Thursday, October 22, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI – KUFUNGA KAMPENI

images
CCM inapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wake na kwa umma wa Watanzania.
Kufunga Kampeni
CCM itafunga kampeni zake kwa utaratibu mpya na kwa kishindo. Kampeni za CCM zitafungwa Kitaifa kwa mikutano mikubwa ya kampeni katika mikoa mitano. Mikutano hiyo itaongozwa na viongozi wa CCM Kitaifa waliopo madarakani na wastaafu. Mikoa hiyo na viongozi watakaoongoza mikutano hiyo ni kama ifuatavyo:
1. Mwanza – Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, Mgombea Urais, na Ndugu Samia Hassan Suluhu, Mgombea Makamu wa Rais
2. Tanga – Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM
3. Mbeya – Ndugu Benjamin William Mkapa, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
4. Mtwara – Ndugu Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
5. Kigoma – Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM
6. Kilimanjaro – Ndugu Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu
7. Mara – Ndugu Joseph Warioba, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu
Kati ya leo na kesho, maeneo mengine yanaweza kuongezeka. Mikutano hii itaanza saa sita mchana na itarushwa, yote kwa pamoja, kwa matangazo ya moja kwa moja ya vituo vya televisheni vitano na vituo vya redio 67. Vilevile, watakaohudhuria katika mikutano hii wataunganishwa moja kwa moja na mkutano wa Mwanza, alipo Mwenyekiti, Mgombea na Mgombea Mwenza, na wataweza kusikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli moja kwa moja kupitia screens zitakazokuwa katika viwanja vyote hivi saba.
Namna hii ya ufungaji wa kampeni itakuwa ni ya kihistoria, na inadhihirisha nguvu ya CCM inayoiwezesha kufanya mikutano mikubwa ya kampeni kwa siku moja katika maeneo mbalimbali nchini. Lakini pia tutaweka historia katika tasnia ya utangazaji wa televisheni hapa nchini kwa kutangaza na kuunganisha kwa pamoja matukio saba kwa wakati mmoja.
Kwa upande wa Dar es Salaam, tutafanya mkutano mkubwa wa ufungaji wa kampeni za Mkoa wa Dar es Salaam, katika Uwanja wa Jangwani, kesho, Ijumaa, tarehe 23 Oktoba 2015. Siku ya Jumamosi, tarehe 24 Oktoba 2015, Wagombea Ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao kwa namna mahsusi.
Tathmini ya Kampeni
Kama Chama, tumeridhika na ubora na ukubwa wa kampeni tulizofanya licha ya changamoto za hapa na pale. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wamefanya kazi kubwa, na kwa bidii kubwa, na maarifa makubwa. Wamekuwa barabarani kwa siku 57 wakifanya mikutano kati ya 8 hadi 12 kwa siku. Imani yetu ya ushindi inatokana na kazi kubwa waliyofanya. Pia, CCM inawashukuru viongozi, wapenzi wa washabiki wake – wa makundi mbalimbali ya kijamii – kote nchini kwa kazi kubwa ya kampeni waliyoifanya.
Kutokana na kazi kubwa na nzuri iliyofanyika, na kutokana na mwenendo wa tafiti huru na tafiti zetu za ndani, CCM inategemea ushindi wa asilimia zisizopungua 69.
Uchaguzi wa Amani
CCM haitachoka kuendelea kusisitiza uchaguzi wa amani na utulivu. Sisi kama chama kikubwa cha siasa nchini, chenye wafuasi wengi zaidi, na chenye dhamana ya uongozi wa dola, tutatimiza wajibu wetu wa kuhimiza utulivu kwa wapenzi, washabiki na wanachama wetu. Tunawataka na wenzetu wafanye hivyo.
Kauli za wenzetu kwamba kura zitaibiwa ni kauli za kutojiamini na kujiandaa kufanya vurugu. Kauli za kwamba washabiki wa UKAWA wakishapiga kura wabaki vituoni kulinda kura si kauli za wanaotaka uchaguzi wa amani.
Kwa utaratibu wetu wa uchaguzi, utaratibu wa pekee kwa Chama kulinda kura zake ni kwa kupitia wakala wa vyama waliopo kwenye kila kituo cha kupiga kura na wenye nguvu na mamlaka ya kisheria ya kushuhudia zoezi zima, kuanzia kupiga kura, kuhesabu kura hadi kutangaza matokeo. Kura zinapigwa na kuhesabiwa vituoni mbele ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Mawakala wa vyama na Waangalizi wa Uchaguzi wa ndani na nje ya nchi. Mawakala wa vyama na Wasimamizi wa Uchaguzi wanaweka sahihi kwenye fomu za matokeo, na matokeo hayo yanatangazwa na kubandikwa kwenye kituo. Kwenye kituo kikuu cha Tume cha kujumlisha matokeo, mawakala wa vyama pia huwepo na Tume hujumlisha matokeo kutoka kwenye fomu za matokeo za vituo vya nchi nzima zilizosainiwa na mawakala wa vyama kwenye kila kituo. Kwa viongozi wa UKAWA kuwaambia watu waingie barabarani au kuvizunguka vituo vya kupigia kura eti ili kulinda kura hakuna maana yoyote zaidi ya kutafuta namna ya kuhalalisha fujo, vurugu na uporaji na kuwazuia watu wengine, hasa wanawake, kupiga kura. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vizuie hili jambo kwa sababu halina nia njema.
Mkakati wa UKAWA ni kufanya vurugu baada ya kushindwa na kutengeneza mazingira ya mgogoro wa kisiasa ili Jumuiya ya Kimataifa iingilie kati na kupendekeza kugawana madaraka. Mkakati huo hautafanikiwa. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vihakikishe ulinzi na usalama wa watu wote na mali zao siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.
CCM haitakubali hata kidogo ushindi wake kuhojiwa au kutiliwa shaka kwa sababu tu ya vurugu zilizoanzishwa na watu wengine.
Siku ya Jumamosi, CCM itatangaza namba maalum za simu kwa Watanzania wote ili siku kabla ya Uchaguzi, siku ya Uchaguzi na mara baada ya uchaguzi, waweze kupiga simu au kutuma ujumbe pale watakapokuwa wanabaini au kushuhudia vitendo vya kuvuruga amani na kuvuruga utaratibu mzima wa Uchaguzi.
Kupokea Matokeo
CCM imeweka utaratibu wa kupokea matokeo kwa kutumia Mawakala wake moja kwa moja vituoni na kupitia mtandao wa Chama. CCM inategemea kuwa na matokeo ya Uchaguzi nchi nzima ifikapo saa nne usiku, siku ya Uchaguzi, tarehe 25 Oktoba 2015.
Imetolewa na:
January Makamba
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
MJUMBE WA KAMATI YA KAMPENI
22 OKTOBA 2015

