Kafulila atua rasmi CCM na Kukabidhiwa Kadi
Baada ya kutangaza kujivua uanachama wa CHADEMA siku ya Jumatano, David Kafulila jana amekabidhiwa kadi ya CCM.
Kafulila
alikabidhiwa kadi ya CCM na Katibu Mwenezi wa CCM, ndg Humphrey
Polepole katika mkutano wa kumnadi mgombea wa udiwani wa chama hicho,
Kata ya Mbweni jijini Dar es salaam
Hapo
awali Kafulila aliwahi kuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na
Maendelo kisha kufuzwa baadae akajiunga na Chama cha NCCR Mageuzi ambapo
alifanikiwa kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini mwaka 2010-2015 na baadaye
kurudi tena Chadema 2016 na hapo juzi jumatano alitangaza kukihama chama
hicho kwa madai upinzani hauna nia ya kupambana na ufisadi.
Kwa
upande wa mkewe ambaye ni Mbunge Viti Maalumu kupitia chama cha
CHADEMA,Jesca Kishoa juzi wakati akizungumza na wanahabari alipingana na
kauli ya mumewe na kusema kwamba, mumewe anapaswa kusema ukweli na
kwamba sababu alizozisema sizo zilizomuondoa ndani ya chama hicho huku
akiongeza kwamba mume wake hana msimamo.
Kafulila
amekabidhiwa kadi hiyo ya CCM ikiwa imebaki siku moja kabla ya
kuhitimishwa kwa kampeni za uchaguzi wa marudio ya nafasi za udiwani kwa
Kata 43 ndani ya Tanzania