Thursday, October 22, 2015

Magazeti

Magazeti ya Tanzania leo October 23, 2015 yameamka na hizi kwenye Udaku, Michezo na hardnews

on
October 23, 2015
.
.
Kutoka Dar es Salaam Tanzania leo Ijumaa Octoba 23, 2015 tayari nimeyakusanya Magazeti yote na stori zake kubwakubwa kukusogezea hapa, headlines baada ya headlines kwenye Magazeti ya Udaku, Michezo na Hardnews, zote ziko hapa
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Hii Ndo Kauli ya Nape Baada Ya Kupata Ajali Mbaya Ya Gari

Mgombea ubunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM amezungumzia ajali mbaya ya gari aliyoipata jana usiku alipokuwa njiani akitokea Dar es Salaam kuelekea Lindi.
Nape ameeleza kuwa yuko salama na alipata majeraha madogo ingawa ajali hiyo ilikuwa mbaya kwa kuwa gari lake lilipinduka na kueuka mara kadhaa baada ya tairi ya mbele ya gari lake aina ya Land Cruiser alilokuwa anaendesha kupasuka.
Gari alilopata nalo ajali, Nape Nnauye“Namshukuru Mungu nimetoka salama na nawaomba wananchi wasiwe na hofu japo ajali ilikuwa mbaya maana gari lilipinduka mara kadhaa, nimepata majeraha madogomadogo na michubuko ila ni mzima,” alisema Nape.
Mgombea huyo wa ubunge alikuwa peke yake kwenye gari hilo na ameeleza kuwa mkanda na ‘air bag’ zilimsaidia kupunguza makali ya ajali hiyo.
“Gari limeharibika vibaya ila ninachoshukuru nilikuwa nimefunga mkanda na ‘air bag’ nazo zimenisaidia,” alisema.

Unachopaswa Kufanya siku ya Uchaguzi- Jumapili

Mpekuzi blog

Keshokutwa ni siku itakayokuwa na mambo mengi kwa sababu ya Uchaguzi Mkuu. Pamoja na ratiba ya kila mmoja lakini kupiga kura ni suala linalowaunganisha Watanzania wote. Ili kumchagua rais, wabunge na madiwani, yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:
 
1.Fika katika kituo cha kupigaji kura katika muda uliotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambao ni kati ya 1:00 asubuhi hadi 10:00 jioni.

2.Baada ya kupiga kura unatakiwa kuondoka eneo la kupigia kura

3.Usifanye kampeni ya aina yoyote siku hiyo.

4.Usivae sare zinazokutambulisha kuwa wewe ni mfuasi wa chama chochote cha siasa.

CM Watoa Ratiba Ya Kufunga Kampeni.....Kikwete Kutikisa Mwanza, Mkapa Kuiteka Mbeya Huku Mwinyi Akiiweka Sawa Mtwara

Mpekuzi blog

CCM inapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wake na kwa umma wa Watanzania.

Kufunga Kampeni
CCM itafunga kampeni zake kwa utaratibu mpya na kwa kishindo. Kampeni za CCM zitafungwa kitaifa kwa mikutano mikubwa ya kampeni katika mikoa mitano. Mikutano hiyo itaongozwa na viongozi wa CCM kitaifa waliopo madarakani na wastaafu. Mikoa hiyo na viongozi wakaoongoza mikutano hiyo ni kama ifuatavyo:
 
1. Mwanza – Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, Mgombea Urais, na Ndugu Samia Hassan Suluhu, Mgombea Makamu wa Rais
2. Tanga – Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM
3. Mbeya – Ndugu Benjamin William Mkapa, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
4. Mtwara – Ndugu Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
5. Kigoma – Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM
6. Kilimanjaro – Ndugu Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu
7. Mara – Ndugu Joseph Warioba, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu

Kati ya leo na kesho, maeneo mengine yanaweza kuongezeka. Mikutano hii itaanza saa sita mchana na itarushwa, yote kwa pamoja, kwa matangazo ya moja kwa moja ya vituo vya televisheni vitano na vituoa vya redio 67. 
 
Vilevile, watakaohudhuria katika mikutano hii wataunganishwa moja kwa moja na mkutano wa Mwanza, alipo Mwenyekiti, Mgombea na Mgombea Mwenza, na wataweza kusikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli moja kwa moja kupitia screens zitakazokuwa katika viwanjani vyote hivi saba.