Ukimwona Mamba kasinzia usidanganyike kabisa, hili ndio pozi lake la mtego !!

on
October 22, 2015
Mamba ni mmoja ya wanyama ambao kama ukikutana nao kwenye maji wana mabalaa yao, unaweza ukamchukulia kwamba sio mnyama mwenye mbio sana ukilinganisha na wanyawa wengine kama Simba na Chui, lakini ukimkuta kwenye maji balaa lake sio dogo !!
Wakati mwingine ni vizuri kujua tabia za wanyama ili kama kwa bahati mbaya ukikutana nae uwe unajua kabisa jinsi ya kuchukua tahadhari mapema.
Leo nimeipata hii ambayo sikuwahi kuijua siku za nyuma, Wataalam wa Australia wamekuja na majibu ambayo huenda ni watu wengi hawajui… kumbe Mamba anaweza kulala kwa kufunga jicho moja huku moja likiwa wazi…hilo ndio pozi lake la kujilinda na kuvizia pia wanyama ambao ndio chakula chake.
gettyimages-53343277-1-736x414
kingine ni kwamba Ubongo wa Mamba unaweza kulala nusu huku nusu ukibaki unafanya kazi sawa kabisa !! Kama na wewe ulikuwa huzijui hizo, basi nimekusogezea ili ikitokea unakutana na mamba amesinzia uwe na tahadhari yako kabisa hata kabla hujamsogelea.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Hili la JWTZ Kuanza Kupeleka Vifaru Mtwara Limekaa aje? Wanawake na Watoto Waanza Kuondoka Mtwara Wakihofia Vurugu

Wakuu nimeona Sauti ya Ujerumani DW wakiripoti kwamba Mtwara watu wamenza kuondoka mara baada ya kuona magari ya kijeshi pamoja na vifaru mtaani sasa inakuwaje kipindi hiki magari ya kijeshi mtaani?

