Tuesday, June 9, 2015

Diamond Platnumz Follows Dr.Dre And 50 Cent's Footsteps By Launching His Own Headphones.

g

Diamond Platnumz is following footsteps of American big names like Dr. Dre, DJ Khalid and 50 Cent in the headphone and earphone business as he is all set to launch his own. 
 
Through his instagram today the east African music superstar revealed at while wishing supermodel Flaviana Matata happy birthday. He will officially launch his headphone at the end of this year. Congratz to him. be inspired

Urais 2015: Chama cha ACT – Wazalendo kutoa fursa kwa watangaza nia



Chama cha ACT-Wazalendo kintarajia kutoa fursa kwa watangaza nia wa nafasi mbalimbali katika mkutano wake wa kitaifa utakaofanyika tarehe 13 mwezi huu.
 
Hatua hiyo inafuatia joto la urais kuanza kupanda ndani ya vyama mbalimbali vya kisiasa nchini kikiwemo chama tawala cha Mapinduzi (CCM).
 
Kwa mujibu wa Katibu Mawasiliano na Uenezi wa Chama wa ACT –wazalendo  Sabini Richard amesema chama hicho kimejipanga kushiriki katika uchaguzi mkuu hivyo kutakuwa na mkutano mkuu utakaofanyika mkoani Tabora.
 
Katika mkutano huo   watahuisha azimio la Arusha  lengo likiwa ni kudumisha misingi ya amani, udugu na uzalendo kwa lengo la kuwaunganisha watanzania pamoja na kuenzi harakati za ukombozi barani Afrika.
 
Katika hatua nyingine, Richard amesema katika mkutano huo hicho wanatarajia kusimamisha wagombea katika nafasi ya Urais na Wabunge na madiwani katika majimbo yote nchini.
mpekuzi blog

Afya ya mke wa rapper Mabesste, Lisa Karl Fickenscher imeanza kuimarika kutokana na hivi karibuni kuwa mbaya.

Lisa anasumbuliwa na tatizo la moyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mabeste ameamua kutoa taarifa za maendeleo ya mke wake: Aje u good? Hey Maendeleo ya Lisa Lisa Karl Fickenscher OR My Wife kiafya Anaendelea vizuri Namshukuru saaana MUNGU pili na kushukuru wewe pia thanks saana Weekend njema.”

Pia Mabeste aliweka picha nyingine akitoka shamba na mke wake na kuandika: Ndio twatoka shamban sahii Mungu endelea kubariki My family.”

Mabeste aliamua kuomba msaada kutoka kwa watu mbalimbali ili kumsaidia kupata fedha za matibabu ya mke wake huyo.

Kila mtu anaamini kuwa Jokate Mwegelo na Alikiba ni mtu na mpenzi wake japo wao hawajathibitisha hilo rasmi licha ya kupost tu picha zao kwenye Instagram na hivyo kukuza zaidi tetesi hizo.

Lakini hatimaye Jokate amefunguka kwa mara ya kwanza kupitia mahojiano yake na Global TV.


  • “Ni kwasababu Alikiba anapenda sana muziki na anajua muziki na anajua style mbalimbali. Halafu ukitaka kuwa the best you obviously need to be around with the best,” alisema Jokate kujibu swali la uhusiano alionao na King Kiba.



  • “Mimi kwanza ni mchanga, kwahiyo nakaa naye karibu ili niweza kujijenga kimuziki, that is it.”

Kina Sheikh Farid Wagoma Kuingia Mahakamani.


Katika halia isiyo ya kawaida, Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho ya Mihadhara ya Kiislamu (Jumiki) visiwani Zanzibar, Sheikh Ahmed Farid na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya kula njama na kujihusisha ya ugaidi nchini waligoma kushuka kwenye basi la magereza ili kuingia mahakamani jana kutokana na hatma ya upelelezi wa kesi yao kutojulikana.

