Monday, July 6, 2015

Habari nilizopata sasa hivi ni kuwa kuna mpango wa haraka unaandaliwa ili kutengua adhabu iliyotolewa kwa wabunge zaidi ya 35 kutohudhuria vikao vya Bunge.

Sababu hasa ni kuwa inavyoonyesha ni kuwa hata wale ambao hawana hiyo adhabu nao wameamua kususia ili kuwaunga mkono wenzao na jambo hilo litakuwa la aibu sana kwa Bunge na Rais kuhutubia wabunge wa CCM Pekee ilihali nchi inajinadi katika jumuia ya kimataifa kama ya demokrasia ya vyama vingi.

Ikumbukwe pia hotuba ya kuvunja bunge kwa JK itakuwa kama ya kuhitimisha uongozi wake na mahusiano yake na mhimili huu unaowakilisha wananchi.

Kinachoogopwa ni picha gani itajengeka kwa mataifa mengine wahisani ukizingatia kutakuwa na mwaliko wa mabalozi na wawakilishi wa mashirika wahisani.

Nikipata updates au yeyote basi tuziweke ili tuone huu mtanange unaishaje ili kuokoa aibu kwa kiongozi wa nchi.

Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
NIkweli dunia imekwisha! Ni vigumu kuamini mtoto mdogo ambaye anahitaji uangalizi na ulinzi kutoka kwa jamii anageuzwa mwanamke na kuingiliwa kwa nguvu hadi mauti. Huu ni unyama na ukatili wa hali ya juu.

Tukio hilo la kutisha lilitokea katikati ya wiki iliyopita, Tabata Msimbazi jijini Dar ambapo mtoto Ester Banzi ,5, (pichani) alikutwa na mauti baada ya kuingiliwa kimwili na mwanaume ambaye inadaiwa alimteka kwanza.
Akizungumza na Gazeti la Uwazi kwenye msiba huo, mama mdogo wa marehemu Ester aliyejitambulisha kwa jina la Watende Hamis huku akitokwa machozi mfululizo, alisema:

“Siku ya tukio, ilikuwa saa 5:30 asubuhi tukiwa nyumbani, dada (mama wa marehemu aitwaye Rebeka) alikuwa ameinjika sufuria ya ugali jikoni kwa ajili ya chakula cha mchana.
“Akamtuma Ester dukani akanunue unga. Alimpa shilingi 1,200. Si mara ya kwanza Ester kutumwa dukani kwa vile ni jirani tu.

“Tulimsubiri Ester arudi na unga lakini alichukua muda mrefu. Ikabidi tumfuate dukani, hatukumuona. Tuliwauliza watoto wenzake ambao anapenda kucheza nao, wakasema walimuona amebeba mfuko cha Rambo huku akiongozana na baba mmoja.


“Basi, tuliendelea kumtafuta bila mafanikio. Ikabidi tutoe taarifa kwa baba yake ambaye akaingiwa na wasiwasi, akaenda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Tabata Shule.“Ndani ya masaa matatu baba yake akatupigia simu kwamba mwili wa Ester umeokotwa huku ukionekana alibakwa na kuharibiwa vibaya.”

Naye kijana anayeuza duka ambalo marehemu alitumwa kununua unga, bila kutaja jina lake alikiri Ester kufika dukani hapo na kupimiwa unga kisha akaondoka.

Baadhi ya wananchi majirani na maeneo hayo waliohojiwa na waandishi wetu kuhusiana na tukio hilo walisema kwamba wao walimuona mtoto huyo akifuatana na mwanamume mmoja, lakini hawakumtilia mashaka kutokana kwamba walifikiri ni ndugu yao.

Mtu mmoja ambaye mwili wa marehemu ulikutwa jirani na nyumba yake, naye alizungumzia tukio hilo:
“Sisi tulisikia sauti ya mtoto akiomba msaada. Tulipata hofu ikabidi tukaangalie eneo lile ndipo tulipouona mwili wa mtoto huyo. Tulipomchunguza tukagundua alibakwa kwani nguo yake ya ndani ilikuwa pembeni.

