Saturday, May 2, 2015

TEAM ZALI YAUWA YAMSHINDA WEMA

WEMA, ZARI WATOANA JASHO


Nisheedah! Gumzo la mjini wiki hii ilikuwa ni shoo ya mchumba wa Nasibu Abdul ‘Diamond’ Zarinah Hassan ‘Zari’ iitwayo Zari All White Party iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar na ile ya Instagram Party ambayo ilimhusu mrembo Wema Sepetu iliyofanyika jijini Mwanza ambapo nyuma ya pazia, warembo hao walitoana jasho kuhakikisha wanafunikana.
Staa wa Bongo movie,Wema Sepetu.
MVUTANO WAANZA
Kwa mujibu wa chanzo, mvutano wa Wema aliyewahi kuwa mchumba wa Diamond na Zari ambaye anammiliki Diamond kwa sasa, uliibuka Alhamisi iliyopita wakati kila mmoja akijiandaa kwenda kwenye shoo inayomhusu.
“Wema na Zari leo ni full kutoana jasho, kila mmoja anataka kuwavuta mashabiki wengi upande wake.
ZARI APEWA SAPOTI
“Zari amepata sapoti kubwa kutoka kwa mpenzi wake wa sasa Diamond kwani walikuwa wanafanya shoo pamoja hivyo alikuwa na kibarua cha kuwakusanya mashabiki wote wa Diamond waende kwenye shoo yake ili Wema asipate watu,” kilisema chanzo hicho.
UPANDE WA WEMA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kwa upande wa Wema, yeye alikuwa na kibarua kizito cha kuwakusanya marafiki zake hususan mastaa wa Bongo Movies wasiende kwa Zari na badala yake waende Mwanza kwenye Instagram Party.
Zarinah Hassan ‘Zari’.
“Ni mnyukano wa aina yake, Wema alikuwa na kibarua kizito kuwashawishi Bongo Movies waikache shoo ya Zari waende Mwanza kwenye Instagram, bahati nzuri alifanikiwa kwani wasanii wengi walimuunga mkono,” kilisema chanzo hicho.
MATUSI
Hadi jana jioni, kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Timu ya Zari (Team Zari) na ile ya Wema (Team Wema) zilikuwa zikirushiana matusi huku kila mmoja akionesha hisia zake.“Hakuna kwenda kwa Zari, twendeni kwa Wema Mwanza, watakaokwenda kwa Zari ni wapuuzi kabisa,” ilisomeka moja ya komenti ya mdau wa timu Wema huku timu Zari ikijibu:“Wajinga wakubwa watakaokwenda kwa Wema, mpango mzima ni kwa Zari na Diamond pale Mlimani City.”
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’.
STEVE AFUNGUKA
Ili kuzidi kupata data zaidi, wanahabari wetu walimtafuta mdau mkubwa wa kuwashawishi watu, mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambaye aliweka bayana kuwa wao kama Bongo Movies, wanamuunga mkono Wema.
“Niweke wazi tu kwamba sisi tutakwenda kwa Wema, hii shoo ya Zari na Diamond itatupitia kushoto kwa kweli,” alisema Steve.
KAJALA KWA ZARI
Kwa upande wake Kajala Masanja alikuwa tofauti na waigizaji wenzake ambapo alipokea kwa mikono miwili mwaliko wa Zari na kuanza kuihamasisha Team Kajala kwenda kwenye shoo  hiyo.
WEMA AFUNGUKA
Jitihada za kumpata Zari aweze kufungukia mvutano huo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kuita bila majibu lakini bahati nzuri Wema alipatikana na kufunguka:“Mimi kama mimi nakwenda katika shoo inayonihusu ya Instagram, hiyo ya Zari siijui. Sijashawishi mtu ila watu wameamua kuniunga mkono, siwezi kuwazuia na hao wanaofikia hatua ya kutukana pia siwezi kuwazuia,” alisema Wema.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Wema Sepetu.
MWISHO UKOJE?
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, shoo ya Zari ilitarajiwa kurindima na mashabiki wake huku Wema akiwa na mashabiki wake waliomuunga mkono hivyo kusababisha mtikisiko wa aina yake mjini.
CHANZO: GPL

