Thursday, October 22, 2015

Hatma ya Kesi ya Kukaa Mita 200 Baada Ya Kupiga Kura Kutolewa Leo

Mpekuzi blog

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo itatoa uamuzi kuhusu shauri la kikatiba lililofunguliwa na Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Amy Kibatala likihoji uhalali wa wapigakura kukaa mita 200 kutoka kwenye vituo vya kupigia kura.

Mwenyekiti wa Jopo la Majaji watatu linalosikiliza kesi hiyo, Sekieti Kihiyo alisema Dar es Salaam jana wakati akiahirisha kesi hiyo iliyotajwa kwa ajili ya maelekezo muhimu alisema, uamuzi huo utatolewa saa 4:00 asubuhi. Pamoja na Jaji Kihiyo, majaji wengine wa kesi hiyo ni Lugano Mwandamba na Aloycius Mujulizi.

Kesi hiyo ilitajwa jana kwa ajili ya maelekezo muhimu. Kesi hiyo imefunguliwa na Amy anayegombea ubunge Viti Maalumu Jimbo la Kilombero, Morogoro, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC).

Amy anaiomba Mahakama itoe tafsiri ya Kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Uchaguzi Sura ya 343 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010, kinachohusu uhalali wa wananchi kukaa meta 200 kutoka katika kituo cha kupiga kura.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa juzi ambapo Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Tulia Ackson akisaidiwa na jopo la mawakili wanane, aliiomba Mahakama itupilie mbali kesi hiyo kwa kuwa kifungu cha sheria kilichotumika siyo sahihi na pia mlalamikaji hajaeleza jinsi gani haki yake itakiukwa.

Alidai sheria ambayo ilitakiwa kutumika ni ya Matumizi ya Sheria na siyo ya Utekelezaji wa haki za msingi. Pia alidai kifungu wanachoomba kitafsiriwe, kinakataza mikutano ya aina yoyote bila kujali umbali wa kituo cha kupigia kura au cha kuhesabia kura.

Isemavyo sheria ya uchaguzi

No comments:

Post a Comment