Tuesday, July 14, 2015


RIHANNA AONYESHA KITUKO

Posted by GLOBAL on July 14, 2015 at 11:00am 0 Comments
Mwanadada mrembo mwimbaji wa RnB, Rihanna.
New York, Marekani

MWANADADA mrembo mwimbaji wa RnB, Rihanna, 27,juzikati alitokelezea akiwa amevaa shati kubwa na kuonekana kituko kwa watu wengi.
Mbaya zaidi, demu huyo asiyeishiwa na vituko, alikuwa amefungua vishikizo karibu vyote vya shati hilo huku akiwa hajavaa blazia, hatua ambayo ilisababisha sehemu ya matiti yake kuonekana.
Kingine ni kwamba nguo hiyo ni ya kiume lakini kumbe alikuwa akionyesha mtindo mpya wa…
Mwanadada mrembo mwimbaji wa RnB, Rihanna.
New York, Marekani
MWANADADA mrembo mwimbaji wa RnB, Rihanna, 27,juzikati alitokelezea akiwa amevaa shati kubwa na kuonekana kituko kwa watu wengi.
Mbaya zaidi, demu huyo asiyeishiwa na vituko, alikuwa amefungua vishikizo karibu vyote vya shati hilo huku akiwa hajavaa blazia, hatua ambayo ilisababisha sehemu ya matiti yake kuonekana.
Kingine ni kwamba nguo hiyo ni ya kiume lakini kumbe alikuwa akionyesha mtindo mpya wa mavazi.

DIRA YA DUNIA JUMATATU 13.07.2015

Posted by GLOBAL on July 14, 2015 at 10:07am 0 Comments

TAMASHA LA NCHI ZA JAHAZI 2015 KUFANYIKA NGOME KONGWE ZANZIBAR KUANZIA JULAI 18 HADI 26

Posted by GLOBAL on July 14, 2015 at 9:50am 0 Comments
 Mjumbe wa bodi wa Tamasha la Jahazi, Fatma Allo (kulia), akizungumza katika mkutano na wadau wa filamu na wanahabari Dar es Salaam leo jioni kuhusu tamasha la nchi za jahazi litakalofanyika kuanzia Julai 18 hadi 26 mwaka huu Ngome Kongwe mjini Zanzibar.Kutoka kushoto ni Meneja wa Tamasha, Daniel Nyalusy na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tamasha la Jahazi, Martin Mhando.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tamasha la Jahazi, Martin Mhando (kushoto), akizungumza kuhusu tamasha hilo kubwa la jahazi. Kulia ni  Mjumbe wa bodi wa Tamasha la Jahazi, Fatma Allo.…

TMT YAZIDI KUNOGA, WAWILI TENA WATOLEWA!

Posted by GLOBAL on July 13, 2015 at 6:00pm 0 Comments
Baadhi ya washiriki wa shindano la kuibua vipaji vya kuigiza la TMT wakiwa kwenye jua la utosi.
Majaji wa TMT kutoka kushoto ni Richie, Monalisa pamoja na Roy.
Washiriki waliotoka…

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya July 14

Mpekuzi blog























WALIOTUHUMIWA MAMLUKI CHADEMA WAVULIWA UONGOZI.