HII NI OFFSIDE IMEZIDI SASA KISA MTIHANI PIA KIGOMA NAYO IPO

Mwili wa mwanafunzi Kiteto Aliyefariki Kwa Kuchapwa Viboko na Walimu wafikishwa Dodoma


MWILI wa mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Matui iliyoko Wilaya ya Kiteto, Mkoa wa Manyara, aliyedaiwa kufariki baada ya kuchapwa viboko na walimu wake, Emmanuel Mbigima (15), umefikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Wakati mwili huo unafikishwa hospitalini hapo jana asubuhi, ulikuwa umewekwa kwenye gari la Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ukisindikizwa na baadhi ya ndugu wa karibu wa familia ya marehemu.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, babu wa marehemu, Emmanuel Ngowi, alisema mwili huo umeletwa hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo ambavyo vimekosekana katika hospitali ya Wilaya ya Kiteto.

"Mjukuu wangu alipigwa na walimu watatu tarehe 20 mwezi huu kutokana na kufeli mtihani wa somo la Kiswahili.

“Tumechukua uamuzi wa kumleta hapa kwa sababu madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto, walishindwa kubaini kichwa kimeathirika kwa kiasi gani kwa kuwa hawana vifaa vya uchunguzi vya  kichwa.

“Hata hivyo, majibu ya uchunguzi wa awali yaliyotolewa katika hospitali hiyo, yalionyesha jicho la kulia lilivuja damu kwa ndani na pia mwili wa marehemu ulikuwa na michubuko miguuni,” alisema Ngowi.

Naye mjomba wa marehemu, Michael Ezekiel alisema matukio ya wanafunzi kupigwa na kupoteza maisha yamekuwa yakijirudia shuleni hapo kwa kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya watuhumiwa.

“Mwaka jana kuna mtoto alipigwa na mwalimu akafariki, lakini mtuhumiwa alipelekwa mahakamani na baadaye kuachiwa kwa madai kuwa mtoto alikuwa ni mgonjwa,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk. Zainabu Chaula, alithibitisha kupokelewa kwa mwili huo na kusema uchunguzi bado unaendelea.

Bodi ya Mikopo Ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Yaanza Kupokea Maombi ya Mikopo Kutoka Kwa Wanafunzi Kwa Mwaka Wa Masomo 2015/2016


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) jana (Ijumaa, Mei 1, 2015) imetoa mwongozo kwa wanafunzi wahitaji wanaotarajia kuomba mikopo na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa masomo 2015/2016 unaotarajiwa kuanza miezi michache ijayo.

Kwa mujibu wa mwongozo huo, ambao unapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz), waombaji wote wamepewa takribani miezi miwili kuwasilisha maombi yao kuanzia Jumatatu, Mei 4, 2015 hadi Jumanne, Juni 30, 2015.

Aidha, wanafunzi wote wahitaji wa mkopo na ruzuku wanapaswa kufanya na kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia mfumo maalum (Online Loans Application and Management System) ulioanzishwa na HESLB kwa ajili ya kupokea maombi hayo. Mfumo huo unapatikana kupitia tovuvi ya Bodi au kwa kufungua kiunganishi chake (http://olas.heslb.go.tz).

Pamoja na mambo mengine, mwongozo huo unafafanua kuwa waombaji wa mara ya kwanza (First Time Applicants) wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tshs 30,000/- kwa na kisha kutumia namba ya muamala (Transaction ID) kuingia katika mtandao na kuanza kujaza fomu za maombi.

“Waombaji wa mara ya kwanza wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tzs 30,000/- ambayo inalipwa mara moja tu na haitarudishwa kwa nia ya M-Pesa,” inasema sehemu ya mwongozo huo uloiotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo.

