Friday, June 12, 2015

Urais 2015: Kambi Ya Lowassa Yazidi Kutanuka........Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Atangaza Rasmi Kumuunga Mkono Edward Lowassa

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Steven Masele, ametangaza kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa katika harakati zake za kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
Masele aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini kabla ya Baraza la Mawaziri kuvunjwa, jana aliibukia katika mkutano wa kutafuta wadhamini wa Lowassa uliofanyika mjini Shinyanga na kusema sasa kada huyo wa CCM anasubiri kupitishwa na vikao vya chama.
 
Akizungumza katika mkutano huo, Masele ambaye pia ni mbunge wa Shinyanga Mjini, alisema yeye pamoja na wana CCM wenzake wanasubiri Kamati Kuu ya CCM ifanye kazi yake kisha wamalizie kumpitisha Lowassa.
 
“Tanzania yote inajua,” alisema Masele na kuuliza “inajua haijui…?” huku akijibiwa na wana CCM, “Inajuaaa…”
 
“Tanzania inajua na dunia nzima inajua kwamba Lowassa yuko hapa. Mimi ni mjumbe wa Mkutano Mkuu, wa NEC wetu wamesema hapa, sisi tumekaa mkao wa kula tunasubiri wafanye kazi yao na sisi tunamalizia kupiga bao tu,” alisema Masele.
 
Mbali na Masele, mawaziri wengine walioonyesha kumuunga mkono Lowassa kwa nyakati tofauti ni pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto, Sophia Simba na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Nyerere aliyemsindikiza kuchukua fomu mjini Dodoma.
 
Katika mkutano huo, alikuwapo pia Mbunge wa Msalala ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige ambaye alimsifia Lowassa kwa utendaji bora alipokuwa Waziri Mkuu na hasa kuwaletea maji wakazi wa Mkoa wa Shinyanga.
 
“Sisi wananchi wa Mkoa wa Shinyanga tuna imani na wewe kwa jambo moja ulilotufanyia. Ulileta maji kutoka Ziwa Victoria. Shinyanga ilikuwa jangwa, lakini ulileta maji, sisi watu wazima tuliona kwa macho,” alisema Maige.
 
Naye Mwenyekiti mstaafu wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, alisema Lowassa ni miongoni mwa viongozi walioandaliwa tangu enzi za Mwalimu Nyerere.
 
“Kuna wakati chama kiliwaandaa vijana wake kwa kuwapeleka chuo kikuu ili wawe viongozi wa baadaye, akiwamo Rais Jakaya Kikwete, Lowassa na wengineo nawahifadhi. Sasa umefika wakati wa Lowassa…,” alisema Guninita.
 
Katika mkutano huo, Lowassa alivunja rekodi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kupata wanachama 7,114 waliojitokeza kumdhamini.
 
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga, Charles Sangula, alisema kati ya wanachama hao, 3,221 walitoka katika wilaya yake, 2,610 Kishapu na 1,283 Kahama.
 
Naye Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Kanali Maulid aliwataka makada wa chama hicho kutochafuana kwa kashfa wakati huu wa uchaguzi, na kuchagua mtu anayekubalika ndani na nje ya chama.
 
“Tumchague mtu anayekubalika ndani na nje ya chama chetu. Lowassa anakubalika. Lakini wako baadhi ya makada wanaochukua fomu na kuanza kuwachafua wenzao. Nashukuru Lowassa hakufanya hivyo,” alisema.
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, alisema kulingana na matokeo ya utafiti uliofanywa na asasi yake ya Tanzana Mzalendo Foundation, Lowassa amekidhi vigezo vyote 10 vya uongozi bora.
 
“Tuna taasisi yetu ya Tanzania Mzalendo Foundation, tumeweka vigezo 10 na vyote Lowassa amepata asilimia 100. Baadhi ya vigezo hivyo ni uzalendo, uvumilivu na kuwa na uamuzi mgumu,” alisema Mgeja.
 
Akizungumza na wana CCM waliokusanyika katika ukumbi huo, Lowassa aliwashukuru na kurudia sababu yake ya kugombea urais.
 
“Nimerudi nyumbani kuwaambia kuwa nimeanza safari ya matumaini. Nilikuwa hapa mwaka 1977 hadi 78, mlinilea vizuri.
 