“Inaonekana huyo mtu hakuchukua muda mrefu kufanya kitendo hicho. Tulimpigia simu Mkuu wa Kituo cha Polisi Tabata Shule, Afande Kobelo akaja na timu yake. Hili tukio nahisi lina ushirikina ndani yake.”

Mmoja wa askari aliyefika katika eneo la tukio ambaye hakutaka kutaja jina lake kwa vile siyo msemaji mkuu wa jeshi hilo alisema mwili wa mtoto huyo ulionekana kuingiliwa kimwili, marehemu alivunjwa shingo na kutobolewa upande wa kushoto kichwani.Marehemu Ester alizikwa wiki iliyopita mkoani Morogoro. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu. Amina.

Ali Kiba received a king’s welcome when he arrived in Kenya for the third cycle of the Coke Studio Africa Recording earlier this week, but that was nothing compared to the love that Kenyans on social media showed him as he was interviewed by Lillian Muli for #OneonOne .

His name shot to the top of the trends as Kenyans on social media reminisced on his golden oldies like Cinderella and Mac Muga. Requests also came streaming in for his new hits Mwana and Chekecha Chekechea.

Kiba, who recently came back to the music scene after a three year hiatus, walked away with six prestigious trophies at the 2015 Kilimanjaro Awards beating internationally acclaimed artist Diamond Platinumz.



Speaking candidly during the Citizen TV interview on Friday night, Kiba rubbished claims that he won the Kilimajaro awards unfairly.

“I feel like I am the best and I deserved the awards that I won. My fans missed my music and they voted for me. That is why I won six out of the seven categories that I was nominated for,” he said.

When asked about his relationship with Diamond, Kiba refuted rumors that they two are on bad terms.

“Don’t believe what you hear out there. There’s no beef between me and Diamond, and there has never been. I can assure you that Diamond and I have never fought over anything,” he said emphatically.

He however intimated that he gets irritated when people compare him to the Mbagala singer.

“I am me and Diamond is Diamond. We each have our own musical styles. I do my music in a way that only I can. So, I will not feel that because Diamond is out there doing collabos with others that I must do the same,” he said.

He was also quick to refute claims that he dedicated his new hit single Mwana to Diamond, but he admitted that he does listen to his Diamond’s songs.

In addition to his music, Ali Kiba is campaigning for conservation of Africa’s wildlife alongside Oscar Award Winning Actress Lupita Nyongo. SOURCE: CITIZENS TV

Mbunge Wa CHADEMA Ajivua Uanachama......Asema Kama CHADEMA Wanaubavu Wakalikomboe hilo Jimbo


MBUNGE wa Mpanda Mjini, Said Arfi, jana aliwaaga wapiga kura wake akiwaeleza kuwa uanachama wake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) utakoma mara baada ya kuvunjwa kwa Bunge la 10 mjini Dodoma.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Kashato mjini hapa jana, Arfi, aliyekiwakilisha chama hicho kwa miaka 10 mfululizo, aliwaambia wananchi kuwa jimbo hilo litakuwa wazi wakati wowote wiki ijayo.
  
“Kama Chadema wana ubavu, waje walikomboe jimbo hili. Mimi ninaifahamu Chadema kuliko mtu yeyote mkoani Katavi kwani nilikuwa Makamu Mwenyekiti (Bara), na sasa nitamuunga mkono yeyote anayefaa kuwa mrithi wangu,” alisema Arfi na kushangiliwa.
  
Mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa, ulikuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kutokana na kuzagaa kwa taarifa za kutaka kufanyiwa fujo kwa Mbunge huyo na watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema.
  
Arfi alisema hatogombea tena Mpanda Mjini; “Lakini nipo tayari kuvaa shati la kijani au la zambarau kumpigia debe mgombea yeyote katika jimbo hili. Ninawajua Chadema na kama wakiendelea kunifuatafuata, nitasema yote.”
  
Kauli hiyo ilitafsiriwa kuwa Arfi sasa atafanya kampeni akiwa CCM au ACT Wazalendo dhidi ya Chadema katika Jimbo la Mpanda Mjini, ambalo kabla yake halikuwahi kutawala na Mbunge mmoja kwa miaka 10 mfululizo.
  
