Profesa Anna Tibaijuka Azomewa Tena Kwa Mara ya Pili Jimboni Mwake.......
Aliyekuwa Mbunge wa Muleba Kusini, Prof Anna Tibaijuka anayewania jimbo
hilo kwa mara ya pili, jana alishushwa jukwaani kwa kuzomewa na wananchi
wake katika kata ya Nshamba wilayani Muleba. Prof Tibaijuka alishushwa
jana wakati wa kampeni za kura za maoni kupitia CCM. Hali ya kuzomewa
ilidumu kwa dakika kadhaa jambo lililofanya Wagombea hao kulazimika
kuondoka. Kwa mara ya kwanza alizomewa juni 8, wakati wa ziara ya katibu
mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika kata hiyo hiyo. Akiwa na Kinana
wananchi walimtuhumu ufisadi wa fedha za Escrow na kushindwa kutekeleza
ahadi ya kuwajengea barabara ya lami.
Source: Mwananchi
Nini maoni yako kuhusu hilo?
Source: Mwananchi
Nini maoni yako kuhusu hilo?
No comments:
Post a Comment