Hii Ndo Kauli ya Nape Baada Ya Kupata Ajali Mbaya Ya Gari
Mgombea ubunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM amezungumzia ajali mbaya ya gari aliyoipata
jana usiku alipokuwa njiani akitokea Dar es Salaam kuelekea Lindi.
Nape ameeleza kuwa yuko salama na alipata majeraha madogo ingawa ajali
hiyo ilikuwa mbaya kwa kuwa gari lake lilipinduka na kueuka mara kadhaa
baada ya tairi ya mbele ya gari lake aina ya Land Cruiser alilokuwa
anaendesha kupasuka.
Gari alilopata nalo ajali, Nape Nnauye“Namshukuru Mungu nimetoka
salama na nawaomba wananchi wasiwe na hofu japo ajali ilikuwa mbaya
maana gari lilipinduka mara kadhaa, nimepata majeraha madogomadogo na
michubuko ila ni mzima,” alisema Nape.
Mgombea huyo wa ubunge alikuwa peke yake kwenye gari hilo na ameeleza
kuwa mkanda na ‘air bag’ zilimsaidia kupunguza makali ya ajali hiyo.
“Gari limeharibika vibaya ila ninachoshukuru nilikuwa nimefunga mkanda na ‘air bag’ nazo zimenisaidia,” alisema.
No comments:
Post a Comment