Washtakiwa hao walifikishwa kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam saa 2:50 asubuhi kwa ajili kusikiliza kesi yao iliyopangwa kutajwa jana.

Kabla ya mgomo huo, washtakiwa hao wanaotoka visiwani Zanzibar, waliiomba mahakama kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kuwatembelea mahabusu kwa ajili ya kusikiliza kero zao kuhusiana na kushitakiwa kwao katika mahakama za Tanzania Bara badala ya mahakama za kwao, Zanzibar.

Viunga vya mahakama hiyo vilifurika askari kanzu na wenye sare za Jeshi la Polisi pamoja na wa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kuimarisha ulinzi.

Hata hivyo, baada ya kufikishwa mahakamani hapo washtakiwa wote 23 waligoma kushuka kwenda kusikiliza kesi yao kwenye ukumbi wa mahakama hiyo.

Saa 4:56 asubuhi, mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Renatus Rutatinisibwa, huku upande wa Jamhuri ukiongozwa na mawakili wa serikali, Peter Njike na George Barasa, wakisaidiana na wakili wa serikali mwandamizi, Tumaini Kweka.

Wakili Njike alidai kuwa washtakiwa wamegoma kushuka kwenye basi la Jeshi la Magereza tangu wafikishwe mahakamani hapo kutoka mahabusu.

Wakili wa utetezi, Abdallah Juma, alidai kuwa upande wao hauna taarifa kuhusiana na  washtakiwa kugoma kuingia mahakamani na kwamba, upande wa Jamhuri ndiyo una wajibu wa kujua chochote kuhusu washtakiwa waliopo mahabusu.
 
Wakili Kweka, alidai kuwa askari magereza wamefanya juhudi za kuwataka washuke kwenye basi ili kuingia mahakamani lakini imeshindikana.

Mheshimiwa, Mei 25 mwaka huu, mahakama yako ilitoa amri kwamba kesi hii itatajwa leo… Jamhuri tunaomba washtakiwa wahesabike kwamba hawajafika mahakamani. Pamoja na kwamba wapo katika viunga vya mahakama, tunaomba mahakama itoe amri wapangiwe tarehe nyingine na wafike mahakamani,” alidai Wakili Kweka wa upande wa Jamhuri.

Hakimu Rutatinisibwa alisema mahakama haiwezi kuwafuata washtakiwa nje ya ukumbi unaoendesha shughuli zake na kwamba, (mahakama) inaendesha kazi zake kwa mujibu wa sheria, hivyo inaahirisha kesi hiyo hadi Juni 18 mwaka huu itakapotajwa tena.

Mbali na Sheikh Farid, watuhumiwa wengine ni Noorid Swalehe, Ally Hamis Ally, Jamal,   Nassoro Hamad, Hassan Bakari, Ahtari Humoud, Mohamed Isihaka, Abdallah Hassan,  Hussein Mohamed,  Juma Sadala,  Said Kassim,  Hamis  Amour,  Abubakar Abdallah, Salum Ali, Salum Amour, Alawi Othuman, Rashid Ally, Amir Hamis, Kassim Salum na Said Shehe pamoja na wenzao.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manne likiwamo la kula njama ya kuingiza watu nchini kushiriki katika vitendo vya ugaidi,, kusaidia na kuwezesha kufanyika vitendo hivyo.

Ilidaiwa kuwa kati ya Januari 2013 na Juni 2014, washtakiwa hao kwa pamoja walipanga njama ya  kutenda makosa hayo ya kula njama za kusaidia na kuwezesha kufanyika vitendo vya kigaidi.

Ilidaiwa kuwa  katika kipindi hicho na maeneo tofauti nchini,  Sheikh Farid na Sheikh Mselem Mselem waliwaingiza Sadick Absaloum na Farah Omary nchini ili kushiriki kutenda makosa ya ugaidi.

