Wema Sepetu, Aunt Ezekiel Watibuana Kisa Zari wa Diamond
Gazeti la Risasi la leo limeripoti kuwa Mataa wa bongo movies ambao ni mashosti wa kufa na kuzikana, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson wanadaiwa kugombana baada ya Aunt ‘kuposti’ kwenye ukurasa wake wa Instagram tangazo lililohusiana na pati ya mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ iliyofanyika Mlimani City jijini Dar wikiendi iliyopita.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao wa sinema za Kibongo, baada
ya Aunt kuposti tangazo hilo akiwalaumu watu wa mtandao wa huduma za
simu waliomtumia ndipo Wema akaona na kuja juu.
Ilielezwa kwamba baada ya Aunt kutupia picha ya tangazo hilo, Wema
alichukizwa na kitendo hicho huku akimuona Aunt kuwa amemsaliti.
Ilisemekana kwamba katika utetezi wake, Aunt hakupendezwa na tangazo hilo alilotumiwa na mtandao huo wa simu.
“Wema alivyoona alichukia na kusema Aunt alikuwa akimsaliti na alitumia
tangazo lile kijanja kwa ajili ya kuwatangazia watu kuhusu pati ya Zari
wakati anajua kabisa kuwa Wema hazipandi na Zari kwa sababu anatoka na
aliyekuwa mchumba’ke (Diamond),” kilisema chanzo hicho.
Katika sakata hilo, kuna watu ambao waliona Aunt hakuwa na kosa
lakini wapo walioona hakuwa sahihi, jambo ambalo lilichochea ugomvi wao
huku wakidaiwa kukesha wakitukanana.
Gazeti hilo lilipozungumza na Aunt kuhusiana na sakata hilo, alikiri
kutokea akisema kuwa hakuwa na maana mbaya kuposti tangazo hilo lakini
kila mtu ana mtazamo wake.
“Mimi sikumaanisha chochote kibaya kuhusu hilo tangazo na wala
sikujua kama kuna mtu anaweza akalichukulia tofauti kabisa na hapo na
mimi ndiyo nashindwa cha kuzungumza,” alisema Aunt.
Alipopigiwa Wema simu yake iliita bila kupokelewa.
No comments:
Post a Comment