Master J Aeleza Kwanini Aliachana na Mke Wake ‘Watu Waelewe tu Kuwa ni Bonge la Mwanamke’
Master J ameamua kuweka wazi sababu za kuachana na mke wake aliyezaa naye watoto watatu wa kike.Akiongea kwenye kipindi cha Mkasi wiki hii, producer huyo mkongwe alidai kuwa pamoja na ndoa yao kufa, mke wake ni mwanamke wa pekee.
“Wewe unaweza kuwa mtu mzuri na yeye anaweza kuwa mtu mzuri lakini when it comes to the matters of the heart ikawa inashindikana,” alisema. “Lakini sio kwamba mtu mmoja yeye ni mbaya, mimi ni mzuri zaidi, hapana. Watu lazima waelewe I can’t take away from her – ni bonge la mwanamke. Anajiheshimu and she is a good mom. Ni basi tu kwamba we were different.”
Hata hivyo Master J amekiri kuwa mke wake na wanae hawajatoa baraka zao kwa uhusiano wake na Shaa.
“Hiyo issue ngumu sana mpaka sasa hivi,” alisema J. “Unajua hii issue inawatesa sana watoto, separation yoyote watoto ndio wanaoteseka, kwahiyo najitahidi sana kuwa nao karibu, tunawasiliana everyday whenever I get time, tunahang out, lakini haijafika stage kwamba tunahang out kihivyo.”
Master Jay Akiwa na Watoto Wake |
Master anadai kuwa kipindi suala hilo limetokea na vyombo vya habari kutaka kujua kutoka kwake alipata shida kuzoea na ilimsumbua.
“Kwa utamaduni wetu sisi hapa Tanzania ni issue nzito sana. Watu kama ndoa imeshindikana wako tayari wakae tu kwenye hiyo ndoa mpaka siku Mungu akikuita but it’s not healthy.”
No comments:
Post a Comment