Friday, October 23, 2015

Picha: Magufuli Ahitimisha kampeni za Urais Jangwani Jijini Dar........Wanafunzi Nao Walibebwa kujaza Uwanja

Mpekuzi blog
Wanafunzi  nao  walichukuliwa
Mpekuzi blog

Lowassa Awapigia Kampeni Wabunge na Madiwani wa CCM LEO

Mpekuzi blog

Kazi  yetu  ni  kupekua  na  kukujulisha  kinachoendelea  hapa  Tanzania  hasa  wakati  huu  wa  kampeni  za  uchaguzi.

Leo  mheshimiwa  Lowassa  alikosea  kidogo  na kujikuta  akiwanadi  wagombea  ubunge  na  udiwani  wa  CCM. 

"Nawaomba  jumapili  mnipe  kura  kwa  wingi, ila  msisahau  kuwachagua madiwani  na  wabunge  wa  CCM  ili  tuiondoe  CCM  madarakani"...Lowassa

Aliyasema  hayo  akiwa  katika  viwanja  vya   Shule ya Jangwani - Ifakara  mkoani  Morogoro.

Tazama  video  hapo  chini

Mpekuzi blog
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

CCM JIMBO LA MFENESINI ZANZIBAR YAFUNGA KAMPENI ZA 2015

1
Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharib Yussuf Mohd  Yussuf  akiwaonyesha Wananchi wa Shehiya ya Bumbwisudi mfano wa karatasi ya kupigia Kura kwa wagomebea Ubunge katika Mkutano uliofanyika Uwanja wa Bumbwisudi kwagoa Jimbo la Mfenesini.
2
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa  Magharib Yussuf Mohd  Yussuf  akimnadi mgombea Uwakilishi Jimbo la Mfenesini Machano Othman Said katika Mkutano uliofanyika Uwanja wa Bumbwisudi kwagoa.
3
Mgombea Uwakilishi CCM Jimbo la Mfenesini Machano Othman Said akizungumza na Wananchi wa Shehiya ya Bubwisudi na kuwaomba kura katika Mkutano uliofanyika Uwanja wa Bumbwisudi kwagoa.
4
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa  Magharib Yussuf Mohd  Yussuf  akimnadi mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Mfenesini Kanal mstaafu Masoud Ali Khamis katika Mkutano uliofanyika Uwanja wa Bumbwisudi kwagoa.
5
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Mfenesini Kanal mstaafu Masoud Ali Khamis akizungumza na Wananchi wa Shehiya ya Bumbwisudi na kuwaomba kura katika Mkutano uliofanyika Uwanja wa bumbwisudi kwagoa.
6
Aliyekuwa Mgombea Udiwani Wadi ya Bumbwisud kupitia ADC Makoe Makolea Mashimba akirudisha Kadi na kujiunga na CCM katika Mkutano wa kufunga Kampeni 2015 Uwanja wa Bumbwisud Jimbo la Mfenesini.
 (PICHA NA ABDALLA OMAR-MAELEZO ZANZIBAR).
0 Comments

MWANZA SHUGHULI ZA SIMAMA

Oct 23, 2015

Mvua kubwa katika Jiji la Mwanza na vitongoji vyake imewalazimu kusimamisha shughuli zao kwa Mvua iliyoanza kunyesha saa  11 Alfajiri hadi saa moja asubuhi  na kuendelea kunyesha 4 ya asubuhi na hadi sasa saa tisa Alaasri yaendelea kunyesha na kusababisha magari yanayo towa huduma katika Jiji hilo kusimama kutokana na mvua hizo na kusababisha shughuli  za  wafanya biashara ndogondogo wanao jiingizia kipato   kushindwa kufanya biashara kwa maeneo kujaa maji na mifereji kujaa maji, hadi sasa nikiandika  taarifa hii sijapata taarifa  yoyote inayohusu maafa au uharibifu wa mali, nitaendelea kuwaletea taarifa hii kupitia ujijirahaa blog, (NA RIPOTA WETU MWANZA UJIJIRAHAA) 

0 Comments

MAMA SAMIA ATUA MJINI ZANZIBAR, KUUNGURUMA NA DK. SHEIN LEO UWANJA WA DEMOKRASIA aka KIBANDA MAITI JIONI HII

Friday, October 23, 2015
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akishuka kwenye ndege baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege Mjini Zanzibar leo, kwa ajili ya mkutano wa kampeni utakaofanyika jioni hii kwenye Viwanja vya Demokrasia au Kibanda maiti
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Mume wake, Hafidh Ameir, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege mjini Zanzibar leo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai
 Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Mjukuu wake, Hamiar Ameir, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege mjini Zanzibar leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tikei ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Msanii wa Bongo Movie alioko katika kundi la kampeni za CCM la 'Mama Ongea na Mwanao' Wema Sepetu alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege mjini Zanzibar leo
Baadhi ya viongozi wa CCM wakisubiri kwa hamu kusalimiana na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege Mjini Zanzibar leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia baadhi ya viongozi alipowasili Uwanja wa Ndege Mjini Zanzibar leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia baadhi ya wasanii wa Bongo Movie alipowasili Uwanja wa Ndege Mjini Zanzibar leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar Vuai Ali Vuai (Kushoto), baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege mjini Zanzibar leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akifurahia ngoma alipowasili Uwanja wa Ndege Mjini zanzibar leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akitazama bidhaa za Kina mama Wajasiriamali, alipowasili Uwanja wa Ndege Mjini Zanzibar leo
 Vijana wakitumbuiza kwa muziki wa matarumbeata kumpokea Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili Uwanja wa Ndege mjini Zanzibar leo
 Baadhi ya waandishi wa habari waliopo katika msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM wakiwa katika gari lao wakati wa mapokezi ya Mgombea huyo, kwenye Uwanja wa Ndege mjini Zanzibar leo
 Bango la kumkaribisha Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia likiwa katika barabara ya Michenzani mjini Zanzibar
 Wazee Maarufu wakisubiri kumpokea Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Zanzibar leo
 Kina mama wakiwa na viavuli kumpokea Mama Samia kwenye Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Zanzibar leo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwa na Muavuli kuwaunga mkono Kinamama waliompokea kwa miavuli kwenye Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandu mjini Zanzibar leo
 Pikipiki zikiongoza Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan kuingia Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Zanzibar leo
 Msafara wa Mama Samia Suluhu Hassan ukiingia kwenye Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui Mjini Zanzibar leo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akisalimia baadhi ya viongozi baada ya kuwasili Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandu mjini Zanzibar leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Young Dee aeleza kilichosababisha akaachana na label yake ya zamani MDB