Na Bryceson Mathias, Kilosa.
NGUVU ya Umma ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Ruaha, Jimbo la Mikumi, Wilaya ya Kilosa, Morogoro, wamewavua Uongozi waliokuwa Viongozi wao na kuweka Kamati ya Muda (Task Force), kwa madai ya kuwa Mamluki ndani ya Chama chao.
Waliovuliwa Uongozi na kubaki na Uanachama ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kata, George Banda, Katibu, Ally Mponda, Katibu Mwenezi, William Temu, Mweka Hazina, Aurelia Mnunga, na Mjumbe wa Kamati Tendaji, Mwalimu Myami.
Katika Kikao cha ndani cha Julai 2 (Ukumbi wa Linas), kilichosimamiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mafunzo wa Chadema Taifa, Benson Kigaila; Baada ya kusikiliza ‘Tuhuma’ za Viongozi hao, aliwauliza wanachama wanataka nini, ambapo wote walipaza Sauti; Wavuliwe Uongozi na kubaki Wanachama!.
Aidha Tuhuma zilizoelekezwa kwa Viongozi hao, ni Kuwafukuza Viongozi wenzao Watatu wa Chadema, kwa kutumia Vifungu visivyokuwemo kwenye Katiba ya Chadema, ilihali wakijua ni kukinyang’anya Chadema Ushindi wake halali na kukifurahisha Chama Mapinduzi(CCM).
Nyingine ni Viongozi hao kuhamisha Vikao vya Chama, ambapo badala ya kufanyia kwenye Ofisi ya Chadema Kata, kwa Miezi zaidi ya Minne walihamishia Vikao na Ofisi kwenye Mgahawa wa mmoja wa Viongozi hao kinyume cha Katiba.
Kiongozi Mpya, Abasi Longa, alikiri kuchaguliwa Mwenyekiti wa Muda kati ya Viongozi waliochaguliwa na Wanachama; Hii ikiwa ni mara tu baada ya kumvua, Banda aliyekuwa Mwenyekiti, ambapo, Joram Zacharia, alithibitisha kuchukua UKatibu aliovuliwa, Mponda.
Mbali ya waliovuliwa nyadhifa kutotaka kuzungumza na Mwandishi hata walipopigiwa simu za Viganjani kuelezea walivypokea kuvuliwa Uongozi na kuwa Wananchama; Aliyekuwa Katibu, Mponda, pekee alikiri kuondolewa, akisema, “Siasa ni Kijiti, lazima tupokezana”.alisema
Hata hivyo, Longa alikiri kupokea Fomu za Viongozi watatu waliovuliwa Uongozi na kubaki Wanachama wa Chadema, Banda, Mponda na Mnunga, ambao wametia nia ya Udiwani wa Kata hiyo.
Awali Mponda, alimthibitia Mwandishi wa habari, kuhusu azma yake kutia nia ya kugombea Udiwani wa Kata hiyo wakiwemo Viongozi wenzake waliovulia Madaraka, jambo ambalo limeendelea kuwawatia Shaka Wana Chadema kuwa, huenda kulikuwa na kitu nyuma ya Pazia

LEO KWENYE KIKAO YUPO MH.LOWASSA MAKALA ZA LEO NYINGI ZITAMUHUSU YEYE TU

Mkutano wa Lowassa wazua taharuki.

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Mkutano wa Waandishi wa habari na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, uliotakiwa kufanyika jana nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam, umehairishwa, huku kukiwa na taharuki juu ya kile alichotarajiwa kukizungumza kwa umma na taarifa mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii zikizagaa.

Sababu za kuahirishwa kwa mkutano huo zinaelezwa kuwa ni kutokana na kuchelewa kufika kwa Lowassa akitokea mjini Dodoma.

Mapema asubuhi jana Waandishi wa Habari walitakiwa kufika nyumbani kwa kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM kwa ajili ya kuzungumza jambo ambalo halikuwekwa wazi.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari tangu majira ya saa 3:30 asubuhi, waliwasili nje ya nyumba hiyo na kuelezwa kuwa Lowassa bado hajafika na hivyo hakuna mkutano kama ilivyokuwa imetengazwa awali.

Taarifa mbalimbali zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na WhatsApp zilikuwa zikieleza kuwa nyumba ya kiongozi huyo imezingirwa na watu wa usalama wa Taifa kwa lengo la kuimarisha ulinzi, huku wengine wakidai kuwa anajiandaa ‘kutimkia’ upinzani baada ya kukosa nafasi ya Urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika mitandao hiyo kuna kiu kubwa ya watumiaji wake kutaka kusikia kauli ya kiongozi huyo baada ya jina lake kuenguliwa katika mchakato huo.

Lowassa alijizoelea umaarufu wakati akiwa Waziri Kuu, wizara alizoziongoza ikiwamo Wizara ya Maji, Maendeleo ya Mifugo, kutokana na umahiri wake wa kusimamia masuala mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, Msemaji wa Lowassa, Abubakari Liongo, alisema mkutano huo wa Waandishi wa habari ulipangwa kufanyika jana majira ya saa 5:00 asubuhi, lakini ulishindikana kutokana na kwamba walichelewa kuwasili kutoka mkoani Dodoma.

“Taarifa zinazosambaa kuwa nyumba ya Mheshimiwa imezingirwa na watu wa ulinzi siyo za kweli, na waandishi waliofika pale asubuhi waliona hilo, pia kuhusu kuhamia upinzani ni maneno ambayo watu wameamua kuyaandika na kusambaza ila hakuna ukweli wowote,” alisema.

Alisema Lowassa atazungumza na waandishi wa habari kama alivyokuwa amepanga, lakini ni baada ya kukamilisha baadhi ya mambo na kwamba kila chombo cha habari kitajulishwa.

