Sunday, August 23, 2015

Maneno ya Batuli Kuhusiana na Moto Uliyo Teketeza Nyumba yake Jana Akiwa Kwenye Uzinduzi wa Kampeni CCM

Staa wa Bongo movie Batuli, leo amepatwa na ajali ya kuungulia nyumba yake kwa moto wakati akiwa kwenye miangaiko yake ya kila siku katika uzinduzi wa kampeni uliyofanyika Jana Jangwani Dar es salaam.
Watu wengine wamehusisha swala hili na mambo ya chuki za kisiasa lakini me namshukuru Mungu hakuna aliyepoteza maisha wa kujeruhiwa katika ajali hii, ndani kulikuwa na mtoto wa ndugu yangu lakini jirani walivunja vioo na kumnusu lakini mali hakuna nilichookoa zaidi ya magari yangu tu"

Aliongezea kwakusema kwasasa yupo kwenye kikao kwaajili ya mipango ya kupata makazi mengine hapo kesho panapo majariwa.

MKAPA: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa....Chama cha Ukombozi ni CCM Tu

Mpekuzi blog

Rais  Mstaafu  wa  awamu  ya  tatu  mh. Benjamini  William  Mkapa  amesema  kuwa  wapinzani  wanaodai  vyama  vyao  ni  vya  ukombozi  ni  Wapumbavu  na  malofa  kwa  kuwa  watanzania  walikwisha  kombolewa  na  chama  cha  ASP  na  TANU  na  kwamba  chama  pekee  cha  ukombozi  kilichobaki  hivi  sasa  ni  CCM  pekee.

Mkapa  ametoa  kauli  hiyo  leo  katika  viwanja  vya  Jangwani  jijini  Dar  es  Salaam wakati  akimnadi  mgombea  urais  wa  CCM, Mh  John Pombe  Magufuli.

Kumsikiliza  Mkapa  akiongea, Tazama  video  hapo  chini.

ANGALIZO:  Matusi  Hayakubaliki. Toa  Mchango  Wako  Kistaarabu  ili  pamoja  tujenge  nchi  yetu.

Rais Kikwete, Mkapa na Makongoro Nyerere Waishambulia UKAWA kwa zamu......Magufuli Aahidi Kuwashughulikia Mafisadi


Rais Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na Mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro Nyerere wameshambulia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Wakizungumza kwa zamu katika Uwanja wa Jangwani jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua kampeni za chama hicho wamesema, mgombea wa UKAWA hana sera za wapinzani.

Katika mkutano huo uliotawaliwa na vijembe kwa UKAWA Rais Kikwete bila kutaja jina amesema, katika umoja huo kuna mgombea anayesimama kama mgombea binafsi kwa kuwa, sera zake ni tofauti na chama anachosimama kugombea.

Alikwenda mbali na kuonesha kushangazwa kuwa, mmoja vyama viwili ambavyo sio msingi wa chadema ndio vimesimama katika ngazi ya urais na mgombea mwenza wake.

Rais Kikwete aliwalenga Mgombe Urais wa Chadema, Edward Lowassa aliyejiunga na chama hicho akitokea CCM pamoja na Juma Duni Haji aliyejiunga na Chadema akitokea Chama cha Wananchi (CUF).

“Wagombea sio wa Chadema. Mmoja ni CCM na mmoja ni CUF.., Pale kuna mgombea urais ambaye unaweza kusema kama mgombea binafsi maana ana sera zisizofanana na chama,” amesema Rais Kikwete na kuongeza “lakini wameyataka wenyewe.”

Hata hivyo Kikwete hakumwacha Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye aliyejiunga na chama hichi siku moja iliyopita.

Kikwete amesema, pamoja na Sumaye kujieleza lakini hakumwelewa alichokuwa akikusudia “nimejaribu kusikiliza anasema nini lakini sikuelewa kabisa,” amesema.
.
Hata hivyo amesema, CCM haikubahatisha kumteua Dk John Magufuli kuwa mteule wa chama hicho katika urais na kwamba, “tumemweka kwa sifa zake, tunataka rais anayeipenda nchi na anayependa wananchi wa nchi hii.”

“Magufuli anayo sifa hiyo. Tumesema, hatutaki kuchukua mgombea mwenye makando kando mengi na tukatumia muda wetu mwingi kujitetea sisi na yeye kabla ya kuomba kura. Tunamtaka mgombea mwaminifu, mwadilifu. Safari hii Mungu kamchagua Magufuli.”