Aidha, mwongozo huo umesisitiza kuwa wanafunzi wenye mikopo na wanaoendelea na masomo katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu hawapaswi kuwasilisha maombi tena.

Bodi imewasihi waombaji na wadau wengine kuusoma na kuuzingatia muongozo huo wakati waote wanapofanya na kuwasilisha maombi.

HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. 
 
Aidha, jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.
 
POSTED  BY; RASHID H.B

VITA UKAWA YAANZA

Mgawanyo wa Majimbo Ndani ya UKAWA: CHADEMA Yapewa 50%, CUF 35%.......Vita ya Maneno Yaibuka, CUF Watuhumiwa Kuwa na Undugu na CCM


WAKATI ugawaji wa majimbo 211 ukikamilika kwa vyama vinavyounda Umoja ya Katiba ya Wananchi (Ukawa), imebainika kwamba Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeibuka na asilimia 50 katika majimbo hayo.
 
 Chama kilichofuata ni Chama Cha Wananchi (CUF) ambacho kinadaiwa kupata asilimia 35-40, NCCR-Mageuzi asilimia 10 huku NRD kinachoongozwa na Emmanuel Makaidi kuachiwa asilimia 1-2.
 
 Taarifa ambazo MPEKUZI imedozwa zinadai kuwa mgawanyo huo umefanywa kwa kuzingatia vigezo vya nguvu za kila chama katika eneo husika.
 
“Ndiyo maana umeona huu mchakato umechukua muda mrefu kwasababu ilikuwa inafanyika tathimini kuona nani ana nguvu wapi na nani ana nguvu eneo gani mwisho wa siku umeona kwa haya 211 wamekubalina,” alisema mtoa taarifa huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe.
 
 Akizungumzia majimbo 12 yaliyoleta utata anasema “Majimbo haya ni sita ya hapa Dar es Salaam ambayo kuna Segerea, Temeke, Ukonga, Ilala na Kinondoni.
 
“Kwa mikoani kuna jimbo la Serengeti, hili linaleta utata kwasababu kuna mvutano kati ya watu wa Chadema na katibu mkuu wa NCCR-Mageuzi Mosena  Nyambabe ambaye analitaka lile jimbo.
 
“Lakini taarifa zilizopo ni kwamba Nyambabe aliangukia pua katika uchaguzi wa serikali za mtaa na Chadema waliibuka kidedea, sasa ameambiwa kuachia jimbo lakini yeye hataki, ndiyo na lenyewe limewekwa  kiporo.
 
 Taarifa hizo zinaendelea kudai kuwa jimbo jingine lililotea mgogoro ni Vunjo linaloshikiliwa na TLP ambapo tayari Mwenyekiti wa NCCR-James Mbatia tayari ameonyesha nia ya kugombea.
 
“Huku nako kuna mgogoro mwingine kwasababu tayari Mbatia ameshatangaza nia na amefanya kazi kubwa katika jimbo hilo, lakini kuna kada mkubwa wa Chadema aliyewahi kugombea jimbo hilo naye ameweka msimamo kwamba ni lazima agombee."
 
 Majimbo mengine yanayotajwa kuweka umoja huo njia panda ni pamoja na Mtwara mjini na Mafia ambapo taarifa kutoka kwa kiongozi mmoja wa Ukawa zinasema kuwa wamepeana siku kumi kuanzia leo (jana) kwa kila kiongozi kuhakikisha amekamilisha mchakato wa kukamilisha utaratibu kwa majimbo yaliyobaki.
 
 Katika makubaliano Jimbo la Vunjo  liliachwa mikononi mwa NCCR-Mageuzi ambapo Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia amejinadi kulichukua kutoka mikononi mwa mbunge wa sasa Agustino Mrema.
 
 Akizungumzia Makaidi kupewa asilimia moja mpaka mbili alisema kuwa inatokana na mzee huyo kuonyesha msimamo ndani ya umoja huo.
 
