Saturday, August 22, 2015

NAPE ATOA SHUKRANI KWA WAKAZI WA MTAMA AAHIDI KUTOWAANGUSHA

Friday, August 21, 2015
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndio mgombea wa ubunge wa Jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa kata ya Majengo wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wa kuwashukuru wananchi hao kwa kumpigia kura nyingi kwenye mchakato wa kura za maoni.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndio mgombea wa ubunge wa Jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM akiwasalimia viongozi mbali mbali wa CCM ngazi za kata na matawi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano uliofanyika Majengo .
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndio mgombea wa ubunge wa Jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa kata ya Majengo wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wa kuwashukuru wananchi hao kwa kumpigia kura nyingi kwenye mchakato wa kura za maoni.
 Wananchi wa Jimbo la Mtama wakishangilia kabla ya mkutano kuanza.
 Wananchi wa Kata ya Majengo ,Mtama wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza mbunge wao mtarajiwa Nape Nnauye .
 Mbunge wa Mchinga Mhe.Said Mtanda akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kushukuru wananchi waliompigia Katibu Mwenezi wa CCM Taifa ,Nape Nnauye uliofanyika Majengo Mtama.
 Wanancnhi wakimsindikiza Nape Nnauye kwenda jukwaani kuhutubia.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Majengo,Mtama na kuwaeleza atakuwa Mbunge wa mfano kwa kutekeleza kila alichoahidi na kuwa karibu na wananchi muda wote.
 Wananchi wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndie mgombea ubunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM.
Mkutano huo uliofanyika sokoni Majengo ulikuwa wa kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura nyingi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndie mgombea ubunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM akisisitiza jambo kwenye mkutano wa kuwashukuru wapiga kura wake.
 Mmoja wa wagombea waliokuwa wanagombea nafasi ya kuiwakilisha Mtama bungeni akiwasalimu wananchi na kuwahakikishia kuwa atashirikiana na Ndugu Nape Nnauye katika kufanikisha ushindi wa CCM.
 Mgombea Diwani wa kata ya Mnara Bi.Halima R. Mwambe akiwasalim wananchi kwenye mkutano huo.
 Wananchi wakifuatilia kwa makini hotuba za shukrani.
Kikundi cha kwaya cha Majengo kikitumbuiza.

Mama Diamond Platnumz Amfunika Zari kwa Mbizi Kwenye Bwawa la Kuogelea


MAMA’KE Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Sandra’ ameonesha umahiri mkubwa wa kuogelea kiasi cha kumfunika mkwe wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwenye bwawa la kuogelea lililopo nyumbani kwa Diamond, Tegeta-Mivumoni jijini Dar.

Mama huyo alionekana akipiga mbizi na mtoto wake Esma, huku akionyesha manjonjo ya kuogelea kwa kasi tofauti na Zari anavyoogelea katika bwawa hilo.

“Bi mkubwa yuko vizuri sasa maana anapiga mbizi siyo mchezo kabisa hata Zari haoni ndani, spidi yake ni kali kuliko Zari,” alisema mwanafamilia mmoja ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini huku akimtumia mwandishi wetu picha za mama Diamond akiogelea.

Hizi Hapa Sababu Halisi za Ukawa Kutokufungua Kampeni Kama ilivyotarajiwa

Panaposemwa uongo na kuachwa kuukanusha basi waweza kuaminiwa. Zimesikika taarifa kwenye mitandao kuwa kutokufungua kampeni leo au kesho ni kutokana na afya ya lowassa kudhoofu.

