Thursday, May 7, 2015

Ray na Davina Nusura Wazichape Ukumbuni......Chanzo cha Varangati Hilo ni Ray Kushika Makalio ya Davina


Mastaa wa Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Halima Yahaya ‘Davina’ nusura wazichape kavukavu katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar baada ya Ray kudaiwa kumshika mwenzake huyo sehemu nyeti.
 
Kwa mujibu wa chanzo ambacho kilikuwa shuhuda wa tukio hilo, Davina alikuwa amekaa na wasanii wengine pamoja na Mlezi wa Bongo Movies, mama Loraa wakipata vinywaji ndipo Ray alipofika na kuharibu shughuli.

“Wakati Davina anaendelea kupata kinywaji na mama Loraa, alitokea Ray akiwa tayari ‘ameshakula vyombo’ na kumshika Davina kalio kitendo kilishomkasirisha sana msanii huyo na kuanza kumcharukia Ray,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
 
“Davina alinyanyua glasi ya kinywaji chake, akammwagia Ray huku akimuuliza kwa nini alimshika makalio ndipo Ray naye alipopandisha hadi wakataka kukunjana.”
 
Baada ya vurugu hizo kuanza kushika kasi, alitokea mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na wenzake ambao waliwasihi wawili hao waachane na mambo hayo.

No comments:

Post a Comment