Thursday, July 23, 2015

Kambi ya Halima Mdee Yafurugika 


KAMBI ya aliyekuwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), imeanza kusambaratika baada ya wafuasi wake kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo.
 
Wafuasi wake hao wakiongozwa na diwani aliyemaliza muda wake katika Kata ya Kunduchi, Janeth Rithe, wamejiunga jana ACT-Wazalendo na kukabidhiwa kadi na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Msafiri Mtemelwa.
 
Wengine waliopewa kadi za ACT ni Mary Mongi aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Bawacha, Jimbo la Kawe, James Wambura (Katibu wa mbunge Kawe) na Manase Busa aliyefanikisha kwa kiasi kikubwa kuhakikisha Mdee anaingia bungeni katika uchaguzi wa 2010.
 
Wamo pia Katibu Bawacha Tawi la Wazo, Modesta Kalukula na Sizya Issa, Yamoyo Salehe, Sheilah Khamis, Tabia Mohamed, Ashura Salehe, Sophia Makoba na Fatuma Mikidadi.
 
Mbali na hao, chama hicho pia kimepokea wanachama wengine 198 kutoka CCM, Chadema na NCCR-Mageuzi waliojiunga kutoka jimbo hilo.
 
Akizungumza baada ya kuwapokea, Msafiri alisema wanachama hao wameungana ili kuendeleza uzalendo kwa Taifa, hivyo chama hicho kinawakaribisha na wengine.

No comments:

Post a Comment