Kabla ya Rais Kikwete kuzungumza, alitanguliwa na Mkapa ambaye amesema, kuna vyama vinawadanganya Watanzania kuwa wanawatafutia ukombozi-wapumbavu.

“Kuna chama kimoja tu cha ukombozi hapa Tanzania, ni CCM iliyotokana nas ASP na TANU. Kuna vyama vinawadanganya Watanzania eti wanataka kuwakomboa wananchi-wapumbavu, nenda nchi zote za jirani uliza chama cha ukombizi Tanzania watakwambia CCM. Nina kila sababu ya kusema wapumbavu,” amesema.

Hata hivyo amesema, haitoshi kusema mtu anauchukia umasikini peke yake.

“Haitoshi kusema unauchukia umasiki, lazima useme unauchukiaje umasikini?” amesema Mkapa.

Lowassa katika hotuba zake mbele ya wananchi kwenye safari zake za kutafuta wadhamini alipokuwa CCM na hata baada ya kuhamia Chadema, amekuwa akisema anauchukia umasikini-haupendi.

Hata hivyo Mkapa amesema, timu ya CCM ni madhubuti kwa kuwa Magufuli anapenda kushirikiana na wenzake, yupo mstari wa mbele katika kutekeleza mambo yote ya umma na kwamba, wakati wote ni mfano wa tabia nzuri kwa vitendo vyake.

Makongoro ndio aliyefungua ukurasa wa mashambulizi kwa UKAWA kwa kumvaa Sumaye baada ya kujiengua CCM.

Makongoro amesema, anamshangaa Sumaye aliyejiunga na vyama vinavyounda UKAWA na kwamba, alipaswa kukubali matokeo ya kushidwa

Makongoro alianza kwa kibwagizo “kuna mmoja-au niache?- kuna yule kaka yangu mmoja nasikia afya yake sio kweli. Kuna huyu mwingine wa jana (Sumaye)?

“Sumaye tumpige kanzu au tumuache hivihivi, kwani angetulia tungeshughulika naye, kajileta mwenyewe sasa mimi nifanyeje, nimpige tobo?” amesema na kuongeza;

“Sumaye akiwa Waziri Mkuu na kaka yangu Kikwete (Rais Kikwete) waliingia kwenye tano bora, Sumaye alikuwemo, kura zake hazikutosha zikatosha za Kikwete, kwa kuwa aliingia tano bora akasema, chama kizuri.

“Miaka 10 baadaye tano bora hakuingia- Sumaye akatuambia mkimpa Lowassa kugombea urais hiki chama mimi nitahama, sasa huyo ni mkweli ama muongo. Hii ndio shida ya kusema uongo, kusema rahisi kuukumbuka tabu,” amesema Makongoro.

Katika mkutano huo, mgombea mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan amesema, atasimamia na kuwawezesha akina mama.

Pia ameahidi kusimamia pesa Sh. Mil 50 zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kupelekwa vijijini.

“Nitasimamia kuwawezesha akina mama, pesa za vijijini Sh. Mil 50 zitatoka kwa ajili ya vijijini nitazisimamia. Mimba za utotoni nitasimamia kuhakikisha zinaondoka, pia nitahakikisha maji yanapatikana na kusaida akina mama wote,” amesema.

Akizungumzia uzowefu alioupata amesema, amekuwa karibu na Makamu wa Rais wa sasa, Dk. Mohammed Gharibu Bilal hivyo hakuna wasiwasi katika nafasi hiyo.

“Nilikuwa kwenye mikono mizuri ya Dk. Bilal, najua kazi zilivyo nawahakikishia Ofisi ya Makamu wa Rais itasiamama vyema kutekeleza ilani ya uchaguzi pamoja na muungano,” amesema.

Dk. Magufuli amewaahidi watanzania kujikita katika kutetea maendeleo ya wananchi kwenye Nyanja zote.

Dk. Magufuli amesema utawala wake utajikita katika masuala ya kilimo, afya, uchumi na amani ya nchi.

“Watanzania natambua mnapenda kuona mabadiliko, nitasimama vizuri katika miradi ya uchumi. Watanzania nawahakikishia shida na matarajio yenu nayajua, nayafahamu na natambua ninao uwezo wa kuyashughulikia.

"Mnataka suala la rushwa, wizi serikalini vikomeshwe haraka. Kwa kuwa palipo na rushwa ufisadi hakuna maendeleo, nitasimamia hilo,”amesema.

Amesema, kama atachaguliwa “nitahakikisha naunda mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi na majizi yafungwe haraka.”