“Nimegombea kwa sababu nimechoshwa na umasikini. Mwaka 1962, Mwalimu Nyerere alitaja maadui watatu wa Tanzania kuwa ni ujinga, umasikini na maradhi. Lakini hadi leo kuna viongozi wa Tanzania wanajivunia umasikini. Kazi ya kiongozi ni kuwatoa watu kwenye umasikini na kuwapeleka kwenye utajiri,” alisema Lowassa.
 
Aliwataka pia wana CCM kujiandikisha ili wawe na sifa ya kupiga kura.
 
Lowassa aliingia Shinyanga saa sita mchana kwa ndege akiwa na msafara wake kisha wakaelekea kwenye ofisi ya CCM mkoa na baadaye ofisi ya wilaya.

Urais 2015: Kambi Ya Lowassa Yazidi Kutanuka........Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Atangaza Rasmi Kumuunga Mkono Edward Lowassa

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Steven Masele, ametangaza kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa katika harakati zake za kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
Masele aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini kabla ya Baraza la Mawaziri kuvunjwa, jana aliibukia katika mkutano wa kutafuta wadhamini wa Lowassa uliofanyika mjini Shinyanga na kusema sasa kada huyo wa CCM anasubiri kupitishwa na vikao vya chama.
 
Akizungumza katika mkutano huo, Masele ambaye pia ni mbunge wa Shinyanga Mjini, alisema yeye pamoja na wana CCM wenzake wanasubiri Kamati Kuu ya CCM ifanye kazi yake kisha wamalizie kumpitisha Lowassa.
 
“Tanzania yote inajua,” alisema Masele na kuuliza “inajua haijui…?” huku akijibiwa na wana CCM, “Inajuaaa…”
 
“Tanzania inajua na dunia nzima inajua kwamba Lowassa yuko hapa. Mimi ni mjumbe wa Mkutano Mkuu, wa NEC wetu wamesema hapa, sisi tumekaa mkao wa kula tunasubiri wafanye kazi yao na sisi tunamalizia kupiga bao tu,” alisema Masele.
 
Mbali na Masele, mawaziri wengine walioonyesha kumuunga mkono Lowassa kwa nyakati tofauti ni pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto, Sophia Simba na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Nyerere aliyemsindikiza kuchukua fomu mjini Dodoma.
 
Katika mkutano huo, alikuwapo pia Mbunge wa Msalala ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige ambaye alimsifia Lowassa kwa utendaji bora alipokuwa Waziri Mkuu na hasa kuwaletea maji wakazi wa Mkoa wa Shinyanga.
 
“Sisi wananchi wa Mkoa wa Shinyanga tuna imani na wewe kwa jambo moja ulilotufanyia. Ulileta maji kutoka Ziwa Victoria. Shinyanga ilikuwa jangwa, lakini ulileta maji, sisi watu wazima tuliona kwa macho,” alisema Maige.
 
Naye Mwenyekiti mstaafu wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, alisema Lowassa ni miongoni mwa viongozi walioandaliwa tangu enzi za Mwalimu Nyerere.
 
“Kuna wakati chama kiliwaandaa vijana wake kwa kuwapeleka chuo kikuu ili wawe viongozi wa baadaye, akiwamo Rais Jakaya Kikwete, Lowassa na wengineo nawahifadhi. Sasa umefika wakati wa Lowassa…,” alisema Guninita.
 
Katika mkutano huo, Lowassa alivunja rekodi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kupata wanachama 7,114 waliojitokeza kumdhamini.
 
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga, Charles Sangula, alisema kati ya wanachama hao, 3,221 walitoka katika wilaya yake, 2,610 Kishapu na 1,283 Kahama.
 
Naye Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Kanali Maulid aliwataka makada wa chama hicho kutochafuana kwa kashfa wakati huu wa uchaguzi, na kuchagua mtu anayekubalika ndani na nje ya chama.
 
“Tumchague mtu anayekubalika ndani na nje ya chama chetu. Lowassa anakubalika. Lakini wako baadhi ya makada wanaochukua fomu na kuanza kuwachafua wenzao. Nashukuru Lowassa hakufanya hivyo,” alisema.
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, alisema kulingana na matokeo ya utafiti uliofanywa na asasi yake ya Tanzana Mzalendo Foundation, Lowassa amekidhi vigezo vyote 10 vya uongozi bora.
 
“Tuna taasisi yetu ya Tanzania Mzalendo Foundation, tumeweka vigezo 10 na vyote Lowassa amepata asilimia 100. Baadhi ya vigezo hivyo ni uzalendo, uvumilivu na kuwa na uamuzi mgumu,” alisema Mgeja.
 