“Makaidi hakuonyesha tamaa kama viongozi wengine wa upinzani baada ya kususia kwenye Bunge la Katiba, hakuonyesha tamaa ya kutaka posho za Bunge la Katiba, aliweka msimamo hadi leo hii, kwahiyo ndani ya Ukawa Mzee Makaidi ameonekana shujaa."
 
 Wadadisi wa masuala ya kisiasa wanadai kuwa Chadema ndiyo chama chenye nguvu ndani ya Ukawa ambapo taarifa za ndani zilidai kuwa katika mchakato wa kugawana majimbo kulikuwa na mvutano mkali huku chama hicho kikitaka kuachiwa majimbo mengi hali iliyobua mgogoro kutoka katika vyama vingine.
 
 Lakini duru za kisiasa zinaendelea kuonyesha kuwa mgawanyo huo pia unaweza usieleweke kwa wanachama wa kawaida wa Chadema wakiwemo wabunge  wao ambao wanashikilia majimbo mbalimbali.
 
MPEKUZI imepata mawasiliano ya kundi moja la wabunge wa Chadema wanalolitumia katika mtandao wa kijamiii likionyesha kushangazwa na baadhi ya vyama kutaka majimbo wanayoyashikilia.
 
 Wabunge walioshiriki mjadala huo  walionyeshwa kushangazwa na kitendo cha CUF kuomba kuachiwa baadhi ya majimbo wanayoyashikilia huku wengine wakionyesha shaka kwamba inawezekana ni njia ya chama hicho kutaka kuvunja umoja huo.
 
 Katika kuonyesha kukasirishwa mmoja wa wabunge alikwenda mbali zaidi na kutoa angalizo kwa viongozi wao wa juu  kuacha kuwaendekeza CUF huku mwingine akipendekeza chama hicho kuwaachia Chadema majimbo ya Zanzibar.
 
 Mbunge huyo aliyataja majimbo ya Zanzibar ambayo wangependa waachie kuwa ni pamoja na Pemba na mji mkongwe.
 
 Mwingine aliyechangia katika majadala huo alisema CUF wana undugu na CCM isije ikawa wametumwa kuubomoa Ukawa, huku mwingine akichangia kwa kusema kama ni mkakati wa kuingia Ikulu kwa upinzani ni sawa lakini kama siyo hivyo kuna sababu za kubishana kulinda majimbo yao.
 
 Majimbo yaliyotajwa kumezewa mate na wabunge hao ni Musoma Mjini,Nyamagana na majimbo mengine mengi huku mmoja wa wabunge waliokuwa wakishiriki mjadala katika kundi hilo alisema kwa muktadha huo Ukawa ni shiidaa huku mwingine akisema ni matusi kwa CUF kutaka majimbo yao.
 
MPEKUZI ilipata wakati mgumu wa kuwapata viongozi hao wa Ukawa kwani hata wale waliofikiwa wamekataa kuzungumzia jambo hilo huku taarifa zikidai kuwa wamepeana onyo kali katika vikao vyao kuhakikisha hakuna anayetoa taarifa za vikao nje.
 
 Katika mkutano wa Juzi, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia alisema Ukawa iko imara  sasa kuliko kipindi cha nyuma na alikanusha chama chake kuandika barua ya kujiondoa katika umoja huo.
 Ukawa ni muungano wa vyama vinne vya upinzani ambapo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NRD.
 Muunganiko huo ulifanyika katika Bunge la Katiba ambapo lengo lake kugomea Katiba Pendekezwa wakiamini wanaburuzwa na chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo baadaye waliamua kuendeleza umoja huo katika mambo mengine ya Urais.
CHANZO  MPEKUZI

WANII WETU

Kigogo Mpya Wa Jack Wolper Anaswa


Achilia mbali akina pedeshee Mangi, Dallas na Gee Modal, kigogo mpya wa staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe safari hii amenaswa laivu wakijiachia kwa raha zao.
 
Kwa mujibu wa chanzo, kigogo huyo ni mtu mwenye fedha zake aitwaye Jimmy Mgaya ambaye ni Mbongo mfanyabiashara aishie nchini Afrika Kusini ‘Sauz’. 
 