Shirika  la  utangazaji  la  Ujererumani,DW  limeripoti  leo  mchana  kuwa idadi kubwa ya watu  wameanza kuondoka  mkoani Mtwara  wakihofia hali ya usalama wakati wa uchaguzi.

Kwa mujibu wa Dw,watu wengi  wanaoondoka  ni wanawake na watoto, hali ambayo inaelezewa inatokana na vurugu za gesi za mwaka 2013,  kuonekana kwa baadhi ya vifaa vya jeshi na wanajeshi wakiwa kwenye vifaru.

Mke wa Mtikila ataka iundwe Tume kuchunguza kifo cha mumewe


Mama Mtikila Ameongea Haya Mbele ya Waandishi wa Habari:


Ndugu Wana-Habari,

Kabla sijawaeleza kilichonilazimisha kuwaomba kuongea nanyinyi, kwanza niwarudishe nyuma kama miaka saba iliyopita, ndipo maisha ya Baba, Mchungaji, Mwenyekiti na mume wangu, Mchungaji Christopher Reuben Mtikila yalipoanzwa kuwindwa:-

MAUWAJI YA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE

Mara tu baada ya kifo cha mbunge huyo, mchungaji Mtikila alitoa ripoti maalumu juu ya mauaji yake ambayo ilimjengea uadui kati ya baadhi ya vyama vya siasa pamoja na wafanyabiashara wakubwa ambao hadi leo ni wapinzani wa serikali hapa nchini.--Mchungaji Mtikila hadi anafikwa na mauti aliendelea kupata upinzani wa aina hiyo hiyo kwa sababu mchungaji Mtikila aliendelea kudai haki ya marehemu Chacha Zakayo Wangwe.

MAUAJI YA BULIGI

Hii ilimwongezea uadui baada ya kusema/kuandika ukweli juu ya watutsi wa nchi jirani kuvamia nchi yetu kwa mtindo wa kujifanya wafugaji wasio hama. L.I.F. ilibaini uharamia huo kuwa hawakuwa wafugaji bali walikuwa askari wa Jeshi la Rwanda waliokuwa na mpango wa kutumika na Chama kimoja cha siasa hapa nchini ili kuleta mapigano yatakayo zaa mapinduzi. Jambo hili lilisababisha Rais wa Rwanda, Paulo Kagame kutamka hadharani kuwa angemkamata Mwenyekiti wa chama chetu cha DP--kwa lengo la kumuua na Serikali yetu inajua hilo. Mara baada ya ripoti hiyo kutolewa na Mchungaji Mtikila "operation Kimbunga" ilizaliwa na kuponya nchi yetu; lakini chuki na uadui uliendelea dhidi ya Mchungaji Mtikila.

MCHAKATO WA URAIS NDANI YA CCM

Ikumbukwe kuwa mara baada ya mchakato wa kutafuta mgombea urais kwa tiketi ya CCM kuanza DP ilitoa ripoti iliyowahusu wagombea sita wa CCM waliotumia mapesa mengi na kuanza kampeni kabla ya muda na kusisitiza kuwa Lowasa ni mtu asiefaa kuwa Rais wa nchi yetu. Na baada ya kuhama CCM, Mwenyekiti wetu aliendelea kutoa tahadhari hadharani jinsi Lowasa asivyofaa kuwa Rais wa nchi yetu hivyo likaendeleza uadui wake na Chama.

VITISHO--KUANZA

Mchungaji Mtikila alipata nafasi ya kuongea katika kipindi kinachorushwa na STAR TV cha asubuhi "TUONGEE" ndipo alipoanza kupata vitisho toka kwa watu mbali mbali wengine kupitia kwenye simu wengine uso kwa uso. Kipindi cha kwanza kilirushwa tarehe 25/9/2015 na kufuatwa na cha tarehe 27/9/2015. Alipotoka studio hiyo asubuhi ya tarehe 27/9/2015 ndipo watu waliodai wametumwa na Mhe. Edward Ngoyai Lowasa na Mhe Frederick Sumaye walimuomba wampe nusu bilioni na apewe maovu ya mgombea urais wa CCM ili afunike-alivyowamaliza wao.

