Saturday, April 9, 2016

TANGAZO
MADIWANI wa manispaa ya Shinyanga  wamekubali shirika la rafiki linalojihusisha na  mradi wa Sauti   kwa utoaji  elimu   ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na kwenye  makundi maalumu kufuata masharti waliyopewa sababu walionekana kwenda kinyume nakushindwa kufuata taratibu.
Masharti hayo ni  kutumia wataalamu wenye sifa,kutokuwa na mtazamo wa kuruhusu ndoa ya jinsia moja,kutosambaza  vifaa tiba kama vile mafuta ya vilainishi pamoja na kuwashirikisha viongozi wa dini na serikali.

Madiwani  waliyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani cha dharura  kilichofanyika mjini hapa ambapo  walidai kuwa shirika hilo limeingia kinyemela nakuanza kutoa elimu kwa wananchi ikiwemo kutotumia wataalamu nakuonekana kuchochea ndoa ya jinsia moja hivyo hawatahitaji  mradi wa shirika hilo kuendelea kuwepo.
Diwani vitimaalum Mariamu Nyangaka  na  diwani wa Moris Mgini wa kata ya Chamaguha  walisema shirika hilo kama litakubali kuendelea na kutoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na makundi maalumu   sawa ila wahakikishe wanafuata masharti watakayopewa na madiwani  ambayo kutumia wataalamu na kutosambaza vifaa tiba kama mafuta kwani walifanya kinyemela  nakupotosha wananchi .
“Kwenye suala la kinga watu lazima wasimamiwe kata ya Kambarage inaongoza  kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi  ndio maana leo tunataka mradi huu uwepo  ila kinachotakiwa  kusiwepo usambazaji wa mafuta ya vilainishi kukubali mafuta hayo ni dalili ya kuruhusu ndoa ya jinsia moja kuendelea kuwepo”alisema  diwani Mshandete.
Naye kaimu mganga mkuu wa manispaa hiyo dkt Edith Kwezi alisema kuwa  maambukizi ya virusi  yameshamili kwa asilimia 4.5  kati ya watu 100 watu 37 wanamaambukizi  pia hivi sasa serikali imeona ni vyema ikatoa elimu katika makundi maalumu suala la  vilainishi ni  vifaa tiba vipo tangu zamani ila vimeongelewa  sio mahala pake hivyo shirika hilo likiri limefanya makosa lirudi kwa wananchi kutoa elimu upya.
Kaimu  katibu tawala wa  wilaya  ya Shinyanga Charles Maugira alisema kuwa  baada ya kupata malalamiko shirika hilo walilifuatilia  nakuzungumza nao  ili kuweza kuboresha na kufuata miongozo kutoka wizarani.
Naye mkuu wa shirika hilo  Gerald Ng’ong’a alisema kuwa  amekiri makosa yaliyojitokeza kamwe hawezi kubadilisha tamaduni za mtanzania na kuiga nje  ikiwa alishtushwa na taarifa zilizokuwa zimeenea ila lengo lake ni kutoa elimu  juu ya maamubikizi ya virusi vya ukimwi na  kwenye makundi maalumu katika kata 15 za manispaa..
Msimamizi  Deusdetit  Mjungu wa shirika la Jphiego kutoka nchini Marekani lililotoa mradi huo kupitia shirika la Rafiki  alisema kuwa kama itaonekana mradi huo kwenda kinyuma na maadili ya mtanzania atajitoa  kwani limekuwa na malengo yake manne ambayo ni kutoa elimu kwenye makundi maalumu na vijana wenye umri kati ya 15 hadi 24 waliokatika hatari ya maambukizi.

MCHEZAJI KANU WA NIGERIA ATOA MAFUNZO KWA WATOTO WA KITUO CHA MICHEZO CHA JAKAYA KIKWETE YOUTH PARK

 Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu (kulia), akiwaelekeza jinsi ya kucheza mpira wachezaji wa Timu ya vijana waliochini ya miaka 20 ya Sunderland alipotembelea Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park kilichopo Kidongo Chekundu Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana. Kanu yupo nchini kwa ziara ya siku tano kwa mwaliko wa Kampuni ya StarTimes Tanzania ambapo jana alitoa msaada wa vyakula, magodoro, sabuni na vyombo vya matumizi ya jikoni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi ya Majimatitu ya Mbagala wilayani Temeke.
 Hapa akiwa katika picha ya pamoja na timu  hiyo ya watoto.
 Akielekeza namna ya kucheza mpira.
 Maelekezo yakiendelea.
 Watoto hao wakichezwa kwa kufuata maelekezo ya Kanu 
(hayupo pichani)
 Kanu akiwagawia fulana wachezaji hao.
 Hapa akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa watoto hao.
 Akiendelea kutoa maelekezo ya jinsi ya kucheza mpira.
 Watoto wa kituo hicho wakimshangilia Kanu (hayupo pichani)
 Kanu akiwa katika picha ya pamoja ya Buguruni Youth Centre.
 Kanu akizungumza na watoto wanaopata mafunzo ya soka katika kituo hicho.
Kanu akikagua timu ya watoto hao.