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Agosti 24










Mgombea Ubunge Jimbo la Ludewa Kwa Tiketi ya CCM, Deo Filikunjombe Apita Bila KUPINGWA

Mpekuzi blog
Mgombea Ubunge katika Jimbo la Ludewa kwa tiketi ya CCM Bw. Deo Filikunjombe, amepita bila kupingwa wilayani humo baada ya Mgombea wa Chadema kushindwa kutimiza Masharti na Taratibu za Ujazaji wa Fomu.

Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Ludewa, Ndg. Wiliam Waziri amesema leo kuwa Mgombea wa Chadema ameshindwa kutimiza taratibu za ujazaji wa fomu hizo hivyo kukosa sifa ya kuwa Mgombea wa Ubunge.

Ndg. Waziri amesema kwamba Kati ya wagombea wanne waliochukua fomu aliyetimiza taratibu ni Mgombea wa CCM, Bw. Deo Filikunjombe pekee;

Wagombea wa DP na TLP waliishindwa kabisa kurejesha fomu huku Mgombea wa Chadema akishindwa kujaza fomu vizuri na kushindwa kurejesha Fomu ya Kiapo cha Maadili ya Sheria za Uchaguzi.

Saturday, August 22, 2015

NAPE ATOA SHUKRANI KWA WAKAZI WA MTAMA AAHIDI KUTOWAANGUSHA

Friday, August 21, 2015
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndio mgombea wa ubunge wa Jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa kata ya Majengo wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wa kuwashukuru wananchi hao kwa kumpigia kura nyingi kwenye mchakato wa kura za maoni.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndio mgombea wa ubunge wa Jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM akiwasalimia viongozi mbali mbali wa CCM ngazi za kata na matawi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano uliofanyika Majengo .
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndio mgombea wa ubunge wa Jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa kata ya Majengo wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wa kuwashukuru wananchi hao kwa kumpigia kura nyingi kwenye mchakato wa kura za maoni.
 Wananchi wa Jimbo la Mtama wakishangilia kabla ya mkutano kuanza.
 Wananchi wa Kata ya Majengo ,Mtama wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza mbunge wao mtarajiwa Nape Nnauye .
 Mbunge wa Mchinga Mhe.Said Mtanda akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kushukuru wananchi waliompigia Katibu Mwenezi wa CCM Taifa ,Nape Nnauye uliofanyika Majengo Mtama.
 Wanancnhi wakimsindikiza Nape Nnauye kwenda jukwaani kuhutubia.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Majengo,Mtama na kuwaeleza atakuwa Mbunge wa mfano kwa kutekeleza kila alichoahidi na kuwa karibu na wananchi muda wote.
 Wananchi wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndie mgombea ubunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM.
Mkutano huo uliofanyika sokoni Majengo ulikuwa wa kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura nyingi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndie mgombea ubunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM akisisitiza jambo kwenye mkutano wa kuwashukuru wapiga kura wake.
 Mmoja wa wagombea waliokuwa wanagombea nafasi ya kuiwakilisha Mtama bungeni akiwasalimu wananchi na kuwahakikishia kuwa atashirikiana na Ndugu Nape Nnauye katika kufanikisha ushindi wa CCM.
 Mgombea Diwani wa kata ya Mnara Bi.Halima R. Mwambe akiwasalim wananchi kwenye mkutano huo.
 Wananchi wakifuatilia kwa makini hotuba za shukrani.
Kikundi cha kwaya cha Majengo kikitumbuiza.

Mama Diamond Platnumz Amfunika Zari kwa Mbizi Kwenye Bwawa la Kuogelea


MAMA’KE Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Sandra’ ameonesha umahiri mkubwa wa kuogelea kiasi cha kumfunika mkwe wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwenye bwawa la kuogelea lililopo nyumbani kwa Diamond, Tegeta-Mivumoni jijini Dar.

Mama huyo alionekana akipiga mbizi na mtoto wake Esma, huku akionyesha manjonjo ya kuogelea kwa kasi tofauti na Zari anavyoogelea katika bwawa hilo.

“Bi mkubwa yuko vizuri sasa maana anapiga mbizi siyo mchezo kabisa hata Zari haoni ndani, spidi yake ni kali kuliko Zari,” alisema mwanafamilia mmoja ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini huku akimtumia mwandishi wetu picha za mama Diamond akiogelea.