Namna hii ya ufungaji wa kampeni itakuwa ni ya kihistoria, na inadhihirisha nguvu ya CCM inayoiwezesha kufanya mikutano mikubwa ya kampeni kwa siku moja katika maeneo mbalimbali nchini. Lakini pia tutafanya historia katika tasnia ya utangazaji wa televisheni hapa nchini kwa kutangaza na kuunganisha kwa pamoja matukio saba kwa wakati mmoja.

Kwa upande wa Dar es Salaam, tutafanya mkutano mkubwa wa ufungaji wa kampeni za Mkoa wa Dar es Salaam, katika Uwanja wa Jangwani, leo, Ijumaa, tarehe 23 Oktoba 2015. 
 
Siku ya Jumamosi, tarehe 24 Oktoba 2015, Wagombea Ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao kwa namna mahsusi.

Tathmini ya Kampeni
Kama Chama, tumeridhika na ubora na ukubwa wa kampeni tulizofanya licha ya changamoto za hapa na pale. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wamefanya kazi kubwa, na kwa bidii kubwa, na maarifa makubwa. 
 
Wamekuwa barabarani kwa siku 57 wakifanya mikutano kati ya 8 hadi 12 kwa siku. Imani yetu ya ushindi inatokana na kazi kubwa waliyofanya. Pia, CCM inawashukuru viongozi, wapenzi wa washabiki wake – wa makundi mbalimbali ya kijamii - kote nchini kwa kazi kwa kazi kubwa ya kampeni waliyoifanya.

Kutokana na kazi kubwa na nzuri iliyofanyika, na kutokana na mwenendo wa tafiti huru na tafiti zetu za ndani, CCM inategemea ushindi wa asilimia zisizopungua 69.

Uchaguzi wa Amani
CCM haitachoka kuendelea kusisitiza uchaguzi wa amani na utulivu. Sisi kama chama kikubwa cha siasa nchini, chenye wafuasi wengi zaidi, na chenye dhamana ya uongozi wa dola, tutatimiza wajibu wetu wa kuhimiza utulivu kwa wapenzi, washabiki na wanachama wetu. Tunawataka na wenzetu wafanye hivyo.

Kauli za wenzetu kwamba kura zitaibiwa ni kauli za kutojiamini na kujiandaa kufanya vurugu. Kauli za kwamba washabiki wa UKAWA wakishapiga kura wabaki vituoni kulinda kura si kauli za wanaotaka uchaguzi wa amani.

Kwa utaratibu wetu wa uchaguzi, utaratibu wa pekee kwa Chama kulinda kura zake ni kwa kupitia wakala wa vyama waliopo kwenye kila kituo cha kupiga kura na wenye nguvu na mamlaka ya kisheria ya kushuhudia zoezi zima, kuanzia kupiga kura, kuhesabu kura hadi kutangaza matokeo. Kura zinapigwa na kuhesabiwa vituoni mbele ya wasimamizi wa uchaguzi, mawakala wa vyama na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi.

Mawakala wa vyama na wasimamizi wa uchaguzi wanaweka sahihi kwenye fomu za matokeo, na matokeo hayo yanatangazwa na kubandikwa kwenye kituo. Kwenye kituo kikuu cha Tume cha kujumlisha matokeo, mawakala wa vyama pia huwepo na Tume hujumlisha matokeo kutoka kwenye fomu za matokeo za vituo vya nchi nzima zilizosainiwa na mawakala wa vyama kwenye kila kituo.

Kwa viongozi wa UKAWA kuwaambia watu waingie barabarani au kuvizunguka vituo vya kupigia kura eti ili kulinda kura hakuna maana yoyote zaidi ya kutafuta namna ya kuhalalisha vujo, vurugu na uporaji na kuwazuia watu wengine, hasa wanawake, kupiga kura. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vizuie hili jambo kwasababu halina nia njema.

Mkakati wa UKAWA ni kufanya vurugu baada ya kushindwa na kutengeneza mazingira ya mgogoro wa kisiasa ili Jumuiya ya Kimataifa iingilie kati na kupendekeza kugawana madaraka. Mkakati huo hautafanikiwa. Tunaviomba vyombo ya ulinzi na usalama vihakikishe ulinzi na usalama wa watu wote na mali zao siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.