Akizungumza na wana CCM waliokusanyika katika ukumbi huo, Lowassa aliwashukuru na kurudia sababu yake ya kugombea urais.
 
“Nimerudi nyumbani kuwaambia kuwa nimeanza safari ya matumaini. Nilikuwa hapa mwaka 1977 hadi 78, mlinilea vizuri.
 
“Nimegombea kwa sababu nimechoshwa na umasikini. Mwaka 1962, Mwalimu Nyerere alitaja maadui watatu wa Tanzania kuwa ni ujinga, umasikini na maradhi. Lakini hadi leo kuna viongozi wa Tanzania wanajivunia umasikini. Kazi ya kiongozi ni kuwatoa watu kwenye umasikini na kuwapeleka kwenye utajiri,” alisema Lowassa.
 
Aliwataka pia wana CCM kujiandikisha ili wawe na sifa ya kupiga kura.
 
Lowassa aliingia Shinyanga saa sita mchana kwa ndege akiwa na msafara wake kisha wakaelekea kwenye ofisi ya CCM mkoa na baadaye ofisi ya wilaya.

Urais 2015: Profesa Lipumba Kuchukua Fomu ya Urais Jumapili ya Wiki hii.......Tukio hilo Litarushwa Moja Kwa Moja na Runinga Kadhaa



Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa  Ibrahim Lipumba, Jumapili atachukua fomu ya kugombea urais ndani ya chama hicho na atawaeleza Watanzania sababu ya kuwania nafasi hiyo. 
 
Akizungumza jana, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho, Shaweji Mketo alisema, Profesa Lipumba ndiye mgombea pekee wa urais aliyetangaza nia ya kuwania nafasi hiyo.
 
Alisema muda wa kutangaza nia kwa wagombea urais kupitia chama hicho ulianza Mei 10 hadi Juni 10, mwaka huu.
 
“Kalenda yetu inaonyesha muda wa mwisho wa kutangaza nia ilikuwa juzi na aliyefanya hivyo ni Profesa Lipumba pekee yake,” alisema.
 
Alisema muda wa kuchukua fomu kwa nafasi ya urais kupitia chama hicho ulianza jana na utakamika Juni 14, mwaka huu.
 
“Mkutano huo utakaoonyeshwa moja kwa moja kupitia runinga,” alisema.
 
Mketo alisema vikao vya Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho vitaanza Julai 11 hadi Julai 12, mwaka huu ili kumpitisha mgombea urais, wabunge na madiwani.
 
“Wagombea watakaopitishwa na Baraza watasubiri vikao vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vitakavyotoa mgombea mmoja katika nafasi ya urais, ubunge na udiwani,” alisema. 
 
Kama Ukawa itamteua Profesa Lipumba ambaye kitaalamu ni mchumi itakuwa ni mara ya tano kuwania nafasi ya urais.
 
Akizungumzia nafasi za ubunge, Mketo alisema kati ya majimbo 189 ya Tanzania Bara, wamepata wagombea kwenye majimbo 133.
 
Alisema majimbo 56 bado hayajapata wagombea na kuwataka wafuasi wa chama hicho wenye sifa kuwania. 
 
Mkurugenzi huyo alisema, bado mchakato wa kura za maoni kwa nafasi za ubunge na udiwani zinaendelea katika kanda mbalimbali.

Urais 2015: January Makamba Apokelewa Kishujaa Mkoani Iringa, Apata Wadhamini 600



Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, ameungwa mkono na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoani Iringa ambako alipata wadhamini zaidi ya 600. 
 
Akizungumza na wadhamini wake hao, January alisema endapo atafanikiwa kuwa rais atahakikisha CCM inalirudisha Jimbo la Iringa Mjini ambalo kwa sasa linaongozwa na Mchungaji Peter Msigwa kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwani ataweka kambi katika mji huo. 
 
Alisema kuwa ataimarisha miundombinu, ikiwa ni pamoja na kutanua kiwanja cha ndege cha Nduli na kukifanya kuwa cha kimataifa ili wananchi waweze kupata ajira kitakappingiza watalii wengi na kuongeza pato la mkoa huo pamoja na  kuzijenga barabara kwa kiwango cha lami. 
 