Hizi Hapa Sababu Halisi za Ukawa Kutokufungua Kampeni Kama ilivyotarajiwa

Panaposemwa uongo na kuachwa kuukanusha basi waweza kuaminiwa. Zimesikika taarifa kwenye mitandao kuwa kutokufungua kampeni leo au kesho ni kutokana na afya ya lowassa kudhoofu.

Sababu ambazo zimefanya Ukawa kutozindua kampeni kama ilivyotarajiwa leo ni kama zifuatavyo:-

1.Maandalizi ya kuandaa kikosi cha kumnadi mgombea yanamalizwa leo
2. Kumaliza mgogoro wa majimbo yaliobaki kutokana na sintofahamu iliyotokea
3. Kuuzima upepo wa magufuli utakaovuma kesho
4. Kuandaa hoja nzito zakujibu baada ya matarumbeta ya ccm yatakayoropoka kesho
5. Kutafuta uwanja wa kampeni utakaokidhi haja
6. Viongozi wa chama wamikoani na wabunge bado hawajawasili Dar kutokana na urudishaji wa fomu za ubunge jana.


chanzo: mwandishi wa habari aliyewasiliana na JJ mnyika muda huu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Mkapa, Mwinyi kumnadi Dk. Magufuli Jangwani.


Marais wastaafu, Ali  Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, wanatarajiwa kushiriki kwenye ufunguzi wa kampeni za kumnadi mgombea wa urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli Jumapili, jijini Dar es Salaam.

Pia uzinduzi huo unatarajiwa kupambwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wakiongozwa na Nasiib Abdul (Diamond) na bendi mbalimbali ikiwamo ya Tanzania One Theatre (TOT).

Kadhalika, wamo marais wastaafu wa Zanzibar, mawaziri wakuu wastaafu, viongozi wakuu wastaafu wa CCM na viongozi wa serikali, makada kutoka mikoa mbalimbali nchini na wananchi wanatarajiwa kuhudhuria.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu ndani ya CCM zinaeleza kuwa baada ya kampeni hizo kuzinduliwa jijini Dar es Salaam, ziara ya kumnadi itaelekea mikoa ya kusini.

Mikoa hiyo ni Lindi, Mtwara na Ruvuma na kwamba ratiba hiyo itafuata hadi kumalizika nchi nzima.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (pichani), alipoulizwa, alisema ratiba kamili itatolewa baadaye kwa vyombo vya habari.

Kuhusu wageni mbalimbali wa heshima ambao wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo alisema hafahamu na kwamba mgeni rasmi ni mgombea mwenyewe ni Dk. John Magufuli.

Nape akizungumzia ilani ya uchaguzi ya chama hicho, alisema inatarajiwa kuzinduliwa siku ya kuzindua kampeni.Mpekuzi jana ilishuhudia uwanja wa Jangwani ukifanyiwa usafi.

Magari ya ya kubeba mizigo yalionekana yakisomba taka na udogo uliokuwa ukichimbwa eneo hilo.

Lowassa Akwama Kuzindua Kampeni Baada ya Kukosa Uwanja wa Kutosha 'Mafuriko' Yake


Wakati mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli, akitarajiwa kuzindua kampeni zake kesho jijini Dar es Salaam, mgombea kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa amekwama kuzindua kampeni zake  kama ilivyotangazwa awali.

Ukawa unaoundwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), National Convention for Construction and Reform – Mageuzi (NCCR-Mageuzi), Chama cha Wananchi (CUF) na National League for Democracy (NLD) umeahirisha uzinduzi kutokana na kukosa mahali patakapotosha ‘mafuriko’ ya watu watakaohudhuria.

Lowassa alitarajiwa kufungua pazia kwa kuzindua kampeni zake kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa jijini Dar es Salaam, lakini serikali imekataza uwanja huo kutumika kwa kampeni za vyama vya siasa.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene, akiongea na waandishi wa habari Jumatano wiki hii, alisema serikali imefikia hatua hiyo kwa vile kusudio la ujenzi wa uwanja huo ni shughuli za michezo pekee na si vinginevyo.

Kampeni zinazoanza kesho  pia zitahusisha wagombea urais kupitia vyama vingine vya siasa vikiwamo ambavyo wagombe wake hawapewi nafasi kubwa ya kuibua ushindani kama itakavyokuwa ama kukaribia kwa CCM na Ukawa.

Pia kuanza kwa kampeni hizi kutawahusisha wagombea ubunge na udiwani watakaoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Afisa Habari wa Chadema iliyo mshirika katika Ukawa, Tumaini Makene, amesema kuwa, Lowassa anayewania Urais akiwa na mgombea mwenza Juma Duni Haji, ameahirisha kuzindua kampeni zake mpaka itakapotangazwa baadaye.

