Friday, January 8, 2016

Kesi ya Mtanzania ( Rashidi Mberesero) Anayetuhumiwa Kwa Ugaidi Kenya Yaanza Kusikilizwa

Mpekuzi blog

Shahidi katika kesi ya shambulio la kigaidi lililofanyika mwaka jana katika Chuo Kikuu cha Garissa, Kenya ameiambia mahakama kuwa Mtanzania Rashidi Mberesero anayetuhumiwa kushiriki, alikuwa akiswali katika msikiti ulio karibu na chuo hicho kwa siku tatu mfululizo.

Kolombo Adao ambaye ni imamu wa Msikiti wa Garissa alidai mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mlimani, Daniel Ogembo kuwa Mberesero aliondoka katika mazingira ya kutatanisha Aprili 2 mwaka jana huku akiacha begi lake msikitini.

“Alikuwa mwerevu mno na aliweza kuisoma Quran. Nilikutana naye mara ya kwanza asubuhi ya Machi 30, 2015 wakati nafungua msikiti,” alieleza shahidi huyo.

Kwa mujibu wa Adao, Mberesero alikuwa muumini wa kipekee kwani kila siku alikuwa akifika msikitini saa 10:35 alfajiri, wakati mwingine kabla ya adhana.

Shahidi huyo alidai kwamba Aprili Mosi mwaka jana alipofungua msikiti asubuhi alimkuta Mberesero akiwa ameshafika na alimpa kipaza sauti aweze kuwaita waumini wanaotakiwa kuswali asubuhi siku hiyo.

“Nilikuwa naumwa kifua siku hiyo. Kwa hiyo nilimpa kipaza sauti atangaze kwa sababu alikuwa anaijua vyema Quran,” shahidi huyo alidai.

Kuhusu sababu za Mberesero kuwapo Garissa, Adao aliiambia mahakama kuwa aliambiwa na kijana huyo kuwa alikwenda kumsalimia mjomba wake lakini alifukuzwa kwa kuwa ni Mwislamu.

“Alinieleza kuwa baba yake ni Mdigo wa Tanga na mama yake ni Mkamba wa Kenya,” alieleza Adao.

Kwa maelezo ya shahidi huyo, siku ya tukio Mberesero ambaye alizoea kuvaa kanzu alionekana amevaa mavazi ya kawaida na kofia kama mtu anayeficha uso.

Mahakama ilielezwa kuwa siku ya tukio aliingia msikitini na kuweka begi lake kwenye kona ya msikiti lakini hakusali na baadaye aliondoka na kuliacha.    

Waziri Kitwanga: Hatua Kali Kuchukuliwa Kwa Yeyote Atakaye Kaidi Kulipisha Gari La Zimamoto Wakati Linaenda Katika Tukio

Mpekuzi blog

Katika kuhakikisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linafanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika kupambana na majanga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ameliagiza jeshi hilo kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote atakayekaidi kulipisha gari la Zimamoto na Uokoaji pindi linapokuwa linawahi  eneo la tukio ili kuweza kuzima moto na kuokoa maisha ya watu  pamoja na mali zao.

Waziri Kitwanga ametoa agizo hilo alipokuwa anamaliza ziara yake katika Makao Makuu ya Jeshi hilo Kanda ya Ilala, Dar es Salaam mara baada ya Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kamisha Jenerali, Pius Nyambacha kubainisha kuwa mojawapo ya changamoto zinazolikumba jeshi hilo ni ukaidi wa baadhi ya wananchi kutotaka kupisha gari la Zimamoto pindi linapokuwa katika harakati za kuwahi eneo la tukio.

 “Hivi hamjui hata msafara wa Rais unalazimika kupisha gari la Zimamoto au wagonjwa? Iweje leo wananchi wasipishe magari hayo? Simamieni sheria hii” Alisisitiza Mhe. Waziri. 

Aidha Mhe. Waziri aliahidi kushughulikia changamoto zote zinazolikabili Jeshi hilo changamoto hizo ni ukosefu wa vifaa, ufinyu wa bajeti pamoja na idadi ndogo ya Askari. 