Mchungaji Mtikila aliwapuuzia mbali wale wajumbe waliyotumwa kwani aliawaambia kuwa yeye siyo malaya wa kuuza utu wake kwa tende na haluwa. Yakumbukwe kuwa mahojiano kwenye hivyo vipindi viwili kwenye STAR TV hayakuwa yanatetea mtu au chama yalikuwa yanatetea Taifa letu lipate Rais anayefaa.

Kwa hiyo basi wale waliochukizwa na mahojiano hayo ni wale amabo hawakubaliani na mawaidha ya Mchungaji Mikila aliyokuwa anawatahadharisha watanzania juu ya Mh. Lowasa kuwa hatari kwa usalama wa taifa letu kama atakuwa Rais wa nchi yetu. Hao watu ndiyo waliopanga mpango mzima wa mauaji ya Mh. Mtikila ambaye ni mume wangu.

Wakati yuko Bunda mjini watu wasiofahamika walimfuatafuata na tarehe 26/9/2015 gari lake lilifukuzwa na gari usiku wakati alipokuwa anatoka Bunda kwenda Mwanza kufanya mahojiano ya tarehe 27/9/2015 na Star Tv.

MPANGO WA MAUAJI HALISI

Mchungaji Mtikila alitafutiwa gari na Victor James Manyahi ambayo ilikuwa na madereva wawili. Mchungaji madereva hakuwajua. Hata mimi madereva hao sikuwajua wala sikuwaona. Walikodiwa kutoka wapi sijui, wala sijui wanafanana vipi. Na wala sijui Victor Manyahi alikodi gari hilo kwa nani na makubaliano yepi sijui.

Kwa hivyo basi, kwenye gari aliyosafiri nayo Mchungaji Mtikila kulikuwamo madereva wawili na Mgaya Patrick (tunayemfahamu). Wakati wanakwenda gari lilipata ajali Makambako. Wakati wanarudi wakapata “ajali” Msolwa Mchungaji akapatwa na mauti peke yake. Ajali ilikuwa mbaya sana-IKAUWA MTU MMOJA AMBAYE NI MCHUNGAJI MTIKILA NA HAKUKUWA MAJELUHI HATA MMOJA.-Cha ajabu kwangu ni kuwa mtu ambaye alikuwa ni mlinzi wa kujitolea (body guard) Mgaya Patrick sijawahi kumuona usoni mwangu kabla na hata baada ya mazishi kuja kuniambia kilichotokea eneo la ajali. Pamoja na juhudi zangu zote za kumpigia simu mara kadhaa aje anijuze Mgaya Patrick hajatokea hadi sasa ndugu zangu wanahabari ninapoongea nanyi. Lakini si kwamba huyu mtu hayupo, yupo lakini sijaonana naye, kwa nini sijui. Je ndugu zangu wanahabari nimuweke Mgaya Patrick kwenye fungu gani?

Ndugu Wana-Habari, baada ya kuwaelezea yote hapo juu nakuja kwenye suala nililowaomba nikutane nanyi ili niongee mbele yenu kuwa sikubaliani na uchunguzi kuwa Mchungaji Christopher Reuben Mtikila amekufa kwa ajali. Sikubaliani na kazi ya Polisi kuwa wamefunga file lao kutokana na Post-mortem report kuwa mauti yaliotokana na ajali. Nafuta kabisa taarifa--iliyotoka katika gazeti la Nipashe chini ya kichwa cha habari kuwa “FAMILIA YAFUNGUKA KIFO CHA MTIKILA”-ilitolewa mapema mno. Kila mwanafamilia alikuwa hajawa tayari kutoa kauli yoyote. Kwa niaba ya Chama na familia ya Mchungaji Christopher Reuben Mtikila naomba tusaidiwe yafuatayo kusudi haki ya mpendwa wetu-ionekane--inatendeka:-

Kwa sababu mtandao umeanza kuficha ukweli ili kulinda wauaji; tunaomba Mheshimiwa Rais aingilie utata wa kifo cha Mheshimiwa Mchungaji Christopher Reuben Mtikila kwa kuunda tume ya uchunguzi isiyohusisha polisi.

