Saturday, April 9, 2016

TANGAZO
MADIWANI wa manispaa ya Shinyanga  wamekubali shirika la rafiki linalojihusisha na  mradi wa Sauti   kwa utoaji  elimu   ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na kwenye  makundi maalumu kufuata masharti waliyopewa sababu walionekana kwenda kinyume nakushindwa kufuata taratibu.
Masharti hayo ni  kutumia wataalamu wenye sifa,kutokuwa na mtazamo wa kuruhusu ndoa ya jinsia moja,kutosambaza  vifaa tiba kama vile mafuta ya vilainishi pamoja na kuwashirikisha viongozi wa dini na serikali.

Madiwani  waliyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani cha dharura  kilichofanyika mjini hapa ambapo  walidai kuwa shirika hilo limeingia kinyemela nakuanza kutoa elimu kwa wananchi ikiwemo kutotumia wataalamu nakuonekana kuchochea ndoa ya jinsia moja hivyo hawatahitaji  mradi wa shirika hilo kuendelea kuwepo.
Diwani vitimaalum Mariamu Nyangaka  na  diwani wa Moris Mgini wa kata ya Chamaguha  walisema shirika hilo kama litakubali kuendelea na kutoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na makundi maalumu   sawa ila wahakikishe wanafuata masharti watakayopewa na madiwani  ambayo kutumia wataalamu na kutosambaza vifaa tiba kama mafuta kwani walifanya kinyemela  nakupotosha wananchi .
“Kwenye suala la kinga watu lazima wasimamiwe kata ya Kambarage inaongoza  kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi  ndio maana leo tunataka mradi huu uwepo  ila kinachotakiwa  kusiwepo usambazaji wa mafuta ya vilainishi kukubali mafuta hayo ni dalili ya kuruhusu ndoa ya jinsia moja kuendelea kuwepo”alisema  diwani Mshandete.
Naye kaimu mganga mkuu wa manispaa hiyo dkt Edith Kwezi alisema kuwa  maambukizi ya virusi  yameshamili kwa asilimia 4.5  kati ya watu 100 watu 37 wanamaambukizi  pia hivi sasa serikali imeona ni vyema ikatoa elimu katika makundi maalumu suala la  vilainishi ni  vifaa tiba vipo tangu zamani ila vimeongelewa  sio mahala pake hivyo shirika hilo likiri limefanya makosa lirudi kwa wananchi kutoa elimu upya.
Kaimu  katibu tawala wa  wilaya  ya Shinyanga Charles Maugira alisema kuwa  baada ya kupata malalamiko shirika hilo walilifuatilia  nakuzungumza nao  ili kuweza kuboresha na kufuata miongozo kutoka wizarani.
Naye mkuu wa shirika hilo  Gerald Ng’ong’a alisema kuwa  amekiri makosa yaliyojitokeza kamwe hawezi kubadilisha tamaduni za mtanzania na kuiga nje  ikiwa alishtushwa na taarifa zilizokuwa zimeenea ila lengo lake ni kutoa elimu  juu ya maamubikizi ya virusi vya ukimwi na  kwenye makundi maalumu katika kata 15 za manispaa..
Msimamizi  Deusdetit  Mjungu wa shirika la Jphiego kutoka nchini Marekani lililotoa mradi huo kupitia shirika la Rafiki  alisema kuwa kama itaonekana mradi huo kwenda kinyuma na maadili ya mtanzania atajitoa  kwani limekuwa na malengo yake manne ambayo ni kutoa elimu kwenye makundi maalumu na vijana wenye umri kati ya 15 hadi 24 waliokatika hatari ya maambukizi.

No comments:

Post a Comment