Na Dotto Mwaibale

MCHEZAJI nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Naijeria, Nwankwo Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika ametembelea na kushiriki kwenye mafunzo na watoto kwenye kituo cha Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park cha jijini Dar es Salaam jana.

Kanu ambaye amekuja kwa shughuli za kampuni hiyo atakuwepo nchini Tanzania kwa muda wa siku tano alifurahi sana kuona watoto wameandaliwa mazingira mazuri kwa ajili ya michezo mbalimbali kwani sio wote waliopata fursa hiyo.

“Wakati mimi ninaanza kucheza mpira hakukuwa na kituo kizuri kama hiki wala jezi, viatu na walimu wazuri mlio nao sasa. Hii ni fursa ya kipekee kwenu nyinyi kuweza kuonyesha 
juhudi za kujifunza ili mje kuwa kama mimi siku za mbeleni. 

Leo mimi nimekuwa maarufu ni kwa sababu nilikuwa na nidhamu, bidii, dhamira na kuwasikiliza walimu wangu walipokuwa wananifundisha. Hatimaye leo hii nina mafanikio makubwa, ninaishi maisha mazuri, wazazi wangu pia wanaishi mahali pazuri, wanasafiri na kupata wanachokitaka kwa sababu tu ya mimi kufanikiwa.” Kanu aliwaambia watoto wa kituo cha Jakaya Kikwete Kampuni ya StarTimes ambayo imo zaidi ya nchi kumi barani Afrika imemtua mchezaji huyo kama balozi katika 
kuwawakilisha katika shughuli mbalimbali. 

Kanu anatarajia kuwa chachu kwa katika kampuni hiyo hususani katika kuboresha na kuongeza vipindi na chaneli za michezo kwani waafrika wengi wanapenda soka.

“Ninaamini mchezo wa soka ndio unaopendwa na watu wengi zaidi duniani na waafrika ni miongoni mwao. StarTimes mpaka sasa wamepiga hatua kubwa katika kulisimamia hili, mpaka sasa tayari wana haki miliki za kuonyesha ligi za Budensiliga na Serie A za Ujerumani na Italia. 

Hiyo ni hatua kubwa kwani wateja wanafurahia michezo hiyo inyoonekana moja kwa moja kwa vifurusushi vya bei nafuu. Kama balozi ninaahidi kushirikiana na kampuni katika kuboresha zaidi vipindi vyake na pia kuishauri kujikita zaidi na michezo ya nyumbani. 

Kama mnavyoona kwa mara ya kwanza tumedhamini ligi daraja la kwanza.” Aliongezea mchezaji Kanu alihitimisha kwa kuwataka watoto wa kituoni hapo kuonyesha bidii, utii na dhamira ya dhati kwa kila wanachokifanya, “Ningependa kuwashauri wadogo zangu kuwa popote utakapokwenda duniani kwenye mchezo wa soka, viwanja na mipira inayotumika ni hii hii wala hakuna tofauti yoyote. 

Hivyo basi sioni kama kuna kitu cha kuwazuia na nyinyi msifanikiwe. Kama nilivyowaambia awali, bidii, nidhamu, dhamira na utii kwa walimu wenu ndio msingi wa mafanikio ya mwanasoka yeyote Yule duniani. Nawatakia kila la kheri na siku nyingine nikija Tanzania naahidi kuwatembelea tena.”

Kwa  upande wake Kocha Mkuu wa Kituo cha Vijana cha Jakaya Mrisho Kikwete,  Eduard Tamayo alielezea furaha yake kwa kampuni ya StarTimes kuandaa kitu kama hiko na kukiteua kituo hiko kuwa mwenyeji wa ugeni wa Kanu nchini Tanzania.

