Thursday, October 22, 2015

MAGUFULI AANZA MIKUTANO YA KILA JIMBO JIJINI DAR ES SALAAM

 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa Ubunge jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Kigamboni jijini Dar es Salaam.

  • Asisitiza yeye atakuwa kiongozi wa maamuzi makini, si magumu
  • Awapongeza CCM, Chadema ,CUF kumpokea kwa shangwe jijini Dar es Salaam
  • Dar yasimama kwa muda, Jiji lawa kijani kila mahali
 Dk. Magufuli amesema wanaosababisha wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kufa kwa kipindupindu watakiona huku akieleza kuna tajiri mmoja amefungua kesi dhidi ya Serikali ambapo amesababisha mradi wa maji kukwama na kwamba akiwa Rais huyo mtu ajiandae maana hawezi kukaa kimya wakati wananchi wanakufa kwa kipindupindu.

 Alisema ngoja nipate urais
Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Temeke Dar es Salaam jana wakati wa mkutano wake wa kuomba kura, Dk.Magufuli alisema anaumizwa na vitendo vinavyofanywa na watu wachache ambao wapo tayari kuona wengine wanakufa lakini wanaaangaia maslahi yao.
“Watanzania najua zimebaki siku nne ili kufanyika kwa uchaguzi mkuu.Najua nitakuwa Rais hao ambao wanatesa wananchi na kusababisha watu kufa kwa kipindupindu sitawavumilia.Watakiona maana siwezi kukaa kimya wakati watu Dar es Salaam wanakunywa maji machafu na matokeo yake wanaugua kipindupindu.
“Mradi wa maji wa Serikali umekwama kwasababu tu kuna mtu mmoja anafedha na ndugu yake anagombea kupitia Ukawa anazuia mradi wa maji usiendelee kwa kufungua kesi mahakamani.Ngoja niwe Rais huyo aliyefungua kesi na hao wanaoshindwa kuamua watakiona.Siwezi kukubali watu wafe kwasababu kuna tajiri ana fedha.Ni bora kesi hiyo ikaamria ili kama Serikali imeshindwa tukate rufaa badala ya kukaa kimya,”alisema.
Alisema kukwama kwa mradi huo kumesababisha wananchi wa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam kukosa maji safi na salama a matokeo yake wananchi wanakufanya kwa kipindupindu na wanaokufa wamo wa CCM, Chadema, CUF, ACT-Wazalendo, NCCR-Mageuzi na hata wasiokuwa na vyama.
Alisema kipindu kinachoendelea Dar es Salaam kinaua wananchi bila kujali dini, rangi wala kabila na kwa mazingira hayo akiwa Rais lazima awachukulie hatua hao ambao wamekuwa sehemu ya kusababisha maisha ya watu kuwa kwenye changamoto lukuki.
Alisema yeye si mkali, lakini ukweli ni kwamba watu ambao wameshindwa kufanya kazi ya kuwatumikia Watanzania hao lazima watamuona mkali lakini ukweli ni kwamba anawapenda watu wote na  kwamba kwake yeye ni kazi tu.
Dk.Magufuli alisema kuwa amekuwa akiongozwa na hofu ya Mungu na kwa mazingira hayo hatakuwa tayari kuona watu wananyanyasika haafu wachache wanafurahia maisha na kuongeza kwenye suala la maji, hao waliofungua kesi na kukwamisha mradi waakunywa maji ya Kilimanjaro wakati wanaokufa wanakunywa maji machafu yenye vimelea vya kipindupindu, hivyo lazima ifike mwisho na bada ya kuapishwa tu ataanza na hao wanaosababisha kuwepo kwa kipindupindu.
Dk.Magufuli alisema kitendo cha tajiri mmoja kujenga nyumba yake juu ya bomba la maji na ameamua kuipeleka Serikali mahakamani na kuongeza “Ngoja niwe Rais haki Amungu atakiona.,”
Dk.Magufuli alisema anatambua kuwa Watanzania wanahitaji kiongozi ambaye atafanya kazi ya kubadilisha maisha yao na kwenye hilo lazima watendaji wa Serikali ya awamu ya tano wahakikishe wanafanya kazi kwa uaminifu mkubwa na watakaoshindwa kufanya kazi hawatakuwa na nafasi kwenye utawala wake.
Alisisitiza anaumizwa anapoona kuna kundi la watu wachache wanasababisha maisha ya wananchi kuwa na changamoto nyingi na kuongeza kuwa hatakuwa na mchezo na wale ambao wapo kwa ajili a maslahi yao  na kuongeza yeye atakuwa Rais wa wote huku akitambua Watanzania wanajitaji maendeleo.
  Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia mbele ya mgombea wa Ubunge jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Wakazi wa Kigamboni wakishangilia jambo wakati mkutano wa kampeni ukiendelea.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhan Madabida akihutubia wakazi wa Mbagala waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli, Zakheem Mbagala.
 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mbagala Zakheem kwenye mkutano wa kampeni za CCM jimbo la Mbagala.
 Wakazi wa Mbagala wakimsikiliza Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Mbagala Issa Mangungu kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika viwanja vya Zakheem, Mbagala.
 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Temeke Ndugu Abbas Mtemvu wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika viwanja vya Mwembeyanga.

 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ubungo kwenye kona ya Ubungo mataa wakati akielekea Sinza kwenye mkutano wa kampeni za CCM.

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ubungo waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya TP Sinza.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akihutubia wakazi wa jimbo la Kinondoni waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli uliofanyika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akihutubia wakazi wa Kinondoni waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kumnadi Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Kinondoni ambao wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanya vya Biafra, Kinondoni , jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
0 comments

No comments:

Post a Comment