CCM haitakubali hata kidogo ushindi wake kuhojiwa au kutiliwa shaka kwasababu tu ya vurugu zilizoanzishwa na watu wengine.
 
Siku ya Jumamosi, CCM itatangaza namba maalum za simu kwa Watanzania wote ili siku kabla ya uchaguzi, siku ya uchaguzi na mara baada ya uchaguzi, waweze kupiga simu au kutuma ujumbe pale watakapokuwa wanabaini au kushuhudia vitendo vya kuvuruga amani na kuvuruga utaratibu mzima wa uchaguzi.

Kupokea Matokeo
CCM imeweka utaratibu wa kupokea matokeo kwa kutumia mawakala wake moja kwa moja vituoni na kupitia mtandao wa Chama. CCM inategemea kuwa na matokeo ya uchaguzi nchi nzima ifikapo saa nne usiku, siku ya uchaguzi, tarehe 25 Oktoba 2015.

Imetolewa na:
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni
22 Oktoba 2015.

Kortini Kwa Kumtukana Rais Kikwete Na Ridhiwan Wakati Akiwa Baa

Mpekuzi blog
Mkazi wa mjini Moshi, Kyefa Joachim Makundi (33), jana alipandishwa kizimbani akikabiliwa na mashitaka ya kumtukana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya  Kikwete.

Mbali na shitaka hilo, mshitakiwa huyo alisomewa shitaka lingine la kumtukana Ridhiwan Kikwete ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze anayemaliza muda wake.

Mshitakiwa huyo alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya mkoa Kilimanjaro, Joachim Tiganga na kusomewa mashitaka hayo na wakili wa Serikali Kanda ya Moshi, Agatha Pima.

Wakili Pima alidai mahakamani kuwa Oktoba 17 mwaka huu katika baa ya Harambee iliyopo katikati ya mji wa Moshi, mshitakiwa alitumia lugha ya matusi dhidi ya Rais Kikwete na mwanae Ridhiwan.

Ingawa matusi hayo hayakuandikwa kwenye hati ya mashitaka, lakini wakili Pima alidai kitendo hicho ni kinyume cha kifungu 89(1) (a) cha kanuni ya adhabu kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Chini ya kifungu hicho, mtu yeyote anayetumia lugha ya matusi, kuudhi, au kudhalilisha dhidi ya mtu mwingine katika hali ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani anatenda kosa la jinai.

Adhabu inayotolewa kwa mtu anayepatikana na hatia katika kosa hilo ni kifungo cha miezi sita jela.

Hata hivyo, mshitakiwa alikana shitaka hilo ambapo mahakama ilisema dhamana ilikuwa wazi ikiwa mshitakiwa atakuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh1.5 milioni kila mmoja.

Hatma ya Kesi ya Kukaa Mita 200 Baada Ya Kupiga Kura Kutolewa Leo

Mpekuzi blog

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo itatoa uamuzi kuhusu shauri la kikatiba lililofunguliwa na Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Amy Kibatala likihoji uhalali wa wapigakura kukaa mita 200 kutoka kwenye vituo vya kupigia kura.

Mwenyekiti wa Jopo la Majaji watatu linalosikiliza kesi hiyo, Sekieti Kihiyo alisema Dar es Salaam jana wakati akiahirisha kesi hiyo iliyotajwa kwa ajili ya maelekezo muhimu alisema, uamuzi huo utatolewa saa 4:00 asubuhi. Pamoja na Jaji Kihiyo, majaji wengine wa kesi hiyo ni Lugano Mwandamba na Aloycius Mujulizi.

Kesi hiyo ilitajwa jana kwa ajili ya maelekezo muhimu. Kesi hiyo imefunguliwa na Amy anayegombea ubunge Viti Maalumu Jimbo la Kilombero, Morogoro, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC).

