Isome Hapa Barua ya Kujiuzulu Aliyoandika Rais Robert Mugabe
Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Robert Mugabe, jana alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kuongoza taifa hilo kwa miaka 37 tangu lilipopata uhuru mwaka 1980.Mugabe katika barua aliyoiandika kwenda wa Spika wa Bunge, alisema uamuzi huo ni wa kwake binafsi na kwamba hajashinikizwa na mtu yeyote.
Katika barua yake ya kujiuzulu, Mugabe aliiandika jana Novemba 21 na kuielekeza kwa Spika wa Bunge, Jacob Mudenda.
Mugabe aliandika kuwa, kwa mujibu wa kufungu cha 90(1) cha Katiba ya Zimbabwe marekebisho ya namba 20 ya mwaka 2013.
“Kufuatia mazungumzo yangu na Spika wa Bunge, Wakili Jacob Mudenda majira ya saa 7:53 mchana, Novemba 21, 2017 kuhusu kutangaza kujiuzulu kama Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mimi Robert Gabriel Mugabe, kwa mujibu wa kifungu cha 90(1) cha Katiba ya Zimbabwe natangaza rasmi kujiuzulu kwangu kama Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe mara moja.”
“Uamuzi wa kujiuzulu ni wangu kwa chama, na nimefanya hivi kwa maslahi ya watu wa Zimbabwe na nia yangu ya kuona makabidhiano ya madaraka yenye amani ambayo yatashikilia amani, utulivu na umoja wa taifa.”
Aidha, Rais Mugabe alisema, “Tafadhali utangazie umma kuhusu kujiuzulu kwangu haraka iwezekanavyo kama inavyotakiwa na kifungu cha 96(1) cha Katiba ya Jamhuri ya Zimbabwe.
“Wako Mwaminifu, Robert Gabriel Zimbabwe, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe,” alihitimisha Rais Mugabe.
Kufuatia kujiuzulu kwa Mugabe, wananchi katika Mji Mkuu wa Zimbabwe, Harare walitoka katika mitaa mbalimbali na kushangilia huku wakisema kuwa ni awamu mpya kwa Zimbabwe sasa kuendelea kiuchumi.