Hii ni mara ya kwanza kwa Arfi kuweka hadharani mustakabali wake kisiasa, lakini kauli yake ya kuwa tayari kuvaa shati la kijana inakwenda tofauti na fununu zilizozagaa mjini hapa kuwa huenda akajiunga na ACT Wazalendo, chama kinachoongozwa na swahiba wake, Zitto Kabwe.
  
Ikumbukwe kuwa mara baada ya Chadema kutangaza kumvua nyadhifa zote Zitto takriban miaka miwili iliyopita, mara moja Arfi alitangaza kuajiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema.

Staa grade one kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefanyiwa kufuru ya bonge la pati na msanii mwenzake kutoka nchini Nigeria, Kingsley Chinweike Okonkwo ‘KCEE’.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu kilichosafiri na staa huyo ambaye yupo nchini humo kwa ziara yake inayofahamika kama ‘Nana Tour’, tangu Diamond alipofika siku ya kwanza akiwa na mameneja wake, Salam, Babu Tale, DJ wake aitwaye Romy Jones na wengine, mastaa kibao wakubwa walikuwa wakihitaji kuwa wenyeji wake.


  • “Jamaa ana uhusiano mzuri sana na mastaa wa Nigeria. Kuna ambao ameshafanya nao kazi kama Yemi Alade, Tiwa Savage, Bracket, Iyanya, KCEE na P Square (bado haijatoka).



  •  “Pia wapo wengine kibao wanaotaka kufanya naye kazi hivyo wanamuwinda.Waliposikia anakuja kufanya ziara ya wimbo wake mpya kila mmoja alitaka kuwa mwenyeji wake.


“Simu zilikuwa nyingi lakini mwisho wa siku KCEE alikuwa ameshafika uwanja wa ndege kutupokea na hiyo ilikuwa rahisi kwake kwa kuwa naye hivi karibuni alimshirikisha katika wimbo wake wa Love Boat,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo kinaendelea kumwaga ubuyu kuwa baada ya kufika nyumbani kwa KCEE, staa huyo mwenye mikoko na majumba ya kutosha nchini humo kupitia muziki, aliwafanyia bonge la ‘sapraiz’ kwa kufungua makabati yake ya rangi ya dhahabu na kuwaonesha tuzo kibao alizozipata kisha wakajimwaga sebuleni ambapo waliandaliwa pati ya madikodiko ya Kinigeria.


  • “KCEE ni kati ya wasanii wenye mafanikio na mali kibao. Jumba tu aliokaribishwa ndani yake lilijengwa kwa kuchanganya nakshinakshi za dhahabu.”


Diamond alitafutwa na  mwandishi kupitia Mtandao wa WhatsApp kuhusiana na mapokezi yake ambapo alifunguka:


  • “Nashukuru kwa Nigeria kunipokea vizuri najihisi kama niko nyumbani, nasema asante sana kwa watu hawa kwani wameonesha sapoti ya nguvu hata katika kunipigia kura katika Tuzo za MTV MAMA,” alisema Diamond na kuongeza.


“Kwa sasa akili yangu yote nimeielekeza kimataifa zaidi baada ya kufanya kolabo za kutosha Afrika.”

Hivi karibuni Meneja wa Diamond, Babu Tale alikaririwa akisema kuwa mashabiki wategemee kolabo ya kimataifa na msanii mkubwa na kudokeza kuwa msanii huyo anaweza kuwa Usher Rymond, Chris Brown, Ne-YO au yeyote mkubwa kutoka Marekani.

Deogratius Mongela na Chande Abdallah
GOOD time! Ndivyo unavyoweza kusema ambapo wakati habari ya mjini ikiwa ni kuhusiana na nyumba yake kupigwa mnada, staa wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ yupo bize jijini Hong Kong, China akila bata, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Kampuni ya Udalali ya MEM Auctioneers and General Brokers ilipewa jukumu la kupiga mnada nyumba ya mwanamuziki huyo iliyopo Mivumoni, Kinondoni jijini Dar baada ya Jide kushindwa kulipa deni alilokopa kutoka taasisi ya fedha ya EFC Tanzania Limited.

