Matokeo haya yameirudishia matumaini Yanga kushinda Kagame Cup 2015…
on
Yanga imepata ushindi wa goli 3-0 mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, magoli ya Yanga yalifungwa na washambuliaji waliosajiliwa msimu huu Malimi Busungu ambaye amefunga magoli mawili dakika 26, 68 huku bao la tatu likifungwa na Geofrey Mwashiuya aliyeingia kipindi cha pili cha mchezo na kupachika goli la tatu dakika ya 73, mchezo uliomalizika kwa Simon Msuva na Amissi Tambwe kukosa penati.
Yanga imerudisha
matumaini kwa mashabiki wake ambao walikuwa na mashaka kama ingepoteza
mechi ya leo kwani nafasi ingekuwa finyu kusonga mbele… Yanga sasa imebakiwa na michezo miwili kati ya KMKM ya Zanzibar July 24 2015 Uwanja wa Taifa na mchezo wa mwisho dhidi ya Khartoum ya Sudan.
No comments:
Post a Comment