CCM YABARIKI UBUNGE WA WEMA
Miss
Tanzania 2006 na Staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu akipokea maelekezo
kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Ikungi, Bw. Alluu Ismaili Segamba
kwenye Mkutano uliofanyika Mkoani Singida wiki iliyopita.
Gladness Mallya
BARAKA! Siku chache baada ya mwanadada anayefanya vizuri
kwenye filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kutangaza nia ya kugombea
ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), chama hicho kimempa baraka
mrembo huyo kwa uamuzi wake huo.
Akistorisha na gazeti hili, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape
Nnauye alisema kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi wowote ule
ilimradi awe mwanachama hai, hivyo kwa Wema kugombea ubunge wa viti
maalum ni haki yake na amefanya uamuzi sahihi.
“Kugombea uongozi ni haki ya kila mwanachama, Wema ana haki, kwanza
ni mwanachama hai na baba yake alikuwa mwanachama mzuri sana wa CCM
mpaka anafariki dunia, hivyo chama chetu huwa hakikutani na watu
barabarani tu, bali wanakuwa ni halali kabisa mpaka wanatangaza
kugombea,” alisema Nape.
Hata hivyo, alisema wasanii wote waliotangaza kugombea kupitia chama
hicho hawajakurupuka bali ni wanachama hai na wamekuwa wakishiriki
kwenye shughuli mbalimbali za kichama, tangu kwenye kampeni za mwaka
2010.
Wasanii wengine waliotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM licha
ya Wema ni Ndumbagwe Misayo ëTheaí (Viti Maalum, Kinondoni) na Wastara
Juma (Viti Maalum Morogoro Vijijini).
No comments:
Post a Comment