Aidha, January, alisema anaamini CCM kitamchagua kiongozi kwa kujiamini na kuwaomba wananchi wapuuze kauli za watu wanaodai kuwa endapo chama hakitawasimamisha katika  nafasi hiyo basi kitasambaratika. 
 
Alisema wananchi wanapaswa kutambua kuwa dhamana ya nchi hii iko mikononi mwa CCM, hivyo akipata nafasi hiyo au asipopata atakuwa mstari wa mbele katika kukirudisha chama pamoja kutokana na kuwa na makundi katika kipindi hiki cha uchaguzi. 
 
Aliongeza kwa kuwaomba wananchi wa mkoa huo kupitisha ushawishi kwa viongozi wanaopitisha majina kuwa wamchague kijana anayekusudia kuleta mabadiliko ya kweli ambaye ndiyo yeye. 
 
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Wenyeviti wa UVCCM mkoani humo, Kaunda Mwaipiana, alisema vijana hao wanamuunga mkono January katika kipindi chote kwani wanaamini anaweza kuivusha nchi hapa ilipo kutokana na hotuba yake nzuri aliyoitoa wakati akitangaza nia iliyobeba mikakati thatibi ya maendeleo. 
 
Naye Mwenyekiti wa Wilaya ya Iringa, Abeid Kiponza, alimpongeza kwa uthubutu wake wa kuomba nafasi hiyo na kwamba kama alivyoona vijana wenzake wa mkoa wa Iringa wameonesha nia ya kumuunga mkono.

Urais 2015: Wassira Awashambulia Wagombea Wenzake......Awabeza Wanaojaza Watu Wengi kwenye Mikutano, Asema hata yeye Akiamua Anaweza!!



Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira amewashambulia  watangaza  nia  wenzake  kwa  madai  kuwa  wanatumia  pesa kusaka uongozi.
 
Alisema Tanzania inapita katika msimu mgumu kisiasa kutokana na baadhi ya watu kutumia mabilioni ya fedha kusaka uongozi wa nchi, wakati uongozi si biashara. 
 
Wasira alitoa kauli hiyo jana wakati akiwashukuru wanachama wa CCM waliojitokeza kumdhamini katika Uwanja wa CCM Kirumba, kama sehemu ya utaratibu wa chama hicho kuelekea mchakato wa kumpata mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu. 
 
“Jamani wakati wa kujaza watu kwenye viwanja bado haujafika, mikutano ya hadhara bado. Kwa hiyo si kwamba hatuwezi kujaza watu, tukitaka tunaweza, lakini wakati bado, utafika tutajaza watu. 
 
“CCM na taifa kwa sasa vipo katika mazingira magumu kisiasa, rushwa sasa inainyemelea kwa kasi kubwa siasa, hii ni hatari sana, kamwe tusije kubali nchi yetu kuwekwa rehani na kundi la mafisadi. 
 
“Mtu ambaye anataka kuiweka rehani nchi kamwe hawezi kuwa na hoja, ndio sababu mmeanza kuona watu wanaishiwa hoja. Mtanzania yoyote yule anayetumia mabilioni kununua nchi mwisho wa siku ataiuza tu,” alisema Wasira huku wadhamini wake wakishangilia. 
 
Wasira alisema tatizo la rushwa katika siasa ni kubwa kiasi cha kuwafanya baadhi ya watu kuamini kuwa wanaweza kuinunua CCM. 
 
“Hivi nani kakutuma kuinunua CCM? Unainunua kwa niaba ya nani. Nchi yetu haipo sokoni, na wala hatujawahi kutangaza tenda ya kuuza nchi, sasa mabilioni kwenye siasa ya kazi gani?” alihoji. 
 
Aliwasihi Watanzania kuwa makini kwa sababu kuna kila dalili nchi inapelekwa sokoni na watu wachache wasio itakia mema. 
 
Kada huyo mkongwe wa CCM aliwataka Watanzania kujiuliza na kutafakari ni wapi mabilioni yanayotumika yanatoka, na kuongeza kuwa wanaotoa fedha hizo uwezo wao kifedha hauonekani katika kulipa kodi. 
 
Aliwataka wananchi kukataa kugeuzwa kuku wa kienyeji, ambapo alitoa mfano wa mtu anayetaka kuwakusanya kuku huwakusanya kwa kuwarushia mtama au pumba, nao hukimbilia kula bila hata kutaza nyuma au kufikiri. 
 