Wanahabari wetu waliokuwa na kibarua cha kumtafuta Jide ili kujua anazungumziaje kuhusu nyumba hiyo kupigwa mnada, walizunguka kwenye viunga lukuki vya Dar ambavyo mwanamuziki huyo huwa anapatikana lakini jitihada hazikuzaa matunda, achilia mbali simu yake ya mkononi kutopatikana.

Wakati gazeti hili likielekea mitamboni, chanzo kimoja kilipenyeza habari kuwa staa huyo wa Wimbo wa Yahaya yupo nchini China ‘anakula ujana’.“Kwa taarifa yenu Jide hayupo Bongo, ametimka zake China kula raha kama vipi fuatilieni kwa mbinu zenu mtabaini hiki ninachowaeleza,” kilinyetisha chanzo chetu, Jumamosi iliyopita.

Kabla ya kuwadadisi wadau wengine wa karibu wa Jide, Ijumaa Wikienda liliingia kwenye ‘peji’ ya Instagram ya mwanamuziki huyo na kukutana na posti iliyoonesha kuwa yupo Dubai akielekea nchini China kuinjoi maisha.
“Dubai-Hong Kong leo nimetoa ushamba sikujua mpaka ndege ikipaa kuna WiFi (huduma ya intaneti) tembea ujionee,” aliandika Jide.

Alipotafutwa Gardner G. Habash ambaye alikuwa mume wa Jide alisema kwa kifupi kuwa hana taarifa zozote kuhusiana na nyumba hiyo kupigwa mnada.
GPL
shinda Tuzo Alizoshinda KILL Awards na Kumbwaga Diamond

Msanii kutoka Tanzania Ali Kiba ambaye amejitokeza tena katika ulingo wa muziki baada ya kupumzika kwa miaka mitatu amepuuzilia mbali madai kwamba alipendelewa katika tamasha la tuzo za Kilimanjaro.
Ali kiba ambaye alipata tuzo sita na kumshinda msanii wa kimataifa Diamond Platinum amesema kamwe hakupendelewa na kwamba ni muziki wake unaopendwa na wengi.
Akizungumza katika mahojiano na runinga ya Citizen siku ya ijumaa usiku nchini Kenya,Kiba amesema kuwa anahisi yeye ndio bora na kwamba ilikuwa haki yake kushinda tuzo hizo.
''Nahisi kwamba mimi ndio bora na nilifaa kushinda tuzo hizi.''Mashabiki wangu waliukosa mziki wangu na ndio maana walinipigia kura na ndio maana nilishinda tuzo sita kati ya saba nilizoteuliwa'',alisema.
Na alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Diamond,Kiba alikana madai kwamba wawili hao hawana uhusiano mwema.
''Sina uadui wowote kati yangu na Diamond na haujakuwa''. Naweza kukuhakikishia kuwa mimi na Diamond hatujapigania kuhusu chochote''.
Hatahivyo amesema kuwa inamkera wakati watu wanapomlinganisha na mwimbaji huyo wa Mbagala.
Alisema:Mimi ni mimi na Diamond ni Diamond


Ruby star wa muziki ambaye ujio wake umekuwa ni wa kishindo kikubwa katika tasnia ya muziki wa Bongo Flava, ametufungulia moyo wake na kuweka wazi namna ambavyo safari yake katika usupa star imebadilisha kabisa mahusiano yake ya kimapenzi.

Kwa taarifa ambayo eNewz inakupa wewe kwa mara ya kwanza kabisa, The Beautiful Ruby ambaye offcourse maisha yake yamebadilika na yanaendelea kubadilika kwa kasi, amelazimika pia kubadili mahusiano yake ya kimapenzi ambapo kwa sasa anatoka na mtu mpya na wanaelewana na kwenda sawa bila kumuweka wazi hasa ni nani huyo.
Ruby ameeleza kuwa, mahusiano yake haya mapya yamemfunza kujishusha na kuwa mfano bora kama kioo cha jamii, huku akifurahia zaidi umaarufu wake kutia nakshi zaidi mahaba katika mahusiano hayo mapya.