Sababu ambazo zimefanya Ukawa kutozindua kampeni kama ilivyotarajiwa leo ni kama zifuatavyo:-

1.Maandalizi ya kuandaa kikosi cha kumnadi mgombea yanamalizwa leo
2. Kumaliza mgogoro wa majimbo yaliobaki kutokana na sintofahamu iliyotokea
3. Kuuzima upepo wa magufuli utakaovuma kesho
4. Kuandaa hoja nzito zakujibu baada ya matarumbeta ya ccm yatakayoropoka kesho
5. Kutafuta uwanja wa kampeni utakaokidhi haja
6. Viongozi wa chama wamikoani na wabunge bado hawajawasili Dar kutokana na urudishaji wa fomu za ubunge jana.


chanzo: mwandishi wa habari aliyewasiliana na JJ mnyika muda huu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Mkapa, Mwinyi kumnadi Dk. Magufuli Jangwani.


Marais wastaafu, Ali  Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, wanatarajiwa kushiriki kwenye ufunguzi wa kampeni za kumnadi mgombea wa urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli Jumapili, jijini Dar es Salaam.

Pia uzinduzi huo unatarajiwa kupambwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wakiongozwa na Nasiib Abdul (Diamond) na bendi mbalimbali ikiwamo ya Tanzania One Theatre (TOT).

Kadhalika, wamo marais wastaafu wa Zanzibar, mawaziri wakuu wastaafu, viongozi wakuu wastaafu wa CCM na viongozi wa serikali, makada kutoka mikoa mbalimbali nchini na wananchi wanatarajiwa kuhudhuria.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu ndani ya CCM zinaeleza kuwa baada ya kampeni hizo kuzinduliwa jijini Dar es Salaam, ziara ya kumnadi itaelekea mikoa ya kusini.

Mikoa hiyo ni Lindi, Mtwara na Ruvuma na kwamba ratiba hiyo itafuata hadi kumalizika nchi nzima.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (pichani), alipoulizwa, alisema ratiba kamili itatolewa baadaye kwa vyombo vya habari.

Kuhusu wageni mbalimbali wa heshima ambao wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo alisema hafahamu na kwamba mgeni rasmi ni mgombea mwenyewe ni Dk. John Magufuli.

Nape akizungumzia ilani ya uchaguzi ya chama hicho, alisema inatarajiwa kuzinduliwa siku ya kuzindua kampeni.Mpekuzi jana ilishuhudia uwanja wa Jangwani ukifanyiwa usafi.

Magari ya ya kubeba mizigo yalionekana yakisomba taka na udogo uliokuwa ukichimbwa eneo hilo.

Lowassa Akwama Kuzindua Kampeni Baada ya Kukosa Uwanja wa Kutosha 'Mafuriko' Yake


Wakati mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli, akitarajiwa kuzindua kampeni zake kesho jijini Dar es Salaam, mgombea kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa amekwama kuzindua kampeni zake  kama ilivyotangazwa awali.

Ukawa unaoundwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), National Convention for Construction and Reform – Mageuzi (NCCR-Mageuzi), Chama cha Wananchi (CUF) na National League for Democracy (NLD) umeahirisha uzinduzi kutokana na kukosa mahali patakapotosha ‘mafuriko’ ya watu watakaohudhuria.

Lowassa alitarajiwa kufungua pazia kwa kuzindua kampeni zake kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa jijini Dar es Salaam, lakini serikali imekataza uwanja huo kutumika kwa kampeni za vyama vya siasa.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene, akiongea na waandishi wa habari Jumatano wiki hii, alisema serikali imefikia hatua hiyo kwa vile kusudio la ujenzi wa uwanja huo ni shughuli za michezo pekee na si vinginevyo.

Kampeni zinazoanza kesho  pia zitahusisha wagombea urais kupitia vyama vingine vya siasa vikiwamo ambavyo wagombe wake hawapewi nafasi kubwa ya kuibua ushindani kama itakavyokuwa ama kukaribia kwa CCM na Ukawa.

Pia kuanza kwa kampeni hizi kutawahusisha wagombea ubunge na udiwani watakaoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Afisa Habari wa Chadema iliyo mshirika katika Ukawa, Tumaini Makene, amesema kuwa, Lowassa anayewania Urais akiwa na mgombea mwenza Juma Duni Haji, ameahirisha kuzindua kampeni zake mpaka itakapotangazwa baadaye.