Amy anaiomba Mahakama itoe tafsiri ya Kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Uchaguzi Sura ya 343 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010, kinachohusu uhalali wa wananchi kukaa meta 200 kutoka katika kituo cha kupiga kura.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa juzi ambapo Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Tulia Ackson akisaidiwa na jopo la mawakili wanane, aliiomba Mahakama itupilie mbali kesi hiyo kwa kuwa kifungu cha sheria kilichotumika siyo sahihi na pia mlalamikaji hajaeleza jinsi gani haki yake itakiukwa.

Alidai sheria ambayo ilitakiwa kutumika ni ya Matumizi ya Sheria na siyo ya Utekelezaji wa haki za msingi. Pia alidai kifungu wanachoomba kitafsiriwe, kinakataza mikutano ya aina yoyote bila kujali umbali wa kituo cha kupigia kura au cha kuhesabia kura.

Isemavyo sheria ya uchaguzi

Bado siku 3….Shauri la kukaa mita 200 baada ya kupiga kura limeendelea leo Mahakama Kuu Dar

Mahakama KUU LEOOO
.
Tukiwa bado tuko kwenye headlines za Uchaguzi 2015 stori inayochukua kasi katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ni kuhusiana na wananchi kusimama mita 200 pale  wanapomaliza kupiga kura siku ya tarehe 25, 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Tulia Ackson..’Mimi siamini kama uamuzi utakuwa umechelewa kwasababu kesi yenye imechelewa kuja kwa hiyo mimi ninaamini wananchi wafuata sheria watafuata taratibu watafuata  yale waliyoelekezwa hata  kwenye vituo vya kura au chochote kile watakachoelekezwa’ – Tulia Ackson
‘Kifungu cha 104 ibara ya ndogo ya kwanza kinayohistoria inayosema kwamba mtu haruhusiwa kufanya mkutano siku ya Uchaguzi  kiliongezwa 1996  kwa hiyo kabla hakikuwepo kwasababu hakukuwa na haja ya hicho kifungu  lakini kwa kuona kwamba kuna hilo hitaji hicho kifungu kikarekebishwa kikaongezewa hilo katazo la mtu kufanya mkutano kwa hiyo kile kifungu cha 104 ibara ya ndogo ya kwanza hakina utata wowote lakini wananchi wanataka kujua uhalisi ni upi ndio kilichotuleta mahakamani’ – Tulia Ackson
Mimi ninaona mjadala unaenda vizuri kwasababu upande wa mleta malalamiko amesikilizwa kwa kirefu mahakamani itapata fursa ya kupima hizi hoja za pande mbili itatoa uamuzi ambao unaona uko sawa kwa kile kifungu kinachobishaniwa na pia kwa mujibu wa katiba, kisheria anayepaswa kulinda kura ni polisi na kifungu cha 72 kimesema wazi’ – Tulia Ackson
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Naibu Mwanasheria Mkuu

Mkuu wa Jeshi (IGP) Apiga Marufuku Mikusanyiko ya Watu siku ya Kupiga Kura

Jeshi la Polisi nchini, limepiga marufuku mikusanyiko ya watu siku ya  kupiga kura kwa madai kwamba imekuwa ndiyo chanzo cha uvunjifu wa amani.

Pia, Jeshi hilo limesema mikusanyiko ya aina yoyote haitakiwi baada kuhitimishwa kwa kampeni  Oktoba 24, mwaka huu badala yake wanaweza kukusanyika na kusherehekea baada ya matokeo kutangazwa.

Tamko hilo limetolewa leo na mkuu wa jeshi (IGP), Ernest Mangu  akiwa kwenye mazungumzo na wanahabari kuhusu Uchaguzi Mkuu utakaofanyika siku ya jumapili.

Amesema uzoefu wa jeshi hilo unaonyesha kuwa uwepo wa watu kwenye mikusanyiko baada kupiga kura una sababisha vitendo vya uvunjifu wa amani.

Alipoulizwa na wanahabari kuruhusiwa kwa mikusanyiko hiyo katika chaguzi zilizopita, Mangu alijibu: “Polisi inafanya kazi na kupanga mikakati yake kutokana na hali halisi ya mazingira ilivyo, uchaguzi huu ni tofauti na zilizopita.”

Mikusanyiko au vikundi hivi  vinachangia pia kuwatisha watu  wasiopiga kura .Ndiyo maana tunasema  kampeni zikiisha  na ukishapiga kura rudi nyumbani kwako. Kikundi au watu watakaokiuka sheria na taratibu za uchaguzi kwa kisingizio cha kulinda kura, jeshi halitawavumilia,” amesema.