Shekh Farid anadaiwa kuwa katika kipindi hicho, akiwa anajua kuwa Sadick na Farah wametenda makosa ya kigaidi, aliwahifadhi.

Baaada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

Lowassa Apata Mapokezi Makubwa Geita.......Azoa Wadhamini 3,000

Mpekuzi blog

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana aliingia wilayani Geita na kupokewa na umati wa wananchi ambako alidhaminiwa na zaidi ya wana CCM 3,000.
Kaimu Katibu wa Wilaya ya Geita, Killian Balindo alisema waliotakiwa kumdhamini Lowassa katika wilaya hiyo ni wanachama 45, lakini waliojitokeza wamefikia zaidi ya 3,000.
 
Akizungumza na wananchi waliokusanyika mbele ya ofisi ya CCM Mkoa wa Geita, Lowassa alisema japo haruhusiwi kufanya kampeni ameahidi kushughulikia matatizo ya maji, wachimbaji wadogo na mawe yaliyoisha dhahabu (magwangala).
 
“Hayo ya bodaboda, mamantilie kushughulikia. Nikiingia ikulu ni kuweka tu kalamu nyekundu. Kazi yangu ikikamilika nitashughulikia magwangala,” alisema Lowassa.
 
Kuhusu wachimbaji wadogo, alisema atawapa kipaumbele kwa kuwamilikisha maeneo ya uchimbaji na mitaji.
 
“Nilipokuwa mbunge miaka ya 80, niliondoa shilingi bungeni kupinga wachimbaji wadogo kunyanyasika. Nitahakikisha kila mchimbaji anapata eneo lake. Serikali inajua maeneo yote yenye madini. Halafu tutawapa fedha ili wawekezaji wakubwa wakija waweze kushindana,” alisema Lowassa.
 
Msafara wa Lowassa ulikuwa na magari, pikipiki na baiskeli huku ikisindikizwa na helikopta ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Msukuma.
 
Awali Lowassa jana aliingia katika Jimbo la Chato linaloshikiliwa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli na kupata mapokezi makubwa ya wanachama waliojitokeza kumdhamini.
 
Dk. Magufuli ambaye pia amechukua fomu za kugombea urais bado hajafika jimboni humo kutafuta wadhamini.
 
Lowassa aliingia Chato saa 8:30 mchana na kuelekea kwenye ukumbi wa ofisi ya CCM wilaya walikokuwa wamekusanyika wana CCM.
 
Akizungumzia udhamini huo, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilayani humo, Deusdedith Katwale, alisema wanachama waliojitokeza kumdhamini wamefikia 430.
 
“Tunashukuru kwa kuipa kipaumbele Chato, hiyo ina maana sana siku zijazo,” alisema Katwale.
 
Naye Lowassa aliwashukuru wanachama hao na kurudia wito wake wa kuchagua rais aliyebobea katika chama.
 
“Tunakwenda kuchagua rais, tutafute mtu anayekijua chama. Angalieni historia yake na rekodi ya mambo aliyofanya,” alisema Lowassa.
 
Awapongeza  wana Pemba
Awali akiwa kisiwani Pemba jana asubuhi, Lowassa amewasifu wanachama wa CCM kisiwani Pemba kwa kujiimarisha dhidi ya upinzani mkali wa Chama cha Wananchi (CUF).
 
Tangu kuanza kwa siasa za upinzani mwaka 1995, CCM imekuwa katika wakati mgumu visiwani Zanzibar, na hasa Pemba.
 
Akizungumza na wana CCM wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba alikokwenda kutafuta udhamini kwa ajili ya kupitishwa kugombea urais kupitia chama hicho, Lowassa alisema wana CCM kisiwani humo wanastahili pongezi.
 
Alisema alifika kisiwani humo mara ya mwisho mwaka 1984 na kwamba akifanikiwa kupata urais atafanya ziara ya muda mrefu kisiwani humo.
 
