Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya
Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa makampuni ya
StarTimes barani Afrika akiwasili katika Jengo la Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete lililopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako
amewatembelea wagonjwa wa moyo leo. Kanu atakiwepo nchini kwa muda wa
siku tano kushiriki shughuli mbalimbali za kampuni na kijamii.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo, Dk
Peter Kisenge katika taasisi hiyo akimkaribisha Nwankwo Kanu Ambaye pia
ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika. Kanu atakuwepo nchini
kwa muda wa siku tano kushiriki shughuli mbalimbali za kampuni na
kijamii.
Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa
makampuni ya StarTimes barani Afrika akimsikiliza Daktari bingwa katika
Taasiai ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Dk Peter Kisenge wakati akitoa taarifa fupi ya taasisi hiyo
Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa
ya Nigeria, Nwanko Kanu akifafanua jambo kwa madaktari wa taasisi ya
moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo hospitali ya taifa ya Muhimbili wakati
alipotembelea hapo
Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa
ya Nigeria, Nwanko Kanu akimsikiliza mmoja wa madaktari wakati
alipotembelea katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo huku madaktari wa hospitali hiyo
wakifuatilia mazungumzo hayo.
Mmoja wa wagonjwa katika Taasisi ya Moyo
ya Jakaya Kikwete ya hospitali ya taifa ya Muhimbili mtoto Mariam Omary
akifurahi baada ya kupata fursa ya kutembelewa na kujuliwa hali na
aliyekuwa mchezaji nyota wa nigeria, Nwanko Kanu ambaye kwa sasa ni
balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika.
Fatuma Shaban akipokea zawadi kutoka kwa
aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Nigeria na kwa sasa ni
balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika Nwankwo Kanu kwa niaba ya
mtoto wake, Ramadhan Shaban ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo kwenye
taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili.
Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya Taifa
ya Nigeria Nwanko Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa makampuni ya
StarTimes barani Afrika akizungumza jambo na madaktari katika chumba cha
wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) alipotembelea taasisi ya
moyo ya Jakaya Kikwete ya hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Aliyekuwa mchezaji nguli wa timu ya taifa
ya Nigeria au Super Eagles, Nwankwo Kanu ambaye pia kwa sasa ni balozi
wa makampuni ya StarTimes barani Afrika leo ametembelea Taasisi ya Moyo
ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
kwa lengo la kujua ni jinsi gani taasisi hiyo inafanya kazi pamoja na
kuwajulia hali wagonjwa wa moyo waliolazwa katika Taasisi hiyo. pia
Akizungumza baada ya kuwasili katika
Taasisi hiyo Kanu ameelezea kuguswa na tatizo la ugonjwa wa moyo hasa
kwa watoto wadogo ambao amewatembelea na kuahidi kubadilishana uzoefu
kuhusu huduma za matibabu zinazotolewa na wataalamu wa tasisi hiyo.
“Tatizo la moyo ni kubwa sana kwa sasa na
limekuwa likiongezeka kwa kasi lakini cha kusikitisha ni kuwa sio kila
mtu anaweza kumudu gharama za matibabu yake. Hivyo basi kuna umuhimu
mkubwa sana kwa serikali na wadau wengine kuanzisha vituo maalumu kama
hivi ili kuwasaidia wasiojiweza.” Alisema Kanu
Katika mazungumzo yake mchezaji huyo wa
nyota wa zamani ambaye aliwahi kuwika na vilabu kama vile vya Arsenal,
Ajax na Inter Milan, amesema kuwa pamoja na kuja kwa shughuli mbalimbali
kama balozi wa kampuni ya StarTimes lakini pia ana nia ya kushirikiana
na watalaamu wa Taasisi hiyo ya Moyo. Alielezea kuwa lengo ni kuwasaidia
matibabu watoto wenye matatizo ya Moyo ambao wazazi wao hawana uwezo na
kwamba watazungumzia suala hilo.
“Nimefarijika sana kuona serikali ya watu
wa Tanzania inachukua hatua stahiki katika kuwasaidia wananchi wake.
Pia ningependa kuchukua fursa hii kuwataka watanzania hasa wanamichezo
kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara kwani ukijua tatizo
mapema ni rahisi kupata matibabu na kupona. Tumeona mifano michache ya
wachezaji maarufu mbalimbali barani Afrika na kwingineko duniani
wakifariki au kunusurika kufa wakiwa katika ya mchezo kutokana na
kutoweka wazi mustakabali wa afya zao.” Alihitimisha balozi huyo wa
StarTimes barani Afrika
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa
Upasuaji kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dkt.
Godwin Godfrey amelezea kuwa tangu Julai mwaka jana mpaka sasa tasisi
hiyo kwa kushirikiana na wataalam kutoka nje ya nchi wamewafanyia
upasuaji watoto zaidi ya 200.
Nwankwo Kanu mbali na kujizolea umaarufu
na heshima kubwa katika medani za soka barani Afrika na Ulaya yeye pia
alifanyiwa upasuaji wa moyo mwaka 1996 na ndipo alipoamua kufungua
taasisi yake ya moyo inayoitwa “The Kanu Heart Foundation.”
Taasisi yake hiyo iliyoko nchini Nigeria
ambako ndiko alipozaliwa aliianzisha kwa madhumuni makubwa ya kusaidia
wenye matatizo kama yake na ameahidi taasisi hiyo kushirikiana na
taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika masuala mbalimbali