Tunaiomba mamlaka ya mawasiliano yaani Tanzania Communications Regulatory Authority, TCRA itusaidie yafuatayo:-

(a)----Mtu aliyeweka picha kwanza alfajiri kuonyesha mauti ya Mhe Mchungaji Mtikila alikuwa wapi? Kwenye tukio? Au ni hao wauaji walikuwa wanatoa taarifa kwa waajiri wao kuwa wamekamilisha kazi!

(b)----Mtu aliyeweka picha ya Dr. Jean-Bosco Ngendahimana kwenye mtandao kuwa ndiye anahusika na mauti ya Mhe. Mch. Mtikila na kumusingizia kuwa amekamatwa na polisi akiwa anajiandaa kukimbia;

(c)-----Wote wanaoendelea kumhusisha Dr. Jean-Bosco Ngendahimana na mauaji ya Mhe. Mchungaji Mtikila, tuwafahamu ili watueleze vizuri.

Ukweli na haki ni vya Mungu hakuna anayeweza kuviua au kuvizuia. Tunategemea Mungu atawatumia watendaji wa Serikali/nchi yetu wenye nia njema, na makusudi yaliyonyooka kwa ajili ya nchi yetu ili Mhe. Mchungaji Mtikila apewe haki dhidi ya wauaji wake.

Asanteni,


Georgia C . Mtikila,

-KM DP/Msemaji-Familia

Sababu Zinazopelekea Wasichana wa Kileo Mpigwe Chini na Wanaume Kimapenzi

Kumekuwa na ulalamishi sana miaka ya karibuni kuwa wanaume sijui tupoje,tunawaacha bila sababu ila kumbe sababu zipo tu ila wengi hawajazijuaga tu.Nimeona nibainishe sababu zangu kadhaa ambazo ni hizi hapa:

1. Hufanyi chaguo sahihi
Marazote unapenda mtu mwenye swaga,status ambaye kila msichana anamtaka bila kujali kuwa swaga si jambo la msingi katika mahusiano ila penzi la kweli na utu.80% ya wale mnaowadiss ndio wana mapenzi ya kweli na utu uliotukuka!Wenye swaga huwa hawana future wanasuuza rungu tu wakati wakiskilizia kali mara nyingi akitokea mkali zaidi ujue ushalia!

2. Kupenda ready made
Jaribuni kuanza mapenzi na mtu sahihi tokea akiwa chini ili mfurahie mafanikio badae.Mara nyingi mwanaume ulieanza nae kwenye msoto hana jeuri ya kukuacha.Unakurupuka kwa mtu mwenye life lake tayari hujui kahaso vipi kuupata mchomoko unaleta shobo za kujitia unamjua sana.Utaumia maana ukizingua kidogo anapita hivi!

3. Kuendekeza uzungu mwingi
Kina dada wengi siku hizi hampendi kuwa chini,hutaki kuishi uhalisia ila unaendekeza u-instagram na tamthilia nyingi kitu ambacho sio sahihi.Ni nani ambaye kila 24/7 kwake sikukuu na jua lilivyo kali hapa bongo.Kila siku shopping kweli? Niwape cheat,wanaume wengi wanalijua hilo so wana row with the tide.Mlume ndago hawezi kuwekeza kwenye bidhaa feki ndio maana mnaona tunaoa midemu mikauzu yenye full uhasilia na ina akili za maisha baada ya miaka miwili/mitatu ya huduma wanakuwa bomba ile mbaya watu wanabaki midomo wazi.Hivyo basi be real jameni...

4.Tamaa tamaa
Hii inaweza isiwe kwa mademu wote ila wengi siku hizi mnamaindisha mapene,mizinga mingi bila kujali kipato cha ME ili yasapoti pointi namba 3 apo juu.Hii itakufanya uwe na mibwana mingi kitu ambacho sio rahisi mwanaume mwenye akili timamu na anayejua thamani ya penzi kukivumilia.Ukimwi upo na unaua jamani! Hamna mwanaume atayependa umchanganyie kimaisha na akigundua tu anatoka baru.

5. Personal traits
Je una akili za maisha(mipango)? ni msafi,msikivu,mvumilivu,unajia mini,mwaminifu,mkweli,huna choyo,sio mswahili kwa sana,unapendeka n.k hivi ni baadhi vitu muhimu sana ambavyo inabidi mwanamke avibalansishe na mbele ya mwanaume sahihi atajitwalia upendo wa kweli.

