Wednesday, November 22, 2017

Zanzibar na Njema Kwa Wageni na Wenyeji wa Zanzibar.

Watalii wanaofika kutembelea Zanzibar hupata fursa za kutembelea katika maeneo mbalimbali ya historia ya Zanzibar katika maeneo mbalimbali ya Visiwa hivi kama walivyokutwa Watalii hawa wakiwa katika maeneo ya mji mkongwe wa Unguja katika mitaa ya shangani wakipiga picha kwa ajili ya kumbukumbu jengo la Marcury shangani. 
Kaim Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamidu shaka muda Mchache uliopita alikuwa akiongea na waandishi wa Habari,akielezea mambo mbalimbali juu ya Umoja huo wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Kupitia mitandao mbalimbali ya Kijamii kama Facebook na Instagram katika Page zao za Uvccm Taifa.
Waziri Mwijage Aweka Jiwe la Msingi Katika Kiwanda cha Usambazaji Vifaa vya Ujenzi

Waziri Mwijage Aweka Jiwe la Msingi Katika Kiwanda cha Usambazaji Vifaa vya Ujenzi


WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijange, leo ameweka jiwe la msingi eneo la Tabata-Matumbi jijini Dar es Salaam ambapo kiwanda hicho kitakuwa kikisambaza vifaa vya ujenzi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwijage ameipongeza kampuni ya CNBM ya China kwa namna ambavyo imedhamiria kuwekeza hapa nchini kwa kuanzisha kituo cha usambazaji wa vifaa hivyo.

Alisema Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na serikali ya Tanzania itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wenye nia njema kwa serikali hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda.

Aliwapongeza pia watu wote wenye nia ya kuwekeza hapa nchini katika miradi mbalimbali ya viwanda kwa upande wa mazao kama vile muhogo, zao ambalo sasa ni muhimu na lenye kuweza hata kuuzika nje ya nchi.

Alisisiza kwamba kituo hicho kitawasaidia Watanzania kujipatia ajira na kuongeza ufanisi kwa vijana nchini kwa kunufaika na kituo hicho.

Naye Balozi mpya wa China hapa nchini, Bi Wang Ke, alimpongeza Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya CNBM, Song Zhiping, kwa kuanzisha kituo hicho ambacho kitakuwa muhimu
Makamu wa Rais wa Zimbabwe Akataa Kurudi Nyumbani

Makamu wa Rais wa Zimbabwe Akataa Kurudi Nyumbani


Wakati Emmerson Mnangagwa alipofutwa kazi wiki mbili zilizopita hakuwa makamu wa rais wa pekee nchini Zimbabwe
Phelekezela Mphoko ni makamu wa rais mwengine ambaye anajulikana kwa kumuunga mkono mkewe rais Mugabe na kulingana na sheria anapaswa kumrithi Mugabe.
Hatahivyo chama cha Zanu PF kimsema kuwa Mnangagwa ataapishwa kufuatia uamuzi uliochukuliwa na kamati yake kuu siku ya Jumapili.
Bwana Mphoko alikuwa ameondoka katika taifa hilo wakati Jeshi lilipochukua mamlaka wiki moja iliopita, na kulingana na gazeti la NewsDay hajarudi nyumbani kwa kuwa anahofia kukamatwa.
Gazeti hilo limenukuu duru akisema kuwa amebadilisha mipango yake ya usafiri.
Alitarajiwa kurudi nchini zimbabwe kufikia siku ya Ijumaa , kutoka Tokyo Japan.
Lakini duru zimesema kuwa anataka tiketi zake za usafiri kubadilishwa ili aelekee Zambia au Msumbiji .
Anajua anaogopa kukamatwa kwa sababu anatakikana kwa kuzuia haki na kufanya ufisadi.
Davina Awatetea Viben Ten " Mapenzi Hayachagui Umri"

Davina Awatetea Viben Ten " Mapenzi Hayachagui Umri"


LICHA ya wengi kuwaponda wanawake wenye umri mkubwa wanaokuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wadogo kiumri ‘viben’ten’, staa wa filamu za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ amewatetea kwa kusema siyo vibaya kwani mapenzi hayana umri.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Davina alisema licha ya kutowahi kuwa na kiben’ten, haoni tatizo kwa wanaokuwa na uhusiano na wanaume hao wadogo kwa kuwa siku zote mapenzi hayachagui umri, dini wala kabila bali mtu hujikuta amependa tu.

“Sijawahi kuwa na kiben’ten huwa naona ni bora kuwa na mtu ambaye tunalingana kiumri au amenizidi kidogo, wanawake wanaokuwa na wanaume hao wadogo siwezi kuwalaumu au kuwacheka kwa sababu mapenzi ni kitu ambacho hakizuiliki wala hakichagui,” alisema Davina.

Dr. Luis Shika kalipwa tena kuuza sura, sasa ni kwenye hii video ya Bongofleva (+video)


Kuna picha zilisambaa juzi kati zikimuonyesha Dr. Luis Shika akiwa na Warembo kwenye kiwanja kimoja cha starehe huku akiwa anakunywa Zanana Juice, sasa imethibitishwa kwamba ile ilikua ni video ya Bongofleva inatengenezwa.
Director Khalfan ambae ndio fundi wa hiyo video ameithibitishia AyoTV na millardayo.com kwamba Dr. Luis Shika amelipwa ili atokee kwenye hiyo video ya Msanii wa Bongofleva ambae alisema hawezi kumtaja kwa sasa.
Hili linakua dili la pili kwa Dr. Luis Shika kulipwa ili kuuza sura ambapo dili la kwanza lilikua ni tangazo la SOKA BET ambako pia alilipwa na kampuni hiyo ilithibitisha kufanya hivyo

Paul Makonda Aibuka Ofisi za Clouds Media Kuwapa Pole


Clouds Wameandika haya Baada ya Paul Makonda Kuwatembelea Kuwapa Pole:
...
"Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, ikiongozwa na RC Paul Makonda wamefika hapa #Mjengoni - #CloudsMediaGroup kutupa pole na kujionea athari zilizosababishwa na moto uliozuka jana asubuhi katika Ofisi zetu hapa Mikocheni. .
.
Tunashukuru kwa yote, tuko salama"

Picha za Irene Uwoya kwenye kaburi la Ndikumana



Mume wa zamani wa Mwigizaji Irene Uwoya, Hamad Ndikumana alifariki ghafla wiki iliyopita huko Rwanda sekunde chache baada ya kuomba soda ya baridi na kunywa ambapo Irene alifanikiwa kusafiri mpaka kwao kwenda kutoa pole kwa familia.
Kwenye hizi picha hapa chini anaonekana akiwa nyumbani kwa kina Ndikumana na ndugu zake na juu ya kaburi la Ndikumana pia ambapo chini mwishoni kuna video fupi ikimuonyesha Irene akipewa baraka na Baba Mzazi wa Ndikumana
Uwoya akiwa na Familia ya Ndikumana
Baada ya taarifa hizo Irene Uwoya alifunga safari baadae na kwenda kutoa pole kwa familia ya Ndikumana ambapo ameonekana akiwa na Mtoto wao Krissh juu ya kaburi la Ndikumana na kuandika “My trust is in you …R.I.P baba krissh”