Chanzo hicho kilishusha data kuwa jamaa huyo ndiye aliyempangia Wolper nyumba ya kifahari iliyopo ushuani Mbezi-Beach jijini Dar.Huku akirusha picha za kimahaba za wawili hao, sosi wetu huyo alisema kuwa Jimmy ni ‘mtu f’lani hivi amazing’ kwa sababu anakata mkwanja kinoma.

Chanzo hicho kilidai kwamba picha za wawili hao wakijiachia  zilipigwa maskani kwa jamaa huyo huko Durban kwenye Jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.
 
Baada ya jitihada za kumsaka mwanaume huyo kugonga mwamba, Wolper alipigiwa simu na kusomewa mashitaka yake juu ya mwanaume huyo ambapo mbali na kukiri kumfahamu Jimmy, alikuwa na haya ya kusema:
 
“Ni kweli namfahamu Jimmy, nilikutana naye kwenye mizunguko yangu nje ya nchi. Si kweli kwamba ni bwana’ngu. Kuhusu picha, nilipiga naye kama rafiki tu na sioni kama ni picha mbaya.”
 
Hivi karibuni Wolper alikiri kuwa na mwanaume lakini akawa anaogopa kumwanika kwa kuogopa kuporwa na wasichana wa mjini hivyo inaaminika ndiye huyo Jimmy.

MSANII MWENYE KIPAJI CHA AINA YAKE AKIWABUDUDISHA WATANZANIA

Tazama Picha Mbali Mbali za Sherehe ya Zari White Party iliyofanyika Usiku wa Jana

HAPO DANGOTE NA MADAME ZARI WAKIWA WANAINGIA
Tazama Picha Mbali Mbali za Sherehe ya Zari White Party iliyofanyika Usiku wa Jana
HAPO MR.DANGOTE AKIVUNJA
MALKIA WA MIPASHO MAMA HADIJA KOPA AKITOA YAKE
HAPO NI SHIKOLOBOY MASTA  SHETA

MR DIAMOND NA  NAY WA MITEGO WAPAGANISHA
MAFANSI WAKIBURUDIKA


VISENT KIGOS  RAY  AKIWEPO


USALAMA ULIIMARISHWA

SHEMEJI YETU

 
 
 

Kikwete: "Nisingekuwa Rais Ningekuwa Msanii Mkali wa Bongo Fleva.".........HOTUBA Nzima ya Rais Kikwete Aliyoitoa Jana Mei Mosi Iko


RAIS Dkt. Jakaya Kikwete, ametamba kuwa angakuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya basi angelikuwa wa “BongoFleva” kutokana na kuwa na sauti nzuri yenye kumudu kuimba nyimbo kwa ufasaha zaidi.


Kauli hiyo aliitoa  jana jijini Mwanza kwenye uwanja wa michezo wa CCM Kirumba wakati wa maadhimisho ya kilele cha sherehe za Mei mosi zilizofanyika Kitaifa jijini Mwanza kwa mwaka huu wa mwisho wa utawala wake.

Dkt. Kikwete aliimba wimbo wa Bendi ya OSS (Ochestra Safari Sound) wenye mashairi yasemayo "Mimi msafiri bado niko njiani sijui lini nitafika... naulizia watu kule ninakokwenda....”  na kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi waliomshangilia ambapo alitamba kuwa na sauti ya mauzo.

“Mmesikia sauti yangu si mbaya sana,  hakika nisingekuwa Rais wa Nchi hii basi nigekuwa msanii wa bongo fleva kama akina Ali Kiba, Diamond na wasanii wengine wakali nikiuza album zangu kwani ningekuwa tishio  kwa kuimba...” alisema.

Rais pia alimpongeza msanii maarufu nchini wa kizazi kipya mwenye mashairi na misamiati ya maneno magumu, Mrisho Mpoto, kwa kumtaka kujibu bango la walimu lililokuwa na ujumbe uliosomeka “Shemeji Unatuachaje??” ambapo alijibu kwa kusema kuwa "kuoa mwalimu nitabu kweli kweli haya nimesikia."