Sikuuu Za Kitaifa- 2016

Mpekuzi blog

MABONDIA KAONEKA NA MAPAMBANO KUZICHAPA FEB 14 TANDIKA

Mabondia Shabani Kaoneka kushoto akitunishiana misuli na Imani Mapambano baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kupambana feb 14 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika maguruwe katikati ni mdau wa mchezo wa masumbwi Zahoro Maganga 'Super Diego' 
Mdau wa mchezo wa masumbwi nchini Zahoro Maganga 'Super Diego' kushoto akimsainisha bondia Shabani Kaoneka kwa ajili ya mpambano wake na Imani Mapambano feb 14 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika maguruwe kulia ni Rais wa TPBO Yassin Abdallah 
Na Mwandishi Wetu
Mabondia Shabani Kaoneka na Imani Mapambano wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya feb 14 uzito wa kg 74 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika maguruwe

mpambano huo wa raundi nane utasimamiwa na oganaizesheni ya ngumi za kulipwa TPBO chini ya rais wake Yassin Abdallah 'ostadhi' mpambano huo wenye kugombaniwa kwa kila mmoja kuwa juu ya mwenzie ambapo bondia Kaoneka ni namba 11 katika viwango vya ubora nchini ambapo amepigana mapambano 13 akishinda 5 kupigwa 5 na sale 3

atakuwa na kibarua kizito cha ku lilia namba yake kwa mtu wa chini yake Imani Mapambano anaeshikilia nafasi ya 12 ya ubora kwa mabondia wa Tanzania akiwa amecheza mapambano 7 akishinda 4 na kupoteza 3

katika mpambano mwingine utawakutanisha mabondia Hassan Mwakinyo atakae pambana na Salumu Salumu katika mpambano wa raundi sita siku hiyo

Picha 12 kutokea Airport Dar Mbwana Samatta alivyotua na tuzo yake


Jan 9 2016 mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika Mbwana Samatta alitua Dar na kupokewa na mashabiki zake kutokea maeneo mbalimbali ya jiji.
vlcsnap-2016-01-09-05h06m33s308
vlcsnap-2016-01-09-05h12m03s294
vlcsnap-2016-01-09-05h13m13s410
vlcsnap-2016-01-09-05h15m15s784
vlcsnap-2016-01-09-05h17m13s867
vlcsnap-2016-01-09-05h17m58s882
vlcsnap-2016-01-09-05h21m18s533
vlcsnap-2016-01-09-05h24m34s675
Shabiki akikomaa kumtazama Samatta
vlcsnap-2016-01-09-05h09m32s756
Thomas Ulimwengu & Zitto Kabwe
vlcsnap-2016-01-09-05h16m02s329
Baba mazaza wa Samatta

Diamond Platnumz ambaye kutokana na kutajwa mara kwa mara kuwania tuzo mbalimbali wanamuita ‘Mondi Bin Awards’, ametajwa kuwania MOREKLUE ALL YOUTH AWARDS 2016 kwa kifupi MAYA Awards za nchini Nigeria, ikiwa ndio nomination yake ya kwanza kwa mwaka huu 2016.
Kwenye kipengele cha African Music Act Diamond anawania pamoja na wasanii wengine wenye majina makubwa Afrika akiwemo, Wizkid, Sarkodie, Fuse ODG, Davido, AKA, Olamide na
Cassper Nyovest.
Tuzo za MAYA zitatolewa January 31, 2016 jijini Lagos, Nigeria.
Ili kuweza kumpigia kura Diamond aweze kushinda tuzo hii ingia HAPA.

BomoaBomoa Yaipasua Kichwa Serikali.......Mwanasheria Wa Nemc Aliyehalalisha Jumba La Mchungaji Rwakatare Afukuzwa Kazi

Mpekuzi blog

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU ZOEZI LA KUHAMISHA WAKAZI WA MABONDENI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

Utangulizi
Nchi yetu ina kingo za mito na mabonde na maeneo mengi hatarishi ambamo watu wanaishi kinyume cha sheria, huku wakiharibu mazingira na kuhatarisha maisha yao.  Kutokana na uhaba wa makazi, hali ni mbaya zaidi katika mabonde ya Jiji la Dar es Salaam, hasa bonde la Mto Msimbazi.
 
Serikali za awamu zote, zimekuwa zikifanya jitihada za kuwaondoa wakazi wa maeneo ya mabondeni wanaoishi katika maeneo hayo kinyume cha sheria lakini mafanikio yamekuwa si ya kuridhisha.

Serikali ya Awamu ya Tano, ambayo moja ya misingi yake mikuu ni utii wa sheria za nchi, imeanza jitihada za kuwaondoa wakazi hawa. 
Tuliamua kuanza na Bonde la Mto Msimbazi kwasababu ndiko kwenye watu wengi na athari kubwa.Sababu zetu kuu za kufanya zoezi hili ni kusafisha mabonde na mito katika jiji la Dar es Salaam na mazingira yanayozunguka ni:-

Kunusuru maisha ya wananchi wanaoishi katika mazingira hatarishi. Eneo la Bonde la Mto Msimbazi lilitangazwa kuwa ni eneo hatarishi kuishi binadamu tangu mwaka 1949 na baadaye 1979.