“Nimefurahi sana kwa ujio aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Naijeria na vilabu vikubwa barani Ulaya kama vile Ajax, Inter Milan na Arsena, Nwankwo Kanu kutembelea hapa na kushiriki mafunzo na watoto. Hii ni bahati kubwa sana kwa watoto hawa kwani ni nadra sana kutokea, kupata mafunzo, kuzungumza, kupata ushauri na kuuliza maswali moja kwa moja kwa Kanu. Ninatumaini itakuwa imewapa motisha kubwa sana.” Alisema  Tamayo

Kocha Mkuu huyo kituoni hapo alihitimisha kwa kuwataka wazazi kuwapeleka na kuwasajili watoto kituoni hapo kwa mafunzo kwani wanapokelewa na kuwapatia mafunzo mazuri kwa kuviendeleza vipaji vyao. Na kwamba kituo hiko ni fursa kwa watanzania hivyo ni vema kukitumia vizuri.

Singida Washukuru kuwa wa Kwanza Mgawo wa Milioni 50/- za Rais Magufuli kwa kila kijiji..Unafuata mkoa huu hapa

Mbunge  wa Viti Maalumu, Aysharose Matembe (CCM), amesema vijana na wanawake mkoani Singida, wameishukuru Serikali kwa kuchagua mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa 10 ya kwanza itakayonufaika na mgawo wa Sh milioni 50 kila kijiji na kila mtaa.

Matembe amesema wako tayari kuzitumia kwa uangalifu fedha hizo kwa kuhakikisha wanaunda vikundi vyenye malengo madhubuti ya kujenga ili wajikwamue kiuchumi.

Mbunge huyo jana alisema Singida ni miongoni mwa mikoa yenye rasilimali nyingi, ikiwemo ardhi yenye rutuba ambayo kwa kiasi kikubwa wananchi wanaitumia kujishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali yanayochangia kukua kwa pato la Taifa.

Alisema amezungumza na wananchi hao ambapo walikiri fedha hizo kuwa na mchango chanya kwa maendeleo ya mkoa na kaya zao, hivyo kila mtendaji atakayehusika kwa namna moja au nyingine na fedha hizo, anapaswa kuwa mwadilifu ili ziwafikie walengwa kwa wakati.

“Kutolewa kwa hizi fedha ni kama kupatikana kwa maji jangwani kwa vijana na wanawake wa Singida, kwa nyakati tofauti nimezungumza nao na wananipa salamu kuishukuru Serikali kwa kuwatambua na kuieleza kwamba wamejipanga kunufaika nazo.

Maalim Seif Sharrif kuelezea mwelekeo wake kisiasa kesho 10 Aprili 2016.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad kesho ataelezea mwelekeo wake kisiasa,ikiwamo kufafanua kiundani uamuzi wa chama hicho kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu.
 
Mgombea huyo wa urais Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ataeleza mambo hayo ikiwa imepita takribani wiki moja tangu Baraza Kuu la chama hicho kutoa msimamo wake wa kutomtambua Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein pamoja na wawakilishi na madiwani.
 
CUF kilisusia kushiriki uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu baada ya Oktoba 28 mwaka jana, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya urais,uwakilishi na udiwani,akisema kulikuwapo na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.
 
Habari kutoka ndani ya chama hicho zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa mkutano wa kiongozi huyo utakuwa wa kwanza kwake,tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio na ataeleza mambo muhimu yatakayotoa picha halisi ya mwelekeo wake na CUF.
 
“Katika mkutano uliopita tamko lilikuwa la Baraza Kuu ila keshokutwa (kesho) Maalim Seif atazungumza kama Katibu Mkuu na aliyekuwa mgombea urais. Kuna masuala mengi atayaeleza kwa kina, hasa hili la uamuzi wa CUF kususia uchaguzi,” zilieleza taarifa hizo.
 
“Atazungumzia kwa kina uchaguzi ulivyokuwa na kujibu maswali ya watu wa kada mbalimbali waliokuwa wakihoji nini hatima ya CUF,baada ya kususia uchaguzi na hivyo kupoteza nafasi za uwakilishi.”

Aliyekuwa mgombea Mwenza wa CHADEMA/UKAWA, Amerejea Cuf hii leo. Haji alikuwa mgombea Mwenza wa Edward Lowassa katika Uchaguzi wa 2015 wakipeperusha Bendera ya CHADEMA

Mhe Said Soud na Juma Ali Khatib wateuliwa kuwa wajumbe wa Baraza la Mapinduzi


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum:
i.            Mhe. Said Soud Said – Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum
ii.          Mhe. Juma Ali Khatib – Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum.
 
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 9 Aprili 2016.
    