“Nilifika hapa mwaka 1984 na sijawahi kurudi tena. Lakini endapo nitafanikiwa safari yangu, nitakuja siku mbili tatu tuzungumze.
 
“Nawapongeza kwa jitihada zenu, licha ya upinzani mkali wa CUF bado mmeendelea kujiimarisha. Nitakuja Pemba siku mbili tatu nitakapofanikiwa ili tuzungumze,” alisema.
 
Lowassa pia alizungumza na wana CCM wa Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba na kuwapongeza kwa jitihada zao za kukilinda chama chao licha ya upinzani mkali.
Lowassa alifanikiwa kupata udhamini wa wana CCM 90 katika wilaya za Wete na Micheweni Mkoa wa Kaskazini.
 
Akizungumzia hali ya chama hicho wilayani Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, mmoja wa makada wa CCM, Juma Amir Juma alisema wanachokitegemea ni rehema za Mwenyezi Mungu.
 
“Hatusemi tutaendelea kushindwa, Mungu ni mkubwa ipo siku tutashinda. Lakini hali ni mbaya sana, kwani kama Mbunge wa CUF anapata kura zaidi ya 5,000 wa CCM anapata kura 500, wapi na wapi? Lakini hatukati tamaa,” alisema Juma.
 
Katibu wa CCM mkoa wa Kaskazini Pemba, Ali Haji Makame, alisema kuna wana CCM wengi walitamani kumdhamini Lowassa, lakini wameshindwa kutokana na idadi maalumu kuwekwa na kanuni za chama hicho ambayo ni wanachama 45 kwa kila wilaya.
 
Lowassa aliwasili Zanzibar juzi na kupokewa na umati mkubwa wa wanachama wa CCM walioandamana naye hadi katikati ya mji wa Unguja.
 
Kwa ujumla Lowassa amepata wadhamini 450 katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Shilole kumzalia Nuh Mziwanda?

Mpekuzi blog

Msanii wa muziki nchini Tanzania Nuh Mziwanda, baada ya kuvuka kiunzi cha skendo ya kumpachika mimba binti na kumkana hadharani, jambo ambapo lilipelekea msukosuko katika penzi lake na mpenzi wake Shilole, hatimaye atamka hadharani mipango yake ya kuazaa na Shilole.
 
Akihojiwa  na eNews  ya  EATV  Mziwanda amesema kuwa yeye na Shilole, wanapenda sana kupata mtoto wao, ila anafahamu kuwa hiyo ni mipango ya Mungu na wakati wowote kutoka sasa ikitokea baraka hiyo watafurahi.
 
Amedai kuwa Mungu akiwajalia kuwa na mtoto furaha yao itaongezeka kwa kuwa kila kitu Mungu ndio mpangaji na kusema kuwa bado yupo kwenye mipango ya ndoa baada ya kutambulishana kwa wazazi.

Profesa Tibaijuka Azomewa kwao na Wananchi Mbele ya Kinana


Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka jana alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuzomewa na wananchi wa jimbo lake mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. 
 
Hali hiyo ilijitokeza jana asubuhi katika Kata ya Nshamba wilayani hapa wakati msafara wa Kinana ulipofika kuzindua mradi wa maji. Kadhia hiyo ilianza baada ya Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera, Ally Idd Ame kumkaribisha mbunge huyo ili awasalimie wananchi. 
 
Hata hivyo, wananchi hao walianza kuzomea kwa zaidi ya sekunde 40 wakipinga Profesa Tibaijuka kupanda jukwaani, hali iliyomlazimu Mkuu wa Wilaya, Francis Isack kupanda jukwaani na kutoa kauli ya kiutawala ili kuwanyamazisha wananchi hao.
 
“Anayetaka kusikiliza abaki na asiyetaka aondoke,” alisema Isack na kuwanyamazisha mamia ya wananchi hao. Baada ya kauli hiyo wananchi walitulia na kuruhusu Profesa Tibaijuka kupanda na kuhutubia kwa muda.
 
