Sunday, July 5, 2015

MUWAKILISHI WA TANZANIA

Nyota ya Diamond Platnumz Inazidi Kung'ara.......Katajwa Kuwania Tuzo za Uganda (Uganda Entertainment Awards 2015 )


Diamond Platnumz ameendelea kutajwa kuwania tuzo mbalimbali barani Afrika.
 
Akiwa ni miongoni mwa wanaowania tuzo za MAMA zitakazotolewa mwezi huu, muimbaji huyo wa ‘Nana’ ametajwa kuwania tuzo zingine za Uganda zijulikanazo kama Uganda Entertainment Awards 2015 (UEA)

Platnumz anawania kipengele cha Best African Act akichuana na Wizkid (Nigeria), Patoranking (Nigeria), Tiwa Savage (Nigeria) na Active

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Septemba 4, 2015 katika hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort (Speke Ball) jijini Kampala, Uganda

Lungi Maulanga alizwa na vibaka


Msanii wa Bongo Movie nchini, Lungi Maulanga amejikuta akilizwa na vibaka baada ya kuibiwa baadhi ya vitu vya ndani wakati akiwa katika mtoko wa usiku hali ambayo imemtia hasara na kumrudisha nyuma kimaendeleo.
 
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa msanii huyo amedai kuwa tukio hilo lililotokea maeneo ya Magomeni, jijini Dar es Salaam limempa Lungi hasara kwani kitendo hicho ni kurudishana nyuma kimaendeleo.
 
Lungi amekiri kulizwa na vibaka hao na kusema kuwa amechoka sasa kwani sio mara ya kwanza kufanyiwa kitendo kama hicho na kusema kuwa anajiandaa kuhama ili kukwepa adha hiyo na kudai kuwa ameibiwa vitu kadhaa ikiwemo Tv na deki.

Picha 12 za Diamond kwenye stage na Wanigeria!


.
.
Show ya road to mama inayoandaliwa na kituo cha runinga maarufu kama  MTV Base kama sehemu ya kusheherekea tuzo za MTV Base mwaka imefanyika Nigeria kwenye hoteli  ya Federal Palace.
Miongoni mwa wasanii waliotumbuiza usiku wa kuamkia leo ni Phyno, Diamond Platnumz, Patoranking na Yemi Alade, Iyanya, Olamide.Hizi ni picha za kutoka kwenye show hiyo.
.
.
.
.
.
Diamond Platnumz.
.
.
.
.
.
Babu Tale akiwa na Yemi Alade.
.
Patoranking.
.
.
.
Phyno.
.
Diamond Platnumz akiwa na Yemi Alade.
.
Diamond Platnumz.

General News

Sentensi nne za Zitto Kabwe akiwataja Watanzania walioficha fedha benki ya Uswis (Pichaz&Audio)

on
Screen Shot 2015-07-04 at 9.21.15 PM
Jana Zitto Kabwe alikua akiwahutubia wakazi wa jiji la Dar es salaam katika viwanja vya Mwembe Yanga na kutaja orosha ya majina ya Watanzania wlaioficha mabilioni ya fedha katika benki ya Uswis.
Haya ni maneno aliyoyazunguza:-
‘Kuna watu wanasema nyinyi kina zitto na wenzako mnaenda kuanzisha chama uoni utagawa kura za wapinzani sisi ACT tunaenda kutafuta asilimia 58 ya wananchi ambao awapigi kura asilimia 42 tunawaachia wagane wenyewe’…..
‘Kuhusu miswada mitatu ya gesi iliyopelekwa bungeni kwa hati ya dharura ili ipitishwe bungeni, maswala ya  mafuta na gesi ni maswala ambayo hatakiwi kufanyiwa haraka ni maswala ambayo yanaitaji concentration kubwa ya wadau wote sio maswala ya kuyapeleka bungeni kwasababu mpo wengi mkayapitisha halafu tukawaingiza watanzania katika matatizo makubwa’.
‘Mwaka 2013 nilienda ufaransa nikakutana na jaji wa ufaransa ambaye alikuwa anafanya uchunguzi kuhusu wafaransa ambao  wameficha hela uswizi katika mafaili ambayo alikuwa ameyapata alipata mafaili ya watanzania ambao wameficha hela uswizi akaniita,nikayapeleka  serikalini ,benki kuu ya Tanzania, kamishina generali wa TRA na tukampa mwanasherilia mkuu wa serikali tukawaambia hawa ambao hawana uchungu na sisi wanatupa nyaraka hizi kwanini nyinyi amtoi taarifa  inavyotakiwa’.
‘Sisi tumepata taarifa kutoka benki moja tawi lake moja benki ya HSBC ya Switzerland ambayo iyo taarifa inawatu 99 watanzania ambao wameweka pesa katika benki hiyo…kwenye taarifa hiyo wengine niwafanyabiashara kiahalali na wengine ni watu ambao wanahusika na kashafa ya  pesa za rada ambao walificha pesa katika mabenki ya uswizi’.
Screen Shot 2015-07-04 at 9.21.50 PM
Screen Shot 2015-07-04 at 9.21.06 PM
Screen Shot 2015-07-04 at 9.20.48 PM
Screen Shot 2015-07-04 at 9.21.15 PM

Screen Shot 2015-07-04 at 9.20.23 PM
Screen Shot 2015-07-04 at 9.20.40 PM
Msikilize hapa mtu wangu…