Bado siku 3….Shauri la kukaa mita 200 baada ya kupiga kura limeendelea leo Mahakama Kuu Dar
Tukiwa bado tuko kwenye headlines za
Uchaguzi 2015 stori inayochukua kasi katika vyombo vya habari pamoja na
mitandao ni kuhusiana na wananchi kusimama mita 200 pale wanapomaliza
kupiga kura siku ya tarehe 25, 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Tulia Ackson..’Mimi
siamini kama uamuzi utakuwa umechelewa kwasababu kesi yenye imechelewa
kuja kwa hiyo mimi ninaamini wananchi wafuata sheria watafuata taratibu
watafuata yale waliyoelekezwa hata kwenye vituo vya kura au chochote
kile watakachoelekezwa’ – Tulia Ackson
‘Kifungu
cha 104 ibara ya ndogo ya kwanza kinayohistoria inayosema kwamba mtu
haruhusiwa kufanya mkutano siku ya Uchaguzi kiliongezwa 1996 kwa hiyo
kabla hakikuwepo kwasababu hakukuwa na haja ya hicho kifungu lakini kwa
kuona kwamba kuna hilo hitaji hicho kifungu kikarekebishwa kikaongezewa
hilo katazo la mtu kufanya mkutano kwa hiyo kile kifungu cha 104 ibara
ya ndogo ya kwanza hakina utata wowote lakini wananchi wanataka kujua
uhalisi ni upi ndio kilichotuleta mahakamani’ – Tulia Ackson
‘Mimi
ninaona mjadala unaenda vizuri kwasababu upande wa mleta malalamiko
amesikilizwa kwa kirefu mahakamani itapata fursa ya kupima hizi hoja za
pande mbili itatoa uamuzi ambao unaona uko sawa kwa kile kifungu
kinachobishaniwa na pia kwa mujibu wa katiba, kisheria anayepaswa
kulinda kura ni polisi na kifungu cha 72 kimesema wazi’ – Tulia Ackson
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Naibu Mwanasheria Mkuu
No comments:
Post a Comment