Tundu Lissu ‘anusa’ bao la mkono Singida Mashariki
Mgombea ubunge wa jimbo la Singida mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Antiphas Mughwai Lissu, amesema kwamba anahofia uchaguzi mkuu hautakuwa huru na wa haki akidai kwamba Jeshi la Polisi limeandaliwa kuhakikisha yeye hatangazwi kuwa mshindi.
Lissu
alisema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mkoani humo
ambapo alibainisha kuwa amepata taarifa kupitia njia ya simu kutoka kwa
meneja wa mkoa wa benki moja mjini hapa na askari polisi wawili, kwamba
jeshi la polisi limeandaa nguvu kubwa kupindua maamuzi ya wapiga kura,
ili mgombea wa CCM atangazwe mshindi
Tundu
Lissu ambaye ni Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, alisema kwa nyakati
tofauti, alipigiwa simu na askari polisi wawili akiwemo wa FFU, na kumpa
taarifa ile ile aliyopewa na meneja wa benki.
Alisema
askari hao walimwambia kuwa jeshi la polisi litatumia magari matatu ya
dareya (yanayotumika kumwaga maji ya kuwasha) na kundi kubwa la askari
na kwamba wameagizwa na viongozi wao,wahakikishe liwalo na liwe, yeye
(Tundu) hatangazwi kushinda ubunge.
Mgombea
huyo alisema kwa akili ya kawaida, jeshi la polisi halipaswi kutuma
nguvu kubwa jimbo la Singida mashariki ambalo toka kampeni zianze,
hapajatokea tukio au dalili za uvunjivu wa amani.
Katika
hatua nyingine, Tundu Lissu ameahidi kwamba endapo atashindwa kihalali,
atakubaliana na matokeo na hatakuwa na kinyongo chochote.Lakini endapo
atashindwa kwa mbinu chafu, hatakubaliana na matokeo hayo machafu.
Naye
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, ACP Sedoyeka, alisema
wamemtaka Lissu kwa kuwa ni mwanasheria, athibitishe tuhuma zake hizo,
ndipo jeshi la polisi liweze kuchukua hatua stahiki.
No comments:
Post a Comment