6. Sex
Inakubidi uwe fresh pia hapa ili uweze kuwa mtamu zaidi.Kuna wanaume ambao wamefanikiwa kutulizwa tuli baada ya kukutana na mashine nzuri sana ukijumlisha na yaliomo kwenye point 5 apo juu wakaamua kuoa kabisa.Wapo! Kwahiyo nafikiri pia umahiri wa kitandani una nafasi kubwa zaidi ya kumtuliza mwanaume sahihi! Ukiwa legelege utaachwa tu maana hamna namna nyingine.

NB: HUU NI MTAZAMO TU WAKUU MSIJENGE CHUKI

Naomba na wengine muongeze sababu nyingine ili wapate majibu kwa nini wanaachwa bila sababu!

Mkuu wa Jeshi (IGP) Apiga Marufuku Mikusanyiko ya Watu siku ya Kupiga Kura


Jeshi la Polisi nchini, limepiga marufuku mikusanyiko ya watu siku ya  kupiga kura kwa madai kwamba imekuwa ndiyo chanzo cha uvunjifu wa amani.

Pia, Jeshi hilo limesema mikusanyiko ya aina yoyote haitakiwi baada kuhitimishwa kwa kampeni  Oktoba 24, mwaka huu badala yake wanaweza kukusanyika na kusherehekea baada ya matokeo kutangazwa.

Tamko hilo limetolewa leo na mkuu wa jeshi (IGP), Ernest Mangu  akiwa kwenye mazungumzo na wanahabari kuhusu Uchaguzi Mkuu utakaofanyika siku ya jumapili.

Amesema uzoefu wa jeshi hilo unaonyesha kuwa uwepo wa watu kwenye mikusanyiko baada kupiga kura una sababisha vitendo vya uvunjifu wa amani.

Alipoulizwa na wanahabari kuruhusiwa kwa mikusanyiko hiyo katika chaguzi zilizopita, Mangu alijibu: “Polisi inafanya kazi na kupanga mikakati yake kutokana na hali halisi ya mazingira ilivyo, uchaguzi huu ni tofauti na zilizopita.”

“Mikusanyiko au vikundi hivi  vinachangia pia kuwatisha watu  wasiopiga kura .Ndiyo maana tunasema  kampeni zikiisha  na ukishapiga kura rudi nyumbani kwako. Kikundi au watu watakaokiuka sheria na taratibu za uchaguzi kwa kisingizio cha kulinda kura, jeshi halitawavumilia,” amesema.

Mangu amesema lengo la kupiga marufuku mikusanyiko hiyo ni kuhakikisha mchakato wa kupiga kura unamalizika katika hali ya amani na utulivu. Amesisitiza kuwa jeshi la polisi linaongozwa na falsafa ya kuelimisha, kushauri, kushawishi na kutumia nguvu inapobidi.

“Tumejiandaa vizuri kukabiliana na watu wote watakaobanika kwenda kinyume na utaratibu. Wananchi wasiwe na wasiwasi siku hiyo, wajitokeze kwa wingi kupiga kura, ulinzi utaimarishwa,” amesema Mangu.

Tuesday, October 20, 2015

Mkuu wa Majeshi DAVIS MWAMUNYANGE Ajitokeza Hadharani Kwenye Uzinduzi wa Uwanja wa Ndege za Kivita Morogoro

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais JAKAYA KIKWETE amezindua awamu ya pili ya ujenzi wa uwanja wa ndege za vita uliopo katika kamandi ya jeshi la anga iliyopo NGERENGERE mkoani MOROGORO.

Akizindua ujenzi huo,Rais KIKWETE amesema mazingira bora ya uwanja huo pamoja na kutumika kwa shughuli za kijeshi, yatawawezesha watu kufanya kazi kwa bidii na kuchochea uboreshwaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika eneo hilo.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. HUSSEIN MWINYI amesema kukamilika kwa mradi huo itakuwa ni hazina kwa jeshi la wananchi na taifa zima huku akisisitiza suala la matumizi ya uwanja huo kuboreshwa.

Naye Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali DAVIS MWAMUNYANGE ameeleza mikakati iliyopo ya kuboresha jeshi hilo, huku mkuu wa jeshi la anga Meja Jenerali JOSEPH KAPWANI akisema uwanja huo utakuwa bora katika nchi za Kusini mwa AFRIKA.