Mangu amesema lengo la kupiga marufuku mikusanyiko hiyo ni kuhakikisha mchakato wa kupiga kura unamalizika katika hali ya amani na utulivu. Amesisitiza kuwa jeshi la polisi linaongozwa na falsafa ya kuelimisha, kushauri, kushawishi na kutumia nguvu inapobidi.

Tumejiandaa vizuri kukabiliana na watu wote watakaobanika kwenda kinyume na utaratibu. Wananchi wasiwe na wasiwasi siku hiyo, wajitokeze kwa wingi kupiga kura, ulinzi utaimarishwa,” amesema Mangu.

VERA SIDIKA is Heartless! Look At What She Is Doing While Her Family Is Busy Mourning For the Loss of Grandmother

Less than a week after her grandmother passed away, Vera Sidika could not miss the opportunity to service one of her sponsors in Nigeria and had to fly out to West Africa but before she jets in, she had to share this.

Check her out:

Zari And Diamond Is Over !......Angry Mama Diamond And Esma Platnumz Talk About It.

According to Globalpublishers Zari and Diamond Platnumz relationship is over !....a source close to Diamond's family says Zari who is now in S.Africa won't return back to Tanzania claiming Diamond's family is fed up by Zari's high profile lifestyle while Diamond's family live the so called Swahili life.
"Diamond's family is the one which is pissed off, you know Zari isn't in Swahili lifestyle, they have been in misunderstanding and now they don't want her anymore, they want Swahili daughter in-law" said the source

When Mama Diamond reached throw phone she was so furious and shouted "even if it is true, I and your Zari are in differences it is non of your business, I don't want interference in my family, what I know is she is not here(Tanzania) but life goes on" said mama Diamond leaving the phone on, after second the phone was picked up by a guy introduced himself as Uncle Salum and told the paparazzi to leave them saying it is more family issue

Then Diamond's sister Esma Platnum took the phone to say "Why are you doing all this?, who interferes your life, about Zari it is over, we have no problem to welcome anyone else, if you know any beautiful lady come with her, our house is very big, and we(Muslim) are allowed to marry even four wives, Zari has ended up there, and we never quarreled with her but we are tired of high profile lifestyle, this time we want our fellow Swahili, Zari is in S.Africa for her children and moving on, we wish her all the best but we never fought"

On the other side, Diamond was unreachable throw his phone, but last week Diamond was quoted as saying he is still with Zari but he can't force her to stay permanently in Dar es salaam as Zari has many businesses both in S.Africa and Uganda so it won't be good to hinder her success.

The two started dating late in 2014 and they have a daughter Latiffah "Princess Tiffah"

Do you believe the two have ended their love...?

MAGUFULI AANZA MIKUTANO YA KILA JIMBO JIJINI DAR ES SALAAM

 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa Ubunge jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Kigamboni jijini Dar es Salaam.

  • Asisitiza yeye atakuwa kiongozi wa maamuzi makini, si magumu
  • Awapongeza CCM, Chadema ,CUF kumpokea kwa shangwe jijini Dar es Salaam
  • Dar yasimama kwa muda, Jiji lawa kijani kila mahali
 Dk. Magufuli amesema wanaosababisha wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kufa kwa kipindupindu watakiona huku akieleza kuna tajiri mmoja amefungua kesi dhidi ya Serikali ambapo amesababisha mradi wa maji kukwama na kwamba akiwa Rais huyo mtu ajiandae maana hawezi kukaa kimya wakati wananchi wanakufa kwa kipindupindu.