 “Kuna wenzetu ambao kwa malengo yao maovu wameamua kuwageuza wananchi na kuwafanya kuku wa kienyeji, wanakuja na fedha zao na wanazitumia kuwakusanya kwenye viwanja, wananchi kataeni, vinginevyo majuto ni mjukuu,” alisema. 
 
Tayari Wasira amekwishapata wadhamini katika mikoa 20, ikiwamo sita ya Tanzania Visiwani na jana alidhaminiwa katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita. 
 
Kwa mujibu wa utaratibu wa CCM, kila mtangaza nia anapaswa kupata wadhamini wasiopungua katika mikoa 15 (12 Tanzania Bara na mitatu Tanzania Visiwani), ambapo jumla ya wadhamini wanapaswa kuwa 450. 
 
Mbali ya Wasira kutimiza sharti hilo ndani muda wa siku 8, alisema atakwenda mikoa yote ya Tanzania ili kudhihirishia kuwa amekusudia na ana nia ya dhati ya kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM, Oktoba, mwaka huu. 
 
Pia alitumia fursa hiyo kuwahakikishia Watanzania kuwa yupo imara kabisa kiakili na kimwili kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika uchaguzi huo, na kusema kama atateuliwa, basi ataongoza kampeni mwanzo hadi mwisho bila kutetereka. 
 
Mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu kwa wana-CCM wanaoomba kuteuliwa utahitimishwa Julai 2, mwaka huu mjini Dodoma, na kufuatiwa na vikao vya mchujo vitakavyoanza Julai 9.

Bajeti kuu ya Serikali 2015/ 2016: Kodi ya Pombe na Sigara Haijaongezwa.....Petrol, Dizel na Mafuta ya taa Kodi Imepanda.....PAYE Imepunguzwa, Penshen Imeongezeka



Kwa mara kwanza Bajeti ya 2015/16, ambayo ni ya mwisho ya Serikali ya Awamu ya Nne, haijaongeza kodi katika bidhaa za pombe na sigara, badala yake imeendelea kupandisha kodi katika mafuta huku ikiminya uingizaji wa bidhaa nchini kwa ajili ya kulinda viwanda na wazalishaji wa ndani na kuongeza ajira.

Pia, bajeti hiyo ya mwisho kwa utawala wa Rais Jakaya Kikwete imeweka kipaumbele katika kugharamia Uchaguzi Mkuu, kuweka msukumo maalum kwenye miradi ya umeme vijijini, maji vijijini, kukamilisha miradi ya kimkakati inayoendelea pamoja na kuwekeza kwenye rasilimali watu.

Bajeti hiyo imeeleza mikakati mbalimbali ya ukusanyaji mapato kwa kufanya mageuzi kwenye mfumo wa kodi, kudhibiti mianya ya matumizi ya fedha za Serikali, kupunguza misamaha ya kodi, kupunguza kero za wastaafu kwa kuwaongezea mafao ya mwezi kutoka Sh50,000 hadi Sh85,000, kupunguza Kodi ya Malipo ya Kadri ya Mapato (Paye) kwa asilimia moja na kuanzisha mafao ya kila mwezi kwa wazee.

Akiwasilisha bajeti hiyo ya mwaka wa fedha wa 2015/16, Waziri Mkuya alipendekeza mabadiliko ya sheria mbalimbali zitakazosaidia kupunguza na kuongeza kodi zitazoisadia Serikali kuongeza mapato ili iweze kufanikisha utekeleji wa bajeti ya Sh22.5 trilioni.

Waziri Mkuya aliliomba bunge liridhie mabadiliko katika Sheria ya Sheria ya Mafuta ya Petroli Sura namba 392 ili kuongeza tozo ya mafuta ya petroli na dizeli kutoka Sh50 hadi Sh100.

Pia, tozo ya mafuta ya taa imependekezwa kuongezwa kutoka Sh50 hadi Sh150 ikiwa ni moja ya njia ya kupunguza uwezekano wa uchakachuaji.

“Hatua ya kuongeza Tozo ya Mafuta ya Petroli inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh139.78 bilioni na fedha zote zitaelekezwa katika mfuko wa Rea kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini,” alisema Mkuya huku baadhi ya wabunge wakionyesha kupinga.

Pia, Mkuya alipendekeza mabadiliko katika Sheria Tozo za Mafuta na Barabara namba 220 ili kuongeza tozo katika mafuta ya Dizeli, Petroli na kwa Sh50 hadi kufikia Sh313.

