Mama Mtikila Ameongea Haya Mbele ya Waandishi wa Habari:
Ndugu Wana-Habari,
Kabla sijawaeleza kilichonilazimisha kuwaomba kuongea nanyinyi, kwanza
niwarudishe nyuma kama miaka saba iliyopita, ndipo maisha ya Baba,
Mchungaji, Mwenyekiti na mume wangu, Mchungaji Christopher Reuben
Mtikila yalipoanzwa kuwindwa:-
MAUWAJI YA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE
Mara tu baada ya kifo cha mbunge huyo, mchungaji Mtikila alitoa ripoti
maalumu juu ya mauaji yake ambayo ilimjengea uadui kati ya baadhi ya
vyama vya siasa pamoja na wafanyabiashara wakubwa ambao hadi leo ni
wapinzani wa serikali hapa nchini.--Mchungaji Mtikila hadi anafikwa na
mauti aliendelea kupata upinzani wa aina hiyo hiyo kwa sababu mchungaji
Mtikila aliendelea kudai haki ya marehemu Chacha Zakayo Wangwe.
MAUAJI YA BULIGI
Hii ilimwongezea uadui baada ya kusema/kuandika ukweli juu ya watutsi wa
nchi jirani kuvamia nchi yetu kwa mtindo wa kujifanya wafugaji wasio
hama. L.I.F. ilibaini uharamia huo kuwa hawakuwa wafugaji bali walikuwa
askari wa Jeshi la Rwanda waliokuwa na mpango wa kutumika na Chama
kimoja cha siasa hapa nchini ili kuleta mapigano yatakayo zaa mapinduzi.
Jambo hili lilisababisha Rais wa Rwanda, Paulo Kagame kutamka hadharani
kuwa angemkamata Mwenyekiti wa chama chetu cha DP--kwa lengo la kumuua
na Serikali yetu inajua hilo. Mara baada ya ripoti hiyo kutolewa na
Mchungaji Mtikila "operation Kimbunga" ilizaliwa na kuponya nchi yetu;
lakini chuki na uadui uliendelea dhidi ya Mchungaji Mtikila.
MCHAKATO WA URAIS NDANI YA CCM
Ikumbukwe kuwa mara baada ya mchakato wa kutafuta mgombea urais kwa
tiketi ya CCM kuanza DP ilitoa ripoti iliyowahusu wagombea sita wa CCM
waliotumia mapesa mengi na kuanza kampeni kabla ya muda na kusisitiza
kuwa Lowasa ni mtu asiefaa kuwa Rais wa nchi yetu. Na baada ya kuhama
CCM, Mwenyekiti wetu aliendelea kutoa tahadhari hadharani jinsi Lowasa
asivyofaa kuwa Rais wa nchi yetu hivyo likaendeleza uadui wake na Chama.
VITISHO--KUANZA
Mchungaji Mtikila alipata nafasi ya kuongea katika kipindi kinachorushwa
na STAR TV cha asubuhi "TUONGEE" ndipo alipoanza kupata vitisho toka
kwa watu mbali mbali wengine kupitia kwenye simu wengine uso kwa uso.
Kipindi cha kwanza kilirushwa tarehe 25/9/2015 na kufuatwa na cha tarehe
27/9/2015. Alipotoka studio hiyo asubuhi ya tarehe 27/9/2015 ndipo watu
waliodai wametumwa na Mhe. Edward Ngoyai Lowasa na Mhe Frederick Sumaye
walimuomba wampe nusu bilioni na apewe maovu ya mgombea urais wa CCM
ili afunike-alivyowamaliza wao.
Mchungaji Mtikila aliwapuuzia mbali wale wajumbe waliyotumwa kwani
aliawaambia kuwa yeye siyo malaya wa kuuza utu wake kwa tende na haluwa.
Yakumbukwe kuwa mahojiano kwenye hivyo vipindi viwili kwenye STAR TV
hayakuwa yanatetea mtu au chama yalikuwa yanatetea Taifa letu lipate
Rais anayefaa.
Kwa hiyo basi wale waliochukizwa na mahojiano hayo ni wale amabo
hawakubaliani na mawaidha ya Mchungaji Mikila aliyokuwa
anawatahadharisha watanzania juu ya Mh. Lowasa kuwa hatari kwa usalama
wa taifa letu kama atakuwa Rais wa nchi yetu. Hao watu ndiyo waliopanga
mpango mzima wa mauaji ya Mh. Mtikila ambaye ni mume wangu.
