Wednesday, July 22, 2015

"Watanzania nani aliyetuloga???"

Watanzania sisi tumekuwa watu wakulaumu na kujisahau,hivi ubongo wetu ni sawa na mnyama ngiri????ANAYE Jisahau kati kati ya mbio zakujiokoa na simba nakusimama eti kaona majani yaliyostawi anayoweza kuyatumia kama kitoweo??

Watanzania wengi tumeshuhudia dhihaka za chadema juu ya Lowasa,walimtuhumu fisadi tena kwenye majukwaa wakisema Lowasa ni fisadi mkubwa asiyestahili kufumbiwa macho,lema naye aliuwaminisha uma Lowasa ni fisadi papa anaye ujumu uchumi asiyestahili kuwapo katika dunia hii,kwa unafki na uzandiki mkubwaa leo hii wamerudi nyuma etii kumuomba ajiunge chadema hizi ni dharau na dhihaka kwa wananchi,hivi watanzania ni wasaaulifu kiwango hiki??NI Lini cdm walifuta kauli hizi chafu dhidi ya Lowasa??WAMETUDHALIIISHIA Mzee wetu tunasema imetosha wasimpake mafuta kwa mgongo wa chupa hawa ni wasaka tongee tu..

Wanamonduli,na ninyi nani aliyewaloga?CHADEMA Ndio iliyouaminisha umma Lowasa fisadi na tanzania yote ikaelewa hivyo, ikapelekea hata CCM kukata jina la lake kwa kuamini uzushi tulio aminishwa , ninyi tena mnarudi kujiunga na cdm???NI Nani aliyewaloga???HIVI Hamjui kukatwa kwa Lowaswa kumechangiwa na uzandiki wa chadema kwa asilimia (99.9)%?? Leo hii na ninyi mmegeuka kumsaliti mzee wetuu,narudia tena nani aliyewaloga??

Mh Lowasa tunaamini anaelewa chadema sio chama kisafi ndio kimechangia kukatwa kwa jina lake,atakuwa amefanya makosa sana kama atajiunga na chadema bado nitauliza Lowasa nani aliyekuloga???

CCM ni mbaya mbaya sana, chadema niwanafiki na wazandiki wasiostahili kufumbiwa macho hata kidogo,ningepata kukutana na mh Lowasa ningemshauri kwa kutunza heshima yake ni bora ajiunge na chama kisichokuwa na kashfa yeyote ile mfano act-wazalendo,kama itashindikana ni vema akabaki huko huko aliko kwa usalama wake na familia yake

By Kessy augustino
mwananch huru

No comments:

Post a Comment