Alisema hatua hiyo ya kuongeza tozo hiyo pia itaongeza mapato kwa takribani Sh136.4 bilioni ambayo alisema yataelekezwa katika mradi wa kusambaza umeme vijijini wa Rea.

Pamoja na maumivu hayo, Mkuya alipendekeza Waziri wa Fedha apatiwe mamlaka ya kusamehe Tozo ya Mafuta ya Petroli kwenye miradi inayotekelezwa kwa misaada ya wafadhili na yenye mikataba isiyohusisha utozaji wa tozo hiyo ili kuondoa usumbufu na ucheleweshaji katika utekelezaji wake.

Katika jitihada za kulinda viwanda vya ndani na kuongeza ajira, Serikali inapendeleza mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mapato namba 332, Sheria ya mauzo ya nje namba 196, Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 na Sheria ya Uwekezaji Tanzania Sura 196.

Waziri Mkuya alibainisha kuwa ili kumpunguzia mzigo mfanyakazi wamependekeza kupunguza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira kutoka asilimia 12 hadi asilimia 11 akibainisha ni dhamira ya Serikali tangu mwaka mwaka 2006/07 kodi hiyo ilipokuwa asilimia 18.5.

Pia, mabadiliko ya Sheria ya Mapato yatashuhudia wafanyabiashara wadogo wakipunguziwa kiwango cha kutozwa kodi kwenye mapato ghafi kwa asilimia 25 ikiwa ni njia ya kuwahamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari. 
 
Mbali na kutoa nafuu hizo, Serikali inatarajia kufanya marekebishao ya Sheria hiyo kwa kuondoa msamaha wa kodi kwenye miradi ya Serikali inayotekelezwa kutokana na mikataba baina ya Serikali na taasisi mbalimbali inayohusisha mikopo ya kibiashara kuanzia Julai Mosi, 2015.

“Hatua hizi za Kodi ya Mapato zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 47.2 bilioni,” alisema Mkuya.

Serikali pia, imependekeza kurejesha msamaha wa tozo ya ufundi stadi kwa sekta ya kilimo ili kutoa unafuu wa kodi kwenye shughuli za kilimo mashambani ambazo hutegemea nguvukazi kwa kiasi kikubwa kabla ya kuanza kupata manufaa kutokana na uwekezaji kwenye kilimo.

Hata hivyo, hali si shwari kwa wafanyabiashara wa bidhaa za ngozi nje ya nchi kutokana na bajeti hiyo kuongeza kiwango cha tozo kinachotozwa kwenye kwenye ngozi ghafi.

Bidhaa zinazosafirishwa kwenda nje ya nchi zitatozwa asilimia 80 ya thamani ya ngozi inapokuwa bandarini (FOB) au dola ya Marekani 0.52 kwa kilo moja kutegemea kiwango kipi ni kikubwa kutoka asilimia 60 ya awali au shilingi 600 kwa kilo moja.

Hatua hiyo, kwa mujibu wa Mkuya inazingatia makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuwianisha viwango vya kodi kwenye ngozi ghafi na pia kuzuia biashara ya magendo na kuhamasisha usindikaji wa ngozi ndani ya ukanda wa Jumuiya ili kuongeza thamani, mapato na ajira.

Hata hivyo, bidhaa za ngozi zilizosindikwa kwa kiwango cha kati zitatozwa asilimia 10 ya kodi ya mauzo ya nje ili kuhamasisha uongezaji thamani wa bidhaa hizo na uwekezaji katika viwanda vya kutengeneza bidhaa za ngozi nchini.

Alisema hatua hizo mbili kwa pamoja zinatarajia kuongeza mfuko wa Serikali kwa Sh920 milioni.

Kampuni zinazozalisha bidhaa za mabomba ya PVC na HDPE zinatarajiwa kupata ahueni baada ya Serikali kuziondoa katika orodha ya bidhaa zinazotambuliwa kuwa ni za mtaji (Deemed Capital Goods) ambazo kwa sasa zinapata msamaha wa kodi kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

“Mapendekezo haya yanazingatia kwamba bidhaa hizi hivi sasa zinazalishwa hapa nchini kwa kiasi cha kutosheleza mahitaji. Hatua hii itasaidia kulinda viwanda vinavyotengeneza mabomba ya aina hiyo na hivyo kuchochea ongezeko la ajira na mapato ya Serikali,” alisema.

