12 na 13 ili akamilishe zoezi la kuwapata wadhamini 435 nchi nzima ili kufanikisha sharti la chama kwa wagombea nafasi ya urais.
Udaku Special Blog

HONGEARA DIAMOND

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kimempatia Mwanamuziki  Diamond Platinumz Tuzo ya  the most inspiring Young Man as a music icon..Tuzo Hiyo ilipokelewa na Mwanamuziki Nick wa Pili kwa Niaba yake kwani yeye alishindwa kufika katika Hafla ya utoaji wa Tuzo hizo kutokana na Ratiba zake kumbana....Hongera Kijana unazidi kutupiga gap tu.......

Niki wa Pili Ameandika Hivi Kupitia Ukurasa wake wa Instagram:


  • nikkwapili Kwaniaba ya @diamondplatnumz @diamondplatnumz mzawa wa tandale katika hii fani yetu tuliyokuwa tunaitwa wahuni....leo yeye ndio the most inspiring (kijana) as a music icon....TUZO IMETOLEWA NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SAALAM , KITIVO CHA MASOKO 4h


Urais 2015: Mwigulu achukua fomu,Asema Kikwete ni Rais wa Mwisho Kutawala Tanzania Masikini

Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba pamoja na Mke wake katika ukumbi wa makao makuu ya CCM Dodoma.
 

Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akiongea na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa NEC Dodoma.
Mke wa Mwigulu Nchemba akiwasalimia Waandishi wa Habari.
Naibu waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba katika mkutano na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais leo.

Naibu Waziri waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba leo amechukua  fomu ya kugombea urais wa  Jamhuri ya muungano wa Tanzania ikiwa atateuliwa  na chama chake cha Mapinduzi kupeperusha bendera  ya Tanzania katika uchagauzi mkuu ujao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari amesema kwamba atahakikisha anaboresha uchumi kwa  wananchi, ikiwa ni  pamoja na kuboresha njia kuu za wananchi kupata kipato. Kufufua viwanda vilivyokufa  ili kutoa ajira kwa vijana pamoja na  kudhibiti madawa ya Kulevya, Rushwa na ufisadi.

Amesisitiza kuwa Rais Kikwete ndiye rais wa mwisho kutawala Tanzania maskini.

Hiki ndio kilichonifikia kuhusu Makongoro Nyerere kuhusishwa na ajali iliyotokea leo Kigoma

20150606040816Headlines kwenye Magazeti leo nyingi zina stori kuhusu Wagombea wa Urais kwa makada wa CCM wameingia kwenye hatua nyingine ya kupita mikoani kwa ajili ya kutafuta wadhamini wao, Makongoro Nyerere ni mmoja wa Wagombea hao ambae stori zilizoenea mitandaoni leo zinahusu msafara wake uliokuwa Kigoma kupata ajali.
 Stori imekuwa kubwa na wengine wameipata taarifa hiyo tofauti na jinsi ajali iliyotokea.. Nimepita MICHUZI BLOG na kuikuta hii stori, gari iliyopata ajali ni gari iliyokuwa imebeba Wasaidizi wa Makongoro Nyerere.. Gari hiyo imepinduka ikiwa kwenye mwendo wa kasi.
Watu walioumia ni wasaidizi hao pamoja na Mwandishi wa Habari mmoja.
20150606040817Kama kuna kingine kitanifikia kuhusu hii ishu nitakusogezea muda wowote mtu wangu.
Pole kwa wote walioumia kwenye ajali hii.

Kuna watu ambao walimuita Mzee Majuto kwenye show wakamuahidi kumlipa mil.2, baada ya show wahusika hawakumlipa… Mzee Majuto ikabidi amtafute Wema Sepetu ambae alimuunganisha na watu hao.

Mzee Majuto amesema Wema aliwatafuta watu hao na wakamlipa hela hiyo jana.. lakini hii sio mara ya kwanza kwa Mzee Majuto kutapeliwa, kumbe aliwahi kusainishwa mpaka Mkataba kwenda kwenye show Mwanza yeye pamoja na akina JB na Steve Nyerere, mwishowe wakatapeliwa hivyohivyo.

U Heard iko kwenye hii sauti mtu wangu, Mzee Majuto kasimulia ishu nzima ilivyokuwa pamoja na huo utapeli wa Mwanza.