“Kama hamnitaki siyo lazima niwe mbunge wenu, mnaruhusiwa kubadili. Huyo aliyewapa viroba asubuhi hii ili mje mnitie aibu mbele ya katibu mkuu wa chama nawaambia hiyo dhambi itawatafuna,” alisema.
 
Aliwaambia wananchi hao kuwa anachokifanya ni kuwatumikia na kuwaletea maendeleo, hasa wanawake...
 
“Mimi sitafuti kazi na wala sina njaa... na kama hela ya kula ninayo. Mimi sigangi njaa na kama mnataka kuwa na kiongozi mganga njaa muwekeni muone atawasaidia vipi,” alisema.
 
Akihitimisha salamu zake kwa wananchi hao alisema kama wana jambo lao la ziada walifanye lakini wamuache aendelee na jitihada za kuwaletea wanawake maji... “Sina kinyongo na yeyote kwa sababu “I am too sophisticated (mstaarabu). Nipo juu ya mambo madogomadogo yanayowasumbua.”
 
Mbunge huyo ambaye hivi karibuni aliondolewa uwaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutokana na kashfa ya Tegeta Escrow, alimweleza Kinana kuwa eneo hilo limekumbwa na upinzani kutoka kwa mtu anayehitaji kulichukua ambaye ni kutoka ndani ya CCM.
 
Profesa Tibaijuka alisema katika ubunge wake amefufua mradi huo wa maji utakaogharimu Sh200 milioni kupitia shirika moja ambalo mkandarasi wake ni wa Umoja wa Mataifa na utekelezaji umeanza miezi minne iliyopita lakini unahujumiwa.
 
“Mradi huu wa Nshamba unahujumiwa na wapinzani wangu kutoka ndani ya CCM na vyama rafiki vya kisiasa, lakini lengo lao ni kunidhoofisha kisiasa, jambo ambalo linadidimiza maendeleo,” alisema Profesa Tibaijuka ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN – Habitat).
 
Kinana na kahawa
Katika ziara hiyo, Kinana aliitaka Serikali mkoani Kagera kusimamia wakulima kuuza kahawa ndani na nje ya nchi ili wanufaike badala ya kuwahusisha na magendo.
 
Kinana alisema wakulima wanahitaji kunufaika na kahawa yao kwa kuwa Serikali haitoi pembejeo kwa zao hilo, hivyo wauze kahawa yao hata kama ni nje ya nchi ilimradi wasivunje sheria
 
Alisema Serikali haina budi kurekebisha sheria za uzalishaji wa zao la kahawa zilizotungwa enzi za ukoloni inayotaja kuwa mkulima akizalisha zao la biashara linakuwa ni mali ya Serikali, jambo ambalo ni kumnyanyasa.
 
Alivitaka vyama vya ushirika kuepuka ukiritimba wa kutoa bei ndogo ya mazao ya wakulima na kutaka wanapowachagua viongozi wa ushirika, waangalie walio na uadilifu katika matumizi ya fedha.
 
Fedha za Mwenge
Akiwa katika visiwa vya Bumbire na Mazinga, Kinana aliitaka Serikali kusitisha uchangishaji wa fedha za Mwenge ambao hautawafikia wananchi, akisema kitendo hicho ni kuwanyanyasa na kuwadhulumu.
 
“Uchangiaji wa mafuta ya Mwenge ni wa hiari, si  kuwalazimisha wananchi na kusababisha Serikali kutoaminiwa na mkichangisha fedha hakikisha Mwenge huo unafika kwa wananchi wa eneo husika,” alisema Kinana.
 
Aliitaka Serikali ihakikishe inawalipa posho askari wake wanaoimarisha ulinzi na usalama majini na nchi kavu badala ya kuwatoza fedha wananchi kuchangia vyombo hivyo vinapokuwa vikitimiza majukumu ya kiserikali visiwani.