Waheshimiwa wote waliotajwa wanaombwa wafike Ikulu Mjini Zanzibar kesho Jumapili tarehe 10 Aprili 2016
saa 3 kamili za Asubuhi kwa ajili ya kuapishwa.
(Dkt. Abdulhamid Y. Mzee),
KATIBU WA BARAZA LA MAPINDUZI
NA KATIBU MKUU KIONGOZI,
ZANZIBAR.
                                                               
9 APRILI, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA PALM VILLEGE MSASANI BEACH WATERFONT LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China. Mradi huo unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront unategemewa kutoa ajira jumla ya watu 2000 utakapokamilika. Kuli Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Jonson Huang.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China. Mradi huo unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront unategemewa kutoa ajira jumla ya watu 2000 utakapokamilika. 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Kampuni ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village Msasani Beach Waterfront akikabidhi Mfano wa hundi yenye jumla ya Tshs. 10,000,000. Kwa Uongozi wa Shule Msingi Mbuyuni kwa ajili ya kuendeleza Shule hiyo. Leo April 09,2016. Kulia Afisa Muandamizi Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wapili kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Geoge Simbachawene, na Waziri Biasha na Uwekezaji Mhe. Charles Mwinjage.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village Msasani Beach Waterfront Leo April 09,2016. Kulia Afisa Muandamizi Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wa tatu kushoto Mwenyekiti wa Kampuni Uwekezaji ya Group 6 Jonson Huang wa pili kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Geoge Simbachawene, na Waziri Biasha na Uwekezaji Mhe. Charles Mwinjage.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa Pazia kuzindua rasmi Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village Msasani Beach Waterfront, leo April 09,2016. Kulia Afisa Muandamizi Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wa tatu kushoto Mwenyekiti wa Kampuni Uwekezaji ya Group 6 Jonson Huang.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront, Leo Aapril 09,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Afisa Muandamizi wa Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wakati wa ghafla ya uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Villege unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Gropu 6 ya China zinazojengwa Msasani Beach Waterfront. (Picha na OMR).


Askari wakisimamia zoezi la kuvunja mlango
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayombo akionesha ndoo zinazotarajiwa kuwekwa mafuta.
Sukari na viroba vya kuweka kwa matayarisho ya kuingizwa sokoni.

Hii ni Sukari iliyomwangwa chini kabla ya kuwekwa kwenye viroba
Na Mwandishi Wetu-Kilwa.
Siku ya tarehe 6/4/2016 maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kikosi cha (FAST)  wakiwa na maofisa wa Polisi walifanya upekuzi kwa lengo la kutafuta magendo kwenye nyumba ya mfanyabiashara Yusuf Barkat Sareh.

Upekuzi huo ulifanyika baada ya kupata taarifa za kiintelijensia zilizofanyiwa kazi muda mrefu.

Bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi zilikamatwa kama zifuatazo
Sukari ya India kilo 50 jumla mifuko 762 Sukari ya nje iliyokamatwa kwenye mifuko ya viwanda vya hapa nchini kilo 25 jumla mifuko 135, Mafuta ya kula lita ishirini (20) aina mbalimbali kutoka nje jumla madumu 49, Betri aina ya tigger katoni 223, Amira katoni 135, Sabuni za kufulia katoni 48

Vitu mbalimbali vilivyokamatwa kama ushahidi wa biashara haramu ya magendo ya sukari. Mashine mbili (2) za kushonea kwenye mifuko ya iliyowekwa sukari inatoka nje ya nchi na kuwekwa kwenye mifuko ya viwanda vya nchini nya sukari vya Kilombero, TPC na Mtibwa Sugar.
Mifuko mitupu mipya ya sukari kilo 25 toka India  2000
Mifuko iliyotumika ya kilo 50 mitupu ya sukari 36,000
mifuko ya sukari iliyotumika ya Viwanda vya Tanzania ya kilo 25 kiasi cha 1150
Madumu mafuta ya nje mchanganyiko ya kula lita 20 kiasi cha 609 Madumu matupu ya lita 10 ya nje kiasi cha 310.
Nyumba hii ndiyo Ofisi ya Bosi ambayo hutumika kuweka bidhaa kabla ya kusambazwa sokoni iliyopo Somanga njia nne eneo la Kikanda Wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi.
sehemu ya kuweka sukari na kupima.
Nyumba inayotumika kuweka sukari
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayombo akizungumza na waandishi.
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA akionesha sukari.
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA 
Aina ya mafuta kutoka nje ya nchi tayari kuwekwa kwenye ndoo kwa kupeleka Sokoni
Polisi akilinda viroba vyenye sukari kutoka nje ya nchi.
Madumu yaliyokua na mafuta ya kula na ndoo zinazotarajiwa kuwekwa mafuta
Nyumba ya mtuhumiwa Yusuf Sareh iliyopo Somanga Njia nne Kikanda.