Ahueni hiyo itawafikia pia watengenezaji wa matela ya kusafirishia mizigo nchini baada ya bajeti hiyo kufuta msamaha unaotolewa kupitia Kituo cha Uwekezaji kwenye matela hayo, hatua itakayowezesha ushindani katika soko, kuhamasisha uwekezaji mkubwa wa kutengeneza matela nchini, kuongeza ajira na kuongeza mapato ya Serikali.

Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza nchini ili watambuliwe kuwa ni mahsusi kwa watatakiwa kutimiza masharti kadhaa ili kupata ahueni ya kikodi, likiwemo la kuwa mtaji wa jumla usiopungua dola za Marekani 300 milioni (630 bilioni) na mtaji huo upitie taasisi za ndani za kifedha.

“Pia anatakiwa kuwa na uwezo wa kutengeneza ajira za moja kwa moja kwa Watanzania zisizopungua 1,500; ikiwa ni pamoja na idadi inayoridhisha katika ngazi za juu za uongozi wa kampuni. Kuwa na uwezo wa kuzalisha fedha za kigeni au kuzalisha bidhaa mbadala wa zile zinazoagizwa nje,” alieleza Mkuya.

Pia, bajeti hiyo inabana uingizaji wa mchele, sukari na vyuma kwa kuongeza ushuru huku bidhaa za nyuzi za kutengezea nyavu, malighafi za kutengenezea pasta na tambi zikiondolewa kodi.

Yaiokoa Sukari
Katika kudhibiti uingizaji wa sukari kiholela na kulinda viwanda vya ndani, Serikali imeongeza kiwango cha ushuru wa forodha kutoka Dola 200 za Marekani kwa tani au asilimia 100 ya thamani ya bidhaa hiyo inapokuwa imefika bandarini, hadi Dola 460 za Marekani kwa tani au asilimia 100 ya thamani ya bidhaa hiyo inapofika bandarini, kutegemea kiwango cha mzigo.

“Sukari inayotumika viwandani hivi sasa hulipiwa ushuru wa forodha wa asilimia 10 badala ya kiwango cha ushuru kilichoainishwa kisheria cha asilimia 100. Katika utaratibu maalumu unaopendekezwa, waagizaji watatakiwa kulipia ushuru wa asilimia 50 na mara baada ya kuzalisha bidhaa viwandani na kuthibitishwa na Mamlaka ya Mapato kwamba sukari hiyo imetumika ipasavyo watarejeshewa asilimia 40,” alisema Mkuya.

Serikali imepunguza ushuru wa mabasi yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 25 kwa kutoza asilimia 10 badala ya 25 kwa ajili ya mradi wa mabasi wa jiji la Dar es Salaam (DART) kwa mwaka mmoja.

Diamond Platnumz na Vanessa Mdee watajwa kuwania tuzo za MTV Africa Music Awards 2015 stori iko hapa