Young Dee ameelezea kwa uchungu kitu kilichosababisha akaachana na label yake ya zamani, Millian Dollar Boys (MDB) baada ya bosi wa kampuni hiyo, Max Rioba kudai amezingua.

Akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM jana, Young Dee alisema hakutaka kuzungumzia suala la Max kwakuwa anaheshimu mchango wake katika muziki wake.

Kama uliona nimekukosea, call me, I will apologize sio kwenda kuzungumzia Instagram,” alisema Young Dee.

Kwahiyo kilichotokea mimi sitaki kumjudge labda alikuwa na hasira. Lakini mimi najua mtu wa karibu ni rahisi kukuathiri kuliko mtu wa mbali. Hayo yote mimi namshukuru kwa mabaya aliyoona kwangu. Wewe unavyotaka mabadiliko sio kila mtu anataka mabadiliko kila kitu ni wewe kama wewe. Mimi namshukuru kama alikuwa kondakta ndio amefanya mabadiliko ya kwenda kumiliki daladala,” alisema Young Dee huku akilia.

Aliongeza, “Mimi sikutaka kusema nimeondoka, sikutaka iwe hivi kwa sababu miaka mingi mimi nimeshatoka kwenye label. Mimi hadi ngoma saa nyingine nalipia mwenyewe, video nyingine tofauti, kuanzia Sio Mchoyo, Fununu. Nagonga beat tu pale halafu najilipia kila kitu. Nyimbo nyingi nataja jina la MDB lakini sio wamelipia wao. Hata ngoma yangu mpya natarajia kuiachia inaitwa ‘Ujanja Ujanja’ nimewataja lakini hawajalipia.”

HUKUMU: Mahakama Kuu Yapiga Marufuku Watu Kukusanyika Baada Ya Mita 200

Mpekuzi blog
Mahakama Kuu Dar leo imetupilia mbali shauri la tafsiri ya sheria ya mpigakura kukaa au kutokaa umbali wa mitaa 200 kutoka eneo la kupiga kura.
 
Kwa mujibu wa majaji waliotoa maamuzi hayo wamesema kuwa, kwa kuwa mikutano ilishakatazwa kuwepo siku ya uchaguzi, hivyo hakuna mkutano, mkusanyiko au vikundi vyovyote vitakavyoruhisiwa siku hiyo na kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
 
Pia wameeleza kuwa siku ya uchaguzi mtu yeyote atakayevaa sare ya chama chochote naye atakuwa amevunja sheria.
 
Kwa upande wa wakili wa utetezi,  Peter Kibatala amesema ameyapokea maamuzi hayo lakini atakata rufaa juu ya shauri hilo kwa manufaa ya chaguzi nyingine zijazo.

Tundu Lissu ‘anusa’ bao la mkono Singida Mashariki


Mgombea ubunge wa jimbo la Singida mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu  Antiphas Mughwai Lissu, amesema kwamba anahofia uchaguzi mkuu  hautakuwa huru na wa haki akidai kwamba Jeshi la Polisi limeandaliwa kuhakikisha yeye hatangazwi kuwa mshindi.

Lissu alisema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mkoani humo ambapo alibainisha kuwa amepata taarifa kupitia njia ya simu kutoka kwa meneja  wa mkoa wa benki moja mjini hapa na askari polisi wawili, kwamba jeshi la polisi limeandaa nguvu kubwa kupindua maamuzi ya wapiga kura, ili mgombea wa CCM atangazwe mshindi

Tundu  Lissu ambaye ni Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, alisema kwa nyakati tofauti, alipigiwa simu na askari polisi wawili akiwemo wa FFU, na kumpa taarifa ile ile aliyopewa na meneja wa benki.

Alisema askari hao walimwambia kuwa jeshi la polisi litatumia magari matatu ya dareya (yanayotumika kumwaga maji ya kuwasha) na kundi kubwa la askari na kwamba wameagizwa na viongozi wao,wahakikishe liwalo na liwe, yeye (Tundu) hatangazwi kushinda ubunge.

Mgombea huyo alisema kwa akili ya kawaida, jeshi la polisi halipaswi kutuma nguvu kubwa jimbo la Singida mashariki ambalo toka kampeni zianze, hapajatokea tukio au dalili za uvunjivu wa amani.

Katika hatua nyingine, Tundu Lissu ameahidi kwamba endapo atashindwa kihalali, atakubaliana na matokeo na hatakuwa na kinyongo chochote.Lakini endapo atashindwa kwa mbinu chafu, hatakubaliana na matokeo hayo machafu.

Naye  Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, ACP Sedoyeka, alisema wamemtaka Lissu kwa kuwa ni mwanasheria, athibitishe tuhuma zake hizo, ndipo jeshi la polisi liweze kuchukua hatua stahiki.

Katika jimbo hilo  Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemsimamisha  Bw.Jonathan Njau kupambana na Tundu Lissu katika uchaguzi huu