Kupanua uwezo wa mito ya Dar es Salaam ili kupitisha maji ya mvua kwa kasi kubwa, hivyo kupunguza uwezekano wa kutokea mafuriko na maafa wakati wa mvua nyingi;Kuzuia milipuko ya magonjwa, hasa ya kipindupindu, hasa wakati wa mvua;

Kuzuia eneo hilo kuendelea kutumika kama maficho ya wahalifu na uhalifu;

Kutoa nafasi kwa Serikali kuandaa na kuendeleza eneo hilo kwa mujibu wa sheria za nchi na mipango miji;

Utaratibu wa Zoezi
Kabla ya nyumba kubomolewa, taasisi hizi zinashirikiana kuhakiki iwapo nyumba anayokaa mkazi ina nyaraka za umiliki na vibali vya ujenzi na iwapo nyaraka hizo zina uhalali wowote. 
 
Nyumba ambazo zimethibitika kuwepo katika maeneo yasiyostahili ndio zinawekwa alama X kuashiria kwamba wakazi wanapaswa kuhama au kubomoa. Baada ya hapo, mkazi hupewa muda wa kubomoa na kuhama mwenyewe.

Kutokana na utaratibu huu, sehemu kubwa ya nyumba zinazobomolewa ni zile ambazo watu wamekwishaamua kubomoa wenyewe. 
 
Baada ya hapo, alama huwekwa kuonyesha mpaka wa bonde. Katika zoezi hili, imebainika kwamba sehemu kubwa ya wakazi wa maeneo ya mabondeni ni wapangaji huku wamiliki wakikaa sehemu nyingine salama.
 Serikali pia imeweka Dawati la Malalamiko katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Tathmini ya Zoezi
Jana, terehe 7 Januari 2016, Mawaziri watatu (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI; na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais; pamoja na Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii), walifanya mkutano wa kutathmini zoezi la kuhamisha wakazi wa mabondeni katika Jiji la Dar es Salaam. 

Mkutano huo ulipokea ripoti ya timu ya wataalam wa Wizara mbalimbali, inayoongozwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, ambayo, pamoja na mambo mengine ilibainisha kwamba sehemu kubwa ya kubaini makazi yaliyojengwa kinyume cha Sheria katika Bonde la Mto Msimbazi imekamilika. 
Ripoti ilieleza kwamba, hadi sasa, wananchi katika nyumba 774  wamehama na nyumba hizo kubomolewa. Ilielezwa pia kwamba kabla ya mkazi kuombwa  kuhama, uhakiki kuhusu uhalali wa makazi anayoishi hufanywa. 
Kutokana na uhakiki huo, jumla ya wakazi 20 walikuwa na hati halali za makazi na wakazi 119 walikuwa na leseni za makazi za muda mfupi. 
Hawa watu hawakuhamishwa. Mawaziri walipokea maelezo kuhusu changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika zoezi hilo.  
Baada ya tafakuri na mjadala, Mawaziri hao walitoka na msimamo ufuatao, kama uamuzi wa Serikali: -

1.Zoezi la kuwaondoa wananchi waishio katika bonde la Mto Msimbazi (eneo hatarishi) litaendelea kwa utaratibu ambao hautaleta mateso na usumbufu kwa wananchi;

2.Katika awamu hii, zoezi litajikita katika Bonde la Mto Msimbazi tu.

3.Kwa wakati huu, watakaohitajika kuhama ni wale tu ambao makazi yao yamo NDANI kabisa ya bonde, kwenye miteremko ya kuingia bondeni na kwenye KINGO za mto;

4.Wale watakaokuwa na nyaraka halali walizopewa na mamlaka za umma, zilizowamilikisha na kuwaruhusu kujenga katika bonde hilo, hawatahamishwa bila kupewa sehemu nyingine za kujenga. Na watumishi wa umma waliowamilikisha maeneo hayo watachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria;

5.Serikali, ndani ya siku tatu zijazo, itaanza zoezi la kuzoa kifusi na kusafisha maeneo ambapo ubomoaji umefanyika.

6.Serikali itaheshimu amri za mahakama kuhusu mapingamizi yaliyowekwa na baadhi ya wakazi wa mabondeni lakini pia itafuatilia kesi hizi ziishe haraka ili taratibu zinazofuatia zifanyike;

7.Serikali itawachukulia hatua za kinidhamu watumishi wake wanaoendesha zoezi hili kinyume na misingi ya sheria zinazotekelezwa, na kinyume na misingi ya haki na uwazi, ikiwemo wanaoweka alama za X zaidi ya mita zilizowekwa kisheria. Limeanzishwa dawati la malalamiko katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kupokea malalamiko au maswali kuhusu zoezi hili.

