Banza Stone aibuka kuufuta uzushi kuwa ameaga dunia
Muimbaji mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja maarufu kama Banza Stone, ameibuka na kuufuta uzushi unaoenea kuwa amefariki dunia.BANZA STONE YUKO HOI, HAZUNGUMZI, AMEGOMA KULA CHAKULA NA KUNYWA DAWA, WASANII WENGI WAMEMTENGA – MAMA MZAZI
Banza Stone ameongea na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Jumatano hii.
- “Ndio naumwa kichwa kina nisumbua sana lakini sasa hivi naendelea vizuri yaani hizo habari za kuzushiwa kifo naona sasa hivi kwangu sijui hata itakuwa mara ya ngapi, maana nimeshazushiwa sana. Mimi mzima na huyo anayeeneza azunguke na mikoa mingine aeneze vizuri,” alisema Banza.
- “Lakini mimi nipo nyumbani hapa Sinza kwa Mama yangu sasa hivi hapa napata juice yaani marehumu anaongea,” aliongeza Banza kwa kicheko.
“Inshallah nikiwa vizuri mashabiki wangu wataniona tu lakini nipo mzima.”
No comments:
Post a Comment