Young Dee aeleza kilichosababisha akaachana na label yake ya zamani MDB
Young Dee ameelezea kwa uchungu kitu kilichosababisha akaachana na label
yake ya zamani, Millian Dollar Boys (MDB) baada ya bosi wa kampuni
hiyo, Max Rioba kudai amezingua.
Akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM jana, Young Dee alisema hakutaka kuzungumzia suala la Max kwakuwa anaheshimu mchango wake katika muziki wake.
“Kama uliona nimekukosea, call me, I will apologize sio kwenda kuzungumzia Instagram,” alisema Young Dee.
“Kwahiyo kilichotokea mimi sitaki kumjudge labda alikuwa na hasira. Lakini mimi najua mtu wa karibu ni rahisi kukuathiri kuliko mtu wa mbali. Hayo yote mimi namshukuru kwa mabaya aliyoona kwangu. Wewe unavyotaka mabadiliko sio kila mtu anataka mabadiliko kila kitu ni wewe kama wewe. Mimi namshukuru kama alikuwa kondakta ndio amefanya mabadiliko ya kwenda kumiliki daladala,” alisema Young Dee huku akilia.
Aliongeza, “Mimi sikutaka kusema nimeondoka, sikutaka iwe hivi kwa sababu miaka mingi mimi nimeshatoka kwenye label. Mimi hadi ngoma saa nyingine nalipia mwenyewe, video nyingine tofauti, kuanzia Sio Mchoyo, Fununu. Nagonga beat tu pale halafu najilipia kila kitu. Nyimbo nyingi nataja jina la MDB lakini sio wamelipia wao. Hata ngoma yangu mpya natarajia kuiachia inaitwa ‘Ujanja Ujanja’ nimewataja lakini hawajalipia.”

No comments:
Post a Comment