Ukimwona Mamba kasinzia usidanganyike kabisa, hili ndio pozi lake la mtego !!
on
October 22, 2015
October 22, 2015
Mamba ni mmoja ya wanyama ambao kama
ukikutana nao kwenye maji wana mabalaa yao, unaweza ukamchukulia kwamba
sio mnyama mwenye mbio sana ukilinganisha na wanyawa wengine kama Simba
na Chui, lakini ukimkuta kwenye maji balaa lake sio dogo !!
Wakati mwingine ni vizuri kujua tabia za
wanyama ili kama kwa bahati mbaya ukikutana nae uwe unajua kabisa jinsi
ya kuchukua tahadhari mapema.
Leo nimeipata hii ambayo sikuwahi kuijua
siku za nyuma, Wataalam wa Australia wamekuja na majibu ambayo huenda
ni watu wengi hawajui… kumbe Mamba anaweza kulala kwa kufunga jicho moja
huku moja likiwa wazi…hilo ndio pozi lake la kujilinda na kuvizia pia
wanyama ambao ndio chakula chake.
kingine ni kwamba Ubongo wa Mamba
unaweza kulala nusu huku nusu ukibaki unafanya kazi sawa kabisa !! Kama
na wewe ulikuwa huzijui hizo, basi nimekusogezea ili ikitokea unakutana
na mamba amesinzia uwe na tahadhari yako kabisa hata kabla hujamsogelea.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa
na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK
ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.
No comments:
Post a Comment