8.Nyumba na majengo ya miaka mingi, yaliyokuwepo miaka mingi kabla ya kutungwa kwa Sheria zinazotekelezwa kwa zoezi hili, hayatabomolewa isipokuwa tu pale maisha ya wakazi yapo hatarini. Wanaoishi katika makazi hayo watapewa miongozo ya hatua za kuhifadhi mazingira na kujiokoa na maafa;

9.Serikali haina dhamira ya kubomoa mahoteli makubwa ya siku nyingi yaliyo karibu na fukwe katika maeneo ya Masaki. Wamiliki wa mahoteli haya watapewa masharti na miongozo ya kuhifadhi mazingira kwa mujibu wa Sheria.

10.Serikali inaweka uratibu wa karibu zaidi miongoni mwa taasisi zake ili hatua za utekelezaji wa sheria za nchi zisiwe chanzo cha taharuki katika jamii.

11.Serikali haina dhamira ya kuwatesa wananchi wake kwa kuwalazimisha kuhama katika makazi yao bila sababu za msingi. Lakini pia Serikali haiwezi kuruhusu wananchi waendelee kukaa katika maeneo ambayo ikinyesha mvua kubwa maisha yao yapo hatarini.
 Itakumbukwa kwamba katika mafuriko ya mwaka 2011, wananchi 49 waishio mabondeni walipoteza maisha. Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Hali ya Hewa, mwaka huu zinatarajiwa kunyesha mvua kubwa kuliko zilizowahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.

12.  Serikali inafuatilia kwa karibu kwa mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya taarifa za wananchi wanaohitaji msaada maalum wa kibinadamu.

Suala la Mchungaji Getrude Rwakatare
Mkutano ulipokea taarifa kuhusu suala linaloongelewa sana la nyumba ya Mchungaji Rwakatare.  Ilielezwa kwamba Mchungaji Rwakatare amejenga nyumba yake pahali ambapo amezuia mtiririko wa mto kwa kujaza kifusi ili kupata eneo zaidi katika eneo la miti ya mikoko, kinyume kabisa na Sheria tatu muhimu.  
Pia ilielezwa kwamba tangu wakati ujenzi unaanza jitihada za kumsimamisha zilifanyika na mamlaka za Serikali za Mitaa lakini ikashindikana kutokana na sababu mbalimbali. Pale Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira lilipoingilia kati na kutaka kuibomoa nyumba hiyo, Baraza lilishtakiwa mahakamani. 
Wakati kesi inataka kuanza kusikilizwa, mwanasheria mdogo wa Baraza, yeye mwenyewe bila kuagizwa wala kuwaarifu wakubwa zake, mnamo tarehe 11 Mei 2015, aliingia makubaliano na mawakili wa Mchungaji Rwakatare kwa niaba ya Baraza ya kuondoa kesi hiyo mahakamani na kukubali, kwa niaba ya Baraza, kutombughudhi kabisa Mchungaji Rwakatare.  
Makubaliano hayo yalisajiliwa na Mahakama kama hukumu tarehe 13 Mei 2015. Mwanasheria huyo alificha makubaliano hayo kwa miezi mitano hadi Oktoba 2015, yalipogundulika na mtumishi mwingine wa Baraza. Mkutano ulielezwa kwamba Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa kufuata taratibu zote, alishaagiza kufukuzwa kazi, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa mwanasheria huyo. 
Mwanasheria huyo alifukuzwa kazi siku ya juzi tarehe 6 Januari 2016 na taarifa zake zimekwishafikishwa TAKUKURU. 
Vilevile, Ofisi ya Makamu wa Rais, iliiagiza Baraza kufungua shauri mahakamani la kuomba “makubaliano” kati yake na Mchungaji Rwakatare yawekwe pembeni kwasababu yalipatikana na njia ya udanganyifu. Shauri hilo lilifunguliwa tarehe 29 Disemba 2015.

Kuhusu Karakana ya Mradi wa Mabasi Yaendayo kwa Kasi (DART)
Mkutano pia ulijulishwa kuhusu hoja inayozungumzwa kwamba wananchi wanaondolewa katika maeneo ya kuishi mabondeni lakini mradi wa DART umeachwa.
 Mkutano ulielezwa kwamba Sheria ya Mazingira (kifungu 57 (2)) inatoa nafasi ya kutolewa ruhusa kwa miradi/shughuli zenye maslahi ya taifa kufanyika katika maeneo ya mabondeni, na kwamba Waziri mwenye dhamana ya mazingira anaruhusiwa kutoa miongozo ya namna ya shughuli hizo zinavyoweza kufanyika bila kuathiri mazingira.
 Mradi wa DART ulipata kibali hicho na una mkataba na Baraza la Mazingira kuhusu hatua za hifadhi ya mazingira zinazopaswa kutekelezwa katika mradi huo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
08.01.2016

Saturday, January 9, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Januari 9

Mpekuzi blog

Mpekuzi blog
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )