Mhe Said Soud na Juma Ali Khatib wateuliwa kuwa wajumbe wa Baraza la Mapinduzi
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amewateua
wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara
Maalum:
i.
Mhe.
Said Soud Said – Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara
Maalum
ii.
Mhe.
Juma Ali Khatib – Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara
Maalum.
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 9 Aprili
2016.
Waheshimiwa wote waliotajwa wanaombwa wafike
Ikulu Mjini Zanzibar kesho Jumapili tarehe 10 Aprili 2016
saa 3 kamili za Asubuhi kwa ajili ya kuapishwa.
saa 3 kamili za Asubuhi kwa ajili ya kuapishwa.
(Dkt. Abdulhamid Y. Mzee),
KATIBU WA BARAZA LA MAPINDUZI
NA KATIBU MKUU KIONGOZI,
ZANZIBAR.
9 APRILI, 2016
No comments:
Post a Comment