Tuesday, October 20, 2015

Mkuu wa Majeshi DAVIS MWAMUNYANGE Ajitokeza Hadharani Kwenye Uzinduzi wa Uwanja wa Ndege za Kivita Morogoro

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais JAKAYA KIKWETE amezindua awamu ya pili ya ujenzi wa uwanja wa ndege za vita uliopo katika kamandi ya jeshi la anga iliyopo NGERENGERE mkoani MOROGORO.

Akizindua ujenzi huo,Rais KIKWETE amesema mazingira bora ya uwanja huo pamoja na kutumika kwa shughuli za kijeshi, yatawawezesha watu kufanya kazi kwa bidii na kuchochea uboreshwaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika eneo hilo.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. HUSSEIN MWINYI amesema kukamilika kwa mradi huo itakuwa ni hazina kwa jeshi la wananchi na taifa zima huku akisisitiza suala la matumizi ya uwanja huo kuboreshwa.

Naye Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali DAVIS MWAMUNYANGE ameeleza mikakati iliyopo ya kuboresha jeshi hilo, huku mkuu wa jeshi la anga Meja Jenerali JOSEPH KAPWANI akisema uwanja huo utakuwa bora katika nchi za Kusini mwa AFRIKA.

magufuli rasi mtarajiwa

MAGUFULI: Mabadiliko Ya Kweli Hayawezi Kuletwa Kwa Kuzungusha Mikono


MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa kwa kuzungusha mikono, bali yatakuja kwa kufanya kazi.

Kutokana na hali hiyo, amesema yeye ndiye anayeweza kuleta mabadiliko ya kweli yanayokwenda na vitendo katika kujenga uchumi wa nchi na watu wake.

Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo jana kwa nyakati tofauti, alipokuwa akizungumza wakati wa  mikutano ya kampeni iliyofanyika katika majimbo ya Buchosa, Geita na Busanda.

Katika mazungumzo yake, Mgufuli aliwataka Watanzania wasidanganywe na baadhi ya wanasiasa wanaowataka wasiipigie kura CCM.

Alisema kwamba, pamoja na baadhi ya wanasiasa kukesha wakihamasisha mabadiliko kwa kutoichagua CCM, jambo hilo halitawezekana kwa kuwa ni sawa na ndoto za mchana.

“Ninasema hapa, eti kuna watu wanahangaika kuzungusha mikono na kusema wanaleta mabadiliko, ni lazima wajue mabadiliko hayawezi kuja kwa mtindo huo.

“China hivi sasa inatisha kwa kuwa na uchumi wa daraja la kwanza duniani na kuna hatari hata ya kutaka kuizidi Marekani.

“Kwa mfumo wao huo, hawakukiondoa madarakani chama tawala ila walifanya mabadiliko ya ndani ya chama na Serikali.

“Ndiyo maana Magufuli ninakuja na mabadiliko ya kwenda ndani ya Serikali na ndani ya CCM. Katika hili, sina mchezo ndugu zangu Watanzania, naomba mniamini,” alisema Dk. Magufuli.

Kwa kuwa Watanzania wameshaamua kumpa urais Oktoba 25, mwaka huu, jambo atakalo anza nalo ni kuunda mahakama ya mafisadi.

Alisema, amezaliwa katika familia maskini na hatakuwa tayari kuona wajasiriamali wadogo wakinyanyaswa na hata kutozwa ushuru ambao umekuwa ukiwakandamiza katika biashara zao.

Alisema anajua eneo la Nkome ni maarufu kwa kilimo cha mananasi daraja la kwanza, lakini bado wakulima wamekuwa wakikosa soko la uhakika.

Kutokana na hali hiyo, atatimiza mkakati wa Serikali yake kwa kujenga kiwanda cha juisi katika  eneo hilo.

“Ni aibu kwa nchi yetu inayozalisha matunda kwa wingi, kukosa kiwanda cha kusindika matunda.

“Napenda kuahidi hapa, nitajenga kiwanda cha juisi kitakachosaidia wakulima wa mananasi kuwa na soko la uhakika badala ya kwenda Geita mjini au Mwanza.

“Tukijenga kiwanda hapa, tutatoa ajira kwa vijana na tutatengeneza juisi yetu badala ya kila siku kuagiza kutoka nje ya nchi, hii ni aibu,” alisema.

MAJONZI: Safari Ya Mwisho Ya Mwenyekiti Mwenza Wa UKAWA Katika Viwanja Vya Karimjee jijini Dar .....Dr. Makaidi Amezikwa katika Makaburi ya Sinza, Dar Es Salam

Baadhi ya matukio ya picha katika ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Dkt Emmanuel Makaidi, Mwenyekiti mwenza wa UKAWA, katika viwanja vya Karimjee, posta, jijini Dar Es Salaam.Dr. Makaidi Amezikwa katika Makaburi ya Sinza, Dar Es Salam


Magufuli jembe chagua kiongozi mahili,shujaaa,jasili,mpenda amani

Masha akamatwa na polisi kwa kufanya kampeni kambi ya wakimbizi


Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha  pamoja na viongozi wengine wa  Chadema Wilaya ya Mpanda, wamekamatwa na polisi leo , kwa kile kinachodaiwa kufanya kampeni katika kambi ya wakimbizi ya Katumba, wilayani Mpanda bila  kuwa na kibali maalum.

Masha ambaye alikihama chama cha CCM hivi karibuni na kujiunga na Chadema amezungumza nasi na kusema ameshikiliwa katika kituo cha polisi cha Mpanda baada ya kufanya kampeni katika kambi hiyo.

“Nilikwenda kufanya kampeni katika kambi hiyo ambayo ina wakimbizi ambao mimi mwenyewe niliwapa uraia mwaka 2009,” amesema Masha na kuongeza:

“Kampeni zinafanyika kule lakini kwa sababu wanazojua wao wametukamata wakati hao wanaoitwa wakimbizi niliwapa uraia kwa amri ya Rais.”

Pamoja na Masha wengine waliokamatwa ni Mgombea ubunge jimbo la Nsimbo, Gerald Kitabu, Abraham Mapunda, Mwenyekiti wa Chadema, Mpanda. Katibu wa Chadema jimbo la Nsimbo,  Stanslaus Selemani,   Dalas Damian, Lameck Constantine Momose na  Francisco  Sylvester .

Kwa mujibu wa Masha, polisi wamewachukua  maelezo  viongozi hao wa Chadema  kuanzia saa 9 mchana  na wamemaliza saa 10 jioni.

“Tulikamatwa kuanzia saa 7:15 mchana tukachukuliwa chini ya ulinzi mkali wa polisi toka Katumba hadi Mpanda mjini na kuanza kuhojiwa,” amesema.

Akizungumza na mtandao  huu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, SACP Dhahiri Kidavashari amesema Masha amekamatwa leo saa 4 asubuhi akiwa na watu wengine sita kwa makosa ya kufanya mkutano bila kibali katika makazi ya wakimbizi.

Kamanda Kidavashari amesema  viongozi hao wa Chadema walitumia  uwanja wa kambi ya wakimbizi ya Kanoge na baadaye Katumba bila kuwa na kibali maalum baada ya kuona kuwa hakuna ratiba ya  mkutano mwingine katika eneo hilo.

“Kufanya mkutano si tatizo, tatizo walifanya hivyo bila kibali, yale ni makazi ya wakimbizi wengine wamepewa uraia lakini wengine hawajapewa,” amesema.