Mkuu wa Jeshi (IGP) Apiga Marufuku Mikusanyiko ya Watu siku ya Kupiga Kura
Jeshi la Polisi nchini, limepiga marufuku mikusanyiko ya watu siku ya kupiga kura kwa madai kwamba imekuwa ndiyo chanzo cha uvunjifu wa amani.
Pia,
Jeshi hilo limesema mikusanyiko ya aina yoyote haitakiwi baada
kuhitimishwa kwa kampeni Oktoba 24, mwaka huu badala yake wanaweza
kukusanyika na kusherehekea baada ya matokeo kutangazwa.
Tamko
hilo limetolewa leo na mkuu wa jeshi (IGP), Ernest Mangu akiwa kwenye
mazungumzo na wanahabari kuhusu Uchaguzi Mkuu utakaofanyika siku ya
jumapili.
Amesema
uzoefu wa jeshi hilo unaonyesha kuwa uwepo wa watu kwenye mikusanyiko
baada kupiga kura una sababisha vitendo vya uvunjifu wa amani.
Alipoulizwa na wanahabari kuruhusiwa kwa mikusanyiko hiyo katika chaguzi zilizopita, Mangu alijibu: “Polisi
inafanya kazi na kupanga mikakati yake kutokana na hali halisi ya
mazingira ilivyo, uchaguzi huu ni tofauti na zilizopita.”
“Mikusanyiko
au vikundi hivi vinachangia pia kuwatisha watu wasiopiga kura .Ndiyo
maana tunasema kampeni zikiisha na ukishapiga kura rudi nyumbani
kwako. Kikundi au watu watakaokiuka sheria na taratibu za uchaguzi kwa
kisingizio cha kulinda kura, jeshi halitawavumilia,” amesema.
Mangu
amesema lengo la kupiga marufuku mikusanyiko hiyo ni kuhakikisha
mchakato wa kupiga kura unamalizika katika hali ya amani na utulivu.
Amesisitiza kuwa jeshi la polisi linaongozwa na falsafa ya kuelimisha,
kushauri, kushawishi na kutumia nguvu inapobidi.
“Tumejiandaa
vizuri kukabiliana na watu wote watakaobanika kwenda kinyume na
utaratibu. Wananchi wasiwe na wasiwasi siku hiyo, wajitokeze kwa wingi
kupiga kura, ulinzi utaimarishwa,” amesema Mangu.
No comments:
Post a Comment