.
.
Good news ninayotaka kukusogezea ni kwamba majina ya wasanii watakaowania tuzo za MTV Africa Music Awards 2015 yametangazwa jana June 11, ambapo Diamond Platnumz na Vanessa Mdee ni miongoni mwa wasanii waliotajwa kuwania tuzo hizo zitakazotolewa  jijini Durban Afrika Kusini.
Diamond Platnumz ametajwa kuwania vipengele vitatu ambavyo ni BEST MALE, BEST LIVE ACT, BEST COLLABORATION huku Vanessa Mdee akiwania kipengele cha BEST FEMALE.
Tuzo hizo zitatolewa Jumamosi July 18, jijini Durban Afrika Kusini.Hapa nimekuwekea orodha kamili ya wasanii watakaowania tuzo hizo za MTV Africa Music Awards 2015.
BEST MALE
Diamond Platnumz  (Tanzania)
Wizkid (Nigeria)
Davido (Nigeria)
AKA (South Africa)
Sarkodie (Ghana)
BEST FEMALE
Vanessa Mdee (Tanzania)
Busiswa (South Africa)
Yemi Alade (Nigeria)
Seyi Shay (Nigeria)
Bucie (South Africa)
BEST GROUP
B4 (Angola)
Beatenberg (South Africa)
Black Motion (South Africa)
P- Square (Nigeria)
Sauti Sol  (Kenya)
BEST NEW ACT TRANSFORMED BY ABSOLUT
Patoranking (Nigeria)
Stonebwoy (Ghana)
Cassper Nyovest (South Africa)
Duncan (South Africa)
Anna Joyce (Angola)
BEST LIVE ACT
Micasa
Big Nuz
Diamond Platnumz (Tanzania)
Flavour
Toofan
BEST COLLABORATION
Diamond ft Iyanya- Bum Bum ( Tanzania/Nigeria)
Toofan ft Dj Arafat – Apero Remix (Togo/Ivory Coast)
AKA ft Burna Boy, Da L.E.S – All Eyes on me (S.A/Nigeria)
Davido ft Uhuru, Dj Buckz -The Sound ( Nigeria/South Africa)
BEST HIP HOP
Youssoupha (DRC)
AKA (South Africa)
K.O (South Africa)
Olamide (Nigeria)
Phyno (Nigeria)
Cassper Nyvost (South Africa)
BEST ALTERNATIVE /POP
Jimmy Nevis
Fuse ODG
Prime Circle
Jeremy Loops
Nneka
BEST FRANCOPHONE
Dj Araphat ( Ivory Coast)
Jovi (Cameroon)
Toofan (Togo)
Tour 2 Garde (Ivory Coast)
Laurette Le Pearle (DRC)
BEST LUSOPHONE
Ary (Angola
Nelson Freitas (Cape Verde)
B4 (Angola)
NGA (Angola)
Yuri Da Cunha (Angola)
BEST SONG
Cassper Nyovest – “Doc Shebeleza”
DJ Fisherman & Naak MusiQ ft. Dream Team, DJ SK, Danger & DJ Tira – “Call Out”
Euphonik ft. Bob Ezy & Mpumi – “Busa”
K.O ft. Kid X – “Caracara”
Lil Kesh ft. Davido & Olamide – “Shoki Remix”
Mavins – “Dorobucci”
Sauti Sol – “Sura Yako”
Toofan – “Gweta”
Wizkid – “Show You The Money”
Yemi Alade – “Johnny”
VIDEO OF THE YEAR
Bebe Cool – Love You Everyday
Davido Ft Uhuru & DJ Buckz – The Sound
Prime Circle – Doors
Riky Rick – Nafukwa
Seyi Shay Ft Wizkid – Crazy
PERSONALITY OF THE YEAR
Basketmouth (Nigeria)
Bonang Matheba (South Africa)
OC Ukeje (Nigeria)
Trevor Noah (South Africa)
Yaya Toure (Ivory Coast)

Ungependa kujua namna wachezaji na makocha walivyong’ara kwenye tuzo za ligi kuu bara – ingia hapa

Screen Shot 2015-06-11 at 11.30.22 PM
Baba mzazi wa mshambuliaji  kutoka Yanga, Simoni Msuva akipokea tuzo ya mchezaji Bora kwa niaba ya Mwanae.
Usiku wa June 11, kulikuwa na utoaji wa tuzo za  wachezaji zilizokuwa chini ya udhamini wa ligi kuu ya Tanzania Bara, kampuni ya simu mkononi ya Vodacom  kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Towers Dar es Salaam.
Katika utoaji wa tuzo hizo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva ameng’ara kwenye tuzo hizo baada ya kutwaa tuzo mbili.
Msuva amebeba tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu dhidi ya beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba SC na Mrisho Ngassa ambaye kwa sasa ni mchezaji wa timu mpya iliyopo Afrika Kusini.
Hii ni list ya walionia tuzo za ligi kuu ya Tanzania Bara akiwemo Kocha, Timu yenye nidhamu pamoja na Golikipa, Refarii.
Kocha bora – Mbwana Makata (prison)
Mchezaji bora – Simon Msuva (Yanga)
Team yenye nidhamu – Mtibwa
Golikipa bora – Shaaban Kado (Coastal Union)
Refarii bora – Israel Nkongo.
Screen Shot 2015-06-11 at 11.29.47 PM
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa akizungumza machache kwenye utoaji wa tuzo hizo.
Screen Shot 2015-06-11 at 11.29.57 PM
Screen Shot 2015-06-11 at 11.30.08 PM
Screen Shot 2015-06-11 at 11.30.22 PM
Screen Shot 2015-06-11 at 11.30.45 PM
Screen Shot 2015-06-11 at 11.30.56 PM
Screen Shot 2015-06-11 at 11.30.56 PM
Screen Shot 2015-06-11 at 11.31.10 PM
Screen Shot 2015-06-11 at 11.31.25 PM
Screen Shot 2015-06-11 at 11.34.13 PM