Tangu kutangazwa kwa mgombea wa kupeperusha bendera ya chama hicho, Dk. John Magufuli, Julai 12, mwaka huu, Lowassa hajajitokeza mbele ya umma kuzungumza lolote, tofauti na wagombe wengine ambao tayari wametangaza kuunga mkono mgombea aliyepitishwa.

Katika mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma, Dk. Magufuli alimtangaza Mgombea mwenza ambaye ni Samia Suluhu Hassan.

Lowassa ni kada aliyetangaza nia ya kuomba ridhaa ya CCM kupeperusha Bendera ya chama hicho, lakini jina lake lilienguliwa katika hatua za awali za Kamati Kuu ya chama hicho ambayo ilitoa majina matano.

Baada ya Kamati Kuu kumaliza kazi yake majira ya saa 6 usiku na majina matano kujulikana, wajumbe watatu, Dk. Emmanuel Nchimbi, Adamu Kimbisa na Sophia Simba, walizungumza na waandishi wa habari kupinga maamuzi ya kamati hiyo na kwamba hawahusiki nayo.

Aidha, Julai 11, mwaka huu, Halmashauri Kuu ya CCM, ilikutana na kutoa majina matatu, huku katika mitaa mbalimbali kukiwa na maandamano ya wafuasi wa Lowassa, wakitaka jina lake kurejeshwa na kuwa miongoni mwa wanaoomba ridhaa ya chama hicho.

Shinikizo hilo lilisababisha majina matatu kutotajwa haraka, na Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, alipoingia ukumbi wa mkutano alipokelewa na nyimbo za kushinikiza jina la Lowassa kurejeshwa miongoni mwa majina yanayotakiwa kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano huo.

Kikwete alishindwa kuendelea na mkutano huo na kuahirisha kwa kile kilichoelezwa ni kutoa nafasi kwa wajumbe kwenda kupata chakula cha mchana, na waliporejea hali ilikuwa tofauti kwani hakukuwa na nyimbo zozote.

Katika mitaa mbalimbali ya mji wa Dodoma hasa karibu na Makao Mkuu ya chama, kulikuwa na maandamano ya baadhi ya wananchama huku wengine wakitambaa barabarani, kushinikiza jina la Lowassa kurejeshwa kuwa miongoni mwa wateule.

Maandamano hayo yaliwakusanya watu kwenye eneo la Nyerere Square wakiimba nyimbo za Lowassa kuwa ndiye raisi wao na kutawanywa na askari waliokuwa wameimarisha ulinzi mjini humo.
CHANZO: NIPASHE

POLE ILA NAAMINI NDIO SABABU HIZI

MAMBO 5 YALIYOMPONZ LOWASSA

Waziri Mkuu wa zamani na aliyekuwa mtangaza nia ya kugombea urais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania, Edward Lowassa akipokea fomu zilizosainiwa na wadhamini wake.
TAYARI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtangaza Waziri wa Ujenzi, John Pombe Joseph Magufuli kuwa mgombea urais mwaka huu huku Samia Suluhu Hassan akiwa mgombea mwenza, lakini bado jina la mgombea aliyekatwa, Edward Lowassa linazungumzika, safari hii yakibainishwa mambo matano yanayoolezwa ndiyo yalichangia kukatwa kwake.

Akizungumza na Uwazi juzi mjini hapa kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, mjumbe mmoja wa Halmashauri Kuu ya CCM-Taifa (Nec) alisema nguvu ya Lowasaa kichama ilikuwa kubwa lakini mambo hayo matano ndiyo yalisababisha akashindwa kufikia hata hatua ya Tano Bora.


“Sisi kama wajumbe, tunajua mengi. Lowassa alikuwa mgombea mwenye nguvu, alikuwa na watu ndani ya Nec, lakini sasa Kamati Kuu (CC) ilimkata kwa vigezo vyake, lakini naamini ndani ya hayo mambo matano ndiyo maana alikatwa.

MAKANISA, MISIKITI YATAJWA
Kwa mujibu wa mjumbe huyo kutoka Mkoa wa Tanga, kitendo cha Lowassa kuchagisha fedha kwa njia ya harambee kwenye misikiti na makanisa akiwa kama mgeni mwalikwa, kulichangia CC ya CCM kumwona kama alianza kampeni mapema.

“Unajua ndani ya makanisa mengi yanasemwa. Baadhi ya watu ndani ya chama chake walisema alianza kampeni mapema kwa vile kule kuzungumza na waumini kuliweza kumpa nguvu ya kisiasa. Hii nayo ilichangia,” alisema mjumbe huyo.