Alisema kuahirishwa kwa uzinduzi huo kunalengo la kutoa fursa kwa Ukawa kujiweka sawa hasa katika kupata uwanja wenye uwezo wa kuwajumuisha watu wengi na nafasi za kuegesha magari.

“Mgombea wetu hatazindua kampeni leo wala kesho, waache hao wengine waanze sisi tunajipanga kupata eneo zuri litakalotosha kwa idadi kubwa ya watu tunaowatarajia ikiwamo na maegesho ya magari,” alisema.

Makene alisema kutokana na uzeofu uliojionyesha wakati mgombea wao akitafuta wadhamini ama kutambulishwa mikoani, wanaamini kuwa mkutano wao utahudhuriwa na watu wengi, hivyo ni muhimu wakatafuta eneo kubwa la kutosha watu wengi na maegesho ya vyombo vya usafiri.
 
Wakati ikitarajiwa kuzindua kampeni zake kesho, CCM imeshatangaza kamati ya watu 32 kwa ajili ya kutafuta ushindi, ikiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahaman Kinana.

Kamati hiyo ilitangazwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, Jumanne  wiki hii ambaye alimuita Kinana kama mwanaharakati wa kivita anayefahamu medani za ushindi.

Uchaguzi wa mwaka huu ambao unatarajiwa kuwa na changamoto kubwa hasa kutokana na mgombea anayeungwa  mkono na Ukawa (Lowassa) akitokea CCM, kuonyesha upinzani mkubwa dhidi ya  CCM alichokuwa mwanachama wake tangu mwaka 1977.

Licha ya kuwa mwanachana, Lowassa ameshika nafasi tofauti ndani ya CCM na serikalini ikiwamo Uwaziri Mkuu aliojiuzulu mwaka 2008.

Lowassa alikuwa pia katika timu ya kampeni za mwaka 2005 ambapo Rais Jakaya Kikwete aliwania nafasi hiyo kwa mara ya kwanza na kupata ushindi wa kishindo.

Hata hivyo, Julai 29, mwaka huu, Lowassa aliamua kujiunga na Chadema ikiwa ni siku chache baada ya jina lake kukatwa katika hatua za awali za kuwachuja watia nia waliotaka kuwania Urais kupitia CCM.

Jumla ya makada 42 wa CCM walijitokeza kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea urais ambapo 38 walirejesha fomu na Magufuli aliibuka kuwa mshindi atakayegombea Urais katika ‘kumrithi’ Rais Kikwete.
 
Macho na masikio ya wapiga kura wengi kuanzia kesho yataelekezwa kwenye uzinduzi wa kampeni hizo kusikia sera za vyama hivyo vikubwa vinavyoshindana kumpata Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwanafunzi kidato cha II auawa akimwokoa mwenzake asibakwe


Mwanafunzi wa kidato cha pili wa Sekondari ya Nyasubi, Ally Jacob ameuawa baada kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni alipokuwa akijaribu kumwokoa mwanafunzi mwenzake asibakwe.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 9:00 alasiri maeneo ya Nyasubi, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. alikuwa akirejea nyumbani kutokea shuleni.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Justus Kamugisha alidai kuwa mwanafunzi huyo aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya shingoni na mwenzake anayesoma Sekondari ya Kishimba.

Kamugisha alisema sababu za Jacob kuuawa ni kujaribu kumsaidia mwanafunzi mwenzake mwenye umri wa miaka 16 (jina linahifadhiwa) ambaye anasoma kidato cha pili Sekondari ya Nyasubi ili asibakwe na mtuhumiwa ambaye alitaka kufanya unyama huo kwa kushirikiana na mkazi mmoja wa Nyasubi.

Alisema watuhumiwa wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.