 Alisema ngoja nipate urais
Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Temeke Dar es Salaam jana wakati wa mkutano wake wa kuomba kura, Dk.Magufuli alisema anaumizwa na vitendo vinavyofanywa na watu wachache ambao wapo tayari kuona wengine wanakufa lakini wanaaangaia maslahi yao.
“Watanzania najua zimebaki siku nne ili kufanyika kwa uchaguzi mkuu.Najua nitakuwa Rais hao ambao wanatesa wananchi na kusababisha watu kufa kwa kipindupindu sitawavumilia.Watakiona maana siwezi kukaa kimya wakati watu Dar es Salaam wanakunywa maji machafu na matokeo yake wanaugua kipindupindu.
“Mradi wa maji wa Serikali umekwama kwasababu tu kuna mtu mmoja anafedha na ndugu yake anagombea kupitia Ukawa anazuia mradi wa maji usiendelee kwa kufungua kesi mahakamani.Ngoja niwe Rais huyo aliyefungua kesi na hao wanaoshindwa kuamua watakiona.Siwezi kukubali watu wafe kwasababu kuna tajiri ana fedha.Ni bora kesi hiyo ikaamria ili kama Serikali imeshindwa tukate rufaa badala ya kukaa kimya,”alisema.
Alisema kukwama kwa mradi huo kumesababisha wananchi wa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam kukosa maji safi na salama a matokeo yake wananchi wanakufanya kwa kipindupindu na wanaokufa wamo wa CCM, Chadema, CUF, ACT-Wazalendo, NCCR-Mageuzi na hata wasiokuwa na vyama.
Alisema kipindu kinachoendelea Dar es Salaam kinaua wananchi bila kujali dini, rangi wala kabila na kwa mazingira hayo akiwa Rais lazima awachukulie hatua hao ambao wamekuwa sehemu ya kusababisha maisha ya watu kuwa kwenye changamoto lukuki.
Alisema yeye si mkali, lakini ukweli ni kwamba watu ambao wameshindwa kufanya kazi ya kuwatumikia Watanzania hao lazima watamuona mkali lakini ukweli ni kwamba anawapenda watu wote na  kwamba kwake yeye ni kazi tu.
Dk.Magufuli alisema kuwa amekuwa akiongozwa na hofu ya Mungu na kwa mazingira hayo hatakuwa tayari kuona watu wananyanyasika haafu wachache wanafurahia maisha na kuongeza kwenye suala la maji, hao waliofungua kesi na kukwamisha mradi waakunywa maji ya Kilimanjaro wakati wanaokufa wanakunywa maji machafu yenye vimelea vya kipindupindu, hivyo lazima ifike mwisho na bada ya kuapishwa tu ataanza na hao wanaosababisha kuwepo kwa kipindupindu.
Dk.Magufuli alisema kitendo cha tajiri mmoja kujenga nyumba yake juu ya bomba la maji na ameamua kuipeleka Serikali mahakamani na kuongeza “Ngoja niwe Rais haki Amungu atakiona.,”
Dk.Magufuli alisema anatambua kuwa Watanzania wanahitaji kiongozi ambaye atafanya kazi ya kubadilisha maisha yao na kwenye hilo lazima watendaji wa Serikali ya awamu ya tano wahakikishe wanafanya kazi kwa uaminifu mkubwa na watakaoshindwa kufanya kazi hawatakuwa na nafasi kwenye utawala wake.
Alisisitiza anaumizwa anapoona kuna kundi la watu wachache wanasababisha maisha ya wananchi kuwa na changamoto nyingi na kuongeza kuwa hatakuwa na mchezo na wale ambao wapo kwa ajili a maslahi yao  na kuongeza yeye atakuwa Rais wa wote huku akitambua Watanzania wanajitaji maendeleo.
  Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia mbele ya mgombea wa Ubunge jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Wakazi wa Kigamboni wakishangilia jambo wakati mkutano wa kampeni ukiendelea.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhan Madabida akihutubia wakazi wa Mbagala waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli, Zakheem Mbagala.
 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mbagala Zakheem kwenye mkutano wa kampeni za CCM jimbo la Mbagala.
 Wakazi wa Mbagala wakimsikiliza Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Mbagala Issa Mangungu kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika viwanja vya Zakheem, Mbagala.
 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Temeke Ndugu Abbas Mtemvu wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika viwanja vya Mwembeyanga.

 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ubungo kwenye kona ya Ubungo mataa wakati akielekea Sinza kwenye mkutano wa kampeni za CCM.

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ubungo waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya TP Sinza.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akihutubia wakazi wa jimbo la Kinondoni waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli uliofanyika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akihutubia wakazi wa Kinondoni waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kumnadi Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Kinondoni ambao wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanya vya Biafra, Kinondoni , jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
0 comments