STAILI YA KUTANGAZA NIA
Mjumbe huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, jambo la pili ambalo lilimtia doa ya kuteuliwa Lowassa ni staili aliyoitumia kutangaza nia.

Alisema: “Unajua CCM inakataza kabisa mtu mwenye kutangaza nia kufanya vitendo vyovyote vyenye dalili ya kampeni. Lowassa alipoyakaribisha yale makundi ya kumshawishi kugombea na kuzungumza na vyombo vya habari pia ilikuwa ni kigingi kwake. Kama itakumbukwa kuwa, kuna wakati Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ilibidi aseme.”

KUFUNGIWA NA KAMATI
“Pia itakumbukwa kuwa, Februari 18, mwaka jana, Kamati Kuu ya CCM iliwafungia makada wake sita kwa kosa la kuanza kampeni mapema jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa chama.

“Lowassa alikuwemo, lakini wengine pia walikuwemo kama Bernard Membe (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), Januari Makamba (Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), William Ngeleja (Mbunge wa Sengerema), na Frederick Sumaye (waziri mkuu msatafu).

“Sasa, walipofunguliwa, Lowassa alionekana kama anaendelea kwa kitendo chake cha kuzungumza na wananchi kwa kupitia kigezo cha makundi kwenda kumshawishi,” alisema mjumbe huyo.

MATAJIRI, WAFANYABIASHARA WAKUBWA
Kitendo cha kudaiwa kuwa na ukaribu na baadhi ya matajiri na wafanyabiashara wakubwa ambao wanatiliwa shaka na baadhi ya wananchi pia kunatajwa kuwa sababu ya CC kuamua kumuweka kando Lowassa.

DOA LA RICHMOND
Licha ya mwenyewe kuwahi kusema mbele ya mkutano mkuu wa Nec wakati fulani kwamba, katika mchakato wa upatikanaji wa tenda ya kufua umeme kwa Kampuni ya Richmond, hakuna alilolifanya bila serikali kuu kujua lakini bado doa lile lililosababisha akajiuzulu uwaziri mkuu limeonekana kuwa kikwazo kwake.

“Ni kweli Lowassa alijiuzulu kwa sababu ya nafasi yake lakini si kwamba alihusika na ufisadi. Lakini nahisi iko haja kwake kuweka bayana kuhusu ule mchakato kwani baadhi ya wanasiasa wenzake wamekuwa wakitumia ishu ile kama jiwe la kumpigia.

“CC iliona kwamba, kama wangempeleka yeye kwenye kinyang’anyiro labda wapinzani wangetumia sakata la Richmond kujizolea kura kwa madai kwamba, Lowassa alijiuzulu kwa sababu hiyo,” alisema mjumbe huyo.

KUTOKA NDANI ZAIDI
Hata hivyo, pia kuna madai kwamba, wajumbe wa CC walimtafakari Lowassa kwa umakini na kugundua kuwa, alitakiwa kukatwa jina mapema kabla ya kuingia kwenye Tabo Bora.

“Kama Kamati Kuu ya CCM ingempitisha Lowassa kwenye Tano Bora, hakuna ambaye angemshinda mbele ya safari kwenye Nec na Mkutano Mkuu. Alikuwa na nguvu kubwa kwa wajumbe. Ndiyo maana wakamdhibiti kule mwanzoni kabisa,” kilisema chanzo kimoja na kuongeza:

“Lakini hata Nec na Mkutano Mkuu walipopelekewa jina la Magufuli walifurahia kwa sababu hana makundi ndiyo maana akazoa hizi kura 2104 na ndiye mgombea aliyepeleka hofu kwenye vyama vya upinzani (Ukawa) kwa sababu hana kashfa.”

KISA CHA KUKATWA MEMBE
Chanzo hicho kilisema kuwa, Bernard Membe ilibidi akatwe ili kutuliza upepo wa kisiasa ndani ya chama.
“Unajua Membe ndiye aliyekuwa mpinzani mkubwa wa Lowassa. Kuingia kwake kwenye Tano Bora na kuachwa Lowassa kusema kweli kulizua taharuki kubwa. Baadhi ya watu walikusudia kuibua uasi. Ndiyo maana ukawasikia wajumbe wakiimba wana imani na Lowassa wakati mwenyekiti wetu (Jakaya Kikwete) akiingia ukumbini.

“Ilibidi jina la Membe likatwe ili kambi ya Lowassa waone kifo cha wengi ni harusi na upepo mbaya ukatulia ndani ya chama la sivyo mpaka leo (Jumapili) kungekuwa bado Tano Bora iko mikononi mwa wajumbe wa Nec,” kilisema chanzo hicho.