Aliwapongeza viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) nchini kwa kumwalika Mpoto “Mjomba” .Mara nyingi amekuwa akitoa ujumbe mzito kupitia fani yake ya muziki na mashairi lakini yakifikisha ujumbe bara bara kwa wananchi katika sherehe mbalimbali za kitaifa na makongamano .

Hotuba  nzima  ya  Rais  Kikwete  Ipo  Hapo  Chini:

MBUNGOFREVA ALIKIBA AIBIWA

Majambazi wamevamia nyumba ya Ali Kiba usiku wa kuamkia leo, picha na taarifa za mwanzo viko hapa

IMG-20150502-WA0002Reporter wa millardayo.com alikuwa mmoja ya watu wa kwanza kupewa taarifa juu ya tukio hili, akafika Kunduchi Dar es salaam ambako Ali Kiba na mdogo wake Abdu Kiba wanaishi.
Nimeongea na Abdu Kiba, amesema yeye alikuwa Masaki, Ali akampigia simu kwamba kuna watu kama 15 hivi wamevamia nyumbani kwao.. waliovamia waliruka ukuta saa tisa usiku, wakavunja mlango wa sebuleni, wakakuta vijana wawili ambao wanaishi nao, wakawapiga na kuwalazimisha wawaoneshe chumba ambacho Ali yumo.. wale vijana wakajibu kwamba Ali hayupo, wakaulizia chumba chake wakaoneshwa chumba cha Abdu Kiba.
Wameingia chumbani wakamkosa Ali Kiba, wameiba vitu vingi vya sebuleni na chumbani pia, pamoja na pesa milioni 2 na nusu zilizokuwa chumbani kwa Abdu.
Abdu amesema alitoa taarifa Polisi, wakafika usiku huo huo na kuanza ukaguzi wa eneo lote la nyumba.
Wakati tukio lote linaendelea Ali alikuwa ndani kwenye chumba kingine, hawakuomuona.
IMG-20150502-WA0000
IMG-20150502-WA0001
IMG-20150502-WA0002
IMG-20150502-WA0003
IMG-20150502-WA0004
IMG-20150502-WA0005
IMG-20150502-WA0006
IMG-20150502-WA0007
IMG-20150502-WA0009
IMG-20150502-WA0018Wale vijana wawili waliokutwa sebuleni wameumizwa kutokana na kupigwa, wametibiwa na kurudi nyumbani.. silaha walizoingia nazo hawajajua ila liko jiwe zito na chuma kizito ambacho kilitumiwa kuvunja milango wakati wanaingia.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

MAGAZETI YETU


 

Magazeti ya Tanzania leo MAY 2 2015 kwenye Udaku, Hardnews na Michezo yameamka na hizi kubwa

DSC02048
Good morning mtu wa nguvu.. Karibu tena Leo May 02 2015 najua huenda MAGAZETI yakachelewa kukufikia hapo ulipo, nimefanya juhudi kuhakikisha unayafahamu yote ya MAGAZETINI TZ asubuhi ya leo kama ilivyo kawaida yangu kila siku kutokea kwenye Udaku, michezo na Hardnews.
Zote zinakufikia hapahapa millardayo.com, unaweza kujiunga na mimi kwenye Facebook, Instagram na Twitter @millardayo zote hizi utazipata.
DSC02048 DSC02049 DSC02050 DSC02051 DSC02052 DSC02053 DSC02054 DSC02055 DSC02056 DSC02057 DSC02058 DSC02059 DSC02060 DSC02061 DSC02063 DSC02064 DSC02065 DSC02066 DSC02067 DSC02068 DSC02069 DSC02070 DSC02071 DSC02072 DSC02073 DSC02074 DSC02075 DSC02076 DSC02077 DSC02078 DSC02079 DSC02080 DSC02081