Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Nchini, Johnson Minja Kufikishwa Mahakamani LEO
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja mwenye shati la Drafti akiongoza na baadhi ya wanachama wa jumuia hiyo. |
Mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya ya Dodoma leo inatarajia kuanza kusikilizwa kwa maelezo ya awali ya kesi ya uchochezi inayomkabili mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara nchini, Johnson Minja.
Mahakama
ilishindwa kusikiliza maelezo hayo ambayo yalikuwa yatolewe April 9
mwaka huu baada ya upande wa mashtaka kuiambia mahakama kuwa ilikuwa
bado haijakamilisha kuandika wa maelezo hayo.
Akitoa maelezo yake mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Dodoma, Rhoda Ngimilanga, wakili mwandamizi wa serikali, Rose Shio aliiomba mahakama kuiahirisha kesi hiyo kwani upande wa mashtaka ulikuwa bado haujaandika maelezo ya awali kwa ajili ya kesi hiyo.
Kauli hiyo iliungwa mkono na wakili wa Mshtakiwa, Godfrey Wasonga ambaye alimwomba hakimu kutoa muda wa mwezi mmoja ili upande wa mashtaka uweze kukamilisha kazi ya uandikaji wa maelezo hayo ya awali ya kesi hiyo.
Mwenyekiti huyo alifikishwa mahakamni hapo kwa mara ya kwanza Januari 28 mwaka huu akikabiliwa na mashtaka mawili ya uchochezi wa kuwashawishi wafanyabiashara kugomea kutumia mashine za kukusanya kodi za EFDs pamoja na kuwachochea wafanyabiashara mjini Dodoma kufanya kosa.
Minja yupo nje kwa dhamana.

No comments:
Post a Comment