Alisema kuahirishwa kwa uzinduzi huo kunalengo la kutoa fursa kwa Ukawa kujiweka sawa hasa katika kupata uwanja wenye uwezo wa kuwajumuisha watu wengi na nafasi za kuegesha magari.

“Mgombea wetu hatazindua kampeni leo wala kesho, waache hao wengine waanze sisi tunajipanga kupata eneo zuri litakalotosha kwa idadi kubwa ya watu tunaowatarajia ikiwamo na maegesho ya magari,” alisema.

Makene alisema kutokana na uzeofu uliojionyesha wakati mgombea wao akitafuta wadhamini ama kutambulishwa mikoani, wanaamini kuwa mkutano wao utahudhuriwa na watu wengi, hivyo ni muhimu wakatafuta eneo kubwa la kutosha watu wengi na maegesho ya vyombo vya usafiri.
 
Wakati ikitarajiwa kuzindua kampeni zake kesho, CCM imeshatangaza kamati ya watu 32 kwa ajili ya kutafuta ushindi, ikiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahaman Kinana.

Kamati hiyo ilitangazwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, Jumanne  wiki hii ambaye alimuita Kinana kama mwanaharakati wa kivita anayefahamu medani za ushindi.

Uchaguzi wa mwaka huu ambao unatarajiwa kuwa na changamoto kubwa hasa kutokana na mgombea anayeungwa  mkono na Ukawa (Lowassa) akitokea CCM, kuonyesha upinzani mkubwa dhidi ya  CCM alichokuwa mwanachama wake tangu mwaka 1977.

Licha ya kuwa mwanachana, Lowassa ameshika nafasi tofauti ndani ya CCM na serikalini ikiwamo Uwaziri Mkuu aliojiuzulu mwaka 2008.

Lowassa alikuwa pia katika timu ya kampeni za mwaka 2005 ambapo Rais Jakaya Kikwete aliwania nafasi hiyo kwa mara ya kwanza na kupata ushindi wa kishindo.

Hata hivyo, Julai 29, mwaka huu, Lowassa aliamua kujiunga na Chadema ikiwa ni siku chache baada ya jina lake kukatwa katika hatua za awali za kuwachuja watia nia waliotaka kuwania Urais kupitia CCM.

Jumla ya makada 42 wa CCM walijitokeza kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea urais ambapo 38 walirejesha fomu na Magufuli aliibuka kuwa mshindi atakayegombea Urais katika ‘kumrithi’ Rais Kikwete.
 
Macho na masikio ya wapiga kura wengi kuanzia kesho yataelekezwa kwenye uzinduzi wa kampeni hizo kusikia sera za vyama hivyo vikubwa vinavyoshindana kumpata Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwanafunzi kidato cha II auawa akimwokoa mwenzake asibakwe


Mwanafunzi wa kidato cha pili wa Sekondari ya Nyasubi, Ally Jacob ameuawa baada kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni alipokuwa akijaribu kumwokoa mwanafunzi mwenzake asibakwe.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 9:00 alasiri maeneo ya Nyasubi, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. alikuwa akirejea nyumbani kutokea shuleni.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Justus Kamugisha alidai kuwa mwanafunzi huyo aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya shingoni na mwenzake anayesoma Sekondari ya Kishimba.

Kamugisha alisema sababu za Jacob kuuawa ni kujaribu kumsaidia mwanafunzi mwenzake mwenye umri wa miaka 16 (jina linahifadhiwa) ambaye anasoma kidato cha pili Sekondari ya Nyasubi ili asibakwe na mtuhumiwa ambaye alitaka kufanya unyama huo kwa kushirikiana na mkazi mmoja wa Nyasubi.

Alisema watuhumiwa wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Monday, August 3, 2015

Stori zote zenye uzito kwenye #Magazeti ya Tanzania Agosti 3 2015 ziko hapa, Udaku, Michezo na Hardnews
DSC09939
.
Good morning mtu wangu..
Kutoka Dar es Salaam Tanzania leo Jumatatu Agosti 3,2015 tayari nimeyakusanya Magazeti yote na stori zake kubwakubwa kukusogezea hapa, headlines baada ya headlines kwenye Magazeti ya Udaku, Michezo na Hardnews, zote ziko hapa
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC09960
.
.
.
.
.
.
DSC09964
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.