Makonda Atangaza Kamati Kusaidia Madereva.
Serikali imetimiza masharti ya madereva kwa kuunda kamati ya kushughulikia kero na matatizo ya madereva ambayo inatarajia kuanza kazi yake Ijumaa.
Akizungumza Dar es Salaam jana,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisema kamati hiyo itakuwa ya kudumu ambayo itakuwa ikishughulikia kero na matatizo ya barabarani nchini.
Kamati
hiyo itaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Uchukuzi, Shabaan Mwinjaka na
wajumbe wake ni Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, wawakilishi watatu kutoka Chama cha Wamiliki wa
Mabasi Tanzania (Taboa) na Kakoa.
Wengine ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na washiriki watano kutoka kwa chama cha madereva nchini.
Wengine ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na washiriki watano kutoka kwa chama cha madereva nchini.
No comments:
Post a Comment