Wakati yuko Bunda mjini watu wasiofahamika walimfuatafuata na tarehe
26/9/2015 gari lake lilifukuzwa na gari usiku wakati alipokuwa anatoka
Bunda kwenda Mwanza kufanya mahojiano ya tarehe 27/9/2015 na Star Tv.
MPANGO WA MAUAJI HALISI
Mchungaji Mtikila alitafutiwa gari na Victor James Manyahi ambayo
ilikuwa na madereva wawili. Mchungaji madereva hakuwajua. Hata mimi
madereva hao sikuwajua wala sikuwaona. Walikodiwa kutoka wapi sijui,
wala sijui wanafanana vipi. Na wala sijui Victor Manyahi alikodi gari
hilo kwa nani na makubaliano yepi sijui.
Kwa hivyo basi, kwenye gari aliyosafiri nayo Mchungaji Mtikila
kulikuwamo madereva wawili na Mgaya Patrick (tunayemfahamu). Wakati
wanakwenda gari lilipata ajali Makambako. Wakati wanarudi wakapata
“ajali” Msolwa Mchungaji akapatwa na mauti peke yake. Ajali ilikuwa
mbaya sana-IKAUWA MTU MMOJA AMBAYE NI MCHUNGAJI MTIKILA NA HAKUKUWA
MAJELUHI HATA MMOJA.-Cha ajabu kwangu ni kuwa mtu ambaye alikuwa ni
mlinzi wa kujitolea (body guard) Mgaya Patrick sijawahi kumuona usoni
mwangu kabla na hata baada ya mazishi kuja kuniambia kilichotokea eneo
la ajali. Pamoja na juhudi zangu zote za kumpigia simu mara kadhaa aje
anijuze Mgaya Patrick hajatokea hadi sasa ndugu zangu wanahabari
ninapoongea nanyi. Lakini si kwamba huyu mtu hayupo, yupo lakini
sijaonana naye, kwa nini sijui. Je ndugu zangu wanahabari nimuweke Mgaya
Patrick kwenye fungu gani?
Ndugu Wana-Habari, baada ya kuwaelezea yote hapo juu nakuja kwenye suala
nililowaomba nikutane nanyi ili niongee mbele yenu kuwa sikubaliani na
uchunguzi kuwa Mchungaji Christopher Reuben Mtikila amekufa kwa ajali.
Sikubaliani na kazi ya Polisi kuwa wamefunga file lao kutokana na
Post-mortem report kuwa mauti yaliotokana na ajali. Nafuta kabisa
taarifa--iliyotoka katika gazeti la Nipashe chini ya kichwa cha habari
kuwa “FAMILIA YAFUNGUKA KIFO CHA MTIKILA”-ilitolewa mapema mno. Kila
mwanafamilia alikuwa hajawa tayari kutoa kauli yoyote. Kwa niaba ya
Chama na familia ya Mchungaji Christopher Reuben Mtikila naomba
tusaidiwe yafuatayo kusudi haki ya mpendwa wetu-ionekane--inatendeka:-
Kwa sababu mtandao umeanza kuficha ukweli ili kulinda wauaji; tunaomba
Mheshimiwa Rais aingilie utata wa kifo cha Mheshimiwa Mchungaji
Christopher Reuben Mtikila kwa kuunda tume ya uchunguzi isiyohusisha
polisi.
Tunaiomba mamlaka ya mawasiliano yaani Tanzania Communications Regulatory Authority, TCRA itusaidie yafuatayo:-
(a)----Mtu aliyeweka picha kwanza alfajiri kuonyesha mauti ya Mhe
Mchungaji Mtikila alikuwa wapi? Kwenye tukio? Au ni hao wauaji walikuwa
wanatoa taarifa kwa waajiri wao kuwa wamekamilisha kazi!
(b)----Mtu aliyeweka picha ya Dr. Jean-Bosco Ngendahimana kwenye mtandao
kuwa ndiye anahusika na mauti ya Mhe. Mch. Mtikila na kumusingizia kuwa
amekamatwa na polisi akiwa anajiandaa kukimbia;
(c)-----Wote wanaoendelea kumhusisha Dr. Jean-Bosco Ngendahimana na
mauaji ya Mhe. Mchungaji Mtikila, tuwafahamu ili watueleze vizuri.
Ukweli na haki ni vya Mungu hakuna anayeweza kuviua au kuvizuia.
Tunategemea Mungu atawatumia watendaji wa Serikali/nchi yetu wenye nia
njema, na makusudi yaliyonyooka kwa ajili ya nchi yetu ili Mhe.
Mchungaji Mtikila apewe haki dhidi ya wauaji wake.
Asanteni,
Georgia C . Mtikila,
-KM DP/Msemaji-Familia